Wasifu unaohitajika kwa Muislam
Maelezo: Wasifu unaohitajika kwa Muislamu upo wazi na wenye usawa na unajumuisha mafundisho ya Kurani na Hadithi. Unajumuisha mahusiano mengi tofauti; kwa Mola wake, nafsi yake mwenyewe, familia yake na watu wanaomzunguka.
- Na islamweb.net
- Iliyochapishwa mnamo 11 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 24 Apr 2023
- Ilichapishwa: 3
- Imetazamwa: 4,905 (wastani wa kila siku: 4)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mtazamo Wake Kwa Mungu
Moja ya sifa za kutofautisha za Muislamu ni imani yake ya kina kwa Mungu na kusadiki kwake kuwa chochote kinachotokea katika ulimwengu na chochote kinachompata, kinatokea tu kupitia mapenzi na amri ya Mungu. Muislamu ameunganishwa kwa karibu na Mungu, humkumbuka kila wakati, anaweka tumaini lake Kwake na ni mtiifu Kwake.
Imani yake ni safi na ya uwazi, haina unajisi na doa lolote la ujinga, ushirikina au udanganyifu. Imani na ibada yake inategemea mafundisho ya Quran na Hadithi sahihi. Anajihisi kuwa muhitaji msaada na msaada wa Mungu kila wakati. Yeye pia hana chaguo maishani mwake ila kujitiisha kwenye mapenzi ya Mungu, kumwabudu Yeye, kujitahidi kuelekea Njia iliyo Sahihi na kufanya matendo mema. Aina hii ya mawazo itamwongoza kuwa mwadilifu na mnyofu katika matendo yake yote, hadharani na kwa faragha.
Muislamu pia hutambua ishara za nguvu isiyo na kikomo ya Mungu katika ulimwengu, na hivyo imani yake kwa Mungu huongezeka. Mungu anasema:
“Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kukhitalifiana usiku na mchana ziko Ishara kwa wenye akili. Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala, na hufikiri kuumbwa Mbingu na Ardhi, wakisema: Mola wetu Mlezi! Hukuviumba hivi bure. Subhanaka, Umetakasika! Basi tukinge na adhabu ya Moto. ” (Kurani 3:190-191)
Mtazamo Wake Juu Yake; Akili, Mwili na Roho
Muislamu anajali sana mahitaji ya mwili wake akiutunza vizuri na kuboresha afya yake nzuri na nguvu. Yeye hufanya hivyo kwa kuwa mwenye bidii, hali kupita kiasi. Badala yake, anakula cha kutosha kudumisha afya na nguvu kwa sababu anaelewa kuwa muumini mwenye nguvu anapendwa zaidi na Mungu kuliko muumini dhaifu. Mtume, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, alisema: “Hakika muumini mwenye nguvu anapendwa zaidi na Mungu kuliko muumini dhaifu. Katika vyote viwili kuna fadhila njema.” Mungu, Mwenyezi, anasema:
“ kuleni, na kunyweni na wala msifanye ubadhirifu. ” (Kurani 7:31)
Yeye pia huzingatia usafi wake wa kibinafsi kwa sababu Mtume, aliweka mkazo mkubwa juu ya hilo. Muonekano wake siku zote ni nadhifu na safi. Usafi wake wa kinywa pia ni msafi sana kwa sababu Mtume alihimiza utumiaji wa siwak (kijiti cha jino kutokana na mti wa Arak). Ila, anafanya haya yote kwa mujibu wa kanuni ya Kiislamu wa sasa; ili kuepuka kuongeza chumvi au ajizi. Mungu, Aliyeinuliwa, anasema:
“Sema: Ni nani aliye harimisha pambo la Mwenyezi Mungu alilo watolea waja wake, na vilivyo vizuri katika riziki. Sema hivyo ni kwa walio amini katika uhai wa duniani, na Siku ya Kiyama vitakuwa vyao wao tu. Namna hivi tunazieleza Ishara kwa watu wanao jua.” (Kurani 7:32)
Mbali na kujijali, Muislamu pia huishugulikia pia akili yake. Hii inafanywa kwa kujiweka mbali na dawa za kulevya na vichocheo. Pia hasisahau kufanya mazoezi mara kwa mara ili kudumisha usawa wa mwili kwa sababu kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya afya ya mwili na afya ya akili. Pia hutunza akili yake kwa kufuata maarifa yenye faida; kidini na kidunia. Mungu anasema:
“Na sema: Mola wangu Mlezi! Nizidishie ilimu.” (Kurani 20:114)
Muislamu pia huzingatia ukuaji wake wa kiroho kama vile ukuaji wake wa kiakili na kiakili. Yeye hufanya hivyo kwa mtindo ulio sawa ambao haushikilii sehemu moja kwa madhara ya sehemu nyingine. Kwa sababu hii, maisha ya Muislamu yanahusu ibada na ukumbusho wa Mungu; sala tano za kila siku, kufunga mwezi wa Ramadhani, nk.
Mtazamo Wake Kwa Watu
Pamoja na wazazi wake, Muislamu ni mfano wa utii wa kweli na upendo. Anawatendea kwa ukarimu na heshima, huruma isiyo na kipimo, adabu kamili na shukrani kuu. Anatambua hali yao na anajua majukumu yake kwao kupitia amri ya Mungu. Mungu anasema:
“Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili ” (Kurani 4:36)
Pamoja na mkewe, Muislamu anaonyesha mfano wa matendo mema na mazuri, utunzaji mzuri, uelewa wa kina wa maumbile na saikolojia ya wanawake, na kutimiza vyema majukumu na wajibu wake.
Pamoja na watoto wake, Muislamu ni mzazi ambaye anaelewa jukumu lake kubwa kwao. Yeye huangalia kila kitu kinachoweza kuathiri maendeleo yao ya Kiiislamu na kuwapa elimu sahihi. Ili waweze kuwa hodari na wajenzi wazuri wa jamii, na kuwa chanzo chema kwa wazazi wao na jamii.
Pamoja na jamaa zake, Muislamu anautunza uhusiano kwa jamaa na anajua majukumu yake kwao. Anaelewa hadhi ya juu waliyopewa jamaa katika Uislamu, ambayo inamfanya aendelee kuwasiliana nao, bila kujali hali ikoje.
Pamoja na majirani zake, Muislamu anafanya vitendo vizuri na kuzingatia hisia za wengine na kujali. Huvumilia unyanyasaji wao na kufumbia macho makosa ya jirani yake pia anahakikisha kutofanya makosa kama hayo yeye mwenyewe.
Uhusiano wa Muisilamu kwa ndugu zake na marafiki ndio uhusiano bora na ulio safi kwa sababu unategemea kupendana kwa ajili ya Mungu. Mapenzi yake kwao na hawi na moyo baridi. Yeye ni mwaminifu kwao na hawasaliti. Yeye ni mkweli na hawadanganyi. Yeye ni mvumilivu na anasamehe. Yeye pia ni mkarimu na anawaombea kwaajili ya furaha yao na ustawi wao.
Katika uhusiano wake kwa jamii na watu wote, Muislamu ana tabia nzuri, raia, mwenye kuheshimiwa, na ana sifa ya mitazamo ambayo Uisilamu inahimiza. Baadhi ya sifa hizi ni: kutokuwa na wivu kwa wengine, kutimiza ahadi zake, upole, uvumilivu, kuepuka kashfa na mambo machafu, kutoingilia kati yale ambayo hayamuhusu, kujiepusha na uvumi, na kujiepusha katika kuchochea fujo.
Hizi ndizo sifa na mitazamo ambayo kila Muislamu hujitahidi kuzifanya kama sehemu ya tabia na wasifu wao. Kwa sababu hii, jamii ambayo ina wakaazi wenye sifa kama hizo ni ile ambayo itafurahiya furaha ya kweli na amani.
Ongeza maoni