Ardhi Saba
Maelezo: Matabaka saba ya ardhi ambayo wanasayansi wamegundua hivi karibuni yalitajwa na Mtume Muhammad miaka 1400 iliyopita.
- Na Imam Mufti
- Iliyochapishwa mnamo 23 Nov 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 04 Jul 2022
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 3,519 (wastani wa kila siku: 3)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Sunnah ya Mtume Muhammad, rehma ziwe juu yake, ni chanzo cha pili cha Uislamu. Kama Qurani, ina taarifa za kisayansi ambazo hazikuweza kupatikani miaka 1400 iliyopita. Kati ya miujiza hiyo ni ardhi “saba”, iliyotajwa na Mtume katika hadithi zake kadhaa:
Hadithi ya 1
Ilisimuliwa kutoka kwa Abu Salama kwamba mgogoro ulitokea kati yake na watu wengine (kuhusu kipande cha ardhi). Alipomwambia Aisha (mke wa Mtume) kuhusu hilo, alisema, 'Ewe Abu Salama! Jiepushe na kuchukua ardhi kwa dhulma, Nabii alisema:
“Yeyote anayenyang'anya hata sehemu moja ya ardhi ya mtu, kina chake katika ardhi saba kitawekwa shingoni mwake.” (Saheeh Al-Bukhari, 'Kitabu cha ukandamizaji.')
Hadithi ya 2
Salim alisimulia kutoka kwa baba yake kwamba Mtume alisema:
'Atakaye chukua sehemu ya ardhi ya watu kwa dhulma, basi Siku ya Kiama atazama chini kwa ardhi saba.' (Saheeh Al-Bukhari, 'Kitabu cha dhulma.')
Hadithi iliyotangulia inakataza dhulma kwa ujumla, hasa kuchukua sehemu ya ardhi ya watu wengine bila haki. Je! Ardhi saba inaweza kuwa nini?
Uchunguzi wa jiolojia umethibitisha ya kwamba ardhi inajumuisha kanda saba, zinazotambuliwa kutoka tabaka la ndani hadi tabaka la nje kama ifuatavyo:
(1) Kiini cha Ndani cha Ardhi: Asilimia 1.7 ya uzito wa Ardhi; kina cha kilomita 5,150 - 6,370 (maili 3,219 - 3,981)
Kiini cha ndani ni imara na hakijaunganishwa na tandiko, kimesimamishwa kwenye kiini kioevu cha nje. Inaaminika kuwa kimekuwa kigumu kutokana na shinikizo la kuganda ambalo hutokea kwa vioevu vingi wakati joto linapungua au shinikizo linaongezeka.
(2) Kiini cha nje Kioevu: Asilimia 30.8 ya uzito wa Ardhi; kina cha kilomita 2,890 - 5,150 (maili 1,806 - 3,219)
Kiini cha nje ni kioevu cha moto, kinachopitisha umeme, na ndani yake mwendo wa mzunguko hutokea. Tabaka hili la mzunguko linachanganyika na mzunguko wa Ardhi ili kuunda athari ya jenereta ambayo inashikilia mfumo wa mikondo ya umeme inayojulikana kama uwanja wa sumaku la Dunia. Pia ina jukumu la shituko ya kichini chini ya mzunguko wa Ardhi. Tabaka hili sio zito kama chuma kilichoyeyushwa, ambacho kinaonyesha kuwepo kwa vipengele vyepesi. Wanasayansi wanadhani ya kwamba asilimia 10 ya tabaka hili ni sulfuri na/au oksijeni kwa sababu vipengele hivi vinapatikana kwa wingi katika ulimwengu na huyeyuka kwa urahisi katika chuma kilichoyeyushwa.
(3) Tabaka la "D" : Asilimia 3 ya uzito wa Ardhi; kina cha kilomita 2,700 - 2,890 (maili 1,688 - 1,806)
Tabaka hili lina unene wa kilomita 200 hadi 300 (maili 125 hadi 188) na linawakilisha takriban asilimia 4 ya uzito wa ganda la tandiko. Ingawa mara nyingi hutambulika kuwa sehemu ya tandiko la chini, mabadiliko ya kizilzala yanaonyesha tabaka la “D” linaweza kutofautiana kikemia na tandiko la chini lililolala juu yake. Nadharia ya Wanasayansi ni kwamba aidha kipengele kimeyeyuka katika kiini, au kiliweza kuzama kwa tandiko lakini sio katika kiini kwa sababu ya wiani wake.
(4) Tandiko la Chini: Asilimia 49.2 ya uzito wa Ardhi; kina cha kilomita 650 - 2,890 (maili 406 -1,806)
Tandiko la chini lina asilimia 72.9 ya uzito wa tandiko-kiini na huenda inajumuisha kwa wingi silikoni, magnesiamu, na oksijeni. Pengine pia inajumuisha chuma, kalsiamu, na alumini. Wanasayansi hufanya hesabu hizi kwa kukisia kuwa ardhi ina kiasi sawa ya vipengele vya anga kama inavyopatikana katika Jua na vimondo ya kale.
(5) Tandiko la Kati (Eneo la Mabadiliko): Asilimia 7.5 ya uzito wa Ardhi; Kina cha kilomita 400 - 650 (maili 250-406)
Eneo la mabadiliko au tabakameso (kwa tandiko la kati), ambalo pia huitwa tabaka la rutuba, lina asilimia 11.1 ya uzito wa tandiko-kiini na ni chanzo cha magma za basalti. Pia lina kalsiamu, alumini, na garneti, ambayo ni madini ya silikati yenye inabeba alumini. Tabaka hili ni nene inapokuwa baridi kwa sababu ya garneti. Linaelea linapokuwa na joto kwa sababu madini haya yanayeyuka kwa urahisi kuunda basalti ambayo inaweza kisha kupanda kupitia tabaka za juu kama magma.
(6) Tandiko la Juu: Asilimia 10.3 ya uzito wa Ardhi; kina cha kilomita 10 - 400 (maili 6 - 250)
Tandiko la juu lina asilimia 15.3 ya uzito wa tandiko-kiini. Vipande vimechimbwa kwa uchunguzi wetu na mikanda ya mlima iliyoharibika na milipuko ya volkeno. Mzeituni (Mg, Fe) 2SiO4 na pyroksini (Mg, Fe) SiO3 zimekuwa madini ya msingi yanayopatikana kwa njia hii. Madini haya na mengine ni kinzani na fuwele kwa joto la juu; kwa hivyo, mengi hukaa nje ya magma inayopanda, aidha kutengeneza vipengele vipya au kutoacha tandiko kamwe. Sehemu ya tabaka la juu iitwayo asthenosphere inaweza kuyeyuka kwa kiasi fulani.
(7) Ganda la Nje
Kiini cha bahari: Asilimia 0.099 ya uzito wa ardhi; kina cha kilomita 0-10 (maili 0 - 6)
Tabaka la nje ya Ardhi linalojumuisha ukanda na tandiko la juu linaitwa lithosphere, au ganda la nje. Kiini cha bahari kina asilimia 0.147 ya uzito wa tandiko-kiini. Sehemu kubwa ya kiini cha Ardhi kimetengenezeka kupitia shughuli za volkeno. Mfumo wa ufa wa bahari, mtandao wa kilomita 40,000 (maili 25,000) wa volkano, huzalisha ukanda mpya wa bahari kwa kiwango cha Kilomita 17 kwa kila mraba kwa mwaka, na kufunika sakafu ya bahari na basalti. Hawaii na Aislandi ni mifano miwili ya mkusanyiko wa marundo ya basalti.
Kiini cha bara kina asilimia 0.554 ya uzito wa tandiko. Hii ni sehemu ya nje ya ardhi inayojumuisha kimsingi ya miamba ya fuwele. Haya ni maadini yanayoelea yenye wiani wa chini, na asilimia kubwa ya madini haya ni Kwatsi (SiO2) na feldspars (silikati yenye upungufu wa chuma). Kiini (cha bahari na bara) ni sakafu ya Ardhi; na hivyo, ni sehemu iliyo baridi zaidi kwenye sayari yetu. Kwa sababu miamba ya baridi huharibika polepole, tunaita ganda hili la nje la nje lithosphere (tabaka la mawe au lenye nguvu).
Hitimisho
Matabaka ya ardhi yanaendana na hadithi iliyotajwa hapo juu ya Mtume, rehma ziwe juu yake. Muujiza ni katika mambo mawili:
(1) Kauli ya hadithi, 'Atazizama ardhi saba Siku ya Kiyama,' Inaonyesha mgawanyiko wa ardhi hizi katika kuzunguka kituo kimoja.
(2) Usahihi ambao Mtume wa Uislamu alitaja tabaka saba za ndani za ardhi.
Njia pekee ambayo mkazi wa jangwa angejua mambo haya miaka 1400 iliyopita ni kama alipata ufunuo kutoka kwa Mungu.
Marejeleo
Beatty, J. K. na A. Chaikin, eds. The New Solar System. Massachusetts: Sky Publishing, Nakala ya tatu, 1990.
Press, Frank na Raymond Siever. Ardhi. New York: W. H. Freeman and Company, 1986.
Seeds, Michael A. Horizons. Belmont, California: Wadsworth, 1995.
El-Najjar, Zaghloul. Treasures In The Sunnah: A Scientific Approach: Cairo, Al-Falah Foundation, 2004.
Ongeza maoni