Maswali Makuu (sehemu 2 ya sehemu 3): Lengo la Maisha
Maelezo: Majibu ya kiislamu kwa swali la pili kati ya baadhi ya 'Maswali makuu' ambayo wanadamu hujiuliza, Mbona Tuko Hapa?
- Na Laurence B. Brown, MD
- Iliyochapishwa mnamo 24 Jan 2022
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 2
- Imetazamwa: 6,458 (wastani wa kila siku: 6)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
SSwali la kwanza kati ya maswali mawili makuu katika maisha ni, “Ni nani aliyetuumba?” Tulizungumzia swali hilo katika makala iliyotangulia na (ninatumai) tulikubaliana kuwa jibu ni “Mungu”. Kwa kuwa sisi ni viumbe, Mungu ndiye Muumba.
Sasa, hebu tugeuke kwa “swali kuu” la pili, ambalo ni, “Kwa nini tuko hapa?”
Naam, kwa nini tuko hapa? Ili tukusanye umaarufu na mali? Kucheza muziki na kuzaa watoto? Kuwa mwanaume au mwanamke aliye tajiri kabisa makaburini, kama tunavyoambiwa kwa utani, “Anayekufa na vinyago vingi zaidi ndiye mshindi?”
Hapana, lazima kuwe na mengi zaidi kwa maisha kuliko hayo, basi hebu fikiria kuhusu hili. Kwanza, angalia vilivyo karibu nawe. Kama wewe huishi pangoni, unazungukwa na mambo ambayo sisi binadamu tuliyatengeneza kwa mikono yetu wenyewe. Sasa, kwa nini tumevitengeneza vitu hivyo? Jibu, bila shaka, ni kwamba tunatengeneza vitu ili vitufanyie kazi fulani maalum. Kwa kifupi, tunatengeneza vitu ili vitutumikie. Hivyo, kwa nini Mungu alituumba, ikiwa sio kumtumikia?
Ikiwa tunamkubali Muumba wetu, na kwamba aliwaumba wanadamu ili wamtumikie, swali linalofuata ni, “Vipi? Tunawezaje kumuabudu Yeye? Bila shaka, swali hili linaweza jibiwa vizuri na yule aliyetuumba. Kama Yeye alituumba tumtumikie, basi anatarajia tufanye kazi kwa namna fulani, ikiwa tutafikia malengo yetu. Lakini tunawezaje kujua namna hiyo ni gani? Tunawezaje kujua kipi Mungu anatarajia kutoka kwetu?
Fikiria hili: Mungu alitupa nuru, ambayo tunaweza kupata njia yetu kupitia kwayo. Hata wakati wa usiku, tuna mwezi unaotoa nuru na nyota za kuongoza watu. Mungu aliwapa wanyama wengine mifumo ya kuongoza yanayofaa kwa mahitaji yao. Ndege zinazohama hama zinaweza kusafiri, hata siku zenye mawingu, zikitumia mbinu ya kuangalia jinsi mwanga unavyogawanyika unapopita kwa mawingu. Nyangumi huhamia kwa “kusoma” viwanja vya sumaku vya Ardhi. Salmoni hurudi kutoka maji makuu ya bahari ili kuzaa katika mahali walipozaliwa wao kwa kutumia harufu. Samaki huhisi harakati za mbali kwa njia ya vipokezi vya shinikizo kwenye miili yao. Popo na pomboo vipofu wa mtoni “huona” kwa kutumia mwangwi. Viumbe fulani vya baharini (kwa mfano Mkunga wa umeme) huzalisha na “kusoma” viwanja vya sumaku, na kuwaruhusu “kuona” katika maji ya matope, au katika weusi wa kina cha bahari. Vidudu vinawasiliana na kemikali. Mimea huhisi jua na kukua kuielekea (phototrophism); mizizi yao huhisi nguvu za mvutano na kukua chini ardhini (geotrophism). Kwa kifupi, Mwenyezi Mungu amewapa uwongofu viumbe vyote katika uumbaji wake. Je, tunaweza kuamini kuwa hangetupa mwongozo wa kipengele kimoja muhimu zaidi cha kuwepo kwetu, yaani raison d'etre—sababu yetu ya kuishi duniani? Kwamba hangetupatia zana za wokovu wetu?
Na mwongozo huu haungekuwa . . . Ufunuo?
Fikiria kwa njia hii: Kila bidhaa ina maelezo na sheria. Kwa bidhaa tata zaidi, ambazo sheria zake hatuelewi, tunategemea miongozo ya mmiliki. Miongozo hii imeandikwa na yule anayejua vizuri bidhaa hizi, ambaye ni mtengenezaji. Mwongozo wa mmiliki kwa kawaida huanza na onyo kuhusu matumizi yasiyofaa ya bidhaa na madhara yake, hatua kuhusu maelezo ya jinsi ya kuitumia bidhaa hiyo vizuri na faida zinazopatikana hapo, na hutoa maelezo zaidi ya bidhaa na mwongozo wa utatuzi wa shida ambapo tunaweza kurekebisha kasoro za bidhaa hiyo.
Sasa, jinsi gani hiyo inatofautiana na ufunuo?
Ufunuo unatuambia nini cha kufanya, kile ambacho si cha kufanya na kwa nini, kinatuambia kile Mungu anatarajia kwetu, na kutuonyesha jinsi ya kusahihisha mapungufu yetu. Ufunuo ni mwongozo wa mmiliki usio na kifani, unaotolewa kama mwongozo kwa yule atakayetumia, yaani sisi wenyewe.
Katika ulimwengu wetu, bidhaa ambazo zinakidhi au kuzidi maelezo yake zinachukuliwa kuwa nzuri, huku zingine... hmm... hebu fikiria kuhusu hili. Bidhaa yoyote ambayo inashindwa kufikia maelezo ya kiwanda aidha hutengenezwa, ikiwa inawezekana, au hurejeshwa. Kwa maneno mengine, huharibiwa. Ghafla mjadala huu unageuka kuwa wa kutisha sana. Kwa sababu katika mjadala huu, sisi ndio bidhaa-bidhaa ya uumbaji.
Lakini hebu tusite kwa muda na kufikiria jinsi tunavyohusiana na vitu mbalimbali vinavyojaza maisha yetu. Vikifanya kile tunachotaka, tunafurahi. Lakini vinaposhindwa, tunavitupa. Vingine vinarudi kwenye duka, vingine hupeanwa kama sadaka, lakini hatimaye vyote vinaishia kwenye takataka, na baadaye... huzikwa au kuchomwa. Vile vile, mfanyakazi asiye na ufanisi hufutwa kazi, au kwa kiingereza, 'fired' (maana yake ni kuchomwa). Sasa, simama kwa dakika na ufikirie kuhusu hilo. Je, neno hilo la kitasfida lilitoka wapi? Hmm... mtu anayeamini masomo ya maisha haya hutokana na masomo ya kidini anaweza kufurahia sana hilo.
Lakini hiyo haimaanishi mifano kama hii haifai. Bali, kinyume na hayo, tunapaswa kukumbuka kwamba maagano ya Kale na Jipya yamejaa vielelezo, na Yesu Kristo alifundisha kutumia mifano.
Hivyo labda itakuwa bora tukiyatilia haya maanani.
Hapana, ninafaa kusahihishwa. Ni lazima tutilie haya maanani. Hakuna mtu aliyewahi kufikiri kuwa tofauti kati ya furaha ya mbinguni na mateso ya motoni ni jambo la utani.
Hatimiliki © 2007 Dkt. Laurence B. Brown; imetumika kwa idhini.
Dkt Brown ni mwandishi wa The Eighth Scroll, kilichoelezwa na Seneta wa Jimbo la Carolina Kaskazini Larry Shaw kama, “Indiana Jones inakutana na The Da Vinci Code. The Eighth Scroll ni kitabu kinachokufanya ushike pumzi, kisichoweza kuwekwa chini baada ya kuanza, kinachopinga maoni ya Kimagharibi kuhusu ubinadamu, historia na dini. Hakina mfano, na ndicho kitabu bora katika kategoria chake!” Dr. Brown pia ni mwandishi wa vitabu vitatu vya kielimu vya ulinganisho wa kidini , Misgod'ed, God'ed, na Bearing True Witness (Dar-us-Salam). Vitabu na makala yake yanaweza kupatikana kwenye tovuti yake, www.EighthScroll.com and www.LevelTruth.com, na yanaweza kununuliwa hapa www.Amazon.com.
Ongeza maoni