Mazungumzo katika Paradiso na Jahannamu (sehemu ya 2 kati ya 3): Malumbano na Majadiliano

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Mazungumzo zaidi yatakayo fanyika baina ya watu wa Peponi na watu wa Jahannamu.

  • Na Aisha Stacey (© 2012 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 11 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 4,336 (wastani wa kila siku: 4)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Malumbano baina ya watu wa Peponi na watu wa Motoni

conversationinParadise2.jpg Malumbano yanayojiri baina ya watu wa Peponi na watu ambao makaazi yao ni Moto wa Jahannamu yanatajwa katika sehemu kadhaa katika Kurani. Tunaposoma na kutafakari juu ya aya hizi tunapaswa kufikiria na kujaribu kujifunza kitu kutokana na kukata tamaa kwa wale wanaokabiliwa na hofu za motoni. Tunapaswa kuhisi hofu yao, na tujifunze kutokana na makosa yao. Kusoma kuhusu wao kwenye Kurani kunatuwezesha kuhisi maumivu yao lakini pia kunatuwezesha kuona jinsi tunavyoweza kuepuka mwisho huo kwa urahisi.

Wataulizana wao kwa wao peponi juu ya wakosefu (washirikina na makafiri): Ni nini kilicho kuleteeni Motoni? Watasema: Sisi hatukuwa miongoni mwa wale walio kuwa wakisali, wala hatukuwalisha mafakiri. Na tulikuwa tukisema kwa maneno ya upotovu, na tulikuwa tukiikanusha Siku ya kiyama, mpaka itufikie hakika ( kifo). (Kurani 74:40 -47)

Na watu wa Peponi watawanadia watu wa Motoni: Sisi tumekuta aliyo tuahidi Mola wetu Mlezi kuwa ni kweli. Je, na nyinyi pia mmekuta aliyo kuahidini Mola wenu Mlezi kuwa ni kweli? Watasema: Ndiyo! Basi mtangazaji atawatangazia: Laana ya Mwenyezi Mungu iwapate walio dhulumu. (Kurani 7:44)

Na watu wa Motoni watawaita watu wa Peponi: Tumimieni maji, au chochote alicho kuruzukuni Mwenyezi Mungu. Nao watasema: Hakika Mwenyezi Mungu ameviharimisha hivyo kwa makafiri, (Kurani 7: 50)

Inabainika kuwa mateso ya wakazi wa Jahannamu yatazidi kwa kuona na kusikia neema waliyopewa watu wa Peponi.

Mazungumzo baina ya watu wa Peponi

Maneno ya Mwenyezi Mungu katika Kurani yanatuambia kwamba watu wa Peponi wataulizana juu ya maisha yao ya zamani.

“Nao watafikiana, wakiulizana. Watasema: Tuliogopa kwa ahali zetu, lakini Mwenyezi Mungu ametuhurumia, na akatuokoa na adhabu ya Moto. (Kurani 52:25 -27)

Aya nyingi zinazoelezea mazungumzo miongoni mwa watu wa Peponi zinathibitisha kwamba wataendelea na tabia zao mema kwa kumsifu Mwenyezi Mungu na kumshukuru kwa neema alizowajalia. Ingawa walikuwa wameamini ahadi ya Mwenyezi Mungu kuwa ya kweli na hivyo kutenda mema ipasavyo, ufahari na ukubwa wa neema ya Pepo utawafanya wazidi kumshukuru Mola.

Na watasema: Alhamdulillahi, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliye tuondolea huzuni zote. Hakika Mola wetu Mlezi bila ya shaka ni Mwenye kusamehe, Mwenye shukrani. Ambaye kwa fadhila yake ametuweka makao ya kukaa daima; humu haitugusi taabu wala humu hakutugusi kuchoka. (Kurani 35:34-35)

Nao watasema: Alhamdulillah, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliyetutimizia ahadi yake, na akaturithisha ardhi, tunakaa katika Bustani popote tupendapo. Basi ni malipo mazuri yaliyoje ya watendao (Kurani 39:74)

Mazungumzo ya Watu wa Jahannamu baina yao

Na watu waliopangiwa kuishi milele katika Moto wa Jahannamu watashtushwa kwa kuwa sanamu au watu waliowaamini na wakawafuata hawawezi kuwasaidia. Na viongozi wanaoitwa 'wenye kiburi' katika Kurani wanaambia wafuasi wao kuwa wao wenyewe walikuwa wamepotea. Basi yeyote aliyewafuata, akawafuata katika maisha yasiyo na rehema.

Watakabiliana wao kwa wao kuulizana. Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia. Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini. Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu. Basi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu.Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu. (Kurani 37:27-32)

Na wote watahudhuria mbele ya Mwenyezi Mungu. Wanyonge watawaambia walio takabari: Sisi tulikuwa wafwasi wenu; basi hebu hamtuondolei kidogo hivi katika adhabu ya Mwenyezi Mungu? Watasema: Lau Mwenyezi Mungu angeli tuongoa basi hapana shaka nasi tungeli kuongoeni. Ni mamoja kwetu tukipapatika au tukisubiri; hatuna pa kukimbilia. (Kurani 14:21)

Na likihukumiwa jambo, yaani jambo la ni nani atakaye pelekwa Peponi, na nani atakaye elekezwa Jahannamu, mkaazi wa Jahannamu mwenye sifa mbaya kabisa, Iblisi mwenyewe, atafunua ukweli mkubwa. Ni ukweli ambao Mungu alitufunulia katika Kurani, lakini ambao watu wengi hawakuutilia maanani. Kwamba yeye, Shet'ani, alikuwa mwongo. Ahadi za Shetani hazikutimia kamwe, ahadi zake zilikuwa tupu na yeye mwenyewe alimwamini Mungu.

Na Shet'ani atasema itapo katwa hukumu: Hakika Mwenyezi Mungu alikuahidini ahadi ya kweli. Nami nalikuahidini; lakini sikukutimizieni. Na sikuwa na mamlaka juu yenu, isipo kuwa nilikuiteni, nanyi mkaniitikia. Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe. Mimi siwezi kuwa mtetezi wenu, wala nyinyi hamwezi kuwa watetezi wangu. Hakika mimi nilikataa tangu zamani kunishirikisha na Mwenyezi Mungu. Hakika madhaalimu watakuwa na adhabu chungu. (Kurani 14:22)

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.