Maelezo Kuhusu Jahanamu (sehemu ya 5 kati ya 5): Mateso ya Jahanamu II
Maelezo: Sehemu ya pili ya maelezo ya mateso, hofu na adhabu ya Jahannamu kama ilivyoelezwa katika dini ya Kiislamu.
- Na Imam Mufti
- Iliyochapishwa mnamo 11 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 6,574 (wastani wa kila siku: 6)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mwenyezi Mungu atazisawiji nyuso za watu wa Jahannamu:
" Siku ambayo nyuso zitanawiri na nyuso zitasawijika. Ama hao ambao nyuso zao zitasawijika wataambiwa: Je! Mlikufuru baada ya kuamini kwenu? Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyo kuwa mnakufuru.’" (Kurani 3:106)
Nyuso zao zitakuwa ni kama zimefunikwa na giza la usiku:
" Na wale walio chuma maovu, malipo ya uovu ni mfano wake vile vile, na yatawafika madhila. Hawatakuwa na wa kuwalinda na Mwenyezi Mungu. Nyuso zao kama kwamba zimefunikwa na vipande vya usiku wa giza. Hao ndio watu wa Motoni, wao humo watadumu.." (Kurani 10:27)
Na hakika Moto utawazunguka makafiri kwa pande zote kama vile madhambi yalivyowazunguka kama shuka inayozunguka mwili:
"Jahannamu itakuwa kitanda chao na juu yao nguo za moto za kujifunika…" (Kurani 7:41)
"Siku itapo wafunika adhabu hiyo kutoka juu yao na chini ya miguu yao, na atasema: Onjeni hayo mliyo kuwa mkiyatenda!." (Kurani 29:55)
"…Na hakika Jahannamu imewazunguka.…"[makafiri] (Quran 9:49)
Moto wa Jahanamu utapanda juu hadi kwa nyoyo. Moto utapenya miili yao mikubwa na kufikia ndani kabisa:
"Hasha! Atavurumishwa katika H'ut'ama Na nani atakujuvya ni nini H'ut'ama? Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa. Ambao unapanda nyoyoni." (Kurani 104:4-7)
Moto utapasua matumbo yao kama ilivyotajwa na Mtume:
"Na ataletwa mtu Siku ya Kiyama na atatupwa Motoni. Kisha matumbo yake yatamwagika Motoni, naye atalazimishwa kutembea na kuzunguka kama punda kwenye miviringo. Na watu wa Motoni watamkusanyikia, na kusema: Ewe fulani, nini mbaya na wewe? Kwani hukutuamrisha tufanye mema na kutukataza tufanye maovu? Naye atasema: Mimi nilikuwa nikiwaamrisha mtende mema, lakini sikuwa nayafanya, na nilikuwa nikiwakataza kufanya uovu, lakini mimi mwenyewe nilikuwa nikiufanya. Kisha ataendelea kuzunguka na kuzunguka kama punda kwenye miviringo."[1]
Mwenyezi Mungu ameeleza minyororo, nira, na pingu za Jahannamu. Watafungwa kwa minyororo na kukokotwa kwa nira kwa shingo zao:
"Hakika Sisi tumewaandalia makafiri minyororo na pingu na Moto mkali." (Kurani 76:4)
"Hakika Sisi tunazo pingu nzito na Moto unao waka kwa ukali kabisa! Na chakula kinacho kwama kooni, na adhabu inayo umiza. ." (Kurani 73:12-13)
"Na tutaweka makongwa shingoni mwao walio kufuru. Kwani wanalipwa ila kwa waliyo kuwa wakiyatenda?" (Kurani 34:33)
"Zitakapo kuwa pingu shingoni mwao na minyororo, huku wanabururwa." (Quran 40:71)
"(Pasemwe): Mshikeni! Mtieni pingu! Kisha mtupeni Motoni! Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabiini!" (Kurani 69:30-32)
Masanamu na miungu mingine iliyo abudiwa badala ya Mwenyezi Mungu, ambao watu wanadhani kuwa ni waombezi wao mbele ya Mwenyezi Mungu, na wakawaleta karibu Naye,watatupwa Jahannamu pamoja nao. Hii itakuwa ni kudhalilisha na kuonyesha kwamba hawa miungu ya uongo hawana nguvu,
"Hakika nyinyi na hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu [2] ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu. Lau kuwa hawa ni miungu, wasingeli ingia. Na wote watadumu humo." (Kurani 21:98-99)
Mkafiri anapoona Jahannamu, atajuta sana, lakini majuto hayatamnufaisha:
" Na watakapo iona adhabu wataficha majuto. Na patahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatadhulumiwa." (Kurani 10:54)
Mkafiri ataomba afe atakapohisi joto na adhabu ya Moto,
"Na watakapo tupwa humo mahali dhiki, hali wamefungwa, wataomba wafe.Msiombe kufa mara moja tu, bali mfe mara nyingi!’" (Kurani 25:13-14)
Mayowe yao yatazidi, na watamwomba Mwenyezi Mungu, wakitumaini kwamba atawatoa katika Jahannamu:
"Na humo watapiga makelele: Mola wetu Mlezi! Tutoe tufanye mema sio yale tuliyo kuwa tukiyafanya!’" (Kurani 35:37)
Watatambua madhambi zao na upotovu wa ukafiri:
"Na watasema: Lau kuwa tungeli sikia, au tungeli kuwa na akili, tusingeli kuwa katika watu wa Motoni!Wakakiri dhambi zao. Basi kuangamia ni kwa watu wa Motoni!." (Kurani 67:10-11)
Maombi yao yatakataliwa:
"Mola wetu Mlezi! Tulizidiwa na uovu wetu na tukawa watu tulio potea.Mola wetu Mlezi! Tutoe humu Motoni. Na tufanyapo tena basi kweli sisi ni wenye kudhulumu. Atasema Mwenyezi Mungu: Tokomeeni humo, wala msinisemeze!’" (Kurani 23:106-108)
Kisha watawaita walinzi wa Jahannamu wakiwataka wamwombe Mwenyezi Mungu ili awapunguzie adhabu:
"Na walio Motoni watawaambia walinzi wa Jahannamu: Mwombeni Mola wenu Mlezi atupunguzie walau siku moja ya adhabu.Nao watasema: Je! Hawakuwa wakikufikieni Mitume wenu kwa hoja zilio wazi? Watasema: Kwani? Watasema: Basi ombeni! Na maombi ya makafiri hayawi ila ni kupotea bure.’" (Kurani 40:49-50)
Wataomba hata maangamizi yao wenyewe ili wajiondolee maumivu:
"Nao watapiga kelele waseme: Ewe Malik! Na atufishe Mola wako Mlezi! Naye aseme: Hakika nyinyi mtakaa humo humo!’" (Kurani 43:77)
Wataambiwa adhabu haitapunguzwa kamwe, ni ya milele:
"Uingieni, mkistahamili au msistahamili - ni mamoja kwenu. Hakika mnalipwa kwa mliyo kuwa mkiyatenda..’" (Kurani 52:16)
Watalia kwa muda mrefu sana:
" Basi nawacheke kidogo; watalia sana. Hayo ni malipo ya yale waliyo kuwa wakiyachuma" (Kurani 9:82)
Watalia mpaka waishiwe na machozi, kisha watalia damu itakayoacha alama yake kama alivyosema Mtume:
"Na watu wa Motoni watalia, nao watalia mpaka wasiwe na machozi. Kisha watalia damu mpaka wawe na njia kwenye nyuso zao, ambapo meli zingewekwa humo zingeli elea."[3]
Kama ulivyoona, maelezo ya Jahannamu katika Kitabu cha Kiislamu ni wazi na chenye michoro, na maelezo ya watu wanao stahili kuingia humo pia yamewekwa wazi. Ni wazi kiasi kwamba anaye iamini Siku ya Kiyama na Akhera ni lazima ataamua angalau asiwe miongoni mwa watu wanaotupwa ndani. Njia bora zaidi, na kwa kweli ya pekee, ya kuepuka hatima hii ni kutafuta kwa makini dini ya kweli ambayo Mungu ameileta kwa wanadamu. Mtu asifuate dini tu kwa sababu ilikuwa ile “aliyozaliwa” nayo, wala asifanye dini kuwa mtindo mpya wa kisasa. Badala yake, anapaswa kuangalia uhalisia wa ulimwengu huu na maisha yajayo, na kuwa na uhakika kwamba amejiandaa kisawasawa kwa hukumu hiyo ambayo hakuna kurudi kutoka kwake, kwa kuishi maisha na mfumo wa imani uliofunuliwa bila mabadiliko kutoka Aliye Juu Mno.
Vielezi-chini:
[1] Saheeh Al-Bukhari, Saheeh Muslim
[2] Ibn Katheer, katika tafsir yake, anaelezea kwamba watu wema na manabii wa zamani, ambao walichukuliwa kwa miungu na vizazi vilivyokuja baadaye bila idhini yao, hawako katika 'kuni za moto'. Ni wale tu 'waliopenda kuabudiwa' na wafuasi wao, ndio watakaotupwa humo pamoja na 'wale walio waabudu', na masanamu mengine yasiyokuwa hai. Kwa watu kama Yesu, Kurani inasema: "Ama wale ambao wema wetu umewatangulia, hao watatenganishwa na hayo…" (Kurani 21:101)
[3] Ibn Majah
Ongeza maoni