Mashahidi wa Yehova ni nani? (sehemu ya 3 kati ya 3): Dhana ya Msingi yenye Dosari

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Ulinganisho mdogo wa imani za Mashahidi wa Yehova na Uislamu.

  • Na Aisha Stacey (© 2012 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 19 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 4,219 (wastani wa kila siku: 4)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Mashahidi wa Yehova (Jehovah’s Witnesses (JW's)) ni dhehebu la Kikristo lenye imani nyingi ambazo hutofautiana na Ukristo wa kawaida. Wanajulikana kwenye uinjilisti wao wenye nguvu, kujishughulisha sana na Siku za Mwisho na tafsiri yao ya kipekee ya Biblia inayoitwa Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ya Maandiko Matakatifu. Katika hitimisho hili la somo letu la dini linayoeleweka kidogo inayojulikana kama Mashahidi wa Yehova tutaangalia baadhi ya imani zinazoonekana kuwa sawa na Uislamu.

Mashahidi wa Yehova wanaamini kwamba Yesu si Mungu. Hii ni kauli inayowakasirisha Wakristo wengi na kuwafanya wengi kuwatangaza mashahidi wa Yehova kuwa Wakristo bandia. Waislamu, kama tunavyojua wanatangaza kimsingi kwamba Yesu si Mungu, kwa hiyo kusoma tu kauli hii ndogo kunaweza kumsababishia Mwislamu kusema, "Oh hii ni sawa na sisi". Lakini je! Hebu tuchimbue zaidi imani yao kuhusu jukumu la Yesu.

JW's inalaani Utatu kama ibada ya sanamu ya kipagani na kwa hivyo inakana uungu wa Yesu. Hata hivyo, wanaamini kwamba ingawa Yesu ni mwana mzaliwa wa Mungu yeye ni mdogo kuliko Mungu. Hivyo mfananisha na Uislamu unaisha ghafla. Mwenyezi Mungu anasema katika mojawapo ya aya kubwa kabisa za Kurani kwamba hazai!

Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anayefanana naye hata mmoja.” (Kurani 112)

Kwa kuongezea ufahamu huu wa kimsingi wenye dosari wa asili ya Mungu, JW's pia wanaamini madai mengine ya kukasirisha (kwa Waislamu). Wanadai maisha ya Yesu, au kile ambacho JW's huita kafara yake, ikawa "fidia" ya kuwakomboa wanadamu kutokana na dhambi na kifo. Wanasema kwamba Mungu aliumba vyote Mbinguni na Duniani kupitia Kristo, “mfanyakazi mkuu,” mtumishi wa Mungu.[1] Katika fasihi yao wenyewe, JW's humrejelea Yesu kama "kiumbe wake wa kwanza (wa Mungu) wa roho, fundi stadi, Yesu kabla ya kuwa mwanadamu"[2]. Wanaendelea kusema kwamba baada ya kufufuliwa kwa Yesu na Mungu, “aliinuliwa” hadi kiwango cha juu zaidi kuliko malaika. Ukanushaji wa haya unapatikana katika maneno ya Mwenyezi Mungu mwenyewe ndani ya Kurani.

Yeye ndiye Muumbaji wa mbingu na ardhi bila ya ruwaza. Itakuwaje awe na mwana naye hakuwa na mke? Naye ndiye aliye umba kila kitu. Naye ni Mwenye kujua kila kitu. Huyo ndiye Allah, Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu, hapana mungu ila Yeye, Muumba wa kila kitu. Basi muabuduni Yeye tu. Naye ni Mtegemewa wa kila kitu.” (Kurani 6:101-102)

Wazo la kuwa Yesu alikuwa fidia ya kuokoa roho zetu au kusamehe dhambi zetu ni dhana inayopingana kabisa na imani ya Kiislamu.

“Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msimseme Mwenyezi Mungu ila kwa lilio kweli. Hakika Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na neno lake tu alilo mpelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake. Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu. Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametukuka Yeye na kuwa na mwana. Ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha.” (Kurani 4:171)

Imani kuwa dhambi ya asili ilisababisha wanadamu kurithi kifo na dhambi pia iko mbali na mafundisho ya Uislamu. Uislamu unatufundisha kwamba wanadamu wamezaliwa bila dhambi na wana mwelekeo wa kawaida wa kumwabudu Mungu peke yake (bila waamuzi). Ili kudumisha hali hii ya kutokuwa na dhambi wanadamu wanahitaji kufuata amri za Mungu na kujitahidi kuishi maisha ya uadilifu. Mtu akianguka katika dhambi, kinachotakiwa ni kufanya toba ya kweli. Mtu anapotubu, Mungu huifuta dhambi hiyo kana kwamba hakuifanya kamwe.

Mashahidi wa Yehova hufundisha kwamba hakuna nafsi inayobaki baada ya kifo na kwamba Yesu atarudi kuwafufua wafu, kurudisha nafsi na mwili pia. Wale waliohukumiwa kuwa waadilifu watapewa uzima wa milele duniani (ambayo itakuwa paradiso). Wale waliohukumiwa kuwa wasio waadilifu hawatateswa bali watakufa na kutoweka. Uislamu unasema nini kuhusu hili?

Kwa mujibu wa Uislamu, maisha yanaendelea kaburini baada ya mwili kuzikwa. Nafsi ya mtu mwaminifu hutolewa kwa urahisi kutoka kwenye mwili, huvikwa vazi la mbinguni na la harufu nzuri, na kuchukuliwa kupitia mbingu saba. Hatimaye roho inarudishwa kaburini, na mtu hufunguliwa mlango wa Peponi, na upepo wake unamjia, na anasikia harufu yake. Anapewa utabiri wa Pepo na anatamani Saa ianze. Nafsi ya mtu asiyeamini, kwa upande mwingine, hutolewa kutoka kwenye mwili wake kwa shida kubwa lakini hatimaye hurudi kwenye mwili. Mtu anateswa kaburini mpaka Saa ianze.

“Na Siku hiyo kipimo kitakuwa kwa Haki. Basi watakao kuwa na uzani mzito, hao ndio watakao fanikiwa. Na watakao kuwa na uzani khafifu, basi hao ndio walio zitia khasarani nafsi zao kwa sababu ya kuzipinga Ishara zetu.” (Kurani 7:8-9)

Kwa sifa yao, JW's huepuka tabia ambazo Mungu hapendi, ikiwemo kusherehekea sikukuu za kuzaliwa na sikukuu zinazotokana na dini za uwongo. Mashahidi wa Yehova hawasherehekei siku zao za kuzaliwa, kwa sababu huonwa kuwa utukufu wa mtu binafsi badala ya Muumba. Kauli hizi hakika zinaendana na imani za Kiislamu. Hata hivyo, kwa sababu dhana ya msingi ya JW's ya Umoja wa Mungu ina dosari tabia zao za kimaadili na maadili yanamaana ndogo sana. Mwenyezi Mungu anatueleza kwa uwazi kabisa juu ya wenye hasara kubwa Siku ya Kiyama.

“Sema: Je, tukutajieni wenye khasara mno katika vitendo vyao? Ni wale ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani kwamba wanafanya kazi nzuri. Hao ni wale walio zikanusha Ishara za Mola wao Mlezi na kukutana naye. Kwa hivyo vitendo vyao vimepotea bure, na wala Siku ya Kiyama hatutawathamini kitu.” (Kurani 18: 103-105)

Kwa hivyo tunapata kuona kuwa hata ikiwa kwa mtazamo wa mwanzo wa Mashahidi wa Yehova wanaonekana kuwa na mfumo wa imani unaoendana na imani za Kiislamu, hii iko mbali na ukweli. Kuangalia kwa uangalifu kunaonyesha kasoro na makosa katika nadharia zao za kimsingi. Inaonekana kwamba Mashahidi wa Yehova wana mambo machache sana yanayofanana na Uislamu au Ukristo. Nadharia zao za Mbingu na Moto, Umoja wa Mungu, Utatu, na uumbaji wa Ulimwengu hazikubaliki kwa Waislamu na inaonekana pia hazikubaliki kwenye madhehebu mengi ya Kikristo.



Rejeleo la maelezo:

[1](http://www.beliefnet.com/Faiths/2001/06/What-Jehovahs-Witnesses-Believe.aspx)

[2] (http://www.watchtower.org/e/ti/article_05.htm)

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.