Maisha baada ya Kifo (sehemu ya 2 kati ya 2): Matunda Yake
Maelezo: Baadhi ya manufaa ya imani ya Akhera, pamoja na hitimisho la sababu mbalimbali za kuamini Kuwepo kwake.
- Na iiie.net (edited by IslamReligion.com)
- Iliyochapishwa mnamo 14 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 5,074 (wastani wa kila siku: 5)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Kurani pia inaelezea kuwa maisha haya ya dunia ni maandalizi ya maisha ya milele baada ya kifo. Lakini wale wanaoyakadhibisha wanakuwa watumwa wa tamaa na matamanio yao, na wanawafanyia mzaha watu wema na wamchao Mwenyezi Mungu. Watu kama hao hutambua upumbavu wao tu wakati wa kifo chao na hutamani bila kufaulu kupewa nafasi nyingine ya kuishi duniani. Hali yao ya huzuni wakati wa kifo, vitisho vya Siku ya Hukumu, na neema ya milele iliyohakikishwa kwa waumini waaminifu yote hayo yametajwa vizuri sana katika aya zifuatazo za Kurani.
“Mpaka yanapomfikia mmoja wao mauti, husema: ‘Mola wangu Mlezi! Nirudishe. Ili nitende mema sasa badala ya yale niliyoyaacha.’ Wapi! Hii ni kauli aisemayo yeye tu. Na nyuma yao kipo kizuizi mpaka siku watapofufuliwa. Basi litakapopulizwa baragumu hapo hautakuwapo ujamaa baina yao siku hiyo, wala hawataulizana. Ama wale ambao mizani zao zitakuwa nzito, hao ndio wenye kufanikiwa. Na wale ambao mizani zao zitakuwa nyepesi, hao ndio waliozitia khasarani nafsi zao, na katika Jehanamu watadumu. Moto utababua nyuso zao, nao watakuwa na nyuso zilizokunjana.” (Kurani 23:99-104)
Imani ya maisha baada ya kifo sio tu kwamba inahakikisha mafanikio ya Akhera, bali pia inaifanya dunia hii kujaa amani na furaha. Hii ni kwa kuwafanya watu binafsi wawajibike na kutokana na kumcha Mwenyezi Mungu: kuogopa adhabu Yake na kutaraji malipo Yake.
Tafakari kuhusu watu wa Uarabuni. Kamari, unywaji pombe, ugomvi wa kikabila, uporaji na uuaji ulikuwa sifa kuu za jamii yao wakati hawakuwa na imani juu ya maisha ya Akhera. Lakini mara tu walipokubali imani ya Mungu Mmoja na maisha baada ya kifo, wakawa taifa lenye nidhamu zaidi duniani. Waliacha maovu yao, wakasaidiana wakati wa shida, na kusuluhisha migogoro yao yote kwa misingi ya haki na usawa. Vilevile, kukana maisha baada ya kifo kuna madhara yake sio tu huko Akhera, bali hata hapa duniani. Taifa zima linapoyakanusha, kila aina ya uovu na ufisadi hushamiri katika jamii hiyo na hatimaye kuangamizwa. Kurani inataja mwisho mbaya wa 'Aad, Thamud na Firauni kwa undani zaidi:
“(Makabila ya) Thamudi na Aadi waliukadhibisha Msiba unaoshtusha [hukumu]. Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno [umeme]. Na ama Aadi waliangamizwa kwa upepo mkali usiozuilika. Aliowapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo bila ya kusita. Utaona watu wamepinduka kama kwamba ni magongo ya mitende yalio wazi ndani.
“Basi je, unamwona mmoja wao aliye baki? Na Firauni na waliomtangulia, na miji iliyopinduliwa chini juu, walileta khatia. Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato uliozidi nguvu. Maji yalipofurika, Sisi tulikupandisheni katika safina, Ili tuyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalosikia liyahifadhi.
“Na litakapopulizwa barugumu mpulizo mmoja tu, na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja, siku hiyo ndiyo Tukio litatukia. Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa.
“...Basi ama atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: ‘Haya someni kitabu changu! Hakika nilijua ya kuwa nitapokea hesabu yangu.’ Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza, Katika Bustani ya juu, Matunda yake yakaribu. Waambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyotanguliza katika siku zilizopita.
“Na ama atakayepewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: ‘Laiti nisingelipewa kitabu changu! Wala nisingelijua nini hesabu yangu. Laiti mauti ndiyo yangelikuwa ya kunimaliza kabisa. Mali yangu hayakunifaa kitu. Madaraka yangu yamenipotea.’” (Kurani 69:4-29)
Hivyo, kuna sababu zenye kusadikisha za kuamini maisha baada ya kifo.
Kwanza, mitume wote wa Mwenyezi Mungu wamewaita watu wao kuyaamini.
Pili, wakati wowote jamii ya wanadamu inapojengwa juu ya msingi wa imani hii, imekuwa jamii bora zaidi na yenye amani, isiyo na maovu ya kijamii na kimaadili.
Tatu, historia inashuhudia kwamba kila imani hii inapokataliwa kwa pamoja na kundi la watu licha ya onyo la mara kwa mara la Mtume wao, kundi hilo lote liliadhibiwa na Mwenyezi Mungu, hata hapa hapa duniani.
Nne, nyenzo za maadili, uzuri na busara za mwanadamu zinaidhinisha uwezekano wa maisha baada ya kifo.
Tano, sifa za Mungu za Haki na Rehema zisingekuwa na maana kama hakuna maisha baada ya kifo.
Ongeza maoni