Waislamu ni nani? (sehemu ya 1 kati ya 2)
Maelezo: Zaidi ya bilioni ya watu kutoka asli zote, nchi na tamaduni – sehemu hii inakupa utangulizi wa kuwa Waislamu ni nani na mchango wao katika dunia.
- Na islamuncovered.com [Edited by IslamReligion.com]
- Iliyochapishwa mnamo 06 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 2
- Imetazamwa: 7,450 (wastani wa kila siku: 7)
- Imekadiriwa na: 132
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Waislamu wanatoka kwenye asili zote, mataifa na tamaduni ulimwenguni kote. Wana lugha mbali mbali, vyakula, mavazi, na mila; hata njia wanazoishi zinaweza kutofautiana. Ila wote wanajichukulia kuwa Waislamu.
Chini ya 15% ya Waislamu Wanaishi katika ulimwengu wa Kiarabu; moja ya tano wanapatikana kusini mwa jangwa la sahara; na jamii kubwa ya Kiislamu ulimwenguni inapatikana Indonesia. Sehemu kubwa ya Asia, na karibu jamuhuri zote za Waasia, ni Waislamu. Waislamu wachache wanapatikana China, India, Urusi, Ulaya, Amerika ya Kaskazini na Amerika ya Kusini.
Zaidi ya bilioni ya watu kutoka asili zote, mataifa na tamaduni ulimwenguni kote ni Waislamu-kuanzia kwenye mashamba ya mpunga ya Indonesia hadi moyo wa jangwa la Afrika; kuanzia majengo marefu ya New York hadi mahema ya Bedouin ndani ya Uarabuni.
Je, Kuenea kwa Uislamu Kuliathiri Vipi Dunia?
Jamii ya Kiislamu imeendelea kukuwa baada ya kufariki kwa Mtume Muhammad. katika miongo kadhaa, idadi kubwa ya watu katika mabara matatu-Afrika, Asia na Ulaya- wamechagua Uislamu kuwa njia yao ya kuishi.
Moja ya sababu za kuenea kwa haraka na kwa amani kwa Uislamu kuwa usafi wa mafundisho yake-Uislamu unasisitiza imani ya Mungu Mmoja. Hii, inaungana na dhana za usawa,haki na uhuru, inayopelekea muunganiko na jamii ya amani. Watu walikuwa huru kusafiri kutoka Uhispania hadi China bila uwoga, na bila kuvuka mpaka wowote.
Wasomi wengi wa Kiislamu walisafiri katika miji hii wakitafuta maarifa. Walitafsiri Kiarabu idadi kubwa ya falsafa na kazi za kisayansi kutoka lugha ya Kigiriki na Kisiria (lugha ya wasomi Wakristo wa Mashariki), kutoka Pahlavi (lugha ya wasomi ya kabla ya uislamu wa Wajemi), na kutoka Sanskrit (lugha ya kale ya Kihindi). Matokeo yake, Kiarabu kikawa lugha ya ulimwengu wa kisomi, watu wakahamia kutoka duniani kote kusoma kwenye vyuo vya Kiislamu.
Hadi 850, kazi nyingi za falsafa na sayansi ya Aristotle; Shule za Plato na Pythagorean ; na kazi muhimu za unajimu za Kigiriki, hesabati na madawa kama vile Almagest ya Ptolemy, Vipengele vya Euclid, na kazi ya Hippocrates na Galen, zililetwa kwenye Kiarabu. Kwa miaka ijayo 700, Kiarabu kimekuwa lugha muhimu ya kisayansi ulimwenguni na hazina kubwa ya hekima na sayansi za zamani.
Mafanikio ya wasomi waliofanya kazi ndani ya tamaduni ya Kiislamu walikwenda mbali zaidi ya kutafsiri na kuhifadhi mafunzo ya zamani. Wasomi hawa walijenga juu ya urithi wa zamani kwa maendeleo ya sayansi zao. Maendeleo haya ilisababisha moja kwa moja mwamko ndani ya Ulaya.
Waislamu walibobea kwenye sanaa, usanifu, unajimu, jiografia, Historia, lugha, fasihi, madawa, hesabati na fizikia. Mifumo mingi muhimu, kama vile algebra, namba za kiarabu, na wazo la sifuri (muhimu katika hisabati ya juu), ilitengenezwa na wasomi wa Kiislamu na kushirikisha medieval Ulaya. Waislamu walivumbua vyombo vya kisasa ambavyo baadae vilifanikisha safari za kigunduzi za vyombo vya Ulaya, kama vile astrolabe, quadrant, na ramani nzuri za kusafiria na chati.
Mchango wa Waiskamu katika Sayansi
Unajimu
Waislamu mara zote wamekuwa wakiwa na wakitamani unajimu. Mwezi na jua vinaumuhimu sana katika maisha ya kila siku ya kila Muislamu. Kwa mwezi, Waislamu wanatambua mwanzo na mwisho wa mwezi kwenye kalenda yao ya mwezi. Kwa jua Waislamu wanafanya mahesabu ya muda wa swala na kufunga.Na kwa njia ya unajimu Waislamu wanaweza kujua mwelekeo sahihi wa Qiblah, ili kuelekea Ka'bah ndani ya Makkah, wakati wa swala.
Kurani Ina marejeo mengi ya kinajimu.
"Yeye [Mungu]ndiye Muumbaji wa mbingu na ardhi…" (Kurani 6:101)
"Na Yeye ndiye aliye umba usiku na mchana na jua na mwezi, vyote katika anga vinaogelea." (Kurani 21:33)
"Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio twenye uwezo wa kuzitanua." (Kurani 51:47)
Marejeo haya, na maagizo ya kujifunza, yaliwahamasisha wasomi Waislamu wa mwanzo kuzisoma mbingu. Waliunganisha kazi za mwanzo za Wahindi, Waajemi na Wagiriki katika muunganiko mpya. Ptolemy's Almagest (Jina tunalolijua ni Kiarabu) ilitafsiriwa, ilisomwa na kukosolewa. Nyota nyingi mpya ziligunduliwa, kama tunavyoona majina ya Kiarabu - Algol, Deneb, Betelgeuse, Rigel, Aldebaran. Zilikuswanywa kwenye jedwali la unajimu, kati ya hizo ni jedwali ya Toledan , ambalo lilikuwa linatumiwa na Copernicus, Tycho Brahe na Kepler. Pia ilijumuishwa almanacs - neno lingine la Kiarabu. Maneno mengine kutoka kwenye Kiarabu ni zenith, nadir, albedo, azimuth.
Wanajimu wa kiislamu ndio walikuwa wa kwanza kuanzisha vituo vya uchunguzi wa anga, mojawapo iliyotengenezwa Mugharah na wakavumbua vifaa kama vile quadrant na astrolabe, iliyopelekea maendeleo sio tu ya unajimu bali hata kwenye safari za baharini, Kuchangia Ulaya kwenye kipindi cha Uvumbuzi.
Ongeza maoni