Madai ya Muhammad katika Utume (sehemu ya 3 kati ya 3): Je, Alikuwa Mwendawazimu, Mshairi, au Mchawi?
Maelezo: Ushahidi wa madai kuwa Muhammad alikuwa nabii wa kweli na siyo muongo. Sehemu ya 3: Uchunguzi wa madai mengine ya uwongo yaliyotolewa na wakosoaji.
- Na Imam Mufti
- Iliyochapishwa mnamo 24 Nov 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 4,524 (wastani wa kila siku: 4)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Alikuwa Mwendawazimu?
Mtu ambaye amejihusisha na wagonjwa wa akili anajua kuwa watu wanaweza kutambuliwa kutokana na dalili zao. Muhammad hakuonyesha dalili zozote za ukichaa kipindi chochote cha maisha yake Hakuna rafiki, mke, au mwanafamilia aliyemshuku au kumwacha kwa sababu ya wazimu. Na kuhusu athari za Mtume kupokea ufunuo, kama vile kutokwa na jasho na mengine kama hayo, ilitokana na uzito wa Ujumbe ambao alilazimika kuubeba na sio kutokana na kifafa au tukio la ukichaa...
Kinyume chake kabisa, Muhammad alihubiri kwa muda mrefu na kuleta Sheria isiyojulikana katika ukamilifu wake na ugumu wake kwa Waarabu wa kale. Ikiwa nabii alikuwa mwendawazimu, ingekuwa dhahiri kwa wale walio karibu yake wakati mmoja katika kipindi cha miaka ishirini na tatu. Ni lini katika historia mtu mwendawazimu alihubiri ujumbe wake wa kumwabudu Mungu Mmoja kwa muda wa miaka kumi, mitatu ambayo yeye na wafuasi wake walikaa uhamishoni, na hatimaye akawa mtawala wa nchi yake? Ni mwendawazimu gani amewahi kuziteka nyoyo na akili za watu waliokutana naye na kupata heshima ya wapinzani wake?
Zaidi, masahaba wake wa karibu, Abu Bakr na Umar walitambuliwa kwa uwezo wao, uungwana, ujuzi, na uhodari. Walikuwa tayari kutoa chochote kwa ajili ya dini aliyoileta. Wakati mmoja, Abu Bakr, alileta mali zake zote anazomiliki kwa Muhammad, rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na alipoulizwa alichowaachia familia yake, akajibu, ‘Niliwaachia Mungu na Mtume Wake!’
Abu Bakr, mfanyabiashara kwa taaluma, baada ya kuchaguliwa kuwa mtawala wa Waarabu wote baada ya Muhammad, alitumia dirhamu mbili tu juu yake na familia yake!
Umar akawa mtawala wa Uarabuni baada ya Abu Bakr na akaiteka Syria, Misri, na kuzitiisha Dola za Uajemi na Rumi. Alikuwa mtu anayejulikana kwa uadilifu wake. Je, mtu anawezaje kupendekeza watu hawa walikuwa wanamfuata mtu mwenye kichaa?
Mungu anapendekeza: simama mbele ya Mungu bila upendeleo au imani zilizotungwa hapo awali, na ujadiliane na mtu mwingine au ulifikirie mwenyewe, mtume huyu hana wazimu, yuko thabiti leo kama ulivyomjua kwa miaka arobaini.
"Sema: Mimi nakunasihini kwa jambo moja tu - ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili-wawili na mmoja-mmoja; kisha mfikiri. Mwenzenu huyu hana wazimu. Yeye si chochote ila ni Mwonyaji kwenu kabla ya kufika adhabu kali.’" (Kurani 34:46)
Watu wa Makka wa zamani walikataa mwito wake kutokana na ushabiki wa kikabila, na hawakuwa wakweli katika shutuma zao za kichaa chake. Hata leo, watu wengi wanakataa kumkubali Muhammad kama nabii kwa sababu tu alikuwa Mwarabu na kujifariji wenyewe kwa kusema lazima alikuwa mwendawazimu au alifanya kazi na shetani. Chuki yao kwa Waarabu inatafsiri katika kumkataa kwao Muhammad, ingawa Mwenyezi Mungu anasema:
"Bali huyu amekuja kwa Haki, na amewasadikisha Mitume." (Kurani 37:37)
Ingawa Waarabu wapagani walimjua Muhammad vizuri sana, lakini bado walimtupia tuhuma za ukichaa, kwakuwa waliichukulia dini yake kuwa ni kufuru dhidi ya mapokeo ya wazee wao.
"Na wanapo somewa Aya zetu zilizo wazi wanasema: Huyu si chochote ila ni mtu anaye taka kukuzuieni na waliyo kuwa wakiabudu baba zenu. Na wakasema: Haya si chochote ila ni uwongo ulio zuliwa. Na walio kufuru waliiambia Haki ilipo wajia: Haya si chochote ila ni uchawi ulio dhaahiri. Wala hatukuwapa Vitabu wavisome, wala hatukuwatumia Mwonyaji kabla yako wewe. Na walikadhibisha walio kuwa kabla yao. Na hawakufikilia hata sehemu moja katika kumi ya tulivyo wapa hao. Nao waliwakadhibisha Mitume wangu. Basi kuangamiza kwangu kulikuwa namna gani!" (Kurani 34:43-45)
Alikuwa Mshairi?
Mwenyezi Mungu anataja tuhuma zao ndani ya Kurani na anajibu:
"Au wanasema: Huyu ni mtunga mashairi, tunamtarajia kupatilizwa na dahari. Sema: Tarajieni, na mimi pia ni pamoja nanyi katika kutarajia. Au hizo akili zao ndio zinawaamrisha haya, au wao basi ni watu majeuri tu? Au ndio wanasema: Ameitunga hii! Bali basi tu hawaamini!" (Kurani 52:30-33)
Mwenyezi Mungu anawaeleza washairi wa wakati huo ili Mtume afananishwe nao:
"Na watungaji mashairi ni wapotofu ndio wanawafuata. Je! Huwaoni kwamba wao wanatangatanga katika kila bonde?[1], Na kwamba wao husema wasiyo yatenda? Isipo kuwa wale walio amini, na wakatenda mema, na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na wakajitetea wanapo dhulumiwa. Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka." (Kurani 26:224-227)
Washairi wa Kiarabu walikuwa mbali zaidi na ukweli, waliongelea juu ya mvinyo, wanawake, vita, na tafrija, tofauti na Mtume ambaye analingania kwenye tabia njema, kumtumikia Mwenyezi Mungu, na kuwasaidia masikini. Muhammad alifuata mafundisho yake kabla ya mtu mwingine yeyote tofauti na washairi wa zamani au wanafalsafa wa siku hizi.
Kurani aliyoisoma Mtume ilikuwa tofauti na mashairi yoyote kwa mtindo wake. Waarabu wa wakati huo walikuwa na sheria kali kuhusiana na mahadhi, kibwagizo, silabi na hitimisho la kila ubeti wa ushairi. Kurani haikuafikiana na kanuni zozote zilizokuwa zikijulikana kwa wakati huo, lakini wakati huo huo, ilishinda aina yoyote ya maandiko ambayo Waarabu waliwahi kuyasikia. Baadhi yao walikuwa waislam baada ya kusikia Aya chache tu za Kurani , kutokana na ujuzi wake kuwa kiini cha kitu kizuri ambacho hakiwezi kutengenezwa na kiumbe yeyote.
Muhammad hakujulikana kamwe kuwa mkutunga shairi kabla ya Uislamu au baada ya utume. Bali Mtume alichukia sana jambo hilo. Mkusanyiko wa kauli zake, unaoitwa Sunna, umehifadhiwa madhubuti na upo tofauti kabisa katika maudhui yake ya kifasihi ukilinganisha na Kurani . Ghala la mashairi ya Kiarabu halina nakala zozote za Muhammad.
Alikuwa Mchawi?
Mtume Muhammad hakuwahi kujifunza wala kufanya uchawi. Badala yake, alilaani kitendo cha uchawi na kuwafundisha wafuasi wake jinsi ya kutafuta ulinzi dhidi yake.
Wachawi wana uhusiano mkubwa na shetani. Ushirikiano wao unawaruhusu kudanganya watu. Mashetani hueneza uwongo, dhambi, uchafu, uasherati, uovu, na kuharibu familia. Kurani inabainisha wale ambao mashetani huwashukia:
"Je! Nikwambieni nani wanawashukia Mashet'ani? Wanamshukia kila mzushi mkubwa mwingi wa dhambi. Wanawapelekea yale wanayo yasikia; na wengi wao ni waongo." (Kurani 26:221-223)
Mtume Muhammad alijulikana na kutambuliwa kuwa mtu mwadilifu mkweli wa neno lake ambaye hakujulikana kuwa amewahi kusema uwongo. Aliamrisha maadili mema na adabu njema. Hakuna mchawi katika historia ya kidunia aliyeleta maandiko kama ya Kurani au Sheria kama yake.
Vielezo-chini:
[1]Maneno ya nahau hutumika, kama wasemavyo wengi, kuelezea kuchanganyikiwa au kutokuwa na lengo - na mara nyingi kujipinga - kucheza na maneno na mawazo. Katika muktadha huu, inakusudiwa kusisitiza utofauti kati ya usahihi wa Kurani , ambayo hauna migongano yote ya ndani, na ubatili ambao mara nyingi unapatikana katika ushairi.
Ongeza maoni