Biblia Inakana Umungu wa Yesu (sehemu ya 4 kati ya 7): Amri Kuu Zaidi Katika Biblia na Kurani.
Maelezo: Ipi ni amri ya kwanza na kuu kuliko zote katika Biblia, ambayo ilisisitizwa na Yesu.
- Na Shabir Ally
- Iliyochapishwa mnamo 18 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 5,550 (wastani wa kila siku: 5)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Wengine watasema kwamba mjadala huu kuhusu umungu wa Yesu hauhitajiki. Wanasema, jambo la muhimu ni kumkubali Yesu kama mwokozi wako binafsi. Badala yake, waandishi wa Biblia walikazia kwamba, ili kuokolewa, ni muhimu kuelewa ni nani hasa aliye Mungu. Kushindwa kuelewa hili kungekuwa ni kukiuka amri kuu na ya kwanza kati ya zote katika Biblia. Amri hiyo ilikaziwa na Yesu, ambaye amani iwe juu yake, wakati mwalimu wa Sheria ya Musa alipomwuliza: “‘Katika amri zote, ni ipi iliyo kuu?’ ‘iliyo kuu zaidi,’ Yesu akajibu , ‘ni hii: Sikia, Ee Israeli, Bwana Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote.’” (Marko 12:28-30).
Angalia jinsi Yesu alikuwa akinukuu amri ya kwanza kutoka katika kitabu cha Kumbukumbu ya Torati 6:4-5. Yesu alithibitisha sio tu kwamba amri hii bado ni halali, lakini pia kwamba ni muhimu zaidi ya amri zote. Ikiwa Yesu alifikiri kwamba yeye mwenyewe ni Mungu, kwa nini hakusema hivyo? Badala yake, alisisitiza kwamba Mungu ni mmoja. Mtu aliyemuuliza Yesu alielewa jambo hilo, na jambo ambalo mtu huyo anasema baadaye linaonyesha wazi kwamba Mungu sio Yesu, kwa kuwa alimwambia Yesu hivi: “‘Umesema vema, mwalimu,’ mtu huyo akajibu. ‘Unasema kweli kwamba Mungu ni mmoja na hakuna mwingine ila yeye.’” (Marko 12:32).
Sasa kama Yesu angekuwa Mungu, angalimwambia mtu huyo hivyo. Badala yake, alimruhusu mtu huyo amrejeze Mungu kuwa mtu mwingine badala ya Yesu, na hata akaona kwamba mtu huyo alikuwa amesema kwa hekima: “Yesu alipoona kwamba amejibu kwa busara, akamwambia, ‘Wewe haupo mbali na ufalme wa Mungu.’” (Marko 12:34). Ikiwa Yesu alijua kwamba Mungu ni Utatu, kwa nini hakusema hivyo? Kwa nini hakusema kwamba Mungu ni mmoja katika watatu, au watatu katika mmoja? Badala yake, alitangaza kwamba Mungu ni mmoja. Waigaji wa kweli wa Yesu watamwiga pia katika tangazo hili la umoja wa Mungu. Hawataongeza neno tatu ambapo Yesu hakusema kamwe.
Je, wokovu unategemea amri hii? Ndiyo, Biblia inasema! Yesu aliweka wazi hili wakati mtu mwingine alipomwendea Yesu ili kujifunza kutoka kwake (angalia Marko 10:17-29). Mtu huyo alipiga magoti na kumwambia Yesu: “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?” Yesu akajibu: “Kwa nini unaniita mwema? Hakuna aliyemwema —isipokuwa Mungu peke yake.” (Marko 10:17-18).
Kwa kusema hivyo, Yesu aliweka wazi tofauti kati yake na Mungu. Kisha akaendelea na jibu la swali la mtu huyo kuhusu jinsi ya kupata wokovu. Yesu alimwambia hivi: “Ukitaka kuingia katika uzima, zitii amri.” (Mathayo 19:17, pia angalia Marko 10:19).
Kumbuka kwamba amri kuu kuliko zote, kulingana na Yesu, ni kumjua Mungu kama Mungu pekee. Yesu alisisitiza zaidi hili katika Injili Kulingana na Yohana. Katika Yohana 17:1, Yesu aliinua macho yake mbinguni na kuomba, akimuita Mungu kama Baba. Kisha katika mstari wa tatu, akamwambia Mungu hivi: “Sasa uzima wa milele ndio huu: Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.” (Yohana 17:3).
Hilo lathibitisha bila shaka kwamba ikiwa watu wanataka kupata uzima wa milele ni lazima wajue kwamba Yule, ambaye Yesu alikuwa akisali kwake, ndiye Mungu wa pekee wa kweli, na lazima wajue kwamba Yesu alitumwa na Mungu wa kweli. Wengine husema kwamba Baba ni Mungu, Mwana ni Mungu, na Roho Mtakatifu ni Mungu. Lakini Yesu alisema kwamba Baba peke yake ndiye Mungu wa pekee wa kweli. Wafuasi wa kweli wa Yesu watamfuata katika hili pia. Yesu alikuwa amesema kwamba wafuasi wake wa kweli ni wale wanaoshikamana na mafundisho yake. Alisema: “Ikiwa mtashika mafundisho yangu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli.” (Yohana 8:31 ). Mafundisho yake ni kwamba watu wanapaswa kuendelea kushika amri, hasa amri ya kwanza ambayo inasisitiza kwamba Mungu yuko peke yake, na kwamba Mungu anapaswa kupendwa kwa mioyo yetu yote na nguvu zetu zote.
Tunampenda Yesu, lakini hatupaswi kumpenda kama Mungu. Leo, wengi wanampenda Yesu kuliko Mungu. Hii ni kwa sababu wanamuona Mungu kuwa mtu wa kulipiza kisasi ambaye alitaka kuwapa adhabu, na wanamwona Yesu kuwa mwokozi aliyewaokoa kutoka kwa ghadhabu ya Mungu. Hata hivyo Mungu pekee ndiye mwokozi wetu. Kulingana na Isaya 43:11 , Mungu alisema: “Mimi, naam, mimi, ni BWANA, na pasipo mimi hakuna mwokozi.” Pia Mungu alisema kulingana na Isaya 45:21-22: “Je, si mimi, BWANA? Wala hakuna Mungu ila mimi, Mungu mwenye haki na Mwokozi; hakuna ila mimi. Nigeukieni mimi na kuokolewa, enyi pande zote za dunia; kwa maana mimi ni Mungu, wala hakuna mwingine.”
Kurani inathibitisha amri ya kwanza na kuielekeza kwa wanadamu wote (angalia Kurani Tukufu 2:163). Na Mwenyezi Mungu anatangaza kwamba waumini wa kweli wanampenda Yeye kuliko mtu mwingine yeyote au kitu chochote kile (Kurani 2:165).
Ongeza maoni