Biblia Inakana Umungu wa Yesu (sehemu ya 7 kati ya 7): Mungu na Yesu Ni Viumbe Wawili Tofauti.
Maelezo: Watu wengi hutumia mistari fulani ya Biblia kama uthibitisho kwamba Yesu ni Mungu. Hata hivyo, aya hizi zote, zinapoeleweka katika muktadha, zinathibitisha kinyume chake!
- Na Shabir Ally
- Iliyochapishwa mnamo 19 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 5,935 (wastani wa kila siku: 6)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Kwa mfano, katika Mathayo 9:2, Yesu alimwambia mtu fulani, “Jipe moyo, mwanangu; umesamehewa dhambi zako.” Kwa sababu hiyo, wengine husema kwamba ni lazima Yesu awe Mungu kwa kuwa ni Mungu pekee anayeweza kusamehe dhambi. Hata hivyo, ukiwa tayari kusoma mistari michache tu zaidi, utaona kwamba watu “...wakamsifu Mungu, aliyewapa wanadamu mamlaka ya namna hii.” (Mathayo 9:8). Hii inaonyesha kwamba watu walijua, na Mathayo anakubali kwamba Yesu sio mwanadamu pekee kupokea mamlaka hayo kutoka kwa Mungu.
Yesu mwenyewe alisisitiza kwamba hasemi kwa mamlaka yake mwenyewe (Yohana 14:10) na hafanyi neno kwa mamlaka yake mwenyewe, bali anazungumza tu yale ambayo Baba amemfundisha (Yohana 8:28). Alichokifanya Yesu hapa kilikuwa kama ifuatavyo. Yesu alimtangazia mtu huyo ujuzi ambao Yesu alipokea kutoka kwa Mungu kwamba Mungu alikuwa amemsamehe mtu huyo.
Angalia kwamba Yesu hakusema, “Nimekusamehe dhambi zako,” bali badala yake, “umesamehewa dhambi zako,” akidokeza kwamba, kama vile wasikilizaji wake Wayahudi, Mungu alikuwa amemsamehe mtu huyo. Yesu, basi, hakuwa na uwezo wa kusamehe dhambi, na katika tukio hilo hilo alijiita “Mwana wa Adamu” (Mathayo 9:6).
Yohana 10:30 hutumiwa mara nyingi kama uthibitisho kwamba Yesu ni Mungu kwa sababu Yesu alisema, “Mimi na Baba tu wamoja.” Lakini, ukisoma mafungu sita yanayofuata, utamkuta Yesu akieleza kwamba adui zake walikosea kufikiri kwamba anadai kuwa Mungu. Kile ambacho Yesu anamaanisha hapa ni kwamba yeye yupo pamoja na Baba katika kusudi. Yesu pia alisali kwamba wanafunzi wake wawe kitu kimoja kama vile Yesu na Baba walivyo wamoja. Kwa wazi, hakuwa akiomba kwamba wanafunzi wake wote waungane kwa namna fulani na kuwa mtu mmoja (angalia Yohana 17:11 na 22). Na Luka anapo elezea kwamba wanafunzi wote walikuwa wamoja, Luka hamaanishi kwamba walikuwa binadamu mmoja, lakini kwamba walishiriki kusudi moja ingawa walikuwa viumbe tofauti (angalia Matendo 4:32). Kwa maana ya kiini, Yesu na Baba ni wawili, kwa maana Yesu alisema wao ni mashahidi wawili (Yohana 8:14-18). Wanapaswa kuwa wawili, kwa kuwa mmoja ni mkuu kuliko mwingine (angalia Yohana 14:28). Yesu alipoomba kuokolewa kutoka msalabani, alisema: “Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; lakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. (Luka 22:42).
Hii inaonyesha kwamba walikuwa na matakwa mawili tofauti, ingawa Yesu aliwasilisha matakwa yake kwa matakwa ya Baba. Matakwa mawili maana yake ni watu wawili tofauti.
Zaidi ya hayo, inaelezwa kwamba Yesu alisema: “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” (Mathayo 27:4 ). Ikiwa mmoja wao alimuacha mwingine, basi lazima wawe ni vitu viwili tofauti.
Tena, inaripotiwa kwamba Yesu alisema: “Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.” (Luka 23:46). Ikiwa roho ya mtu inaweza kuwekwa kwenye mikono ya mwingine, lazima wawe viumbe viwili tofauti.
Katika matukio haya yote, Yesu yuko chini ya Baba. Yesu alipo piga magoti na kuomba ni wazi hakuwa akiomba kwake mwenyewe (angalia Luka 22:41). Alikuwa akiomba kwa Mungu wake.
Katika Agano Jipya lote, Baba pekee ndiye anayeitwa Mungu. Kwa kweli, vheo vya “Baba” na “Mungu” vinatumiwa kutaja mtu mmoja, sio watatu, wala kamwe sio Yesu. Hii pia iko wazi kutokana na uhakika wa kwamba Mathayo alibadilisha cheo cha “Baba” mahali na kueka cheo cha “Mungu” katika angalau sehemu mbili katika Injili yake (linganisha Mathayo 10:29 na Luka 12:6, na Mathayo 12:50 na Marko 3:35). Ikiwa Mathayo yuko sahihi kufanya hivyo, basi Baba peke yake ndiye Mungu.
Je, Yesu alikuwa Baba? Hapana! Kwa sababu Yesu alisema: “Wala msimuite mtu yeyote duniani ‘baba,’ kwa maana mna Baba mmoja, naye yuko mbinguni.” (Mathayo 23:9 ). Kwa hiyo Yesu sio Baba, kwa kuwa Yesu alikuwa amesimama duniani aliposema hivyo.
Quran inataka kuwarudisha watu kwenye imani ya kweli ambayo ilifundishwa na Yesu, na wanafunzi wake wa kweli walioendelea na mafundisho yake. Mafundisho hayo yalisisitiza kuendelea kujitolea kwa amri ya kwanza kwamba Mungu yuko peke yake. Katika Quran, Mungu anawaelekeza Waislamu kuwaita wasomaji wa Biblia warudi kwenye imani hiyo ya kweli. Mwenyezi Mungu amesema katika Quran:
Sema: “Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu.” (Kurani, 3:64)
Ongeza maoni