Maelezo ya Kurani kuhusu asili ya Ulimwengu
Maelezo: Maelezo ya kisayansi na Kurani kuhusu uumbaji wa ulimwengu.
- Na islam-guide.com
- Iliyochapishwa mnamo 23 Nov 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 24 Dec 2023
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 4,713 (wastani wa kila siku: 4)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Dondoo: Sayansi ya Kosmolojia ya kisasa, ya kiuchunguzi na ya kinadharia, inaonyesha wazi kwamba, kuna wakati ulimwengu wote haukuwa chochote ila wingu la 'moshi' (yaani, wingu jeusi zito na gesi zenye joto jingi).[1] Hii ni mojawapo ya kanuni za kosmologia ya kisasa zisizo pingika. Wanasayansi sasa wanaweza kuona nyota mpya zinazoundwa kutokana na mabaki ya 'moshi' huo (tazama picha 1 na 2).
Nyota zenye kung'aa tunazoziona usiku zilikuwa, kama vile ulivyokuwa ulimwengu wote, katika nyenzo hiyo ya 'moshi'. Mungu amesema katika Kurani:
“Kisha akaziekelea mbingu, na zilikuwa moshi...” (Kurani 41:11)
Kwa kuwa ardhi na mbingu zilizo juu (jua, mwezi, nyota, sayari, galaksi n.k.) zimeundwa kutokana na 'moshi' huo huo, tunathibitisha ya kuwa ardhi na mbingu zilikuwa kipengele kimoja kilichounganishwa. Kisha kutoka kwa 'moshi' huu mkubwa, ziliundika na kutengana. Mwenyezi Mungu amesema katika Kurani:
“Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana , kisha Sisi tukazibandua? ...” (Kurani 21:30)
Dr. Alfred Kroner ni kati ya wanajiolojia mashuhuri duniani. Yeye ni Profesa wa Jiolojia na Mwenyekiti wa Idara ya Jiolojia katika Taasisi ya Sayansi za Ardhi, Chuo Kikuu cha Johannes Gutenberg, Mainz, Ujerumani. Alisema: “Unapofikiria mahali Muhammad alitoka. Nadhani ni vigumu kwamba angeweza kujua kuhusu mambo kama asili ya ulimwengu, kwa sababu wanasayansi wamegundua tu kwa miaka michache iliyopita, kwa kutumia mbinu tata ya kiteknolojia. [2]. (Kutazama video ya RealPlayer ya maoni haya, bonyeza hapa). Pia alisema: “Mtu ambaye hakujua kitu kuhusu fizikia ya nyuklia karne kumi na nne iliyopita hakuweza, nadhani, kuwa katika nafasi ya kujua kutoka kwa akili yake mwenyewe, kwa mfano, kwamba dunia na mbingu zilikuwa na asili sawa.”[3] (Kutazama video ya RealPlayer ya maoni haya, bonyeza hapa).
Vielezi-chini:
[1]Dakika Tatu za Kwanza, Mtazamo wa Kisasa wa Asili ya Ulimwengu, Weinberg, uk. 94-105.
[2]Msemo huu umenukuliwa kutoka kwa Huu ndio Ukweli (videoe). Ili kupata nakala ya video hii, zuru ukurasa huu.
[3]Huu ndio Ukweli (video).
Ongeza maoni