Matendo ya Utu kwa Wanyama

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Huruma na rehema ya Uislamu sio tu inamuhusu binadamu, lakini pia inaenea kwa viumbe vyote ulimwenguni.

  • Na Imam Mufti
  • Iliyochapishwa mnamo 14 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 11 Dec 2023
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 4,092 (wastani wa kila siku: 4)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Humane_Treatment_of_Animals_001.jpgMungu, Muumba wa wanadamu na wanyama, amewafanya wanyama kuwa watiifu kwetu. Tunawategemea wanyama kwa chakula tunachokula na maziwa tunayokunywa. Tunawaleta wanyama ndani ya nyumba zetu kwa upendo na kushirikiana nao. Tunaokoka na magonjwa makubwa na tunaishi kwa muda mrefu kwa sababu ya utafiti wa matibabu kuhusu wanyama. Tunatembelea mbuga za wanyama na tangisamaki kupata kuukubali utofauti wa kuvutia wa maisha ya hapa duniani. Tunafaidika na mbwa waliofunzwa kikamilifu katika ugunduzi wa dawa za kulevya, kuongoza vipofu, na kusaidia walemavu. Mungu anasema kwenye Kurani:

"Na mifugo amekuumbieni nyinyi, wana (manyoya na ngozi zinazokupeni) joto na manufaa mengineyo, na katika hao mnakula (nyama zao). Nanyi mna kwao (hao mifugo) mandhari nzuri pale mnapowarudisha jioni (kutoka malishoni) na pale mnapowapeleka asubuhi (malishoni). Na hukubebeeni mizigo yenu mpaka mji msioweza kuufikia ila kwa mashaka ya nafsi. Hakika Mola wenu ni Mwenye kukuhurumieni, Mrehemevu. (Na amekuumbieni) farasi na nyumbu na punda ili muwapande na (wawe) pambo (kwenu), na ameumba (vipando vyenginevyo) msivyovijua. " (Kurani 16:5-8)

Rehema ya Uislamu inaenea zaidi ya wanadamu kwa viumbe vyote vilivyo hai vya Mungu. Uislamu unakataza ukatili kwa wanyama. Miaka elfu moja na mia nne iliyopita, muda mrefu kabla ya harakati za kisasa za haki za wanyama kuanza na kuchapishwa katika kitabu cha Peter Singer, "Ukombozi wa Wanyama," mnamo 1975, Uislamu ulihitaji ukarimu kwa wanyama na kwa kuwafanyia ukatili ikiwa sababu ya kutosha ya mtu kutupwa motoni!

Kipindi fulani, Mtume wa Rehema alizungumza juu ya msamaha wa Mungu kwa sababu ya vitendo vya kibinadamu kwa wanyama. Aliwaambia wenzake hadithi ya mtu ambaye alikuwa na kiu njiani. Alipata kisima, aketeremka chini ndani yake hadi kwenye maji, na akakata kiu. Alipotoka nje alimuona mbwa anayetokwa na machozi akilamba tope kwa kiu kali. Mwanamume huyo aliwaza moyoni mwake, ‘Mbwa amekuwa na kiu kama mimi!’ Mtu huyo alishuka tena kwenye kisima na akampatia mbwa huyo maji. Mungu alithamini kazi yake nzuri na akamsamehe. maswahaba wake wakauliza , ‘Mtume wa Mungu, je tunapata thawabu kwa kuwatendea wema wanyama?’ Akasema, ‘Kuwa thawabu katika (kufafanya wema kwa) kila kiumbe.’[1]

Katika tukio lingine, Mtume Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, alielezea adhabu ya Mungu kwa mwanamke ambaye alitupwa Jahannamu kwa sababu ya paka. Alimuweka kwa kumfungia, hakumlisha wala kumuacha huru ili akajilishe mwenyewe.[2]

Uislamu uliweka kanuni za uchinjaji wa kiutu. Uislamu unasisitiza kwamba njia ya kuchinja inapaswa kuwa ile ambayo sio chungu zaidi kwa mnyama. Uislamu unahitaji chombo cha kuchinjia kisinolewe mbele ya mnyama. Uislamu pia unakataza kuchinja mnyama mmoja mbele ya mwingine. Katu, kabla ya Uislamu, ulimwengu haukushuhudia kujali kama huku kwa wanyama.

Matendo ya utu kwa wanyama yanaweza kufupishwa kama ifuatayo:

Kwanza, Uislamu unahitaji kuwa wanyama-pendwa au wanyama wa shamba wapewe chakula kizuri, maji, na mahali pa kuishi. Pindi Mtume alipopita karibu na ngamia aliyekonda kwa sababu ya njaa, alisema:

"Mcheni Mungu kwakuzingatia wanyama hawa ambao hawawezi kusema kwa mapenzi yao. Ikiwa unawaendesha, watibu ipasavyo (kwa kuwafanya wawe na nguvu na kama hayo), na ikiwa unapanga [kula], watibu ipasavyo (kwa kuwafanya wanene na kuwa na afya njema)." (Abu Dawud)

Pili, mnyama hapaswi kupigwa au kuteswa. Mara tu Mtume wa Rehema alipita karibu na mnyama aliyepigwa chapa usoni. Alisema, 'Je! Haijakufikia kwamba nimemlaani yule anayeweka alama kwenye uso wa mnyama au kumpiga kwenye uso wake?'[3] Nabii wa Rehema alimshauri mkewe kumwendea ngamia mwenye fujo aliyempanda kwa upole.[4] Kufanya wanyama wapigane wao kwa wao kama burudani pia ilikatazwa na Mtume.[5]

Tatu, Uislamu unakataza kutumia wanyama au ndege kama shabaha wakati wa kufanya mazoezi ya kupiga risasi. Wakati Ibn Umar, mmoja wa masahaba wa Mtume Muhammad alipoona watu wengine wakifanya mazoezi ya upinde wakitumia kuku kama shabaha, alisema:

"Mtume alimlaani mtu yeyote ambaye alifanya kitu kilicho hai kuwa shabaha(kwa mazoezi)."

Mtume Muhammad pia amesema:

"‘Yeyote anayeua ndege au kitu kingine chochote bila haki yake, Mungu angemuuliza juu yake. ’Ikasemwa:‘ Ewe Mjumbe wa Mungu! Ni haki gani inayostahili? ’Akasema:‘ Kumuua kwa chakula… na usikate kichwa chake, na kukitupa!’" (Targheeb)

Upigaji risasi wa njiwa walio hai kipindi fulani ilikuwa mchezo wa Olimpiki na leo kupiga risasi njiwa kunaruhusiwa katika maeneo mengi.

Nne, kuwatenganisha vifaranga kutoka kwa mama zao hairuhusiwi katika Uislamu.

Tano, ni marufuku kumkata mnyama masikio, mkia au sehemu zingine za mwili bila sababu maalumu.

Sita, mnyama mgonjwa aliye chini ya uangalizi wa mtu anapaswa kutibiwa vizuri.

Kupitia sheria na kanuni hizi zilizowekwa kisheria kuhusu wanyama, Waislamu wanapata heshima na ufahamu wa kuwa viumbe wengine hawatakiwi kutumiwa na kunyanyaswa kwa mapenzi ya mtu, lakini kuwa wao wapo, kama wanadamu, wana haki ambazo wanapaswa kupewa ili kuhakikisha kuwa haki na rehema ya Uislamu itimizwe kwa wote wakaao hapa duniani.



Rejeleo la maelezo:

[1] Saheeh Al-Bukhari

[2]Saheeh Al-Bukhari

[3]Abu Dawud, Saheeh Muslim

[4] Saheeh Muslim

[5]Abu Dawud, Al-Tirmidhi

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.