Kusudi la Uumbaji (sehemu ya 3 kati ya 3): Tamaduni za Kihindu
Maelezo: Utangulizi kwa swali la kushangaza zaidi katika historia ya binadamu, na mjadala kuhusu vyanzo ambavyo vinaweza kutumika kupata jibu. sehemu ya 3: Uchunguzi wa Maandiko ya Kihindu, na hitimisho kwa jambo hilo.
- Na Dr. Bilal Philips
- Iliyochapishwa mnamo 10 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 3,495 (wastani wa kila siku: 3)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Kila kitu ni Mungu
Maandiko ya Kihindu yanafundisha kwamba kuna miungu mingi, umwilisho wa miungu, watu ambao ni Mungu na kwamba kila kitu ni Mungu, Brahman. Licha ya imani kwamba nafsi (atman) za viumbe vyote vilivyo hai ni Brahman, mfumo wa matabaka wenye ukandamizaji uliibuka ambapo Brahmans wenye matabaka ya kuhani, waadhama wa kiroho tangu kuzaliwa kwao. Wao ni walimu wa Vedas na wanawakilisha ubora wa usafi wa ibada na ufahari wa kijamii. Kwa upande mwingine, tabaka la Sudra linatengwa kutoka kwa hadhi ya kidini na wajibu wao wa pekee katika maisha ni “kutumikia kwa unyenyekevu” matabaka mengine matatu na maelfu ya matabaka ndogo ndogo yanayokuja chini yao.
Kulingana na wanafalsafa wa Kihindu, lengo la wanadamu ni kutambua utukufu wao na kufuata njia (marga) ya kuelekea ukombozi (moksha) kutoka gurudumu la kuzaliwa upya -kufufuka kwa nafsi ya binadamu (atman) katika ukweli wa mwisho ambao ni Brahman. Kwa wale wanaofuata njia ya bhakti, lengo ni kumpenda Mungu kwa sababu Mungu aliumba binadamu “kufurahia uhusiano - kama baba anavyofurahia watoto wake” (Srimad Bhagwatam). Kwa Hindu wa kawaida, lengo kuu la maisha ya kidunia liko katika kuendana na majukumu ya kijamii na ibada, kwa sheria za jadi za maadili kwa ajili ya tabaka la mtu - njia ya karma.
Ingawa sehemu kubwa ya dini ya maandiko ya Vedic, ambayo yanahusu mila ya sadaka kwa moto, imefichwa na mafundisho ya Kihindu yanayopatikana katika maandiko mengine, mamlaka kamili na utakatifu wa Veda bado ni nguzo kuu kwa takriban madhehebu na mila zote za Kihindu. Veda inajumuisha makusanyo manne, ya zamani zaidi ikiwa ni Rigveda (“Hekima ya Mistari”). Katika maandiko haya, Mungu anaelezwa kwa maneno yanayochanganya sana. Dini inayojitokeza katika Rigveda ni ushirikina hasa unaohusisha miungu yenye kupendeza inayohusishwa na anga na hewa , na ya muhimu zaidi ikiwa Indra (mungu wa mbingu na mvua), Baruna (mlezi wa utaratibu wa anga), Agni (moto wa dhabihu au kafara), na Surya (jua). Katika maandiko ya baadaye ya Vedic, dhima ya miungu ya mapema ya Rigvedic inapungua, na ushirikina huanza kubadilishwa na kafara kwa ulimwengu (pantheism) na mungu wa viumbe vyote (Prajapati). Katika Upanishad (mafundisho ya siri kuhusu utaratibu wa ulimwengu), Prajapati inaungana na dhana ya Brahman, ukweli mkuu na kiini cha ulimwengu, na kuchukua nafasi ya utambulisho wowote maalum, hivyo kubadilisha kisasili kiwe falsafa halisi. Ikiwa yaliyomo katika maandiko haya yangekuwa yote ambayo binadamu alipaswa kuchagua ili kupata uongozi, binadamu angepaswa kudhani kuwa Mungu alijificha Yeye mwenyewe pamoja na lengo la uumbaji kutoka kwa wanadamu.
Mwenyezi Mungu si mwenye kuchanganya wala hataki ugumu kwa watu. Kwa hivyo alipofunua mawasiliano yake ya mwisho kwa wanadamu miaka elfu moja mia nne iliyopita, Alihakikisha kwamba ilihifadhiwa kikamilifu kwa vizazi vyote vya binadamu vijavyo. Katika maandiko hayo ya mwisho, Qurani (Kurani), Mungu alifunua kusudi lake la kuumba wanadamu, na kupitia kwa njia ya nabii wake wa mwisho, alifafanua maelezo yote ambayo mwanadamu angeweza kuelewa. Ni kwa misingi ya ufunuo huu na maelezo ya kinabii ndipo [lazima] tuchambue majibu sahihi ya swali “Kwa nini Mungu aliumba mwanadamu?”...
Ongeza maoni