Uzuri wa Uislamu (sehemu ya 1 kati ya 3): kutokuwa na elimu hauwezi Kuficha Uzuri na Ukweli
Maelezo: Maelezo mafupi ya baadhi ya uzuri wa Uislamu.
- Na Aisha Stacey (© 2012 IslamReligion.com)
- Iliyochapishwa mnamo 03 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 4,957 (wastani wa kila siku: 4)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Kwa wakati huu katika historia ya kiislamu, hata kama dini ya kiislamu inahukumiwa kwa matendo ya wachache, ni vizuri kutupilia mbali mabaya yanayoonyeshwa mtandaoni na vyombo vya habari na utathmini uzuri ambao ni kiungo kikuu cha maisha yanayotambulika kama uislamu. Kuna ukuu na utukufu katika Uislamu ambao mara nyingi hufunikwa na matendo ambayo hayana nafasi katika Uislamu au na watu ambao huzungumza juu ya mada ambazo hawaelewi kwa kina na kirefu. Uislamu ni dini, hulka na mienendo za maisha zinazo wahimiza waislamu wajitahidi na wafike mbali na watende yanayoridhisha wanao karibu nao na mbali na hayo yawe ya kuridhisha mwenyezu mungu aliyetuumba.
Uzuri wa Uislamu ni vitu hivyo ambavyo ni sehemu ya dini na hufanya Uislamu kuwa maarufu. Uislamu hujibu maswali yote ya milele ya wanadamu. Nilitoka wapi? Kwanini niko hapa? Je! Hii ndiyo yote kweli? Inajibu maswali haya kwa uwazi na kwa njia nzuri. Kwa hivyo basi, wacha tuanze safari yetu na kugundua na kutafakari juu ya uzuri wa Uislamu.
1. Majibu ya maswali yako yote juu ya maisha yako katika Kurani
Quran ni kitabu kinachoelezea utukufu wa Mungu na maajabu ya uumbaji wake pia ni ushuhuda wa Rehema na Uadilifu Wake. Sio kitabu cha historia, kitabu cha hadithi, au kitabu cha kisayansi ingawa ina aina zote hizo na zaidi. Korani ni zawadi kuu ya Mungu kwa wanadamu – ni kitabu kama hakuna kingine chochote, kwani ina majibu ya mafumbo ya maisha. Hujibu maswali na kutuuliza tuangalie zaidi ya kupenda mali na kuona kwamba maisha haya si ktu ila ni kama kusimama kwa muda mfupi kwenye njia ya uzima wa milele. Uislamu unatoa lengo wazi na kusudi la maisha. Na alivyonena mwenyezi katika kitabu chake alisema hivi
"Na mimi (Mungu) sikuwaumba majini na wanadamu, ila kuniabudu Mimi (Peke Yangu)." (Qur'ani tukufu 51:56)
Kwa hivyo ndicho kitabu cha muhimu zaidi na Waislamu hawana shaka kuwa ni sawa kabisa leo kama ilivyokuwa wakati ilipotremushwa kwa mara ya kwanza kwa Nabii Muhammad rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake. Tunapouliza maswali haya muhimu zaidi tunataka kuwa na uhakika kwamba majibu tunayopokea ni ya ukweli. Kujua kuwa majibu yanatoka kwa kitabu ambacho ni Neno la Mungu lisilobadilika wala kubadilishwa kwa hivyo inatia nafsi utulivu na kuipa faraja. Mungu alipoteremsha Kurani aliahidi kuihifadhi milele. Maneno tunayosoma leo ni sawa na yale hifadhiwa na kuandikwa na masahaba wa Nabii Muhammad.
"Sisi ndio tumeteremsha ukumbusho (yaani Qur'ani) na hakika sisi tutailinda na ufisadi." (Qur'ani Tukufu 15: 9)
2. Furaha ya kweli inaweza kupatikana katika Uislamu
Furahini na uwe na furaha endelea kuwa na nia na uwe na amani.[1] Hivi ndivyo Uislam hutufundisha kwani amri zote za Mungu zinazingatia kuleta furaha kwa mwanadamu. Ufunguo wa furaha ni katika kuelewa na kumwabudu Mungu. Ibada hii hutumika kama ukumbusho wake mwenyezi na inatuweka kila wakati tukimkumbuka na kwa hivyo tunajiepusha na maovu, kutenda dhuluma na kunyanyasa. Inatuinua kuwa waadilifu na wenye tabia njema. Kwa kufuata amri Zake, tunaishi maisha ambayo yanatuongoza kwa bora katika mambo yetu yote. Tunapoishi maisha ya maana kama hayo, basi na hapo tu ndipo tunaweza kuona furaha karibu nasi wakati wowote na hata nyakati ngumu zaidi. Ipo hata kwa kugusa mkono, katika harufu ya mvua au nyasi mpya zilizokatwa iko kwenye vuguvugu ya moto katika usiku wa baridi au upepo baridi siku ya joto. Raha zinaweza kufanya mioyo yetu kuwa na furaha ya kweli kwa sababu ni dhihirisho la Rehema na Upendo wa Mungu.
Hali ya kibinadamu inamaanisha kuwa kati ya huzuni kubwa kunaweza kuwa wakati wa furaha na wakati mwingine wakati wa kukata tamaa tunaweza kupata nanga katika vitu vinavyotuletea furaha. Mtume Muhammad alisema, “Kwa kweli mambo ya muumini ni ya kushangaza! Yote ni kwa faida yake. Akipewa wepesi basi anashukuru, na hii ni nzuri kwake. Na akikwazwa kwa magumu ya dunia, anavumilia, na hii ni nzuri kwake."[2]
3. Katika Uislamu tunaweza kuwasiliana na Mungu kwa urahisi wakati wowote wa mchana au usiku
Kila wanadamu huzaliwa bila kujua kwamba Mungu ni Mmoja. Lakini wale ambao hawajui jinsi ya kuwasiliana na Mungu au kuanzisha uhusiano naye huwa wanaona kuwapo kwao kutatanisha na wakati mwingine hata huwahuzunisha. Kujifunza kuwasiliana na Mungu na kumwabudu kunampa maisha maana mzima.
Kulingana na Uislamu, Mungu anapatikana wakati wowote na mahali popote. Tunahitaji kumwita tu na Yeye atajibu wito huo. Nabii Muhammad alitushauri tumwite Mungu kila wakati. Alituambia kwamba Mungu alisema;
"Mimi ni kama vile mtumwa Wangu anafikiria mimi, (yaani nina uwezo wa kumfanyia kile anachofikiria ninaweza kumfanyia) na niko pamoja naye ikiwa Ananikumbuka. Ikiwa ananikumbuka mimi mwenyewe, mimi pia, namkumbuka yeye mwenyewe. na ikiwa ananikumbuka katika kundi la watu, namkumbuka katika kundi ambalo ni bora zaidi kuliko wao, na ikiwa anakuja karibu na upana mmoja kwangu, ninaenda karibu naye dhiraa moja; na ikiwa anakuja karibu na dhiraa moja Kwangu, ninaenda umbali wa mikono miwili iliyonyooshwa karibu naye; na ikiwa anakuja kwangu akitembea, ninamkimbilia."[3]
Katika Qur'ani Mungu anasema, “Nikumbuke nami pia nitakukumbuka…” (Qur'ani 2: 152)
Waumini wanamwomba Mungu kwa lugha yoyote, wakati wowote na mahali popote. Wanamwomba Yeye, na wanashukuru. Waislamu pia husali kwa njia ya kiibada mara tano kila siku na cha kufurahisha neno la Kiarabu la sala ni 'salah', ambalo linamaanisha unganisho. Waislamu wameunganishwa na Mungu na wanaweza kuwasiliana naye kwa urahisi. Hatuko peke yetu au mbali na Rehema za Mungu, Msamaha na Upendo.
Ongeza maoni