Utabiri wa Muhammad

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Tabiri za Mtume Muhammad zilitimia katika uhai wake na baada ya kifo chake. Tabiri hizi ni uthibitisho wa wazi wa utume wa Muhammad rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.

  • Na Imam Mufti
  • Iliyochapishwa mnamo 24 Nov 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 25 Sep 2023
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 4,740 (wastani wa kila siku: 4)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

The_Prophecies_of_Muhammad_001.jpgMoja ya njia ambazo mtu huthibitisha utume wake ni ukweli, iwe inahusiana na matukio ya zamani, katika maisha yao ya kila siku, au mambo yajayo. Zaidi ya Quran, kuna maneno mengi ya Mtume Muhammad ambayo yana utabiri uliotolewa katika maisha yake unaohusu vitu vya karibu na vya mbali. Baadhi yake yametimia, mengine yanangojea kutimia. Hudhaifah, mwanafunzi wa Muhammad, anatuambia:

"Mtume aliwahi kutoa hotuba mbele yetu ambapo alitaja kila kitu [ishara zote] kitakachotokea mpaka Saa ya Mwisho bila kuacha chochote. Baadhi yetu tunakumbuka na wengine kusahau. Baada ya hotuba hiyo, nilikuwa nikiona matukio yanayotokea ambayo yalitajwa kwenye hotuba hiyo, lakini nilikuwa nimeyasahau kabla ya kutokea. Hapo ningetambua matukio kama vile mwanadamu anapomtambua mwanadamu mwingine ambaye hakuwepo kisha akamuona na kumtambua." (Saheeh Al-Bukhari)

Kuna takribani tabiri 160 zinazojulikana na kuthibitishwa za Mtume Muhammad ambazo zilitimia katika maisha yake na kizazi cha kwanza baada yake.[1] Tutazitaja baadhi yake hapa.

(1) Kabla ya Vita vya Badr, pambano la kwanza na Wapagani wa Makkah katika mwaka wa pili wa kuhama kutoka Makka mnamo 623 CE, Mtume Muhammad alitabiri mahali sahihi ambapo kila mwanajeshi mpagani wa Makka angeangukia. Wale walioshuhudia vita hivyo waliona utabiri huo ukitimia kwa macho yao wenyewe.[2]

(2) Mtume Muhammad alitabiri kuwa Vita vya Muungano (al-Ahzab) vingekuwa vya uvamizi wa mwisho ambao kabila la Quraish (Wapagani wa Makkah) wangevifanya dhidi ya Waislamu. Ilipiganwa katika mwaka wa tano wa uhamiaji, 626 BK na ulikuwa mzozo wa mwisho wa kijeshi kati ya pande hizo mbili. Watu wote wa Makkah waliukubali Uislam baada ya miaka michache[3]

(3) Mtume alimfahamisha binti yake, Fatima, kwamba atakuwa mtu wa kwanza wa familia yake kufa baada yake. Kuna tabiri mbili kwa moja: Fatima ataishi zaidi ya baba yake; Fatima atakuwa mtu wa kwanza wa familia yake kufa baada yake. Zote mbili zilitimia.[4]

(4) Mtume Muhammad alitabiri kwamba Yerusalemu ingeshindwa baada ya kifo chake.[5] Utabiri huo ulitimia, kulingana na Encyclopedia Britannica: "Mwaka 638 pindi Khalifa wa Kiislamu, Umar I, alipoingia Yerusalemu."[6]

(5) Mtume Muhammad alitabiri ushindi kwa Uajemi.[7] Ulichukuliwa na kamanda wa Umar, Sa’ad ibn Abi Waqqas. Kwa maneno ya Encyclopedia Britannica:

"…uvamizi katika eneo la Wasasania ulichukuliwa haraka na Makhalifa, au manaibu wa Muhammad, huko Madina - Abu Bakr na Umar ibn al-Khattab… ushindi wa Waarabu huko Al-Qadisiyyah mnamo 636/637 ulifuatiwa na kutolewa kwa mji mkuu wa msimu wa baridi wa Sasania huko Ctesiphonkwenye Tigris. Vita vya Nahavand mnamo 642 vilikamilisha ushindi wa Wasasani."[8]

(6) Mtume Muhammad alitabiri ushindi wa Misri.[9] Kwa maneno ya Encyclopedia Britannica:

"Amr… alianza uvamizi mwaka 639 akiwa na jeshi dogo la watu wapatao 4,000 (waliimarishwa baadaye). Kwa kile kinachoonekana kasi ya kushangaza majeshi ya Byzantine yalitikiswa na kuondoka Misri 642… Fafanuzi mbalimbali zimetolewa kwa kasi ambayo ushindi huo ulipatikana."[10]

(7) Mtume alitabiri mapambano na Waturuki.[11] Mgogoro wa kwanza ulitokea kwenye ukhalifa wa Umar mwaka wa 22 Hijiriya.[12]

(8) Mtume alitabiri vita vya kwanza vya baharini vingefanywa na Waislamu vitashuhudiwa na Umm Haram, mwanamke wa kwanza kushiriki katika msafara wa majini. Pia alitabiri shambulio la kwanza dhidi ya Constantinople.[13]

Vita vya kwanza vya baharini katika historia ya Waislamu vilikuwa mwaka wa 28 Hijra katika utawala wa Mu’awiya. Ilishuhudiwa na Umm Haram kama ilivyotabiriwa na Mtume Muhammad, na Yazid ibn Mu’awiya aliongoza shambulio la kwanza la Constantinople mwaka wa 52 Hijra.[14]

(9) Utabiri kwamba Rumi, Uajemi na Yemeni zitachukuliwa ulitolewa wakati wa Vita vya Ushirikiano mwaka 626 BK.,[15] katima mazingira magumu, kama inavyoelezwa na Quran:

"Walipo kujieni kutoka juu yenu, na kutoka chini yenu; na macho yalipo kodoka, na nyoyo zikapanda kooni, nanyi mkamdhania Mwenyezi Mungu dhana mbali mbali. Hapo ndipo Waumini walipo jaribiwa, na wakatikiswa mtikiso mkali.Na walipo sema wanaafiki na wale wenye maradhi katika nyoyo zao: Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawakutuahidi ila udanganyifu tu.’" (Kurani 33:10-12)

(10) Mtume Muhammad alitabiri mwongo anayedai kuongea kwa jina la Mungu atauawa mikononi mwa mtu mwadilifu katika maisha ya Muhammad.[16] Al-Aswad al-Ansi, nabii muongo huko Yemen, aliuawa wakati wa uhai wa Mtume na Fayruz al-Daylami.[17]

Kuna takribani tabiri 28 za ziada zinazohusu nyakati za mwisho ambazo zinangojwa kutimizwa.

Hakika tabiri hizi zilizo hifadhiwa vyema ni dalili za wazi za Utume wa Muhammad, rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Hakuna njia inayowezekana ya Mtume kuweza kujua matukio haya isipokuwa kama amepewa habari na Mwenyezi Mungu Mwenyewe, yote hayo yametendeka ili kuthibitisha zaidi uhalali wa Muhammad, kuwa yeye hakuwa muongo, bali ni Mtume aliyeletwa na Mwenyezi Mungu. kuokoa wanadamu kutokana na Moto wa Jahannamu.



Vielezi-chini:

[1] Zimekusanywa na Dr. Muhammad Wali-ullah al-Nadavi katika tasmini yake iitwajo, ‘Nubuwwat al-Rasul,’ kutoka Chuo Kikuu cha al-Azhar University, Cairo, Misri.

[2]Saheeh Muslim, Abu Ya’la.

[3] Saheeh Al-Bukhari, Bazzar, na Haithami.

[4]‘Sharh’ Saheeh Muslim,’ na Imam al-Nawawi.

[5]Saheeh Al-Bukhari.

[6] "Jerusalem." Encyclopædia Britannica kuanzia Encyclopædia Britannica Premium Service. (http://www.britannica.com/eb/article-61909)

[7] Saheeh Muslim.

[8] "Iran." Encyclopædia Britannica kuanzia Encyclopædia Britannica Premium Service. (http://www.britannica.com/eb/article-32160)

[9] Saheeh Muslim.

[10] "Egypt." Encyclopædia Britannica kuanzia Encyclopædia Britannica Premium Service. (http://www.britannica.com/eb/article-22358)

[11] Saheeh Al-Bukhari, Saheeh Muslim.

[12] Ibn Kathir’s ‘al-Bidaya wal-Nihaya.’

[13] Saheeh Al-Bukhari, Saheeh Muslim.

[14] Ibn Kathir’s ‘al-Bidaya wal-Nihaya.’

[15] Saheeh Al-Bukhari.

[16]Saheeh Al-Bukhari.

[17]Encyclopedia ya Uislam.

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.