Kutafuta kwa utulivu na amani ya ndani (sehemu ya 1 kati ya 4): Vikwazo vya Kufikia Amani ya Ndani
Maelezo: Mtazamo wa jinsi watu wanavyofafanua amani ya ndani na jinsi wanavyojitahidi kuipata; angalia pia vizuizi vinavyotuzuia kupata amani ya ndani.
- Na Dr. Bilal Philips (transcribed from an audio lecture by Aboo Uthmaan)
- Iliyochapishwa mnamo 03 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 08 Jan 2024
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 5,692 (wastani wa kila siku: 5)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mada ya utulivu au amani ya ndani hushugulikia hitaji la kilimwengu. Hakuna mtu katika ulimwengu ambaye hatamani amani ya ndani ama ukipenda utulivu wa ndani wa nafsi. Sio tamaa ambayo ni mpya kwa wakati wetu bali ni jambo ambalo kila mtu amekuwa akitafuta kwa miaka bila kujali rangi, imani, dini, rangi, utaifa, umri, jinsia, utajiri, uwezo au maendeleo ya kiteknolojia.
Watu wamefuata njia tofauti tofauti katika jitihada za kupata utulivu au amani ya ndani, wengnine kupitia kukusanya mali na utajiri, wengine kupitia dawa za kulevya; wengine kupitia muziki, wengine kupitia tafakuri za kimawazo; wengine kupitia waume na wake zao, wengine kupitia kazi zao na wengine kupitia mafanikio ya watoto wao. Na mengineyo mengi.
Bado utafiti unaendelea. Katika wakati wetu tumeongozwa kuamini kwamba ubunifu na maendeleo ya kiteknolojia na kisasa vitatuletea raha, na kupitia hizi tutapata amani ya ndani.
Isitoshe, ikiwa tungechukuwa taifa lenye maendeleo zaidi ya kiteknolojia na viwanda vya kisasa ulimwenguni kama Marekani basi tungegundua kwamba kile ambacho tumeongozwa kuamini sio ukweli. Takwimu zinaonyesha kuwa huko Amerika idadi ya watu milioni 20 wanakabiliwa na unyogovu; na unyogovu ni nini isipokuwa ukosefu wa utulivu na amani ya ndani? Isitoshe, katika mwaka 2000 idadi ya vifo vilivyotokana na mauaji ya kibinafsi viliongezeka maradufu ya kiwango cha wale waliokufa kutokana na Ukimwi. Walakini, vyombo vya habari kwa kawaida yao, tunasikia habari zaidi kuhusu waliokufa kwa Ukimwi kuliko wale wanaokufa kwa kujiua. Watu wengi hufa kutokana na kujiua huko Amerika kuliko kwa mauaji, na viwango vya mauaji wenyewe ni kubwa.
Kwa hivyo ukweli ni kwamba maendeleo ya kiteknolojia na kisasa haijatuletea amani ya ndani na utulivu. Bali, licha ya faraja ambayo kisasa imetuletea, tuko mbali zaidi na amani ya ndani na utulivu wa nafsi kuliko vile babu zetu walikuwa.
Amani ya ndani ni sehemu kubwa ya maisha yetu ambayo hatuwezi ona wala kuihisi na mikono yetu.
Wengi wetu hukosea kulinganisha raha za kibinafsi kwa amani ya ndani kwa ndani; tunapata vitu vya raha kutoka kwa vitu kadhaa iwe ni utajiri, mahusiano ya kimapenzi au mengineyo mengi. Lakini hizi hazidumu, zinakuja na kwenda. Ndio tuna raha za kibinafsi mara kwa mara na tunafurahishwa na vitu mingi mara kwa mara, lakini hii sio amani ya ndani. Amani ya ndani ya kweli ni hali ya utulivu na kuridhika ambayo hutupitisha katika majaribiyo na shida zote za maisha.
Tunapaswa kuelewa kuwa amani sio kitu ambacho kitakuwepo katika ulimwengu huu kwa sababu tunapofafanua amani kulingana na kamusi inasema kwamba amani ni uhuru kutoka kwa vita au mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Je! Hii ina wapi? Daima kuna vita au aina fulani ya machafuko ya wenyewe kwa wenyewe yanayotokea mahali fulani ulimwenguni. Tunapoangalia amani kulingana na kiwango cha serikali basi amani ni uhuru kutoka kwa machafuko ya umma na usalama, lakini wapi ulimwenguni tunayo hii kamili? Tukiangalia amani katika kiwango cha kijamii, familia na kazi basi amani ni uhuru kutoka kwa kutoafikiana na malumbano, lakini je! Kuna mazingira ya kijamii ambayo kamwe hayana kutoafikiana au malumbano? Kulingana na eneo basi ndio, tunaweza kuwa na mahali penye utulivu na amani, kwa mfano amani na utulivu katika baadhi ya visiwa , lakini amani hii ipo kwa muda kidogo tu, baadaye dhoruba au kimbunga kitakuja.
Mungu anasema:
"Hakika, nimemuumba mja katika taabu (mapambano)." (Kurani 90: 4)
Hii ndio hali ya maisha yetu tuko katika taabu na mapambano, nyakati za shida na nyakati za raha.
Ni maisha yaliyojaa majaribio kama vile Mungu anasema:
"Na hakika, tutakujaribu kwa mtihani ya hofu, njaa, upungufu wa mali, maisha na matunda, lakini tumpelekee habari njema As-Saabirin (wanaosubiri)" (Kurani 2: 155)
Ili kukabiliana na hali zetu, hali ya shida na mapambano ambayo tunayopitia, uvumilivu na subira ndio ufunguo.
Lakini ikiwa tutarudi kwa amani ya ndani ambayo tunatafuta, basi uvumilivu hauwezi kujidhihirisha ikiwa hatuna amani ya ndani.
Tunaishi katika ulimwengu wa shida na mapambano lakini bado ndani yetu tunaweza kupata amani ya ndani, amani na mazingira na ulimwengu tunamoishi.
Ni wazi kwamba kuna vizuizi vingine ambavyo vinatuzuia kupata amani. Kwa hivyo kwanza tunapaswa kutambua vizuizi katika maisha yetu ambavyo vinatuzuia kufikia amani ya ndani na kutafuta namna kuziondoa. Vizuizi havitaondolewa kwa kufikiria tu kwamba tunahitaji kuviondoa tunapaswa kuchukuwa hatua kadhaa kufikia hili. Kwa hivyo tunawezaje kuondoa vizuizi hivi ili tuweze kufikia kile kinachotuwezesha tupate amani ya ndani?
Hatua ya kwanza ni kujua tatizo lenyewe na tuwe maakini nayo kwani tusipoijua hatutaweza kuyaondoa.
Hatua ya pili ni kukubali vizuizi ndani yetu. Kwa mfano hasira ni moja ya kizuizi kikubwa kwa amani ya ndani ikiwa mtu ana hasira, anawezaje kuwa na amani ya ndani katika hali hiyo? Haiwezekani. Kwa hivyo mtu huyo anahitaji kutambua kuwa hasira ni kikwazo kwa ukosefu amani ya ndani.
Ikiwa mtu anasema kwamba "Ndio, ni kizuizi lakini sikasiriki", basi mtu kama huyo ana shida. Hajakubali kikwazo hicho kama shida na yuko katika hali ya kujikana mwenyewe. Kwa hivyo hawezi kuiondoa.
Tukiangalia vizuizi maishani tunaweza kuvipanga katika mada au maudhui anuwai: shida za kibinafsi, maswala ya kifamilia, shida za kifedha, shinikizo la kazi na mchanganyiko wa kiroho. Na kuna maswala mengi chini ya mada hizi.
Ongeza maoni