Maelezo ya moto wa Jahannamu (sehemu ya 1 kati ya 5): Utangulizi

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Majina ya Jahannamu na uwepo wake wa milele, na walinzi wake.

  • Na Imam Mufti
  • Iliyochapishwa mnamo 13 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 31 Aug 2024
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 9,178
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

A_Description_of_Hellfire_(part_1_of_5)_001.jpgUislamu unafundisha kwamba Jahannamu ni mahali pa kweli palipotayarishwa na Mwenyezi Mungu kwa wasiomuamini Yeye, na wanaasi dhidi ya sheria zake, na wanawakataa Mitume wake. Jahannamu ni mahali halisi, si hali tu ya mawazo au kipengele cha kiroho. Hofu, maumivu, uchungu, na adhabu zote ni za kweli, lakini ni tofauti kiasili kuliko za dunia. Jahannamu ni udhalilishaji mbaya zaidi na hasara usio na kifani. Na hakuna kitu kibaya zaidi kuliko Jahannamu:

"Mola wetu Mlezi! Hakika unayemtia Motoni umemhizi; na waliodhulumu hawana wasaidizi." (Kurani 3:192)

"Je, hawajui ya kwamba anaye shindana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi huyo atapata Moto wa Jahannamu adumu humo? Hiyo ndiyo hizaya kubwa." (Kurani 9:63)

Majina ya Jahannamu

Moto wa Jahannamu una majina tofauti katika maandiko ya Kiislamu Kila jina linatoa maelezo tofauti. Baadhi ya majina yake ni:

Jaheem – moto - kwa sababu ya moto wake mkali.

Jahannam - shimo la moto - kwa sababu ya kina cha shimo lake.

Ladthaa - moto mkali - kwa sababu ya miali yake wake.

Sa’eer - mwali mkali - kwa sababu umewaka na kuwashwa.

Saqar - kwa sababu ya kiwango cha joto lake.

Hatamah - vipande vilivyovunjika au vifusi - kwa sababu huvunja na kusaga kila kitu kinachotupwa ndani yake.

Haawiyah - pengo au shimo - kwa sababu anayetupwa ndani yake anatupwa kutoka juu hadi chini.

Pepo na Jahannamu Zipo na ni za Milele

Jahannamu ipo wakati huu na itaendelea kuwepo milele. Haitaisha kamwe, na wakazi wake watabaki ndani yake milele. Hakuna atakayetoka Jahannamu ila wale walioamini umoja wa Mwenyezi Mungu katika maisha haya, na wakawaamini manabii waliotumwa kwao (kabla ya kuja kwaMuhammad). Washirikina na makafiri watakaa humo milele. Imani hii imeshikiliwa tangu zamani na inatokana na aya zilizo wazi katika Kurani na taarifa zilizothibitishwa kutoka kwa Mtume wa Uislamu. Kurani inazungumzia Jahannamu katika mfumo wa wakati uliopita na inasema kwamba tayari ilishaumbwa:

"Na uogopeni Moto ambao umeandaliwa kwa ajili ya makafiri." (Kurani 3:131)

Nabii wa Uislamu alisema:

"Na atakapo kufa mmoja kati yenu anaonyeshwa pahala pake( kwenye ahera) asubuhi na jioni. Akiwa yeye ni miongoni mwa watu wa Peponi basi anaonyeshwa mahali pa watu wa Peponi. Na akiwa yeye ni katika watu wa Motoni basi ataonyeshwa pahala pa watu wa Motoni. Anaambiwa: Hii ndio kikao chako mpaka Mwenyezi Mungu akufufueni Siku ya Kiyama." (Saheeh Al-Bukhari, Saheeh Muslim)

Katika ripoti nyingine, Nabii alisema:

"Hakika nafsi ya Muumini ni ndege anaye kaa juu ya miti ya Peponi, mpaka Mwenyezi Mungu airudishe kwenye mwili wake Siku ya Kiyama." (Muwatta of Malik)

Maandiko haya yanabainisha kuwa Jahannamu na Pepo zipo, na nafsi zitaziingia kabla ya Siku ya Kiyama. Akizungumza kuhusu udaima wa Jahannamu, Mungu anasema:

"Watataka watoke Motoni, lakini hawatatoka humo, na watakuwa na adhabu inayo dumu." (Kurani 5:37)

"…wala hawatakuwa wenye kutoka Motoni." (Kurani 2:167)

"Hakika wale walio kufuru na wakadhulumu hawi Mwenyezi Mungu kuwasamehe wala kuwaongoa njia. Isipo kuwa njia ya Jahannamu. Humo watadumu milele" (Kurani 4:168-169)

"Hakika Mwenyezi Mungu amewalaani makafiri, na amewaandalia Moto unaowaka na watadumu humo milele." (Kurani 33:64-65)

"Na wenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa Jahannamu wadumu humo milele." (Kurani 72:23)

Walinzi wa Jahannamu

Malaika wenye nguvu wamesimama juu ya Jahannamu wasiomuasi Mwenyezi Mungu. Wanafanya hasa kama walivyoagizwa. Mungu anasema:

"Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayo amrishwa." (Kurani 66:6)

Kuna walinzi kumi na tisa wa Jahannamu kama Mungu anavyosema:

"Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar. Na nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar? Haubakishi wala hausazi, na unababua ngozi iwe nyeusi! Juu yake wapo kumi na tisa (walinzi wa Jahannamu)." (Kurani 74:26-30)

Wala mtu asidhani kwamba watu wa Motoni watawashinda walinzi wa Jahannamu kwa sababu idadi yao ni kumi na tisa tu. Kila mmoja wao ana nguvu ya kuangamiza wanadamu wote peke yake. Mungu anawaita Malaika hawa kama Walinzi wa Jahannamu katika Kurani:

"Na walio Motoni watawaambia walinzi wa Jahannamu: Mwombeni Mola wenu Mlezi atupunguzie walau siku moja ya adhabu!’" (Kurani 40:49)

Jina la malaika mkuu anayelinda Jahannamu ni Malik, kama ilivyoelezwa katika Kurani:

"Hakika makafiri watakuwa katika adhabu ya Jahannamu wadumu humo milele. Wala hawatapunguziwa adhabu, nao wataangamizwa kwa majuto makubwa na huzuni na wenye kukata tamaa. Na hatukuwadhulumu, lakini wao walikuwa madhaalimu. Na watlilia: Ewe Malik! Na atukomesha Mola wako Mlezi. Atasema: Hakika nyinyi mtadumu milele. Hakika Sisi tumewaletea Haki, lakini wengi wenu mnachukia Haki" (Kurani 43:74-78)

Mbaya Nzuri zaidi

Maelezo ya Moto wa Jahanamu (sehemu ya 2 kati ya 5): Muonekano wake

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Maeneo, ukubwa, viwango, milango na kuni za Jahannamu, pamoja na mavazi ya wenyeji.

  • Na Imam Mufti
  • Iliyochapishwa mnamo 13 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 7,710
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Maeneo Yake

Hakujatajwa kabisa kwa Qur'ani wala hadithi ya Mtume Muhammad jambo linaloonyesha Jahannamu iko wapi. Hakuna ajuaye iko wapi isipokuwa Mwenyezi Mungu. Kutokana na baadhi ya ushahidi wa kilugha na mukhtadha wa baadhi ya hadithi za mtume, baadhi ya wasomi wamesema kuwa Jahannamu iko mbinguni, na wengine wanasema kuwa iko katika ardhi ya chini.

Ukubwa Wake

Jahannamu ni kubwa sana na kina chake ni kirefu mno. Tunajua hili kupitia njia kadhaa.

Kwanza, watu wasiohesabika wataingia Jahannamu, kila mmoja, kama ilivyoelezwa katika hadithi, akiwa na meno ya mwisho yenye ukubwa wa mlima Uhud (mlima kwenye mji wa Madina) [1] Umbali kati ya mabega ya wenyeji wake pia umeelezwa kuwa sawa na matembezi za siku tatu.[2] Jahannamu itakuwa makao ya makafiri wote na wenye dhambi tangu mwanzo wa wakati na bado kutakuwa na nafasi ya wengine wengi. Mungu anasema:

"Siku tutapo iambia Jahannamu: Je! Umejaa? Nayo itasema: Je! Kuna ziada?’" (Kurani 50:30)

Moto wa Jahannamu unafananishwa na kinu kinachosaga maelfu na maelfu ya tani za nafaka na kisha kinasubiri zaidi.

Pili, jiwe linalotupwa kutoka juu ya Jahannamu litachukua muda mrefu sana kufikia chini. Mmoja wa maswahaba wa Nabii, rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, anaeleza jinsi walivyokuwa wamekaa pamoja na Nabii, na wakasikia sauti ya kitu kinachoanguka. Nabii akauliza kama wanajua ni nini? Waliposhindwa kujua, alisema:

"Hili lilikuwa jiwe lililotupwa Jahannamu miaka sabini iliyopita, likawa bado katika njia ya Jahannamu mpaka sasa."[3]

Ripoti nyingine inasema:

"Na lau kuwa likitupwa jiwe kubwa kama ngamia saba wajawazito kutoka juu ya Jahannamu, lingelivuka humo kwa muda wa miaka sabini, na lisingelifika chini."[4]

Tatu, Malaika wengi wataleta Jahannamu Siku ya Kiyama. Mungu anazungumzia hilo:

"Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo..." (Kurani 89:23)

Mtume alisema:

"Siku hiyo italetwa Jahannamu kwa kamba sabini elfu, ambazo kila moja zitashikiliwa na Malaika sabini elfu."[5]

Nne, ripoti nyingine inayoonyesha ukubwa wa Jahannamu ni kwamba jua na mwezi vitakunjwa ndani Jahannamu Siku ya Kiyama.[6]

Viwango Vyake

Jahannamu ina viwango tofauti vya joto na adhabu, na kila moja huhifadhiwa kulingana na kiwango cha ukafiri na dhambi za wale wanaoadhibiwa. Mungu anasema:

"Hakika wanaafiki watakuwa katika t'abaka ya chini kabisa Motoni." (Kurani 4:145)

Kiwango cha chini cha Jahannamu, ndicho chenye joto zaidi. Na lau kuwa wanafiki watapata adhabu mbaya kabisa, basi hao watakuwa katika sehemu ya chini kabisa ya Jahannamu.

Mungu anaelezea ngazi za Jahannamu katika Qur'ani:

"Na wote wana daraja mbali mbali kutokana na yale waliyo yatenda." (Kurani 6:132)

"Je! Aliye yafuata ya kumridhisha Mwenyezi Mungi ni kama yule aliye stahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na makaazi yake yakawa Jahannamu? Napo ni mahala pabaya pa kurejea. Hao wana vyeo mbali mbali kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona yote wayatendayo." (Kurani 3:162-163)

Milango ya Jahannamu

Mungu anaongelelea kuhusu milango saba ya Jahannamu katika Kurani:

"Na bila shaka Jahannamu ndipo pahali pao walipo ahidiwa wote. Ina milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu walio tengewa." (Kurani 15:43-44)

Kila mlango una sehemu iliyopangwa ya aliyehukumiwa atakayeingia kupitia mlango huo. Na kila mmoja ataingia kulingana na vitendo vyake, na atawekewa kiwango cha Jahannamu ipasavyo. Na watakapo letwa makafiri Jahannamu milango yake itafunguliwa, wataingia humo, na watadumu humo milele:

"Na walio kufuru wataongozwa kuendea Jahannamu kwa makundi. Mpaka watakapo ifikia itafunguliwa milango yake, na walinzi wake watawaambia: Kwani hawakukujilieni Mitume miongoni mwenu wakikusomeeni Aya za Mola wenu Mlezi na kukuonyeni mkutano wa siku yenu hii? Watasema: Kwani! Lakini limekwisha thibiti neno la adhabu juu ya makafiri.’" (Kurani 39:71)

Wataambiwa baada ya kuingia:

"Ingieni milango ya Jahannamu mdumu humo. Na makaazi ya wanao takabari ni maovu mno." (Kurani 39:72)

Malango yatafungwa na hakutakuwa na tumaini la kutoroka kama Mungu asemavyo:

"Hakika walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni. Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande.[7]" (Kurani 90:19-20)

Zaidi ya hayo, Mungu anasema katika Qur'ani:

"Ole wake kila safihi, msengenyaji! Aliye kusanya mali na kuyahisabu. Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele. Hasha! Atavurumishwa katika Hutama (motoni). Na nani atakujuvya ni nini H'ut'ama? huo ni Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa. Ambao unapanda nyoyoni. Hakika huo utafungiwa nao Kwenye nguzo zilio nyooshwa." (Kurani 104:1-9)

Na milango ya Jahannamu pia hufungwa kabla ya Siku ya Kiyama. Nabii wa Uislamu alizungumza juu ya kufunga kwayo katika mwezi wa Ramadhani.[8]

Kuni Zake

Mawe na makafiri wajeuri ndio kuni za Jahannamu kama asemavyo Mwenyezi Mungu:

"Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe..." (Kurani 66:6)

"…Basi uogopeni Moto ambao kuni zake ni watu na mawe, walio andaliwa kwa ajili ya makafiri." (Kurani 2:24)

Na chanzo kingine cha kuni za Jahannamu ni miungu iliyo abudiwa badala ya Mwenyezi Mungu:

"Hakika nyinyi na hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu. Lau kuwa hawa ni miungu, wasingeli ingia. Na wote watadumu humo." (Kurani 21:98-99)

Mavazi ya Wakazi Wake

Na Mwenyezi Mungu anatuambia kwamba mavazi ya watu wa Motoni yatakuwa nguo za Motowalizoundiwa:

"…Basi walio kufuru watakatiwa nguo za moto, na yatamiminwa juu ya vichwa vyao maji yanayo chemka." (Kurani 22:19)

"Na utawaona wakosefu siku hiyo wamefungwa pingu, na nguo zao za lami, na nyuso zao zimefunikwa na Moto." (Kurani 14:49-50)



Vielezi-chini:

[1] Saheeh Muslim

[2] Saheeh Muslim

[3] Mishkat

[4] Sahih al-Jami’

[5] Saheeh Muslim

[6] Tahawi katika Mushkal al-Aathaar, Bazzar, Baihaqi, na wengine.

[7] Kulingana na maelezo ya Ibn Abbas (‘Tafsiri ya Ibn Kathir’).

[8] Tirmidhi.

Mbaya Nzuri zaidi

Maelezo kuhusu Jahanamu (sehemu ya 3 kati ya 5): Chakula na vinywaji vyake

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Joto la Jahannamu, na vyakula na vinywaji vilivyoandaliwa wenyeji.

  • Na Imam Mufti
  • Iliyochapishwa mnamo 14 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 6,960
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Joto kali, chakula, na vinywaji vya watu wa Jahannamu vinaelezwa katika vitabu vya dini ya Kiislamu.

Joto Lake

Mungu anasema:

"Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni? watakuwa katika upepo wa moto, na maji yanayo chemka, na kivuli cha moshi mweusi isiyo cha kuburudisha wala kustarehesha." (Kurani 56:41-44)

Kila kitu ambacho watu hutumia kujibaridisha katika dunia hii — hewa, maji, kivuli — hakitakuwa na maana ndani ya Jahannamu. Hewa ya Jahannamu itakuwa upepo wa moto, na maji yatakuwa ya kuchemka. Kivuli hakitakuwa na faraja au baridi, kivuli cha Jahannamu kitakuwa kivuli cha moshi mweusi kama ilivyoelezwa katika aya:

"Na kivuli cha moshi mweusi." (Kurani 56:43)

Katika kifungu kingine, Mungu anasema:

"Na yule ambaye mizani yake itakuwa nyepesi. Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya, Na nini kitachokujuilisha nini hiyo (Hawiya) ?Ni Moto mkali." (Kurani 101:8-11)

Mwenyezi Mungu anaeleza jinsi kivuli cha moshi wa Jahannamu kitakavyopanda juu ya Moto. Moshi unaotoka Jahannamu utagawanywa katika nguzo tatu. Kivuli chake hakitatoa baridi wala kulinda dhidi ya Moto mkali. Cheche za kuruka zitakuwa kama majumba makubwa yanayofanana na safu ya ngamia wanaoandamana:

"Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu, ambayo haikingi moto wala hakiwaepushi na mwako, na hakika moto huo unatoa macheche kama majumba, kana kwamba ni Ngamia wa rangi ya manjano (waliofungwa pamoja wakifuatana)." (Kurani 77:30-33)

Moto huchoma kila kitu, bila kuacha chochote. Unachoma ngozi kufikia hadi mifupa, na kuyeyusha yaliyomo tumboni, ukiruka hadi kwa mioyo, na kufichua viungo muhimu. Mwenyezi Mungu anaongelea juu ya ukubwa na ukali wa Moto:

"Hakika nitakuja kumtia kwenye Moto wa Saqar. Na nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar? Haubakishi wala hausazi ( haiwachi chochote bila kuchomwa) na unababua ngozi iwe nyeusi." (Kurani 74:26-29)

Nabii wa Uislamu alisema:

"Moto kama tunavyo ujua ni kipande cha sehemu sabini ya Moto wa Jahannamu. Na mtu akasema: 'Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, inatosha kama ilivyo'!. Akasema: 'Ni kana kwamba sehemu sitini na tisa ziliongezwa juu ya moto kama tunavyoujua.’" (Saheeh Al-Bukhari)

Moto hauzimiki kamwe:

"Basi onjeni (matokeo ya maovu yenu). Hatutakupa ongezeko ila katika adhabu tu." (Kurani 78:30)

"…Kila moto ukifanya kusinzia tutazidi kuuchochea uwake kwa nguvu." (Kurani 17:97)

Kamwe adhabu haitapunguzwa wala makafiri kupewa nusura.

"…Hawatapunguziwa adhabu wala hawatanusuriwa." (Kurani 2:86)

Chakula cha Wakazi Wake

Na chakula cha watu wa Motoni kinaelezwa katika Qur'ani. Mungu anasema:

"Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba ambacho hakinenepeshi wala hakiondoi njaa." (Kurani 88:6-7)

Chakula hakinenepeshi wala hakitaonja vizuri. Hakitakuwa ila ni adhabu kwa watu wa Motoni. Katika vifungu vingine, Mungu anaelezea mti wa zaqqum, chakula maalum cha Jahannamu. Zaqqum ni mti wa kuchukiza, mizizi yake huingia ndani kwa sakafu ya Jahannamu, na matawi yake yaenea kote. Matunda yake mabaya ni kama vichwa vya mashetani. Anasema:

"Hakika Mti wa Zaqqum, chakula cha mwenye dhambi ni kama shaba iliyo yayushwa, hutokota matumboni kama kutokota kwa maji ya moto." (Kurani 44:43-46)

"Je! Kukaribishwa hivi (peponi) si ndio bora, au mti wa Zaqqum? Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa walio dhulumu. Hakika huo ni mti unao toka katikati ya Jahannamu, mashada ya matunda yake kama kwamba vichwa vya mashet'ani. Basi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo, kisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji ya moto yaliyo chemka. Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu." (Kurani 37:62-68)

"Kisha nyinyi, mlio potea, mnao kanusha, Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu na kwa mti huo mtajaza matumbo na juu yake mtakunywa maji yanayo chemka, tena mtakunywa kama wanavyo kunywa ngamia wenye kiu. Hiyo ndiyo karamu yao Siku ya Malipo." (Kurani 56:51-56)

Watu wa Jahannamu watapata njaa kiasi kwamba watakula mti wa kuchukiza wa zaqqum. Na watakapojaza matumbo yao, itaanza kutikisika kama mafuta yanayochemka, na kusababisha mateso makubwa. Wakati huo watakimbilia kunywa maji ya moto sana. Watakunywa kama ngamia walio na kiu, wala haitazima kiu yao. Badala yake viungo vyao vya ndani vitakatikakatika. Mungu anasema:

"…watapewa kunywa maji ya moto, ili kuyakata matumbo yao." (Kurani 47:15)

Misitu ya miiba pamoja na zaqqum itawavuta na kushika katika koo zao kutokana na harufu yake mbaya:

"Hakika Sisi tunazo pingu nzito na Moto unao waka kwa ukali kabisa na chakula kinacho kwama kooni, na adhabu inayo umiza." (Kurani 73:12-13)

Nabii wa Uislamu alisema:

"Na lau kuwa tone kutoka zaqqum lingekuwa duniani, watu wa dunia na riziki zao zote zingeoza. Basi ni vipi kwa yule atakaye kula?" (Tirmidhi)

Na chakula kingine wanachopewa watu wa Jahannamu ni usaha utokao katika ngozi zao, na uchafu unaotoka katika sehemu za siri za watu wazinifu, na ngozi yenye kuoza na nyama ya wanaochomwa motoni. Hiyo ndiyo 'sharubati' ya watu wa Motoni. Mungu anasema:

"Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea huruma, wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni. Chakula hicho hailiwi ila wakosefu." (Quran 69:35-37)

"Ndio hivi! Basi na wayaonje maji ya moto na ya usaha, na adhabu nyenginezo za namna hii." (Kurani 38:57-58)

Hatimaye, baadhi ya wenye dhambi watalishwa Moto kutoka Jahannamu kama adhabu. Mungu anasema:

"Hakika wanao kula mali ya mayatima kwa dhulma, hapana shaka yoyote wanakula matumboni mwao moto, na wataingia Motoni." (Kurani 4:10)

"Hakika wale wafichao aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu katika Kitabu, wakanunua kwa thamani ndogo, hao hawali matumboni mwao isipokuwa moto." (Kurani 2:174)

Vinywaji Vyake

Mwenyezi Mungu anasimulia katika Qur'ani kinywaji cha watu wa Jahannamu:

"watapewa kunywa maji ya moto, ili kuyakata matumbo yao." (Kurani 47:15)

"…Na wakiomba msaada watasaidiwa kwa kupewa maji kama mafuta yaliyo tibuka. Yatayowababua nyuso zao. Kinywaji hicho ni kiovu mno! Na matandiko hayo ya kupumzikia ni maovu mno." (Kurani 18:29)

"Ambaye nyuma yake ipo Jahannamu, na atanywishwa maji ya usaha. Awe anayagugumia, wala hawezi kuyameza. Na mauti yawe yanamjia kutoka kila upande, naye wala hafi. Na zaidi ya hayo ipo adhabu nyengine kali vile vile." (Kurani 14:16-17)

"Ndio hivi! Basi na wayaonje maji ya moto na ya usaha." (Kurani 38:57)

Vinywaji ambavyo watu wa Jahannamu hupata ni kama vifuatavyo:

·Maji ya moto sana kama Mungu anavyosema:

"Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto yanayo chemka." (Kurani 55:44)

"Watanyweshwa kutoka chemchem inayo chemka." (Kurani 88:5)

·Usaha unaotiririka kutoka mwili na ngozi ya mkafiri. Mtume alisema:

"Mtu yeyote ambaye hunywa za kulevya atafanywa kunywa matope ya khabal.“ Wakamuulizaa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni matope gani haya ya khabal? Akasema: “Jasho la watu wa Jahannamu au usaha ya watu wa Motoni.’" (Saheeh Muslim)

·Kinywaji kama mafuta ya moto kilichofafanuliwa hivi na Mtume:

"Ni kama mafuta ya moto, yanapoletwa karibu na uso wa mtu, ngozi ya uso huanguka ndani yake." (Musnad Ahmad, Tirmidhi)

Mbaya Nzuri zaidi

Maelezo Kuhusu Jahanamu (sehemu ya 4 kati ya 5): Mateso ya Jahanamu I

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Sehemu ya kwanza ya taswira ya mateso, hofu, na adhabu ya Jahanamu kama ilivyoelezwa katika vitabu vya kidini vya Kiislamu.

  • Na Imam Mufti
  • Iliyochapishwa mnamo 11 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 7,120
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

A_Description_of_Hellfire_(part_4_of_5)_001.jpgMoto wa Jahannamu utakuwa mkali sana hadi watu watakuwa tayari kuacha mali zao na milki walizozipenda, ili wapate kujiokoa:

"Hakika wale walio kufuru, na wakafa hali ni makafiri haitakubaliwa kutoka kwa yeyote wao fidia ya dhahabu ya kujaza dunia nzima lau wangeli itoa. Hao watapata adhabu chungu, wala hawatakuwa na wa kuwanusuru." (kurani 3:91)

Mtume wa Uislamu alisema:

"Siku ya Kiyama atatolewa katika Watu wa Jahannamu, mtu aliyepata anasa zaidi kabisa za dunia, na ataingizwa katika Moto wa Jahannamu. Kisha ataulizwa: Ewe mwana wa Adam! Je! Umewahi kuona kitu kizuri? Je! Umewahi kufurahia anasa zozote?” Atasema: Hapana, naapa kwa Mwenyezi Mungu, Ewe Mola."[1]

Sekunde chache tu motoni na mtu atasahau nyakati zote nzuri alizokuwa nazo. Mtume wa Uislamu anatujulisha:

"Siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu atamwuliza yule ambaye adhabu yake katika Moto itakuwa nyepesi zaidi: Iwapo ungemiliki vyovyote unavyovitaka duniani, je, ungevitoa ili upate kujiokoa? Naye atasema: Ndio! Na Mwenyezi Mungu atasema: Nilitaka kidogo mno kuliko hicho ulipo kuwa katika viuno vya Adam, nimekutaka usinishirikishe na chochote katika ibada, lakini ukasisitiza kuwashirikisha wengine na Mimi."[2]

Hofu na ukali wa Moto ni wa kutosha kumfanya mtu kupoteza akili yake. Angekuwa tayari kuacha kila kitu anachopenda ili aokolewe kutoka humo, lakini kamwe hataokoka. Mungu anasema:

"Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe, Na mkewe, na nduguye, Na jamaa zake walio kuwa wakimkimu, Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye. La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa, Unao babua ngozi ya kichwa!" (Kurani 70:11-16)

Adhabu ya Jahannamu pia hutofautiana kwa matabaka. Adhabu ya baadhi ya matabaka ya Jahannamu itakuwa kubwa kuliko mengine. Watu watawekwa katika tabaka lao kulingana na matendo yao. Mtume wa Uislamu alisema:

"Na wapo ambao Moto utawafikia vifundoni mwao, na wengine kwa magoti, na wengine kwenye viuno vyao, na wengine hata shingoni mwao.."[3]

Na akazungumzia mwenye adhabu nyepesi kabisa katika Jahannamu:

"Na atakaye pata adhabu ndogo kabisa miongoni mwa watu wa Jahannamu Siku ya Kiyama atakuwa mtu, ambapo chini ya upinde wa miguu yake patawekwa kaa la moto. Ubongo wake utachemka kutokana nalo."[4]

Mtu huyu atafikiri hakuna mtu mwingine anayeadhibiwa kwa ukali zaidi kuliko yeye mwenyewe, ingawa atakuwa ndiye anayepokea adhabu nyepesi zaidi.[5]

Aya nyingi za Kurani zinazungumzia matabaka mbalimbali ya adhabu wa watu wa Jahannamu:

"Hakika wanaafiki watakuwa katika t'abaka ya chini kabisa Motoni, wala hutompata yeyote wa kuwanusuru." (Kurani 4:145)

"Na itapo fika Saa ya Kiyama patasemwa: Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!" (Kurani 40:46)

Na hakika Moto wa Mwenyezi Mungu utachoma ngozi ya watu wa Jahannamu. Ngozi ni kiungo kikubwa zaidi katika mwili na ndipo maumivu ya kuchomwa husikika. Mungu atabadilisha ngozi iliyoteketezwa na kuibadilisha na ngozi mpya ili ipate kuteketea tena, na hii itaendelea bila kuisha kamwe:

"Hakika wale walio zikataa Ishara zetu tutawaingiza Motoni. Kila zitapo wiva ngozi zao tutawabadilishia ngozi nyengine ili waionje hiyo adhabu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima." (Kurani 4:56)

Adhabu nyingine ya Jahannamu ni kuyeyushwa. Maji yenye joto kali sana yatamwagiwa juu ya vichwa vyao, na yatayeyusha vilivyomo ndani:

"… na yatamiminwa juu ya vichwa vyao maji yanayo chemka. Kwa maji hayo vitayayushwa viliomo matumboni mwao, na ngozi zao pia." (Kurani 22:19-20)

Mtume Muhammad alisema:

"Maji yenye joto kali yatamwagika juu ya vichwa vyao na yatapasua njia yao hadi yakatekate matumbo yao, na kuyatoa; mpaka yatoke kwa miguu yao, na kila kitu kinayeyuka. Kisha watarejeshwa kama walivyo kuwa."[6]

Mojawapo ya njia ya Mwenyezi Mungu ya kuwadhalilisha makafiri katika Jahannamu, ni kuwakusanya Siku ya Kiyama wakikokotwa kwa nyuso zao, wakiwa vipofu, na viziwi, na mabubu.

"Na tutawakusanya Siku ya Kiyama hali wakikokotwa juu ya nyuso zao, nao ni vipofu na mabubu na viziwi. Na makaazi yao ni Jahannamu. Kila moto ukifanya kusinzia tutazidi kuuchochea uwake kwa nguvu." (Kurani 17:97)

"Na watakao kuja na uovu, basi zitasunukishwa nyuso zao Motoni. Je! Kwani mnalipwa isipo kuwa mliyo kuwa mkiyatenda?’" (Kurani 27:90)

"Moto utababua nyuso zao, nao watakuwa na nyuso zilizo kunjana." (Kurani 23:104)

"Siku ambayo nyuso zao zitapinduliwa pinduliwa katika Moto. Watasema: Laiti tungeli mt'ii Mwenyezi Mungu, na tungeli mt'ii Mtume!.’" (Kurani 33:66)

Adhabu nyingine chungu ya makafiri ni kukokotwa kifudifudi Motoni. Mungu anasema:

"Hakika wakosefu wamo katika upotofu na wazimu. Siku watakapo kokotwa Motoni kifudifudi waambiwe: Onjeni mguso wa Jahannamu!’" (Kurani 54:47-48)

Watakokotwa kifudifudi kwa nyuso zao, huku wakiwa wamefungwa minyororo na pingu:

"Ambao wamekanusha Kitabu na yale tuliyo watuma Mitume wetu. Basi watakuja jua. Zitakapo kuwa pingu shingoni mwao na minyororo, huku wanabururwa Katika maji ya moto, kisha wanaunguzwa Motoni," (Kurani 40:70-72)



Vielezi-chini:

[1] Saheeh Muslim

[2] Saheeh Al-Bukhari

[3] Saheeh Muslim

[4] Saheeh Al-Bukhari

[5] Saheeh Muslim

[6] Tirmidhi

Mbaya Nzuri zaidi

Maelezo Kuhusu Jahanamu (sehemu ya 5 kati ya 5): Mateso ya Jahanamu II

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Sehemu ya pili ya maelezo ya mateso, hofu na adhabu ya Jahannamu kama ilivyoelezwa katika dini ya Kiislamu.

  • Na Imam Mufti
  • Iliyochapishwa mnamo 11 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 6,577
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Mwenyezi Mungu atazisawiji nyuso za watu wa Jahannamu:

" Siku ambayo nyuso zitanawiri na nyuso zitasawijika. Ama hao ambao nyuso zao zitasawijika wataambiwa: Je! Mlikufuru baada ya kuamini kwenu? Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyo kuwa mnakufuru.’" (Kurani 3:106)

Nyuso zao zitakuwa ni kama zimefunikwa na giza la usiku:

" Na wale walio chuma maovu, malipo ya uovu ni mfano wake vile vile, na yatawafika madhila. Hawatakuwa na wa kuwalinda na Mwenyezi Mungu. Nyuso zao kama kwamba zimefunikwa na vipande vya usiku wa giza. Hao ndio watu wa Motoni, wao humo watadumu.." (Kurani 10:27)

Na hakika Moto utawazunguka makafiri kwa pande zote kama vile madhambi yalivyowazunguka kama shuka inayozunguka mwili:

"Jahannamu itakuwa kitanda chao na juu yao nguo za moto za kujifunika…" (Kurani 7:41)

"Siku itapo wafunika adhabu hiyo kutoka juu yao na chini ya miguu yao, na atasema: Onjeni hayo mliyo kuwa mkiyatenda!." (Kurani 29:55)

"…Na hakika Jahannamu imewazunguka.…"[makafiri] (Quran 9:49)

Moto wa Jahanamu utapanda juu hadi kwa nyoyo. Moto utapenya miili yao mikubwa na kufikia ndani kabisa:

"Hasha! Atavurumishwa katika H'ut'ama Na nani atakujuvya ni nini H'ut'ama? Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa. Ambao unapanda nyoyoni." (Kurani 104:4-7)

Moto utapasua matumbo yao kama ilivyotajwa na Mtume:

"Na ataletwa mtu Siku ya Kiyama na atatupwa Motoni. Kisha matumbo yake yatamwagika Motoni, naye atalazimishwa kutembea na kuzunguka kama punda kwenye miviringo. Na watu wa Motoni watamkusanyikia, na kusema: Ewe fulani, nini mbaya na wewe? Kwani hukutuamrisha tufanye mema na kutukataza tufanye maovu? Naye atasema: Mimi nilikuwa nikiwaamrisha mtende mema, lakini sikuwa nayafanya, na nilikuwa nikiwakataza kufanya uovu, lakini mimi mwenyewe nilikuwa nikiufanya. Kisha ataendelea kuzunguka na kuzunguka kama punda kwenye miviringo."[1]

Mwenyezi Mungu ameeleza minyororo, nira, na pingu za Jahannamu. Watafungwa kwa minyororo na kukokotwa kwa nira kwa shingo zao:

"Hakika Sisi tumewaandalia makafiri minyororo na pingu na Moto mkali." (Kurani 76:4)

"Hakika Sisi tunazo pingu nzito na Moto unao waka kwa ukali kabisa! Na chakula kinacho kwama kooni, na adhabu inayo umiza. ." (Kurani 73:12-13)

"Na tutaweka makongwa shingoni mwao walio kufuru. Kwani wanalipwa ila kwa waliyo kuwa wakiyatenda?" (Kurani 34:33)

"Zitakapo kuwa pingu shingoni mwao na minyororo, huku wanabururwa." (Quran 40:71)

"(Pasemwe): Mshikeni! Mtieni pingu! Kisha mtupeni Motoni! Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabiini!" (Kurani 69:30-32)

Masanamu na miungu mingine iliyo abudiwa badala ya Mwenyezi Mungu, ambao watu wanadhani kuwa ni waombezi wao mbele ya Mwenyezi Mungu, na wakawaleta karibu Naye,watatupwa Jahannamu pamoja nao. Hii itakuwa ni kudhalilisha na kuonyesha kwamba hawa miungu ya uongo hawana nguvu,

"Hakika nyinyi na hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu [2] ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu. Lau kuwa hawa ni miungu, wasingeli ingia. Na wote watadumu humo." (Kurani 21:98-99)

Mkafiri anapoona Jahannamu, atajuta sana, lakini majuto hayatamnufaisha:

" Na watakapo iona adhabu wataficha majuto. Na patahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatadhulumiwa." (Kurani 10:54)

Mkafiri ataomba afe atakapohisi joto na adhabu ya Moto,

"Na watakapo tupwa humo mahali dhiki, hali wamefungwa, wataomba wafe.Msiombe kufa mara moja tu, bali mfe mara nyingi!’" (Kurani 25:13-14)

Mayowe yao yatazidi, na watamwomba Mwenyezi Mungu, wakitumaini kwamba atawatoa katika Jahannamu:

"Na humo watapiga makelele: Mola wetu Mlezi! Tutoe tufanye mema sio yale tuliyo kuwa tukiyafanya!’" (Kurani 35:37)

Watatambua madhambi zao na upotovu wa ukafiri:

"Na watasema: Lau kuwa tungeli sikia, au tungeli kuwa na akili, tusingeli kuwa katika watu wa Motoni!Wakakiri dhambi zao. Basi kuangamia ni kwa watu wa Motoni!." (Kurani 67:10-11)

Maombi yao yatakataliwa:

"Mola wetu Mlezi! Tulizidiwa na uovu wetu na tukawa watu tulio potea.Mola wetu Mlezi! Tutoe humu Motoni. Na tufanyapo tena basi kweli sisi ni wenye kudhulumu. Atasema Mwenyezi Mungu: Tokomeeni humo, wala msinisemeze!’" (Kurani 23:106-108)

Kisha watawaita walinzi wa Jahannamu wakiwataka wamwombe Mwenyezi Mungu ili awapunguzie adhabu:

"Na walio Motoni watawaambia walinzi wa Jahannamu: Mwombeni Mola wenu Mlezi atupunguzie walau siku moja ya adhabu.Nao watasema: Je! Hawakuwa wakikufikieni Mitume wenu kwa hoja zilio wazi? Watasema: Kwani? Watasema: Basi ombeni! Na maombi ya makafiri hayawi ila ni kupotea bure.’" (Kurani 40:49-50)

Wataomba hata maangamizi yao wenyewe ili wajiondolee maumivu:

"Nao watapiga kelele waseme: Ewe Malik! Na atufishe Mola wako Mlezi! Naye aseme: Hakika nyinyi mtakaa humo humo!’" (Kurani 43:77)

Wataambiwa adhabu haitapunguzwa kamwe, ni ya milele:

"Uingieni, mkistahamili au msistahamili - ni mamoja kwenu. Hakika mnalipwa kwa mliyo kuwa mkiyatenda..’" (Kurani 52:16)

Watalia kwa muda mrefu sana:

" Basi nawacheke kidogo; watalia sana. Hayo ni malipo ya yale waliyo kuwa wakiyachuma" (Kurani 9:82)

Watalia mpaka waishiwe na machozi, kisha watalia damu itakayoacha alama yake kama alivyosema Mtume:

"Na watu wa Motoni watalia, nao watalia mpaka wasiwe na machozi. Kisha watalia damu mpaka wawe na njia kwenye nyuso zao, ambapo meli zingewekwa humo zingeli elea."[3]

Kama ulivyoona, maelezo ya Jahannamu katika Kitabu cha Kiislamu ni wazi na chenye michoro, na maelezo ya watu wanao stahili kuingia humo pia yamewekwa wazi. Ni wazi kiasi kwamba anaye iamini Siku ya Kiyama na Akhera ni lazima ataamua angalau asiwe miongoni mwa watu wanaotupwa ndani. Njia bora zaidi, na kwa kweli ya pekee, ya kuepuka hatima hii ni kutafuta kwa makini dini ya kweli ambayo Mungu ameileta kwa wanadamu. Mtu asifuate dini tu kwa sababu ilikuwa ile “aliyozaliwa” nayo, wala asifanye dini kuwa mtindo mpya wa kisasa. Badala yake, anapaswa kuangalia uhalisia wa ulimwengu huu na maisha yajayo, na kuwa na uhakika kwamba amejiandaa kisawasawa kwa hukumu hiyo ambayo hakuna kurudi kutoka kwake, kwa kuishi maisha na mfumo wa imani uliofunuliwa bila mabadiliko kutoka Aliye Juu Mno.



Vielezi-chini:

[1] Saheeh Al-Bukhari, Saheeh Muslim

[2] Ibn Katheer, katika tafsir yake, anaelezea kwamba watu wema na manabii wa zamani, ambao walichukuliwa kwa miungu na vizazi vilivyokuja baadaye bila idhini yao, hawako katika 'kuni za moto'. Ni wale tu 'waliopenda kuabudiwa' na wafuasi wao, ndio watakaotupwa humo pamoja na 'wale walio waabudu', na masanamu mengine yasiyokuwa hai. Kwa watu kama Yesu, Kurani inasema: "Ama wale ambao wema wetu umewatangulia, hao watatenganishwa na hayo…" (Kurani 21:101)

[3] Ibn Majah

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

(Soma zaidi...) Ondoa