Kusudi la Uumbaji (sehemu ya 1 ya 3): Utangulizi
Maelezo: Utangulizi wa swali la kutatanisha zaidi katika historia ya binadamu, na mjadala kuhusu vyanzo ambavyo vinaweza kutumika kupata jibu. Sehemu ya 1: Chanzo cha jibu.
- Na Dr. Bilal Philips
- Iliyochapishwa mnamo 10 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 16 Jul 2023
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 3,934 (wastani wa kila siku: 4)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Utangulizi
Madhumuni ya uumbaji ni mada ambayo hutatanisha kila mwanadamu wakati fulani katika maisha yake. Kila mtu kwa wakati fulani au mwingine anajiuliza swali la “Kwa nini ninaishi?” au “Kwa nini niko hapa duniani?”
Utofauti na utata wa mifumo yanayowazunguka wanadamu na ulimwengu huonyesha kwamba lazima kuna Mkuu aliyewaumba. Kilichobuniwa kinaonyesha mbuni. Wanadamu wanapoona nyayo kwenye ufuo, wanaelewa kwamba kuna mtu alikuwa ametembea huko wakati fulani hapo awali. Hakuna mtu anayefikiria kwamba mawimbi kutoka baharini yalifunika mchanga na kwa bahati kuweka nyayo zinazoonekana hasa kufanana na nyayo za kibinadamu. Wanadamu pia huelewa kiasili kwamba waliletwa duniani ili kutimiza lengo fulani. Kwa kuwa tendo la kimakusudi ni zao la kiasili ya akili ya kibinadamu, binadamu huelewa kwamba aliyewaumba, mwenye hekima kuu, lazima amefanya hivyo kwa lengo maalum. Kwa hivyo, binadamu wanahitaji kujua kusudi la kuwepo kwao ili kuyaelewa maisha haya na kufanya kinacholeta manufaa kwao.
Hata hivyo, katika miaka yoye ya historia ya binadamu, kumekuwa na wachache miongoni mwa wanadamu ambao wamekanusha kuwepo kwa Mungu. Vipengele, kwa maoni yao, ni vya milele na wanadamu ni matokeo ya kibahati ya mchanganyiko wa ajali wa vipengele vyake. Kwa sababu hiyo, kulingana nao, swali la “Kwa nini Mungu alimuumba mwanadamu?” bado halina jibu. Kulingana na wao, hakuna madhumuni ya kuwepo kwa mwanadamu duniani. Hata hivyo, idadi kubwa ya wanadamu katika miaka yote ya historia ya wanadamu wameamini na kuendelea kuamini kuwepo kwa Muumba mkuu ambaye aliumba ulimwengu huu kwa lengo. Kwao ilikuwa ni muhimu kujua kuhusu Muumba na lengo ambalo aliwaumbia wanadamu.
Jibu
Ili kujibu swali la “Kwa nini Mungu aliumba mwanadamu?” ni lazima kwanza tujue ni kutoka kwa mtazamo upi swali linaulizwa. Kutokana na mtazamo wa Mungu ungemaanisha, “Ni nini kilichosababisha Mungu kuumba binadamu?” huku mtazamo wa kibinadamu ungemaanisha “Kwa nini Mungu aliumba binadamu?” Mitazamo yote mbili inawakilisha vipengele vya swali muhimu la “Kwa nini naishi?” ... vipengele vyote vya swali vitachunguzwa kulingana na taswira ya ufunuo wa Mungu. Hii sio mada inayoweza kukisiwa na wanadamu, kwa sababu kukisia kwa binadamu hakuwezi eleza ukweli wowote katika suala hili. Je, wanadamu wanaweza kueleza vipi ukweli wa kuwepo kwao wakati hawawezi kuelewa jinsi ubongo wao wenyewe au akili zao hufanya kazi? Kwa sababu hiyo, wanafalsafa wengi ambao wamekisia juu ya swali hili kwa miaka wamekuja na majibu yasiyohesabika, yote ambayo yanategemea mawazo ambayo hayawezi kuthibitishwa. Maswali juu ya mada hii yamesababisha hata wanafalsafa kadhaa kudai kwamba hatupo kikweli na kwamba ulimwengu wote ni fikra tu na sio halisi. Kwa mfano, mwanafalsafa wa Kigiriki Plato (428-348 KK) alisema kuwa ulimwengu wa kila siku wa kubadilika badilika, ambao mtu huja kujua kwa kutumia akili zake, sio ukweli wa msingi, lakini ni ulimwengu wa kivuli na sio halisi. Wengine wengi, kama ilivyoelezwa hapo awali, walidai na kuendelea kudai kwamba hakuna kusudi la kuumbwa kwa binadamu hata kidogo. Kulingana na wao, kuwepo kwa binadamu ni jambo la kibahati tu. Hatuwezi kuwa na lengo kama maisha yamebadilika kutokana na kipengele kisicho na uhai kilichokuja kuwa hai tu kwa bahati. Wanaodhaniwa kuwa 'binamu wa binadamu 'tumbili na nyani, hawasumbuliwi na maswali ya kuwepo kwao, basi kwa nini wanadamu wanapaswa kuwa na wasiwasi nao?
Ingawa watu wengi huweka swali la kwa nini tumeumbwa kando baada ya kutafakari kwa muda mfupi, ni muhimu sana kwa wanadamu kujua jibu. Bila ujuzi wa jibu sahihi, wanadamu hawawezi kutofautishwa na wanyama wengine waliowazunguka. Mahitaji ya wanyama na tamaa za kula, kunywa na kuzaa huanza kuwa lengo la kuwepo kwa binadamu, na juhudi za kibinadamu zinalenga uwanja huu mdogo. Utimizaji wa mahitaji ya kimwili unapokuwa lengo muhimu zaidi katika maisha, kuwepo kwa binadamu kunakosa maana na mwanadamu huwa na kiwango kama cha wanyama wa chini kabisa. Wanadamu watatumia vibaya akili zao walizopewa na Mungu wanapokosa kuelewa lengo lao la kuishi. Akili ya binadamu itatumia uwezo wake kuunda madawa ya kulevya na mabomu na itajihusisha na uasherati, ngono, ushoga, urogi, kujiua, nk. Kwa kutoelewa madhumuni ya maisha, kuwepo kwa binadamu kunapoteza maana yake yote na hivyo hupotea, na malipo ya uzima wa milele wa Furaha katika Akhera hupotea kabisa. Kwa hivyo, ni muhimu sana kwa mwanadamu kujibu kwa usahihi swali la “Kwa nini tuko hapa?”
Binadamu mara nyingi hugeuka kwa wanadamu wenzao ili kupata majibu. Hata hivyo, mahali pekee ambapo majibu ya wazi na sahihi ya maswali haya yanaweza kupatikana ni katika vitabu vya ufunuo wa Mungu. Ilikuwa ni dharura Mungu aeleze lengo la maisha kwa binadamu kupitia manabii Wake, kwa sababu binadamu hawawezi kupata majibu sahihi kivyao. Manabii wote wa Mungu waliwafundisha wafuasi wao majibu ya swali la “Kwa nini Mungu aliumba mwanadamu?”
Ongeza maoni