Ushindi wa Warumi na Sehemu ya Chini kabisa Ardhini

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Kurani yaeleza kuhusu eneo la chini kabisa ardhini.

  • Na Sherif Alkassimi (© 2008 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 23 Nov 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 17 Jul 2022
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 3,446 (wastani wa kila siku: 3)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

The_Victory_of_the_Romans_and_the_Lowest_Point_on_Earth_001.jpgMwanzoni mwa karne ya 7, Falme mbili zenye nguvu zaidi wakati huo zilikuwa Ufalme wa Byzantium [1] na Ufalme wa Kiajemi. Katika miaka ya 613 - 614 B.K, Falme hizo mbilizilikwenda vitani, na Warumi wakashindwa vikali mikononi mwa Waajemi. Dameski na Yerusalemu zote zilitawaliwa na Waajemi. Katika sura ya Warumi, kwenye Kurani Takatifu, inasemekana kuwa Warumi walikuwa wameshindwa vibaya ila hivi karibuni wangepata ushindi:

“Warumi wameshindwa, Katika nchi iliyo karibu. Nao baada ya kushindwa kwao watashinda. Katika miaka michache. Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake.” (Kurani 30:2-4)

Aya hizi hapo juu, zilifunuliwa karibu na 620 B.K, takriban miaka 7 baada ya Warumi wakristo kushindwa vikali mikononi mwa Waajemi wanaoabudu sanamu katika miaka ya 613 — 614 B.K. Kwa kweli, Warumi walikuwa wameshindwa vibaya sana hadi ilionekana vigumu kwa Dola yenyewe kudumisha hata uwepo wake, tupilia mbali kuwa na ushindi tena.

Sio tu Waajemi, lakini pia Waavari, Waslavi na Walombadi (sehemu hizi ziko Kaskazini na Magharibi ya Dola ya Warumi) walihatarisha pakubwa uhuru wa Dola ya Warumi. Waavari walikuwa wamefika hadi kuta za Konstantinopo na walikuwa karibu wamteke Mfalme mwenyewe. Magavana wengi walikuwa wamemwasi Mfalme Heraclius, na Dola ilikuwa karibu kuanguka. Mesopotamia, Syria, Palestina, Misri na Armenia, ambazo hapo awali zilikuwa chini ya Utawala ya Warumi, zilivamiwa na Waajemi. Kwa kifupi, kila mtu alikuwa anatarajia Dola ya Warumi kuharibiwa, lakini kwa wakati huo aya za kwanza za sura ya Warumi zilifunuliwa kutangaza kwamba Warumi wangeweza kurejea na kushinda katika muda wa miaka michache. Muda mfupi baada ya ufunuo huu, Mfalme wa Byzantium aliagiza dhahabu na fedha zote katika makanisa kuyeyushwa na kugeuzwa kuwa pesa ili kukidhi gharama zinazohitajika za jeshi, na kugharamia vita zake ili kurejesha maeneo yaliyopotea.

Karibu miaka 7 baada ya ufunuo wa aya za kwanza za sura ya Warumi, Mnamo mwezi wa Desemba, 627 B.K, vita vilitokea kati ya Dola ya Byzantium na Dola ya Kiajemi katika eneo karibu na Bahari ya Chumvi, [2] na wakati huu ilikuwa ni jeshi la Byzantium ambalo liliwashinda Waajemi. Miezi michache baadaye, Waajemi walilazimika kufanya mkataba na Warumi ambao uliwalazimisha kurudisha maeneo waliyoyachukua kutoka kwao. Kwa hivyo, mwishoni, ushindi wa Warumi uliotangazwa na Mungu katika Kurani ulikuja kutimia kwa njia ya kimiujiza.

Muujiza mwingine uliofunuliwa katika aya zilizotajwa ni kutangazwa kwa taarifa ya kijiografia ambao hakuna mtu angeweza kugundua katika kipindi hicho. Katika aya ya tatu ya sura ya Warumi, ilitajwa kuwa Warumi walishindwa katika nchi iliyo chini kabisa, na kwa tafsiri nyingine, “katika nchi iliyo karibu ” (Kurani 30:3). Kwa kiasi kikubwa, mahali ambapo vita kuu vilifanyika (huko Dameski na Yerusalemu) viko katika eneo kubwa la ardhi iliyo chini inayoitwa Bonde Kuu la Ufa. Bonde Kuu la Ufa ni ufa mkubwa wa kilomita 5,000 katika ukonde wa ardhi unaotoka kaskazini ya Syria katika Mashariki ya Kati ya Asia hadi Msumbiji, Afrika Mashariki. Ncha ya kaskazini inapitia Syria, Lebanon, Palestina na Yordani. Ufa huo unaendelea kusini hadi Ghuba ya Aden, kisha kupitia Afrika ya Mashariki, halafu hatimaye unaishia kwenye bonde la chini la mto Zambezi nchini Msumbiji.

Taarifa ambalo limegunduliwa hivi karibuni, kwa usaidizi wa picha za satelaiti, ni kwamba eneo karibu na Bahari ya Chumvi (liko katika Bonde Kuu la Ufa ) ndilo la chini kabisa duniani. Eneo la chini kabisa duniani ni mwambao wa Bahari ya Chumvi, lenye urefu wa karibu mita 400 [3] chini ya usawa wa bahari. Ya kwamba ni eneo la chini kabisa ina maana kwamba maji haitoki baharini. Hakuna sehemu ya ardhi duniani iliyo chini kabisa kuliko mwambao wa Bahari ya Chumvi.[4]

Dead Sea Rift Valley

Bonde la Ufa la Bahari ya Chumvi, Israeli na Yordani Oktoba 1984. Kinachoonekana kutoka urefu wa maili 190 za bahari (kilomita 350) katika picha hii iliyo wima, ni Bonde la Ufa la Bahari ya Chumvi linalotoka kusini kuelekea kaskazini kupitia Mashariki ya Kati. Sakafu ya Bahari ya Chumvi, futi 1292 (mita 394) chini ya usawa wa bahari, ni sehemu ya chini kabisa duniani. (Kwa hisani ya: Maabara ya Sayansi na Uchambuzi wa Picha, Kituo cha Anga cha NASA cha Johnson , Picha #: STS41G-120-56, http://eol.jsc.nasa.gov)

Kwa hivyo inabainika kuwa nchi au mkoa kwenye bonde la ufa karibu na Bahari ya Chumvi ndio inayozungumziwa katika Kurani kuwa ndio “ardhi ya chini kabisa.” Hii ni miujiza ya kweli ya Kurani kwa sababu hakuna mtu aliyeweza kujua au kutabiri ukweli huo katika karne ya 7 kutokana na ya kwamba satelaiti na teknolojia ya kisasa hazikupatikana wakati huo. Kwa mara nyingine tena, maelezo pekee yanayowezekana ni kwamba Mtume Muhammad, rehma ziwe juu yake, alikuwa amepokea ufunuo kutoka kwa Mungu, Muumba na Mwanzilishi wa ulimwengu.



Footnotes:

[1] Warabu pia huita Byzantium kama nchi ya Warumi.

[2] Historia ya Uajemi Sehemu ya I: Uajemi ya Kale ya Watu wa Scott

[3] (http://hypertextbook.com/facts/2000/SanjeevMenon.shtml)

[4] (http://www.elnaggarzr.com/index.php?l=ar&id=51&cat=6)

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.