Angel, Mkristo wa Zamani, Marekani
Maelezo: Kutoka kwa familia na jamii iliyovunjika, mwanamke mmoja anapata msaada kutoka kwa marafiki wengine wa Kiislamu.
- Na Angel (Edited by IslamReligion.com)
- Iliyochapishwa mnamo 17 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 2,021 (wastani wa kila siku: 2)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Kila Muislamu ana hadithi kuhusu safari yake ya kuelekea Uislamu. Kila moja kati ya hadithi hizi ni ya kuvutia na yenye hekima kwangu. Hakika Mwenyezi Mungu humwongoza amtakaye, na amtakaye tu. Najisikia nimebarikiwa sana kwa kuwa mmoja wa walioteuliwa. Hii hapa hadithi yangu.
Daima niliamini kuna Mungu mmoja. Maisha yangu yote, wakati wa shida, nilimwomba Mungu anisaidie hata nilipokuwa mtoto. Nakumbuka nikilia nikiwa kwa magoti yangu jikoni, nikipiga kelele na kulia. Nilikuwa nikimwomba Mungu asimamishe maumivu yangu. Dini kwa upande mwingine kamwe haikuwa na mantiki kwangu. Nilivyokua ndivyo nilivyoiona kitu kisichoelweka kwangu. Watu wanadhani wao ndio wapatanishi kati yako na Mungu.
Nilihisi vile vile kuhusu Yesu, [rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake]. Inakuwaje mtu huyu atatuokoa sote kutoka kwa madhambi zetu? Kwa nini tuna haki ya kutenda dhambi kwa sababu yake tu? Niliikataa Biblia katika matoleo yake yote, nikiamini kitu kilichotafsiriwa na kuandikwa upya mara nyingi hakiweza kuwa maneno halisi ya Mungu. Nilipokuwa na umri wa miaka kumi na mitano, nilikata tamaa na wazo la kumpata Mungu.
Nilipokuwa nikikua, familia yangu ilikuwa familia ya wastani ya Kimarekani. Kila mtu niliyemjua alikuwa na matatizo yaliyofanana. Baba yangu alikuwa mfanyakazi wa mkono mwenye bidii na mraibu wa pombe. Kadiri muda ulivyoendelea ndivyo hali yake ilivyokuwa mbaya zaidi, na hivyo upotovu wake ulizidi. Unyanyasaji wa kijinsia, unyanyasaji wa kimwili, na hofu ziliweka alama juu ya utoto wangu ambao ungedhihirika maisha yangu yote. Alifariki nilipokuwa katika darasa la sita. Wazazi wangu walikuwa wameachana wakati huo. Nilikuwa mtoto mdogo zaidi kati ya watoto wanane. Mama yangu angeenda kufanya kazi ili kukimu mahitaji yetu, na nilikuwa nyumbani peke yangu mara nyingi.
Nilikuwa mmoja wa watoto hao ambao hujiondoa kutoka kwa jamii, ambao wanawaogofya watu wanapoingia chumbani. Nilianza kuvaa nguo nyeusi na mapambo nyeusi. Nilisikiliza muziki wa zamani na kuwaza kuhusu kifo. Kifo hakikuonekana kwangu kama jambo la kuogofya bali kama suluhisho la tatizo hili lililoendelea kuzidi. Nilihisi upweke wakati wote, hata nikiwa karibu na marafiki. Nilijaribu kujaza pengo hilo na sigara, kisha pombe, ngono, madawa ya kulevya na kisha chochote ambacho kingenitoa kutoka kwa mawazo yangu mwenyewe. Nilijaribu kujiua mara kumi na tano. Maumivu haya ndani yangu kamwe hayakupungua licha ya kila kitu nilichokijaribu.
Nilikuwa katika chuo kikuu nilipobeba mimba ya mwanangu, niliogopa juu ya afya ya mtoto wangu na sikuweza kumpeana. Nilifanya kazi bila kusita ili kukita mahitaji yake. Nilikusanya maumivu yote na hasira ndani ya moyo wangu, na kubadilisha maisha yangu kwa kiwango fulani. Kwa wakati huu, sikumwamini mtu yeyote. Miaka mitatu baadaye, nilianza kuona wanaume tena. Nilipatana na mwanaume mmoja. Kusema kweli nilitaka maisha bora zaidi. Kama ilivyokuwa uzoefu wangu wa zamani, ulimwengu wangu ulikuja kuanguka. Nilikuwa na umri wa miaka 25 na nilikuwa mjamzito na binti yangu na kumaliza uhusiano na mchumba wangu baada ya yeye kunidanganya mara nyingi na kunipiga na kunidhuru kimwili. Sikujua cha kufanya baada ya hapo.
Wakati huo nilikuwa nikimfanyia kazi mwanaume mmoja wa Mpakistani ambaye alikuwa Muislamu. Sikuangalia vyombo vya habari kamwe au hata kujali kinachoendelea. Kuwa Muislamu kwangu hakukuwa tofauti na dini nyingine yoyote. Baada ya muda nilijuana na marafiki kadhaa Waislamu. Nilianza kutambua kitu tofauti sana. Walikuwa na maadili haya yasiyokuwa na ugeugeu. Walikuwa watiifu kwa Mungu hadi walisali mara tano kila siku. Usizungumzie hata ukweli kwamba hawakulewa au kutumia madawa ya kulevya. Kwa kizazi changu haya yalikuwa maadili ya watu wa zamani, labda kama ya babu zako.
Binti yangu alipozaliwa, huwezi kuamini mshangao wangu wakati mmoja wa wanaume hawa aliniletea zawadi. Nilishtushwa kipumbavu. Alimshika na kuzungumza naye. Sijawahi kuona wanaume waliowafanyia hivyo watoto wachanga. Wema uliongezeka tu kwa miezi minne iliofuata. Siwezi kueleza upendo ambao tulionyeshwa. Polepole nilianza kudadisi zaidi dini yao. Nilikuwa na hamu ya kujua ni aina gani ya dini inaweza kuleta maadili kama hizi kwa watu.
Nilikuwa nikiishi nyumba na watu saba nilipoamua usiku mmoja kumwomba mwenzangu niliyeishi naye tarakilishi yake. Niliogopa sana kuwaudhi marafiki zangu kwa kuwauliza maswali, kwa hivyo nikageuka kwenye mtandao. Tovuti ya kwanza niliyoifungua ilikuwa http://www.islam-brief-guide.org. Nilistaajabishwa sana. Ilikuwa ni kama nguo nyeusi imeinuliwa kutoka mwili wangu, na nawaapieni kwamba sijawahi kuhisi kuwa karibu sana na Mungu kabla ya hapo. Kwa ndani ya saa ishirini na nne, nilitoa Shahadah yangu.
Hadi leo muda wangu mwingi hutumika kwa utafiti. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu kuna kitu kilikuwa kimesimamisha hasira, na maumivu. Kwa kweli nilihisi upendo na uchaji Mungu. Mungu alikuwa amebadilisha maumivu ndani yangu na nuru yake, na imani. Tangu uongofu wangu, Mungu amenibariki kweli. Mungu alinipa nguvu ya kuwacha sigara, na pombe, na sijatumia madawa ya kulevya kwa takriban miaka miwili sasa. Nimeolewa na Muislamu wa ajabu sana. Amewachukua watoto wangu na kuwafanya kuwa wetu. Nina kitu ambacho nilikitaka daima - familia, [wa kutukuzwa ni Mwenyezi Mungu].
Ongeza maoni