Utabiri wa Kurani ulioelekezwa kwa Muhammad

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Kuna tabiri mbalimbali zilizotajwa ndani ya Kurani ambazo zilimzungumzia Mtume Muhammad. Utimilifu wa tabiri hizi umeandikwa vyema katika vitabu vya Seerah, au wasifu wa Mtume kama ilivyoandikwa na wanafunzi wake.

  • Na Imam Mufti
  • Iliyochapishwa mnamo 10 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 29 Jan 2023
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 2,864 (wastani wa kila siku: 3)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Kuingia kwenye Msikiti Mkuu wa Makka (al-Masjid al-Haram)

Prophecies_of_the_Quran_Addressed_to_Muhammad_001.jpgKatika mwaka wa sita baada ya Mtume kulazimishwa kuhama kutoka Makka kwenda Madina, alijiona akitembelea Makka na kuhiji katika maono yaliyotajwa ndani ya Kurani:

"Hakika Mwenyezi Mungu amemtimizia Mtume wake ndoto ya haki. Bila ya shaka nyinyi mtauingia msikiti wa al-Haram, Inshallah, kwa amani, na hali mmenyoa vichwa vyenu na mmepunguza nywele[1], Hamtakuwa na khofu. Yeye anajua msiyo yajua. Basi atakupeni kabla ya haya Ushindi karibuni." (Kurani 48:27)

Mwenyezi Mungu alitoa ahadi tatu:

(a) Muhammad angeingia kwenye Msikiti Mkuu wa Makka.

(b) Muhammad angeingia kwa usalama.

(c) Muhammad na masahaba zake wangeweza kuhiji na kutimiza taratibu zake.

Kwa kupuuza uadui wa watu wa Makka, Mtume Muhammad aliwakusanya masahaba zake na kuanza safari ya amani kuelekea Makka. Lakini watu wa Makkah waliendelea kuwa na uadui na akalazimika kurejea Madina. Maono hayo yalibaki bila kutimizwa; hata hivyo, mkataba wa muhimu ulitiwa saini kati ya Mtume na watu wa Makka, ambao ungethibitisha umuhimu wake mkubwa. Kutokana na mkataba huu Muhammad alihiji kwa amani na masahaba zake mwaka uliofuata. Maono hayo yalikuwa yamepata utimilifu wake.[2]

Utabiri wa Kurani; ‘Wasioamini Watashindwa’

Waislamu walikuwa chini ya mateso makali huko Makka chini ya mkono wa wapagani. Kipindi kimoja walitengwa kwa miaka mitatu, na uhaba wa chakula muda mwingine uliendana na njaa.[3] Mazungumzo yoyote ya ushindi yalikuwa hayakuweza kufikiriwa. Licha ya uwezekano wote, Mungu alitabiri huko Makka:

"Wingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma." (Kurani 54:45)

Kitenzi cha Kiarabu yuhzamu kinatanguliwa na sa (kiambishi awali cha Kiarabu kinachoashiria wakati ujao), na kufanya utofauti wa utabiri utakaotimia siku zijazo. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, miaka miwili baada ya Mtume kuhama kutoka Makka kwenda Madina watu wa Makkah walishindwa katika Vita vya Badr na kulazimishwa kurudi nyuma.[4] Umar, khalifa wa pili wa Waislamu baada ya Mtume alikuwa akisema kuwa walikuwa hawajui utabiri wa Kurani utatimia vipi hadi wao wenyewe walipoushuhudia ukitimia katika vita maarufu vya Badr! (Saheeh Al-Bukhari)

Utabiri wa Kurani; ‘Walioamini Watapata Mamlaka ya Kisiasa’

Licha ya ukandamizaji mkali kutoka kwa watu wa Makka, Waislamu walipewa habari njema kutoka kwa Mungu:

"Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu." (Kurani 24:55)

Jinsi gani ahadi hiyo kutoka kwa Mwenyezi Mungu ingetimizwa kwa Waislamu waliodhulumiwa, kuteswa ndani ya Makka ilikuwa ni vigumu kufikiriwa wakati ilipotolewa, hata hivyo, ilitimizwa. Hakika, Mwenyezi Mungu aliwaweka Waislamu salama na akawapa uwezo wa kisiasa baada ya miaka kadhaa.

"Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu walio tumwa, Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakao nusuriwa." (Kurani 37:171-172)

Mwanzoni, Waislamu walianzisha dola yao wenyewe, kwa mwaliko wa watu wa Madina, Mwenyezi Mungu alipowaamuru wahamie huko kutoka Makka. Kisha, ndani ya uhai wa Mtume, dola hiyo ilipanuka na kushika hatamu kwenye Rasi yote ya Uarabuni, kutoka Ghuba ya Akaba na Ghuba ya Uarabuni hadi Bahari ya Uarabuni upande wa kusini, pamoja na sehemu ambayo Waislamu walikuwa wamefukuzwa (Makka yenyewe). Amri hii ilikuwa ikiendelea, kwani upanuzi wa utawala wa kisiasa na kidini wa Waislamu haukuishia kwenye Rasi ya Uarabuni. Historia inatoa ushuhuda hai kuwa Waislamu waliozungumziwa na aya hizi walitawala ardhi za dola za zamani za Uajemi na Warumi, upanuzi ambao uliwashangaza na kuwavutia wanahistoria wa dunia. Kwa maneno ya Encyclopedia Britannica:

"Ndani ya miaka 12 baada ya kifo cha Muhammad, majeshi ya Uislamu yalitwaa Siria, Iraqi, Uajemi, Armenia, Misri, na Cyrenaica (Libya ya sasa)."[5]

Utabiri wa Kurani kuhusu Wanafiki na Kabila la Banu Nadhir

Mwenyezi mungu anasema ndani ya Kurani:

"Pindi wakitolewa hawatatoka pamoja nao, na wakipigwa vita hawatawasaidia. Na kama wakiwasaidia basi watageuza migongo; kisha hawatanusuriwa." (Kurani 59:12)

Pickthall

(Kwani) hakika kama wakifukuzwa hawatoki nao, na wakishambuliwa hawatawasaidia, na lau wangeli wanusuru wangeli geuka na kukimbia, na wasingeli shinda.

"Huwaoni wanao fanya unaafiki wanawaambia ndugu zao walio kufuru katika Watu wa Kitabu: Mkitolewa na sisi lazima tutatoka pamoja nanyi, wala hatutamt'ii yeyote kabisa dhidi yenu. Na mkipigwa vita lazima tutakusaidieni. Na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa hao hakika bila ya shaka ni waongo. Pindi wakitolewa hawatatoka pamoja nao, na wakipigwa vita hawatawasaidia. Na kama wakiwasaidia basi watageuza migongo; kisha hawatanusuriwa." (Kurani 59:11-12)

Utabiri ilitimia pale Banu Nadhir walipofukuzwa Agosti 625 CE kutoka Madina; wanafiki hawakufuatana nao au kuja kuwasaidia.[6]

Utabiri wa Kurani kuhusu Mapambano Yajayo

"Maadui hawatakudhuruni ila ni maudhi tu. Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa." (Kurani 3:111)

"Na lau makafiri wangeli pigana nanyi basi bila ya shaka wangeli geuza migongo, kisha wasingeli pata mlinzi wala msaidizi." (Kurani 48:22)

Kihistoria, baada ya aya hizi kuteremshwa, makafiri katika Bara uarabuni hawakuweza kuwahimili Waislamu tena.[7]

Tunaona kutokana na tabiri zilizojadiliwa katika makala haya ni kuwa madai mengi ya wapinzani wa Utume wa Muhammad hayana msingi wowote. Wameegemeza ukosoaji wao juu ya changamoto katika kuonyesha yale aliyoyatabiri Muhammad, rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kama ni chochote, na yale yaliyotimia katika utabiri wake.[8] Kwa kudhihirishwa, alitabiri, kwa mwongozo wa Mungu, na kwa udhihirisho, yale aliyoelekezwa kutuambia yalitokea. Kwa hiyo, kwa kigezo cha wapinzani, Muhammad alikuwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Mtume wa mwisho kutumwa, kwa kauli zake zote mbili katika Sunnah (hadithi za maisha yake) na neno la Kurani.


Vielezi-chini:

[1] Baadhi ya ibada za Hajj.

[2]Angalia ‘Rehema Kwa Walimwengu,’ na Qazi Suliman Mansoorpuri, juzuu ya 1, uk. 212 na ‘Madinan Society At The Time Of The Prophet,’ cha Dk. Akram Diya al Umari, juz. 2, uk. 139.

[3] ‘Muhammad: Maisha Yake Yanategemea Vyanzo vya Awali Zaidi’ na Martin Lings, uk. 89.

[4]‘Mercy For the Worlds,’ na Qazi Suliman Mansoorpuri, juz. 3 uk. 299‘Madinan Society At The Time Of The Prophet,’ cha Dk. Akram Diya al Umari, juz. 2, uk. 37.

[5] "arts, Islamic."Encyclopædia Britannica kutoka Encyclopædia Britannica Premium Service. (http://www.britannica.com/eb/article-13813)

[6]‘Muhammad: His Life Based on the Earliest Sources' na Martin Lings, uk. 204. ‘Rehema Kwa Walimwengu,’ cha Qazi Suliman Mansoorpuri, juz. 3 uk. 302.

[7] ‘Risala Khatim al-Nabiyeen Muhammad,’ na Dr. Thamir Ghisyan.

[8] Nawe ukisema moyoni mwako, Tutajuaje neno asilolinena Bwana? Atakaponena nabii kwa jina la BWANA, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena BWANA; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope. (Biblia, Toleo Jipya la American Standard, Kumbukumbu ya Torati 18:21-22)

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.