Waislamu ni nani? (sehemu ya 2 kwa 2)
Maelezo: Zaidi ya bilioni ya watu kutoka asli zote, nchi na tamaduni – muendelezo wa Mchango wa Muislamu katika sayansi.
- Na islamuncovered.com
- Iliyochapishwa mnamo 04 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 4,637 (wastani wa kila siku: 4)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Jiografia
Wasomi wa kiislamu wamekuwa makini na jiografia. Kwa hakika, wasiwasi mkubwa wa Waislamu kwenye suala la jiografia kulitokana na dini yao. Kurani inawahimiza watu kusafiri ulimwenguni kuona ishara za Mwenyezi Mungu na miundo kila sehemu. Uislamu unamtaka kila Muislamu kupata elimu kidogo ya jiografia ili kujua mwelekeo wa Qiblah (mwelekeo wa Ka'bah ndani ya Makkah) ili uweze kuswali mara tano kwa siku. Waislamu pia wanauzoefu wa kusafiri mbali kufanya biashara pia kufanya Hajj na kusambaza dini yao. Himaya ya Kiislamu ya mataifa ya mbali iliwezesha wasomi-wachunguzi kukusanya kiwango kikubwa cha taarifa za kijiografia na hali ya hewa kuanzia Atlantiki hadi Pasifiki.
Moja ya majina maarufu kwenye upande wa jiografia, hata Magharibi, ni Ibn Khaldun na Ibn Batuta, wanatambulika kwa kazi zao zilizoandikwa kwa uchunguzi wao wa kina.
Ndani ya 1166, Al-Idrisi, Msomi wa Kiislamu aliyefahamika vizuri ambaye alihudumu kwenye mahakama ya Sicilian, alitengeneza ramani iliyo sahihi, ikiwemo ramani ya dunia ikiwa na mabara yote na milima yake, mito na miji maarufu. Al-Muqdishi alikuwa mwanajiografia wa kwanza kutengeneza ramani iliyo sahihi kwa rangi.
Ila ilikuwa, zaidi, kwa usaidizi wa mabaharia wa Kiislamu na vumbuzi zao ambazo Magellan aliweza kuzunguka Rasi ya Tumaini Zuri, na Da Gama na Columbus alikuwa na mabaharia wa Kiislamu kwenye safari yake katika meli.
Ubinadamu
Kutafuta maarifa ni jukumu la kila Muislamu, mwanaume na mwanamke. Vyanzo vikuu vya Uislamu, ni Kurani na Sunnah (Utamaduni wa Mtume Muhammad), Unawahamasisha Waislamu kutafuta maarifa na kuwa wasomi, kwani hii ndio njia bora ya kumjua Allah (Mungu), kuthamini uumbaji wake wa kustajabisha na kushukuru. Hivyo Waislamu walikuwa na tamaa ya kutafuta maarifa, yote ya kidini na kimaisha, na katika miaka michache ya kazi ya Muhammad, Jamii kubwa iliibuka na kung'aa. Matokeo yake kuenea kwa vyuo vya Kiislamu; Al-Zaytunah ndani ya Tunisia, na Al-Azhar ndani ya Cairo ukirudi nyuma miaka 1,000 kuna vyuo vya zamani utavikuta duniani. Hakika, vilikuwa mifano kwa vyuo vikuu vya mwanzo vya Ulaya, kama vile Bologna, Heidelberg,na Sorbonne. Hata shule zinazofahamika kofia na gauni asili yake ni chuo cha Al-Azhar.
Waislamu wamefanya maendeleo makubwa katika fani mbali mbali, kama vile jiografia, fizikia, kemia, hesabati, madawa, famasioloji, usanifu, isimu na unajimu. Aljebra na namba za Kiarabu zilitambulishwa na wasomi wa Kiislamu. Mnajimu, unne, na vifaa vingine vya usafiri na ramani vilitengenezwa na wasomi wa Kiislamu na kucheza sehemu maalumu kwaajili ya maendeleo ya ulimwengu, inayojulikana sana ndani ya zama za uvumbuzi wa Ulaya.
Wasomi wa Kiislamu waliisoma jamii ya kale kuanzia Ugiriki na Roma na India. Shughuli za Aristoto, Ptolemy, Euclid na wengine ilitafsiriwa kwa Kiarabu. Wasomi wa Kiislamu na wanasayansi kisha wakaongeza ubunifu wao wa mawazo, uvumbuzi na ugunduzi, mwisho kupeleka maarifa haya mapya Ulaya, iliyopelekea moja kwa moja kuwa na Muamko. Majadiliano mwengi ya kisayansi na tiba, yalitafsiriwa Kilatin, ilikuwa maandishi yenye vigezo na vitabu vya marejeo mwazo wa karne ya 17 na 18.
Hesabati
Inavutia kuona Uislam unalazimisha binaadamu kusoma na kuuchunguza ulimwengu. Kwa mfano, Kurani Tukufu inasema:
"Tutawaonyesha Ishara zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao wenyewe mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli." (Kurani 41:53)
Mualiko huu wa kuchunguza na kutafuta kumewafanya Waislamu wavutiwe na unajimu, hesabati, kemia, na sayansi nyingine, na walikuwa na uwelewa thabiti wa uhusiano wa jiometri, hesabati, na unajimu.
Waislamu walivumbua alama ya sifuri (neno "cipher" linatokana na Kiarabu sifr), na kuzikusanya namba kwenye mfumo wa desimali - msingi wa 10. Cha kuongezea, walivumbua alama kuonyesha thamani isiyojulikana, m.f. thamani kama ya x.
Mwanahesabati mkubwa wa Kiislamu, Al-Khawarizmi, alivumbua somo la algebra (al-Jabr), ambalo liliendelezwa na wengine, anaejulikana sana Umar Khayyam.kazi ya Al-Khawarizmi, katika tafsiri ya Kilatini, ilileta namba za Kiarabu ikiwa na hesabati huko Ulaya, kwa kupitia Hispania. Neno "algorithm" lilitoka katika jina lake.
Wanahisabati wa Kiislamu pia walibobea kwenye jiometri, kama tunavyoweza kuona kwenye usanii wa michoro, na alikuwa Al-Biruni (ndiye pia alibobea kwenye fani ya historia ya asili, hata jieology na mineloji) ambaye alianzisha trigonometri kama tawi tofauti la hesabati. Wanahesabati wengine wa Kiislamu walifanya maendeleo makubwa katika nadharia ya namba.
Madawa
Ndani ya Uislamu, mwili wa binadamu ni chanzo cha kuthamini, kwakuwa umeumbwa na Allah Mtukufu (Mungu). jinsi unavyofanya kazi, jinsi ya kuusafisha na kuwa salama, jinsi ya kuzuia magonjwa kutokana na kushambuliwa au kuponya magonjwa hayo, limekuwa jambo la umuhimu kwa Waislamu.
Mtume Muhammad, rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema:
"Mungu akuumba ugonjwa, ila aliuumbia kinga yake, ila umri. Ikiwa dawa itawekwa, mgonjwa atapona kwa ruhusa ya Mungu."
Hii ilikuwa motisha kubwa ya kuwahamasisha wanasayansi wa Kiislamu kuchunguza, kuendeleza, na kutumia sheria za kiuhakika. Umakini uliwekwa kwenye madawa na huduma za afya. Hospitali ya kwanza ilitengenezwa Baghdad ndani ya 706 AK. Waislamu pia walitumia mabanda ya ngamia kama hospitali ndogo, ambazo zilikuwa zinahama kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Tangu mwazo wa dini haikukataza, Wasomi wa Kiislamu walitumia wafu kusoma anatomia na fiziolojia na kuwasaidia wanafunzi wao kuelewa jinsi gani mwili unafanya kazi. Utafiti huu wa kuhakika uliwezesha fani ya upasuaji kukua kwa haraka.
Al-Razi, Anajulikana Magharibi kama Rhazes, daktari maarufu na mwanasayansi, (d. 932) alikuwa mmoja ya madaktari wakubwa duniani katika zama za Kati. Alijikita kwenye uchunguzi wa kiuhakika na dawa za matibabu na hakuwa na mfano wake kama mchunguzi. Pia aliandika nakala ya usafi wa mahospitali. Khalaf Abul-Qasim Al-Zahrawi alikuwa mwanaupasuaji maarufu ndani ya karne ya kumi na moja, anajulikana Ulaya kwa kazi yake, Concessio (Kitab al-Tasrif).
Ibn Sina (d. 1037), anajulikana zaidi magharibi kama Avicenna, alijulikana kuwa daktari bora hadi kwenye zama za sasa. Kitabu chake maarufu, Al-Qanun fi al-Tibb, kinabaki kuwa kitabu chenye kiwango hata Ulaya, kwa zaidi ya miaka 700. Kazi ya Ibn Sina inaendelea kusomwa na msingi ndani ya Mashariki.
Michango mingine muhimu ilitolewa katika pharmacology, kama Ibn Sina's Kitab al-Shifa' (Kitabu cha uponyaji), na afya ya jamii. Katika kila mji mkuu ndani ya Ulimwengu wa Kiislamu kuna idadi ya hospitali bora, baadhi ya hizo hospitali zinazofundisha, na nyingi katika hizo zimejikita katika magonjwa mahususi, ikiwemo kiakili na kihisia. Ottomans walijulikana sana kwa kujenga hospitali na kuwa na kiwango cha juu cha usafi.
Ongeza maoni