Utabiri wa Unabii wa Muhammad Katika Bibilia (Sehemu ya 1 kati ya 4): Mashahidi wa Wataalamu
Maelezo: Ushuhuda kutoka Bibilia kuwa Muhammad si Mtume wa uongo. Sehemu ya 1: Changamoto katika kuchambua utabiri wa bibilia, na shuhuda ya wasomi walioshuhudia kuwa Muhammad alizungumziwa katika Bibilia.
- Na Imam Mufti
- Iliyochapishwa mnamo 23 Nov 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 24 Oct 2022
- Ilichapishwa: 3
- Imetazamwa: 47,916
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Masuala ya utangulizi
Biblia ni maandiko matakatifu ya Uyahudi na Ukristo. Biblia ya Kikristo ina Agano la Kale na Agano Jipya, huku matoleo ya Kikatoliki na ya Kiorthodoksi ya Mashariki ya Agano la Kale yakiwa makubwa kidogo kwa sababu ya kukubalika kwa vitabu fulani ambavyo havikubaliwi kama maandiko na Waprotestanti. Biblia ya Kiyahudi inajumuisha tu vitabu vinavyojulikana kwa Wakristo kama Agano la Kale. Zaidi ya hayo, mipangilio ya vitabu vinavyokubalika vya Wayahudi na vya Wakristo vinatofautiana sana.[1] Mtume Muhammad ametabiriwa katika Agano la Kale na Agano Jipya.
Yesu na Mitume wake wanaaminiwa kuwa waliongea Kiaramu. Kiaramu kiliendelea kutumika katika matumizi makubwa hadi takriban 650 BK, kilipobadilishwa na Kiarabu. [2] Biblia ya leo, hata hivyo, haitoki kwa miswada ya Kiaramu, bali kwa matoleo ya Kigiriki na Kilatini.
Kunukuu utabiri wa Biblia haumaanishi ya kwamba Waislamu wanakubali kuwa Biblia ya leo kwa ukamilifu wake ni ufunuo wa Mungu. Kwa imani ya Kiislamu kuhusu maandiko yaliyopita, tafadhali bofya hapa
Sio sharti kwa nabii kukubalika kuwa lazima atabiriwe na manabii wa awali. Musa alikuwa nabii kwa Farao ingawa hakutabiriwa na mtu yeyote kabla yake. Ibrahimu alikuwa nabii wa Mungu kwa Nimrodi, lakini hakuna mtu aliyetabiri kuja kwake. Nuhu na Lutu na wengine walikuwa manabii wa kweli wa Mungu, lakini hawakutabiriwa. Ushahidi wa ukweli wa nabii hautegemei utabiri wa manabii wa zamani, lakini unajumuisha ujumbe halisi ulioletwa naye, miujiza na zaidi.
Kujadili mambo ya unabii ni suala nyeti. Inahitaji kuangalia kwa kina matoleo ya Biblia na tafsiri zake, miswada iliyogunduliwa hivi karibuni na kutafuta maneno ya Kiebrania, ya Kigiriki, na ya Kiaramu na kuyachunguza. Kazi inakuwa ngumu zaidi wakati: “kabla ya vyombo vya uchapishaji kuvumbuliwa (karne ya 15), nakala zote za Biblia zinaonyesha tofauti za kimaandishi. “[3] Hili si jambo rahisi kwa watu wa kawaida. Kwa sababu hiyo, ushuhuda bora unatoka kwa wataalamu wa kale na wa kisasa katika mambo hayo ambao walikubali utabiri.
Tuna kumbukumbu za Wayahudi na Wakristo wa kale, watawa na marabi, ambao walishuhudia kwamba Muhammad alikuwa utimilifu wa utabiri mahususi wa Biblia. Wafuatao ni baadhi ya mifano ya watu hawa.
Mtume Anayesubiriwa
Wayahudi na Wakristo wa Arabia kabla ya Uislamu walikuwa wakisubiri mtume. Kabla ya kutokea kwa Muhammad, Arabia ilikuwa makao ya Wayahudi, Wakristo, na Waarabu Walioabudu masanamu ambao, mara kwa mara, walikwenda vita kati yao. Wayahudi na Wakristo wangesema: 'Wakati umefika wa Nabii asiye andika wala kusoma atakayefufua dini ya Ibrahimu kutokea. Na tutaungana naye, na tutapigana vita vikali dhidi yenu.' Muhammad alipotokea, baadhi yao walimuamini, na wengine walikataa. Hii ndiyo sababu Mungu alifunua:
"Na kilipo wajia Kitabu [Kurani] kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kinacho thibitisha waliyo nayo- na wao walikuwa wakitafutia ushindi kuwashinda makafiri- yalipo wajia yale waliyo kuwa wakiyajua waliyakanusha. Basi laana ya Mwenyezi Mungu juu yao wakanushao." (Kurani 2:89)
Shahidi wa kwanza alikuwa Buhra, mtawa Mkristo, aliyetambua unabii wa Muhammad alipokuwa bado mdogo na kumwambia mjomba wake:
"…Mpwa wako ana bahati kubwa mbele yake, hivyo mrudishe nyumbani haraka."[4]
Shahidi wa pili alikuwa Waraqah ibn Nawfal, msomi Mkristo aliyefariki punde baada ya mkutano wa faragha na Muhammad. Waraqah alimshuhudia Muhammad kuwa alikuwa Nabii wa wakati wake na kupokea ufunuo kama Musa na Yesu.[5]
Wayahudi wa Madina walikuwa wakisubiri kwa hamu kuwasili kwa nabii. Mashahidi wa tatu na wa nne walikuwa Marabi wao maarufu wa Kiyahudi, Abdullah ibn Salam na Mukhayriq.[6]
Mashahidi wa sita na wa saba walikuwa pia rabi wa Kiyahudi wa Yemeni, Wahb ibn Munabbih, na Ka'b al-Ahbar (alikufa 656 BK). Ka'b alipata vifungu vingi vya sifa na maelezo ya Nabii yaliyotabiriwa na Musa katika Biblia.[7]
Quran inasema:
"Je! Haikuwa kwao ni Ishara kwamba wanayajua haya wanazuoni wa Wana wa Israili?" (Quran 26:197)
Vielezi-chini:
[1]"Bible." Encyclopædia Britannica kutoka Encyclopædia Britannica Premium Service. (http://www.britannica.com/eb/article-9079096)
[2]"Aramaic language." Encyclopædia Britannica kutoka Encyclopædia Britannica Premium Service. (http://www.britannica.com/eb/article-9009190)
[3]"biblical literature." Encyclopædia Britannica kutoka Encyclopædia Britannica Premium Service. (http://www.britannica.com/eb/article-73396)
[4]‘Muhammad: His Life Based on the Earliest Sources’ Martin Lings, uk. 29. ‘Sirat Rasul Allah’ Ibn Ishaq ilitafsiriwa na A. Guillame, uk.. 79-81. ‘The Quran And The Gospels: A Comparative Study,’ uk. 46 Dr. Muhammad Abu Laylah wa Chuo kikuu cha Azhar .
[5] ‘Muhammad: His Life Based on the Earliest Sources’ Martin Lings, uk. 35.
[6] ‘The Quran And The Gospels: A Comparative Study,’ uk. 47 Dr. Muhammad Abu Laylah of wa Chuo kikuu cha Azhar .
[7] ‘The Quran And The Gospels: A Comparative Study,’ p. 47-48 by Dr. Muhammad Abu Laylah of Azhar University.
Ongeza maoni