Utabiri wa Mtume Muhammad Katika Bibilia (sehemu ya 2 ya 4): Utabiri wa Muhammad katika Agano la Kale
Maelezo: Ushahidi kutoka Bibilia kuwa Muhammad si Mtume wa uwongo. Sehemu ya 2: Uchambuzi kuhusu jinsi utabiri ulio katika Kumbukumbu la Torati 18:18, na vile sifa za Muhammad zinaafikiana na utabiri huu zaidi ya wengine.
- Na Imam Mufti
- Iliyochapishwa mnamo 23 Nov 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 4
- Imetazamwa: 51,446 (wastani wa kila siku: 45)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Kumbukumbu la Torati 18:18 "Mimi (Mwenyezi Mungu) nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe (Musa), nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.'
Wakristo wengi wanaamini utabiri huu uliotabiriwa na Musa unahusu Yesu. Hakika Yesu alitabiriwa katika Agano la Kale, lakini kama itakavyokuwa wazi, utabiri huu haufanani naye, bali unaafikiana zaidi na Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake. Musa alitabiri yafuatayo:
1. Mtume huyo atakuwa kama Musa
.
Kipengele cha Ulinganisho |
Musa |
Yesu |
Muhammad |
Kuzaliwa |
alizaliwa kawaida |
alizaliwa kimiujiza, mama yake alikuwa bikira |
alizaliwa kawaida |
Lengo |
Mtume tu |
Inasemekana ni mtoto wa Mungu |
Mtume tu |
Wazazi |
baba na mama |
mama pekee |
baba na mama |
Maisha ya kifamilia |
alioa na kuzaa watoto |
hakuoa |
alioa na kuzaa watoto |
Kukubaliwa na watu wake |
Wayahudi walimkubali |
Wayahudi walimkataa[1] |
Waarabu walimkubali |
Mamlaka ya kisiasa |
Musa alikuwa nao (Hesabu 15:36) |
Yesu aliukataa[2] |
Muhammad alikuwa nao |
Ushindi juu ya wapinzani wake |
Farao alikufa majini |
inasemekana alisulubiwa |
Watu wa Makka walishindwa |
Kifo |
Kifo cha kawaida |
inadaiwa kuwa alisulubiwa |
Kifo cha kawaida |
Kuzikwa |
alizikwa kwa kaburi |
kaburi tupu |
alizikwa kwa kaburi |
Uungu |
si mungu | wakristo wanaamini ni mtoto wa mungu | si Mungu |
Alianza uhubiri kwa umri wa |
40 |
30 |
40 |
Kufufuka duniani |
hakufufuka | inadaiwa alifufuka |
hakufufuka |
2. Nabii aliyesubiriwa atatoka kati ya Ndugu wa Wayahudi
Aya tunayoongelea ni wazi kwa kusema kwamba nabii atatokea miongoni mwa Ndugu wa Wayahudi. Ibrahimu alikuwa na wana wawili: Ishmaeli na Isaka. Wayahudi ni wazao wa mwana wa Isaka, Yakobo. Waarabu ni watoto wa Ishmaeli. Hivyo, Waarabu ni ndugu wa taifa la Kiyahudi.[3] Bibilia inasema:
‘Naye (Ishmaeli) atakaa mbele ya uso wa ndugu zake wote.’ (Mwanzo 16:12)
‘Naye (Ishmaeli) akakata pumzi, akafa. Akakusanywa kwa watu wake.’ (Mwanzo 25:18)
Wana wa Isaka ni ndugu wa Waishmaeli. Vivyo hivyo, Muhammad ni miongoni mwa ndugu wa Waisraeli, kwa sababu alikuwa mzao wa Ishmaeli mwana wa Ibrahimu.
3. Mungu Ataweka Maneno Yake katika Mdomo wa Nabii Anayesubiriwa
Kurani inasema kuhusu Muhammad:
"Wala hatamki kwa matamanio. Hayakuwa haya ila ufunuo ulio funuliwa (Kurani 53:3-4)
Hii inafanana sana na fungu la Kumbukumbu la Torati 18:18:
"nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao, mfano wako wewe (Musa), nami nitatia maneno yangu kinywani mwake; naye atawaambia yote nitakayomwamuru." (Kumbukumbu la Torati 18:18)
Nabii Muhammad alikuja na ujumbe kwa walimwengu wote, na kutoka kwao, Wayahudi. Wote, ikiwa ni pamoja na Wayahudi, wanapaswa kukubali unabii wake, na hii inasadikishwa na maneno yafuatayo:
"MWENYEZI MUNGU, Mungu wenu atawateulieni nabii aliye kama mimi kutoka miongoni mwenu, nanyi mtamsikiliza huyo." (Kumbukumbu la Torati 18:15)
4. Onyo kwa Watakaokataa
Utabiri unaendelea:
Kumbukumbu la Torati 18:19 "Yeyote ambaye hatasikia maneno atakayosema nabii huyo kwa jina langu, mimi mwenyewe nitamwadhibu."
Waislamu, kwa upande mwingine, huanza kila sura katika Kurani kwa jina la Mungu kwa kusema:
Bismillah ir-Rahman ir-Raheem
"‘Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu"
Yafuatayo ni masimulizi ya baadhi ya wasomi walioamini kuwa utabiri huu unamfaa Muhammad.
Shahidi wa Kwanza
Abdul-Ahad Dawud, ambaye alikuwa Mchungaji zamani, ambapo aliitwa kwa wakati huo David Benjamin Keldani, BD, padri Mkatoliki wa madhehebu ya Umoja wa Wakaldayo (soma wasifu wake hapa).Baada ya kukubali Uislamu, aliandika kitabu kinachoitwa, 'Muhammad katika Biblia. ' Anaandika kuhusu utabiri huu:
“Kama maneno haya hayamuongelei Muhammad, basi bado hayajatimia. Yesu mwenyewe hakudai kamwe kuwa yeye ndiye nabii aliyetajwa. Hata wanafunzi wake walikuwa na maoni sawa: walisubiri ujio wa pili wa Yesu ili utabiri utimie (Matendo ya Mitume 3:17-24). Hadi sasa ni dhahiri kwamba ujio wa kwanza wa Yesu haukuwa ujio wa Nabii huyo na ujio wake wa pili hauwezi kutimiza maneno hayo. Yesu, kama inavyoaminiwa na Kanisa lake, atatokea kama Hakimu wala si kama mtoaji sheria; lakini aliyeahidiwa atakuja na “sheria ya moto” katika mkono wake wa kuume."[4]
Shahidi wa Pili
Muhammad Asad alizaliwa kama Leopold Weiss mwezi Julai 1900 katika mji wa Lvov (Lemberg ya Kijerumani), ambao sasa upo nchini Poland, ambayo ilikuwa chini ya Dola la Austria. Alikuwa mzawa wa ukoo ambao ulikuwa na mstari mrefu wa marabi , mstari uliovunjwa na baba yake, ambaye alichagua kuwa wakili. Asad mwenyewe alipata elimu nyingi ya dini ambayo ingemruhusu kuendeleza mila ya familia ya urabbi. Alikuwa mjuzi katika Kiebrania akiwa mdogo na pia alikuwa akifahamu Kiaramu. Alikuwa amejifunza Agano la Kale katika mfumo wake asili pamoja na maandishi na maoni ya Talmud, Mishna na Gemara, na alikuwa amejiingiza katika mambo ya undani ya ufafanuzi wa Biblia, Targum.[5]
Akiongelea aya ya Kurani:
"Wala msichanganye kweli na uwongo na mkaificha kweli nanyi mnajua." (Kurani 2:42)
Muhammad Asad anaandika:
“Kwa 'kuichanganya ukweli kwa uwongo ' maana ni kupotosha maandishi ya Biblia, ambayo Qur'ani mara nyingi huwashtaki Wayahudi (na ambayo tangu hapo imethibitishwa kwa upinzani wa kweli wa maandishi), huku 'kuficha ukweli' inahusu kutokujali kwao au kupeana tafsiri ya uongo kwa makusudi kuhusu maneno ya Musa katika kifungu cha Biblia, 'Mungu wenu atawateulieni nabii aliye kama mimi kutoka miongoni mwenu, nanyi mtamsikiliza huyo." (Kumbukumbu la Torati 18:15) na maneno yanayosemekana ni ya Mungu mwenyewe, 'nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao, mfano wako wewe (Musa), nami nitatia maneno yangu kinywani mwake; naye atawaambia yote nitakayomwamuru." (Kumbukumbu la Torati 18:18) “Ndugu” wa wana wa Israeli ni wazi kuwa ni Waarabu, na hasa kundi la Musta'riba ('Walioarabishwa') miongoni mwao, ambalo linaingilia ukoo wa Ishmaeli na Ibrahimu; na kwa kuwa ni kundi hili ambalo kabila la Nabii wa Arabia linatoka, yaani Quraish, vifungu vilivyo juu vya Biblia vinapaswa kuchukuliwa kumaanisha ujio wake."[6]
Vielezi-chini:
[1] "He (Jesus) came unto his own, but his own received him not" (Yohana 1:11)
[2] Yohana 18:36.
[3] ‘Muhammad: His Life Based on the Earliest Sources’ na Martin Lings, p. 1-7.
[4] Ibid, uk. 156
[5]‘Berlin to Makkah: Muhammad Asad’s Journey into Islam’ Ismail Ibrahim Nawwab kwenye nakala ya Januari/Februari 2002 ya Gazeti la Saudi Aramco.
[6]Muhammad Asad, ‘The Message of The Kurani’ (Gibraltar: Dar al-Andalus, 1984), uk. 10-11.
Ongeza maoni