Rehema ya Mungu (sehemu ya 1 kati ya 3): Mungu mwingi wa Rehema, Mgawaji wa Rehema.
Maelezo: Ufafanuzi wa vitendo wa majina mawili ya Mwenyezi Mungu yanayorudiwa mara kwa mara: ar-Rahman na ar-Raheem, na asili ya Rehema yote ya Mwenyezi Mungu.
- Na Imam Mufti
- Iliyochapishwa mnamo 03 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 03 Jan 2022
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 7,355 (wastani wa kila siku: 7)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Ikiwa mtu angeuliza, ‘Ni nani Mungu wako?’ Jibu la Muislamu lingekuwa, ‘Mwingi wa Rehema, Mgawaji wa Rehema.’ Kulingana na vyanzo vya Kiislamu, manabii, huku wakikazia hukumu ya Mungu, pia walitangaza rehema Yake. Katika maandiko ya Kiislamu, Mwenyezi Mungu anajitambulisha kama:
“Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mwenye kuyajua yaliyo fichikana na yanayo onekana. Yeye ndiye Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.” (Kurani 59:22).
Katika msamiati wa Kiislamu ar-Rahman na ar-Raheem ni majina binafsi ya Mungu Aliye Hai. Yote yamechukuliwa kutoka kwa nomino rahmah, ambayo inaashiria "rehema", "huruma", na "huruma ya upendo". Ar-Rahman inaelezea asili ya Mwenyezi Mungu ya kuwa Mwenye kurehemu, wakati ar-Raheem inaelezea matendo Yake ya rehema yaliyotolewa kwa viumbe Vyake, utofauti iliofichika, lakini ambao unaonesha rehema zake zote.
"Sema, ‘Mwombeni Allah (Mwenyezi Mungu), au mwombeni (Rahman) Mwingi wa Rehema, kwa jina lolote mnalo mwita – Kwani Yeye ana majina mazuri....’" (Kurani 17:110)
Majina haya mawili ni baadhi ya Majina ya Mwenyezi Mungu yanayotumika sana katika Quran: ar-Rahman imetumika mara hamsini na saba, wakati ar-Raheem imetumika mara mbili zaidi (mia na kumi na nne).[1] Moja huwasilisha hisia kubwa ya ukarimu na upendo, Mtume alisema:
"Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkarimu, na anapenda ukarimu. hutoa kwa upole asiyetoa kwa ukali." (Saheeh Muslim)
Zote pia ni sifa za kimungu zinazoashiria uhusiano wa Mungu na uumbaji.
"Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote; Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu." (Kurani 1:2-3)
Katika sala ambayo Waislamu huisoma angalau mara kumi na saba kwa siku, huanza kwa kusema:
"Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu. Sifa njema zote ni za Mwenyeezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote; Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu.." (Kurani 1:1-3)
Maneno haya yenye nguvu yanaibua jibu la Mungu:
"Mja anaposema: ‘Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote’ Mimi (Mwenyezi Mungu) husema: ‘Mja wangu amenisifu.’ Anaposema: ‘Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu.,’ Mimi (Mwenyezi Mungu) husema: ‘Mja wangu amenitukuza.’" (Saheeh Muslim)
Majina haya mara kwa mara yanamkumbusha Muislamu kuhusu rehema ya Mwenyezi Mungu inayomzunguka. Sura zote isipokuwa moja tu za Maandiko ya Kiislamu zinaanza kwa maneno, ‘Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.’ Waislamu huanza kwa Jina la Mungu kuonyesha utegemezi wao wa mwisho juu Yake na kujikumbusha juu ya rehema ya Mungu kila wakati wanapokula, kunywa, kuandika barua, au kufanya jambo lolote la maana. Roho huchanua katika ulimwengu. Dua mwanzoni mwa kila tendo la ki ulimwengu huifanya kuwa la muhimu, ikiita baraka ya Mungu juu ya tendo hilo na kulitakasa. Kanuni hii ni mapambo maarufu katika maandishi na mapambo ya usanifu.
Kutoa rehema kunahitaji mtu ambaye ameonyeshwa rehema. Anayeonyeshwa rehema lazima awe mhitaji. Rehema kamilifu ni kuwajali wale wanaohitaji, ambapo rehema isiyo na kikomo inaenea kwa wale wanaohitaji au wasio na uhitaji, inaenea kutoka kwa ulimwengu huu hadi maisha ya kushangaza baada ya kifo.
Katika mafundisho ya Kiislamu, wanadamu wanafurahia uhusiano binafsi na Mungu Mwenye Upendo, Mwenye Rehema, aliye tayari kusamehe dhambi na kuitikia maombi, lakini Yeye si mwenye huruma wa kibinadamu wa kuhisi huzuni na huruma kwa mtu aliye katika dhiki. Mungu haji kuwa mwanadamu ili kuelewa mateso. Badala yake, rehema ya Mungu ni sifa inayolingana na utakatifu Wake, inaleta usaidizi wa kimungu na upendeleo.
Rehema za Mungu ni nyingi sana:
"Sema: Mola Mlezi wenu ni Mwenye rehema iliyo enea.….’" (Kurani 6:147)
Kuenea kwa uwepo wote:
"…na rehema yangu imeenea kila kitu…." (Kurani 7:156)
Uumbaji wenyewe ni kielelezo cha upendeleo wa kimungu, rehema na upendo. Mungu anatualika kutazama athari za rehema yake karibu nasi:
"Basi ziangalie athari za rehema ya Mwenyezi Mungu, jinsi anavyo ihuisha ardhi baada ya kufa kwake!..." (Kurani 30:50)
Mungu Anawapenda wenye Huruma
Mungu anapenda huruma. Waislamu wanauona Uislamu kuwa ni dini ya rehema. Kwao, Mtume wao ni rehema ya Mwenyezi Mungu kwa watu wote.
"Na hatukukutuma, (ewe Nabii), ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote" (Kurani 21:107)
Kama vile wanavyoamini kuwa Yesu alikuwa rehema ya Mungu kwa watu:
"Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu." (Kurani 19:21)
Mmoja wa mabinti wa Mtume Muhammad rehma na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alimpelekea habari za mtoto wake aliyekuwa mgonjwa. Akamkumbusha kuwa Mwenyezi Mungu ndiye anaye toa, ndiye anaye twaa, na kila mtu ana muda maalumu. Akamkumbusha kuwa mvumilivu. Habari za kifo cha mwanawe zilipomfikia, machozi ya huruma yalitiririka machoni pake. Wenzake walishangaa. Mtume wa Rehema alisema:
"Hii ni huruma Mungu ameiweka ndani ya mioyo ya waja wake. Katika waja wake wote, Mungu huwahurumia tu wenye huruma." (Saheeh Al-Bukhari)
Wamebarikiwa wenye kurehemu, kwani watahurumiwa, kama Mtume Muhammad alivyosema:
"Mungu hatamrehemu mtu asiye na huruma kwa watu." (Saheeh Al-Bukhari)
Pia alisema:
"Mwingi wa rehema huwaonea huruma wenye kurehemu. Warehemu waliomo ardhini, na Yeye aliye juu ya mbingu atakurehemu." (At-Tirmidhi)
Rejeleo la maelezo:
[1] Badala yake, ‘Mwenye Rehema’ halionekani kuwa jina la kimungu katika Biblia. (Kitabu cha kiyahudi, ‘Majina ya Mungu,’ uk. 163)
Ongeza maoni