Dawood Kinney, Mkatoliki wa Zamani, Marekani
Maelezo: Baada ya kujiingiza katika anasa za vijana wengi, Dawood anapata imani yake katika Uislamu baada ya kukataliwa na Kanisa Katoliki.
- Na Dawood Kinney
- Iliyochapishwa mnamo 14 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 2,551 (wastani wa kila siku: 2)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Kadiri ninavyoweza kukumbuka nilipokuwa mtoto, nakumbuka nikishangazwa daima na ulimwengu huu tunamoishi; jinsi kila kitu kinavyofanya kazi kikamilifu. Nilikuwa nikilala nje usiku juu ya bustani ya wazazi wangu, nikitazama nyota, nikishangazwa na ukubwa usiojulikana wa mbingu. Na pia nilikuwa nikishangazwa na jinsi mwili wa mwanadamu ulivyofanya kazi pamoja, moyo unapiga, huku mapafu yakileta hewa, bila msaada kutoka kwangu. Na tangu wakati huo, nilijua siku zote, kuwa kulikuwa na Muumba anayeshughulikia na kuhusika na yote haya.
Lakini nilipokua na kufikia ujana, ilikuwa rahisi sana kushindwa na msongo wa marika, na nilipoteza matumaini kwa mambo ya Mungu na badala yake nikazama katika unywaji pombe, ngono na michezo ya hapa na pale ya kijana anayekulia Marekani. Nilipoendelea kukua, tamaa yangu ikawa ni fedha, nguvu, nyumba bora, gari yenye kasi, na mwanamke mzuri - shughuli ambazo hazina maana kubwa.
Niliishi hivyo kwa miaka mingi, nikipoteza polepole udhibiti wa maisha yangu, nikifikiri nilikuwa nikitafuta furaha, huku yote niliyokuwa nikiyapata ni huzuni zaidi, kuchanganyikiwa, na kuharibu maisha yangu.
Kwa wakati mmoja, nilishindwa kudhibiti maisha yangu na kupoteza matumaini. Itikio langu la kwanza lilikuwa ni kugeuka kwa Mungu, na, kwa kuwa nililelewa Kikatoliki, niligeuka kwa kanisa hilo. Wakati huo, nilikuwa nimemtaliki mke wangu na kuoa tena na nikakuja kujua kwamba Kanisa Katoliki halikunitaka tena. Huku nikiwa na hasira na maumivu, lakini pia nikitambua haja ya kuwa na utaratibu wa kiroho katika maisha yangu, niligeuka kwa Ubuddha.
Dhehebu la kibuddha nililojihusisha nalo lilifuata mapokeo ya Kitibeti, ambapo umuhimu unawekwa kwa kupata uwezeshwaji, ambao kimsingi ni baraka kutoka kwa Wabudha mbalimbali. Baada ya muda fulani nilitambua kwamba kihakika sikuwa najiboresha kiroho, bali nilikuwa nikizunguka tu kote nikipata uwezeshwaji mbalimbali, huku nikifanya matambiko. Ghafla, nilitambua kwamba moja ya mambo ya mwisho ambayo Buddha alisema kabla ya kufa kwake ilikuwa kwamba hapaswi kuabudiwa. Nilitambua matambiko haya yote yalikuwa na MSINGI katika kumwabudu sio tu “Buddha”, lakini pia Wabuddha wengine wengi. Nilikata tamaa sana na kurejea kwa njia yangu ya zamani ya kujiingiza katika pombe na anasa. Na mara nyingine tena, nikawa na huzuni usioisha, ila mara hii ulikuja na madhara ya kihisia ambayo yalianza kujionyesha kwa njia za kutisha na za kujiangamiza.
Nilipokuwa kijana, nilipenda sana muziki wa Cat Stevens (kwa sasa Yusuf Islam). Niliposikia alisilimu, nilikuwa katika jeshi la wanamaji la Marekani wakati huo na hii ilikuwa wakati wa “mgogoro wa mateka” nchini Iran. Kwa hivyo, niliamini hapo hapo kuwa Cat Stevens ameshakuwa mgaidi, na nilikuwa na imani hiyo kwa miaka mingi.
Miezi michache iliyopita, nikasikia kwamba alikuwa anaenda kuongea kwenye televisheni, na nilitaka kusikia kuhusu mtu huyu wazimu ambaye alikuwa ameacha maisha mazuri na kuwa mgaidi. Naam, bila shaka, nilikuwa nimepigwa butwaa na mazungumzo hayo, kwa sababu hakuwa mgaidi, bali ni mtu aliyezungumza vizuri, mwenye amani, aliyetangaza upendo, na uvumilivu, na mantiki. Siku iliyofuata, nilianza kutafiti Uislamu kwenye mtandao. Niliona hotuba katika RealAudio ya ndugu, Khaled Yasin, na kusema kweli, hotuba hii ilinibadilisha sana.
Hotuba ya kwanza ya Ndugu Khaled ndio ilinibadilisha vizuri, lakini zingine mbili za ndugu Yusef (Cat Stevens) kwa kweli zinazungumza na sisi ambao hatukulelewa katika jamii ya Kiislamu. Kila kitu kilieleweka KIMANTIKI, uwepo wa Mungu ulikuwa RAHISI sana kueleweka! Ningewezaje kuwa mjinga wakati huu wote???
Nilivyojifunza zaidi ndivyo nilivyohakikisha kwamba hii ilikuwa kweli njia niliyokuwa nikitafuta. Ilikuwa na nidhamu ya kimwili, ya kiakili, na ya kiroho ambayo inamwelekeza mtu kwa amani na furaha ya kweli. Lakini muhimu zaidi, ina njia hiyo ya Mungu. Kutangaza Shahadda yangu ilikuwa hatua ua KUNADHIFISHA, na tangu wakati huo, nimekuwa, kwa mara nyingi ... nikilia na kulia na kulia. Uzuri ulioje!
Nimekaribishwa kwa mikono wazi na ndugu na dada zangu wote wa Kiislamu kutoka duniani kote; ninafurahia sana hili, nikijua kuwa, licha ya shida au changamoto zozote, nimezungukwa na familia yangu ya Kiislamu ambayo kamwe haitaniacha ilhali mimi ni mwislamu mwenzao. Hakuna kikundi kingine cha watu kilichowahi kunitendea hivyo.
Bado nina njia ndefu na ngumu sana mbeleni. Kukubali ukweli wa Uislamu ni sehemu rahisi, kutembea Njia Iliyo Nyooka ndio sehemu ngumu, hasa iwapo mtu alikuwa amejiweka imara katika jamii ya wasio waislamu. Lakini ninamwomba Mungu kila siku anipe nguvu na mwongozo, na ninachukua hatua moja kwa wakati, nikijaribu kuboresha Uislamu wangu kidogo kidogo kila siku.
Ongeza maoni