Monotheazimu – Mungu Mmoja

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Monotheazimu katika Uislam ni nini?

  • Na Aisha Stacey (© 2009 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 03 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 2,575 (wastani wa kila siku: 2)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Monotheism__One_God_001.jpgDini ya Uislamu inategemea Msingi wa imani moja, kwamba hakuna mungu ila Mungu. Wakati mtu anakubali Uisilamu au Muislamu anataka kuhuisha au kuthibitisha imani yake, wanakiri imani hiyo kuwa hakuna mungu ila Mungu na kwamba Muhammad ndiye mjumbe wake wa mwisho. Ashadu a la ill laha il Allah wa Ashadu anna Muhammadan Rasulullah, Akisema maneno haya, ushuhuda wa imani, ndio nguzo ya kwanza kati ya tano au misingi ya dini ya Uislamu. Kuamini Mungu ndio nguzo ya kwanza kati ya nguzo sita za imani.[1]

Waislamu wanaamini kuwa kuna Mungu Mmoja tu. Yeye peke yake ndiye wakutegemewa na Muumba wa ulimwengu. Yeye hana washirika, watoto, au jamaa. Yeye ndiye Mwingi wa Rehema, Mwenye Hikima Zaidi na Mwadilifu. Yeye ndiye msikiaji yote, mwonaji yote, na anayejua yote. Yeye ndiye wa kwanza, ndiye wa mwisho.

“Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. Allah-us-Samad ( Mwenyezi Mungu Mkusudiwa (kwa haja zote), Hakuzaa wala hakuzaliwa; Wala hana anaye fanana naye hata mmoja. ” (Kurani 112)

“Yeye ndiye Muumbaji wa mbingu na ardhi bila ya ruwaza. Itakuwaje awe na mwana naye hakuwa na mke? Naye ndiye aliye umba kila kitu. Naye ni Mwenye kujua kila kitu. La ilaha illa Huwa (hakuna aliye na haki ya kuabudiwa isipokuwa Yeye), Huyo ndiye Allah, Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu, hapana mungu ila Yeye, Muumba wa kila kitu. Basi muabuduni Yeye tu. Naye ni Mtegemewa wa kila kitu. Macho hayamfikilii bali Yeye anayafikilia macho. Naye ni Mjuzi, Mwenye khabari. ” (Kurani 6:101-103)

Imani hii wakati mwingine huitwa Monotheazimu ambayo hutokana na maneno ya Kiyunani 'monos' maana yake tu na 'theos' maana yake mungu. Ni neno jipya katika lugha ya Kiingereza na limetumika kuashiria Mungu aliye mkuu ma mwenye nguvu, Ndiye anayewajibika kwa maisha, yule anayelipa au kuadhibu. Monotheazimu moja kwa moja inapingana na Ushirikina, ambayo inahusu imani ya mungu zaidi ya mmoja, na kwa Ukafiri, kutokuamini miungu yote.

kama tutazingatia maana ya jumla ya neno 'Monotheazimu ' Uyahudi, Ukristo, Uislamu na Uzoroastrianism, na baadhi ya falsafa za Kihindu zinaweza kujumuishwa. Ila, ni kawaida zaidi kutaja Uyahudi, Ukristo, na Uislamu kama dini tatu za Monotheazimu na kuziweka pamoja; hata hivyo, kuna tofauti dhahiri kati ya Ukristo na Uislamu.

Dhana ya utatu inayopatikana katika madhehebu mengi ya Kikristo inajumuisha mambo ya uwingi. Imani ya kuwa Mungu mmoja kihali flani kuna miungu mitatu (baba, mwana, na roho mtakatifu) inapingana na dhana ya Monotheazimu iliyorithiwa katika Uislamu, ambapo Umoja wa Mungu hauna shaka. Baadhi ya vikundi vya Kikristo, pamoja na wale wanaojulikana kama Washirika wanaamini kuwa Mungu ni Mmoja na hawezi kuwa Mungu na mwanadamu kwa wakati mmoja. Wanachukulia maneno ya Yesu katika Yohana 17: 3, "Mungu Mmoja wa Kweli" . Ila, Wakristo wengi hawaungani na imani hii.

Katika dini ya Uislamu imani ya Mungu Mmoja, bila washirika au washirika ni muhimu. Ni kitovu cha dini na ndio kiini cha Kurani. Kurani inawataka wanadamu kumwabudu Mungu peke yake na kuacha kuabudu miungu ya uwongo au washirika. Kurani inatuhimiza tuangalie maajabu ya uumbaji na kuelewa ukuu na nguvu za Mungu, na inazungumza moja kwa moja juu ya majina, sifa, na matendo Yake. Kurani inatuamuru kukataa chochote kinachoabudiwa badala ya, au pamoja na Mungu.

“Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.” (Kurani 51:56)

Uislamu mara nyingi hujulikana kama Monotheazimu halisi. Haija changanywa na dhana za ajabu au ushirikina. Imani ya Mungu Mmoja inahusu uhakika. Waislamu humwabudu Mungu peke yake, hana washirika, jamaa, au wasaidizi. Ibada inaelekezwa kwa Mungu tu, kwa kuwa Yeye ndiye pekee anayestahili kuabudiwa. Hakuna kitu kikubwa kuliko Mungu Peke Yake.

“Sema: Alhamdu Lillahi! Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu! Na amani ishuke juu ya waja wake alio wateuwa. Je! Mwenyezi Mungu ni bora, au wale wanao washirikisha naye?"(Hakika,Mungu ni Mbora)

Siyo Yeye (bora zaidi ya miungu yenu) yule aliye ziumba mbingu na ardhi, na akakuteremshieni maji kutoka mbinguni, na kwa hayo tukaziotesha bustani zenye kupendeza? Nyinyi hamna uwezo wa kuiotesha miti yake. Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali hao ni watu walio potoka.

Siyo Yeye (bora zaidi ya miungu yenu) yule aliye ifanya ardhi mahali pa kutua, na akajaalia ndani yake mito, na akaweka milima? Na akaweka baina ya bahari mbili kiziwizi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali wengi wao hawajui.

Siyo Yeye (bora zaidi ya miungu yenu)yule anaye mjibu mwenye shida pale anapo mwomba, na akaiondoa dhiki, na akakufanyeni warithi wa ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ni machache mnayo yazingatia.

Siyo Yeye (bora zaidi ya miungu yenu) yule anaye kuongoeni katika giza la bara na bahari, na akazipeleka pepo kuleta bishara kabla ya rehema zake? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ametukuka Mwenyezi Mungu juu ya wanao washirikisha naye.

Siyo Yeye (bora zaidi ya mnayoiita miungu yenu) anaye uanzisha uumbaji, kisha akaurejesha? Na nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema: Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema kweli. ” (Kurani 27:59-64)



Rejeleo la maelezo:

[1] Nguzo sita za imani ni kumwamini Mungu, malaika zake, mitume wake na wajumbe, vitabu vyake vyote vilivyofunuliwa, Siku ya Hukumu, na nguvu ya kimungu.

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.