Sue Watson, Profesa, Mchungaji, Mpanda Kanisa na Mmisionari, Sasa yuko Saudi Arabia
Maelezo: Mwanafunzi wa miaka minane wa masomo rasmi ya theolojia anakubali Uislamu kutokana na uthabiti wa ujumbe wake.
- Na Sue Watson
- Iliyochapishwa mnamo 17 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 2,373 (wastani wa kila siku: 2)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
“Ni nini kimekutokea?” Hili lilikuwa swali la kwanza nililokumbana nalo na wanafunzi wa zamani, marafiki, na wachungaji wenzangu waliponiona baada ya kuukubali Uislamu. Nadhani nisingeweza kuwalaumu, sikuwa mtu mwenye kufikiriwa wa kuweza kubadili dini. Hapo awali, nilikuwa profesa, mchungaji, mpanda kanisa na mmishonari. Iwapo kuna mtu aliyekuwa na msimamo mkali basi ni mimi.
Nilikuwa nimehitimu tu Shahada ya Uzamili ya kidini kutoka katika seminari miezi mitano kabla. Ilikuwa baada ya wakati huo nilikutana na mwanamke ambaye alikuwa amefanya kazi Saudi Arabia na alikuwa amesilimu. Bila shaka, nilimuuliza kuhusu wanavyotendewa wanawake katika Uislamu. Nilishtushwa na jibu lake, haikuwa vile nilivyotarajia, hivyo niliendelea kuuliza maswali mengine yanayohusiana na Mungu na Muhammad [rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake]. Alinifahamisha kwamba angenipeleka kwenye Kituo cha Kiislamu ambapo wangeweza kujibu maswali yangu vizuri zaidi.
Kuombewa, kunamaanisha kumwomba Yesu ulinzi dhidi ya roho za mashetani, kwa kuona kwamba yale tuliyofundishwa kuhusu Uislamu ni dini ya Mashetani na ya Kishetani. Baada ya kufundisha Uinjilisti, nilishtushwa sana na mtazamo wao, ulikuwa thabiti na wa moja kwa moja. Hakuna vitisho, hakuna unyanyasaji, hakuna udanganyifu wa kisaikolojia, hakuna ushawishi ! Hakuna lolote kati ya haya, "Hebu na tuwe na somo la Quran nyumbani kwako," ni kama somo la Biblia. Sikuweza kuamini! Walinipa vitabu na kuniambia ikiwa nina maswali fulani wangeweza kuyajibu ofisini. Usiku huo nilisoma vitabu vyote walivyotoa. Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kusoma kitabu kuhusu Uislamu kilichoandikwa na Muislamu, tulijifunza na kusoma vitabu vinavyohusu Uislamu vilivyoandikwa na Wakristo pekee. Siku iliyofuata nilitumia saa tatu ofisini nikiuliza maswali. Hii iliendelea kila siku kwa wiki, wakati huo nilikuwa nimesoma vitabu kumi na mbili na nilijua kwa nini Waislamu ni watu wagumu zaidi ulimwenguni kubadilika kwenda kwenye Ukristo. Kwa nini? Maana hakuna cha kuwapa!! (Katika Uislamu) Kuna uhusiano na Mungu, msamaha wa dhambi, wokovu, na ahadi ya Uzima wa Milele.
Kwa kawaida, swali langu la kwanza lilijikita katika uungu wa Mungu. Ni Mungu yupi huyu ambaye Waislamu wanamwabudu? Tulikuwa tumefundishwa kama Wakristo kwamba huyu ni mungu mwingine, mungu wa uwongo, wakati, kwa hakika, Yeye ni Mjuzi wa Yote Ajuaye Yote, Muweza wa Yote Mwenye Nguvu Zote, na Mungu Aliye popote - Yule Mmoja na wa Pekee asiye na washirika au wakufanana nae. Inashangaza kuona kwamba kulikuwa na maaskofu katika kipindi cha miaka mia tatu ya kwanza ya Kanisa waliokuwa wakifundisha kama Waislamu wanavyoamini, kwamba Yesu [rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake] alikuwa nabii na mwalimu!! Ilikuwa tu baada ya kuongoka kwa Mtawala Konstantino kwamba yeye ndiye aliita na kuanzisha fundisho la Utatu. Yeye, mwongofu wa Ukristo ambaye hakujua chochote kuhusu dini hii, alianzisha dhana ya kipagani ambayo inarudi nyuma hadi nyakati za Babeli. Nafasi, hata hivyo, hainiruhusu kwenda kwa undani kuhusu somo hili, lakini Mungu akipenda, tutazungumza wakati mwingine. Ila, lazima nionyeshe kwamba neno UTATU halipatikani katika Biblia katika tafsiri zake nyingi wala halipatikani katika lugha asilia za Kigiriki au Kiebrania!
Swali langu lingine la muhimu lilijikita kwa Muhammad [rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake]. Muhammad huyu ni nani? Niligundua kuwa Waislamu hawamuombi kama Wakristo wanavyomuomba Yesu. Yeye si mpatanishi na kwa hakika, ni haramu kumuomba. tunamuombea baraka ziwe juu yake mwishoni mwa maombi yetu lakini ni sawa sawa, tunamuombea baraka Ibrahimu. Yeye ni Nabii na Mtume, Nabii wa mwisho. Kwa hakika, mpaka sasa, miaka elfu moja mia nne na kumi na nane(1,418) baadaye hapajakuwa na nabii baada yake. Ujumbe wake ni kwa Wanadamu Wote, kinyume na ujumbe wa Yesu au Musa (amani iwe juu yao wote wawili) ambao ulitumwa kwa Mayahudi. “Sikilizeni Waislaeli” Lakini ujumbe ni ujumbe uleule wa Mungu. “Bwana Mungu wako ni Mungu Mmoja na usiwe na miungu mingine ila Mimi.” (Marko 12:29)
Kwa sababu sala ilikuwa sehemu muhimu sana ya maisha yangu ya Kikristo nilipendezwa na kutaka kujua nini Waislamu walikuwa wakiomba. Kama Wakristo, tulikuwa wajinga juu ya kipengele hiki cha imani ya Kiislamu kama vile katika vipengele vingine. Tulifikiri na kufundishwa, kwamba Waislamu walikuwa wakiinamia Al-Kaaba (ya Makka), kwamba huyo ndiye alikuwa mungu wao na kitovu cha mungu huyu wa uongo. Tena, nilishtuka kujua kwamba namna ya maombi imeagizwa na Mungu, Mwenyewe. Maneno ya sala ni ya sifa na kuinuliwa. Mtazamo wa swala (udhu au kuosha) katika usafi uko chini ya uongozi wa Mungu. Yeye ni Mungu Mtakatifu na hatutakiwi kumkaribia kiholela, bali ni jambo la busara atuambie jinsi tunavyopaswa kumkaribia.
Mwishoni mwa juma hilo baada ya kutumia miaka minane (8) ya masomo rasmi ya theolojia, nilijua kiufahamu (maarifa ya kichwa) kwamba Uislamu ulikuwa wa kweli. Lakini sikuukubali Uislamu wakati huo kwa sababu sikuuamini moyoni mwangu. Niliendelea kusali, kusoma Biblia, kuhudhuria mihadhara katika Kituo cha Kiislamu. Nilikuwa nikiuliza kwa bidii na kutafuta mwongozo wa Mungu. Si rahisi kubadili dini yako. Sikutaka kupoteza wokovu wangu kama kungekuwa na wokovu wa kupoteza. Niliendelea kushtuka na kustaajabishwa na nilichokuwa najifunza kwa sababu si kile nilichofundishwa ambacho Uislamu unaamini. Katika kiwango changu cha Uwalimu, profesa niliyekuwa naye aliheshimiwa kama mamlaka juu ya Uislamu lakini mafundisho yake ya Ukristo, kwa ujumla, yamejaa Kutokueleweka. Yeye na Wakristo wengi kama yeye ni waaminifu lakini wamekosea kwa dhati.
Miezi miwili baadaye baada ya kusali kwa mara nyingine tena nikitafuta mwongozo wa Mungu, nilihisi kitu kinaanguka ndani ya nafsi yangu! Niliketi, na ilikuwa mara ya kwanza nilipaswa kutumia jina la Mungu, na nikasema, “Mungu, ninaamini wewe ni Mungu Mmoja na wa Pekee wa Kweli.” Kulikuwa na amani iliyonishukia na tangu siku hiyo miaka minne iliyopita hadi sasa sijajuta kamwe kuukubali Uislamu. Uamuzi huu haukuja bila khasia. Nilifukuzwa kazi nilipokuwa nikifundisha katika Vyuo viwili vya Biblia wakati huo, nikitengwa na wanafunzi wenzangu wa zamani, maprofesa, na wachungaji wenzangu, kukataliwa na familia ya mume wangu, nilieleweka vibaya na watoto wangu wakubwa na kutiliwa shaka na serikali yangu. . Bila imani inayomwezesha mwanadamu kusimama dhidi ya nguvu za Shetani, nisingeweza kustahimili haya yote. Ninamshukuru sana Mungu kwamba mimi ni Muislamu na naomba niishi na kufa nikiwa Muislamu.
“Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote. Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu.” (Kurani 6:162-163)
Dada Khadijah Watson kwa sasa anafanya kazi kama mwalimu wa wanawake katika moja ya Vituo vya Da’wah (Mwaliko kwenda kwenye Uislamu) huko Jeddah, Saudi Arabia.
Ongeza maoni