Kristin, Mkatoliki wa zamani, Marekani (sehemu ya 1 kati ya 2)
Maelezo: Mkristo wa zamani anajadili mambo ya Kikristo ambayo aliyaona hayapatani na akili na alivyozingatia Uyahudi.
- Na Kristin
- Iliyochapishwa mnamo 17 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 5,127 (wastani wa kila siku: 5)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Utafiti wangu wa dini ulianza nikiwa katika shule ya sekondari nilipokuwa na umri wa miaka 15 au 16. Nilikuwa nikishirikiana na kundi la watu wabaya ambao nilidhani walikuwa marafiki zangu, lakini baada ya muda nilitambua watu hawa walikuwa hawana maana yoyote. Niliona mwelekeo gani maisha yao yalikuwa yakielekea, na haukuwa mzuri. Sikutaka watu hawa wawe na athari yoyote juu ya mafanikio yangu kwa siku zijazo, kwa hivyo niliwachana nao kabisa. Ilikuwa vigumu mwanzoni kwa sababu nilikuwa peke yangu bila marafiki. Nilianza kutafuta kitu cha kujiunga nacho na kitu ambacho ningeweza kukitegemea na kuhusisha maisha yangu nacho... kitu ambacho hakuna mtu angeweza kukitumia kuharibu mustakabali wangu nacho. Kwa kawaida, niligeuka kumtafuta Mungu. Hata hivyo, kujua Mungu alikuwa nani na ukweli ulikuwa nini halikuwa jambo rahisi. Kwani, hivi ukweli ni nini?! Hili lilikuwa swali langu la msingi nilipoanza kutafuta dini.
Katika familia yangu, kumekuwa na mabadiliko mengi ya kidini. Familia yangu ina Wayahudi na aina chache za Ukristo ndani yake, na sasa, Alhumdulilah (wa kutukuzwa ni Mwenyezi Mungu) ina Uislamu.
Mama yangu na baba yangu walipoana, walihisi kulikuwa na haja ya kuamua watawalea watoto wao kwa dini gani. Kwa kuwa Kanisa Katoliki lilikuwa ndilo chaguo pekee kwao (mji wetu una watu 600 tu) wote wawili wakawa wakatoliki na kutulea mimi na dada yangu kama Wakatoliki. Nikirudi kupitia hadithi za ubadilishaji wa dini katika familia yangu, inaonekana kwamba yote ni mabadiliko ya kutafuta masilahi ya kibinafsi. Sidhani walikuwa wanamtafuta Mungu kikweli, bali walitumia dini kama njia tu ya kufikia lengo fulani. Hata baada ya mabadiliko haya yote ya mbeleni, dini haikuwa na umuhimu mkubwa kwa mama, baba na dada yangu, na kwangu mimi pia. Yetu ilikuwa kama zile familia unaowaona kanisani wakati wa Krismasi na Pasaka. Siku zote nilihisi kuwa dini ilikuwa kitu tofauti na maisha yangu, siku 6 kwa wiki kwa maisha yangu na siku moja kwa wiki kwa ajili ya kanisa, katika siku chache nilipokwenda. Kwa maneno mengine, sikuwa na ufahamu wa Mungu wala jinsi ya kuishi kulingana na mafundisho yake kila siku.
Sikukubaliana na baadhi ya sera za Kikatoliki kama:
1) Kukiri dhambi kwa kuhani: Nilifikiria kwa nini sikuweza kukiri tu kwa Mungu bila ya kwenda kupitia mwanadamu ili kumfikia?
2) Papa “Mkamilifu ”- Itakuwaje mwanadamu, ambaye hata si mtume, awe mkamilifu?!
3) Kuabudu watakatifu- je, hii haikuwa ukiukaji wa moja kwa moja wa amri ya kwanza? Hata baada ya miaka 14 ya kulazimishwa kuhudhuria shule ya Jumapili, majibu niliyopokea kwa maswali haya na mengine yalikuwa, “Unahitaji tu kuwa na imani!!” Je, nafaa kuwa na imani kwa sababu mtu ALINIAMBIA hivyo?! Nilidhani imani inapaswa kutokana na ukweli na majibu ambayo yaliafikiana na mantiki. Nilikuwa na nia ya kupata baadhi ya majibu haya.
Sikutaka ukweli wa wazazi wangu, au marafiki, au mtu mwingine yeyote. Nilitaka ukweli wa Mungu. Nilitaka kila fikira niliyoshikilia iwe kweli kwangu kwa sababu niliiamini kabisa, kwa moyo na roho. Niliamua kwamba iwapo ningepata majibu ya maswali yangu, ningetafuta kwa akili wazi, na nilianza kusoma...
Niliamua kwamba Ukristo haungekuwa dini yangu. Sikuwa na uadui wowote binafsi na Wakristo, lakini nimeona kuwa dini yenyewe ilikuwa inatofautiana kwa wingi, hasa niliposoma Biblia. Katika Biblia, tofauti nilizokutana nazo na mambo ambayo hayakunikaa akilini kabisa yalikuwa mengi kiasi kwamba nilihisi aibu kwamba sijawahi kujiuliza kuhusu hayo mbeleni au hata kuyaona!
Kwa kuwa baadhi ya watu katika familia yangu ni Wayahudi, nilianza kuchunguza Uyahudi. Nilidhani jibu linaweza kuwa pale. Kwa hivyo kwa mwaka mmoja nilifanya utafiti juu ya kitu chochote kuhusu Uyahudi, namaanisha utafiti WA KINA!! Kila siku nilijaribu kusoma na kujifunza kitu (bado najua kuhusu sheria za Kiorthodoksi za Kiyahudi za kosha!). Nilikwenda maktabani na kuangalia kila kitabu kuhusu Uyahudi ndani ya muda wa miezi miwili. Kwenye mtandao, nilikwenda kwenye sinagogi, nikazungumza na Wayahudi wengine katika miji ya jirani na kusoma Torati na Talmud. Hadi nilimuita mmoja wa marafiki zangu wa Kiyahudi kuja kunitembelea kutoka Israeli! Nilidhani labda nimepata kile nilichokuwa nikitafuta. Hata hivyo, ile siku nilitakiwa kwenda sinagogi na kukutana na rabi kuhusu uwezekano wa kuingia rasmi kwenye Uyahudi, nilijiondoa. Kusema kweli sijui nini ilinizuia kuondoka nyumbani siku hiyo, lakini nilisimama tu nilipokuwa karibu kwenda nje ya mlango na kurudi ndani na kukaa chini. Nilihisi kana kwamba nilikuwa katika mojawapo ya ndoto hizo ambapo unajaribu kukimbia lakini kila kitu kinakwenda polepole. Nilijua rabi alikuwa pale akinisubiri, lakini sikumpigia hata kumwambia kuwa naja. Rabbi hakunipigia pia. Kuna kitu kilikuwa hakiko...
Baada ya kujifunza kwamba Uyahudi pia haukuwa jibu, nilifikiri (pia baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa wazazi wangu) kujaribu Ukristo mara nyingine. Nilikuwa na, kama nilivyosema, historia nzuri katika misingi kutokana na miaka yangu ya shule za Jumapili, lakini nilikuwa nataka kujua zaidi na kupata ukweli nyuma ya misingi hii. Uzuri wake ulikuwa wapi, usalama wake ulikuwa wapi na ningeweza vipi kuikubali kimantiki? Nilijua kwamba iwapo ningezingatia Ukristo, Ukatoliki haukuwa hiari kwangu. Nilikwenda kwa kila kanisa lingine la Kikristo katika mji wangu, Kilutheri, Pentekoste, Watakatifu wa Siku za Mwisho (Mormoni), na makanisa yasiyo ya madhehebu. Sikupata kile nilichokuwa nikitafuta - majibu!! Haikuwa mazingira ya watu ndio niliyokataa; ilikuwa ni utofauti kati ya madhehebu ndio ulinisumbua. Niliamini kulikuwa na njia moja sahihi, kwa hivyo ningewezaje kuchagua dhehebu “sahihi”? Katika makadirio yangu ilikuwa haiwezekani kwa Mungu mwenye huruma kuwaacha wanadamu na chaguo kama hilo. Nilikuwa nimepotea...
Ongeza maoni