Jermaine Jackson, Marekani (sehemu ya 2 kwa 2)
Maelezo: Kaka wa nyota maarufu duniani Michael Jackson anasimulia jinsi alivyoukubali Uislamu. Sehemu ya 2.
- Na Jermaine Jackson (edited by www.IslamReligion.com
- Iliyochapishwa mnamo 17 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 5,243 (wastani wa kila siku: 5)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Je, wanafamilia wengine wana maoni gani kukuhusu?
Niliporudi Marekani, mama yangu alikuwa tayari amesikia habari za kusilimu kwangu. Mama yangu ni mwanamke wa dini na mstaarabu. Nilipofika nyumbani, aliuliza swali moja tu, "umechukua uamuzi huu ghafla, au ni matokeo ya mawazo ya kina na marefu nyuma yake?" "Nimeamua baada ya kufikiria sana," nilijibu, niseme tunajulikana kama familia ya kidini. Chochote tunachomiliki, ni kwa sababu ya baraka za Mungu. Basi kwa nini tusiwe na shukrani Kwake? Hii ndiyo sababu tunashiriki kikamilifu katika taasisi za misaada. Tulituma dawa kwa nchi maskini za Kiafrika kupitia ndege maalum. Wakati wa vita vya Bosnia, ndege zetu zilihusika katika kusambaza misaada kwa [walioathirika]. Sisi ni wasikivu kwa mambo kama haya kwa sababu tumeshuhudia umaskini wa kutisha. Tulikuwa tunaishi katika nyumba ambayo ilikuwa na uwezo mdogo wa mita chache miraba.
Je, uliwahi kuujadili Uislamu na dada yako nyota wa pop Janet Jackson?
Kama watu wengine wa familia yangu, kusilimu kwangu kwa ghafla kulikuwa ni mshangao mkubwa kwake. Hapo mwanzo alikuwa na wasiwasi. Ameweka kichwani mwake jambo moja tu kwamba Waislamu wana wake wengi, wana wake kama wanne. Nilipoeleza ruhusa hii iliyotolewa na Uislamu kuhusiana na hali ya jamii ya sasa ya Marekani, aliridhika. Huu ndio ukweli kwamba usherati na ukafiri ni jambo la kawaida sana katika jamii ya kimagharibi. Licha ya ukweli kwamba wameolewa, wanaume wa magharibi hufurahia mahusiano ya nje ya ndoa na wanawake kadhaa. Hili limesababisha kuharibika kwa maadili katika jamii hiyo. Uislamu unalinda mfumo wa kijamii kutokana na uharibifu huu.
Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, mwanamume akivutiwa na mwanamke kihisia, basi kwa heshima yake anapaswa kuupa uhusiano huu sura ya kisheria vinginevyo lazima aridhike na mke mmoja tu. Kwa upande mwingine, Uislamu umeweka masharti mengi sana ya ndoa ya pili kiasi kwamba sidhani kwamba Muislamu wa kawaida anaweza kumudu masharti haya kifedha. Kuna karibia asilimia moja ya Waislamu katika ulimwengu wa Kiislamu ambao wana zaidi ya mke mmoja. Kwa maoni yangu, mwanamke katika jamii ya Kiislamu ni kama ua linalolindwa vyema na ambalo ni salama kutokana na mwonekano unaopenya wa watazamaji. Ingawa jamii ya kimagharibi haina dira ya kufahamu hekima na falsafa hii.
Je, ni hisia zipi unazozipata unapoitazama jamii ya Kiislamu?
Kwa maslahi makubwa ya wanadamu, jamii ya Kiislamu inawasilisha sehemu salama zaidi kwenye sayari hii. Kwa mfano, chukua mfano wa wanawake. Wanawake wa Kimarekani wanavaa mavazi yao kwa namna ambayo inawapa vishawishi wanaume kwa unyanyasaji. Lakini hili haliwezekani katika jamii ya Kiislamu. Mbali na hilo, dhambi na maovu yaliyoenea yameharibu mfumo wa maadili wa jamii ya magharibi. Ninaamini kama kuna sehemu yoyote iliyobaki ambapo utu bado unaonekana, haiwezi kuwa mahali pengine popote isipokuwa katika jamii ya Kiislamu. Muda ungefika ambapo ulimwengu ungelazimika kukubali ukweli huu.
Je, maoni yako ni yapi kuhusu vyombo vya habari vya Marekani?
Vyombo vya habari vya Marekani vinakabiliwa na mikanganyiko ya kibinafsi. Chukua mfano wa Hollywood. Hadhi ya msanii inapimwa kwa kuzingatia mfano wa gari lake, kiwango cha mgahawa anaotembelea n.k. Hiki ndicho chombo cha habari kinachomuinua mtu kutoka mavumbini hadi angani. Hawamchukulii msanii kama mwanadamu. Lakini nimekutana na wasanii wengi sana huko Mashariki ya Kati. Hawana kiburi kilichopotea ndani yao.
Angalia tu CNN, wanatia chumvi sana kuhusu baadhi ya habari ya kuwa inaonekana kama hakuna kitu kingine kilichotokea isipokuwa tukio hilo duniani. Habari za moto katika misitu ya Florida zilipewa kipaumbale sana hadi zilitoa hisia kwamba ulimwengu wote umeshika moto. Katika ukweli, lilikuwa eneo dogo, ambalo liliathiriwa na moto huo.
Nilikuwa Afrika wakati mlipuko wa bomu ulipotokea katika Jiji la Oklahoma. Vyombo vya habari, bila uthibitisho wowote, vilianza kudokeza kuhusika kwa Waislamu katika mlipuko huo. Baadae Huyo Mhujumu akatokea kuwa MKRISTO!!! Tunaweza kusema mtazamo huu wa vyombo vya habari vya Marekani kama ujinga wa makusudi.
Je, unaweza kudumisha uhusiano kati ya wasifu wako wa Kiislamu na utamaduni wa familia yako?
Kwa nini isiwe hivyo? Uhusiano huu unaweza kuwepo kwa ajili ya kufanikisha mambo mazuri.
Baada ya kusilimu, uliwahi kumuona Muhammad Ali?
Muhammad Ali ni rafiki wa familia yetu. Nimekutana naye mara kadhaa, baada ya kusilimu. Ametoa mwongozo wenye manufaa kuhusu Uislamu
Je, umetembelea msikiti wa Shah Faisal katika jiji la Los Angeles?
Ndiyo, bila shaka! Huu ni msikiti mzuri. Nina nia ya kujenga msikiti kama huo katika eneo la Falise kwa sababu hakuna misikiti katika eneo hili na jamii ya Kiislamu haina rasilimali za kutosha kununua kipande cha ardhi kwa ajili ya msikiti katika eneo la kifahari kama hilo. Mungu akipenda, ningefanya.
Ni nani asiyejua huduma za Saudi Arabia kwa sababu tukufu ya Uislamu?
Bila shaka imefadhili kwa furaha miradi ya misikiti. Lakini vyombo hivi vya habari vya Marekani hata haviihurumii Saudi Arabia; inaeneza habari za ajabu sana kuhusu nchi hii. Nilipotembelea Saudi Arabia kwa mara ya kwanza, nilipata hisia kwamba kungekuwa na nyumba za udongo na mtandao mbaya sana wa mawasiliano. Lakini nilipofika huko, kwa mshangao wangu mkubwa, niliona kitamaduni ni nchi nzuri zaidi ulimwenguni.
Je, ni nani aliyekushawishi, kwa jinsi Uislamu unavyohusika?
Watu wengi wamenivutia. Lakini ukweli ni kuwa kwanza naigeukia Quran Tukufu, Hivyo siingii katika hatari ya kupotea njia. Hata hivyo, kuna wanazuoni wengi wa Kiislamu ambao mtu anaweza kujivunia. Mungu akipenda, ninapanga kwenda Saudi Arabia na familia yangu kufanya Umra.
Mke na watoto wako ni Waislamu pia?
Nina watoto wa kiume saba na mabinti wawili ambao, kama mimi, wana mwelekeo wa Uislamu. Mke wangu bado anausoma Uislamu. Anasisitiza kwenda Saudi Arabia. Ninaamini InshaAllah [Mwenyezi Mungu Akipenda], angejiunga na Uislamu haraka. Mwenyezi Mungu atupe ujasiri na ustahimilivu wa kubaki katika dini hii ya kweli ya Uislamu. (Amina)
Ongeza maoni