Maelezo kuhusu Jahanamu (sehemu ya 3 kati ya 5): Chakula na vinywaji vyake

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Joto la Jahannamu, na vyakula na vinywaji vilivyoandaliwa wenyeji.

  • Na Imam Mufti
  • Iliyochapishwa mnamo 14 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 6,775 (wastani wa kila siku: 6)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Joto kali, chakula, na vinywaji vya watu wa Jahannamu vinaelezwa katika vitabu vya dini ya Kiislamu.

Joto Lake

Mungu anasema:

"Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni? watakuwa katika upepo wa moto, na maji yanayo chemka, na kivuli cha moshi mweusi isiyo cha kuburudisha wala kustarehesha." (Kurani 56:41-44)

Kila kitu ambacho watu hutumia kujibaridisha katika dunia hii — hewa, maji, kivuli — hakitakuwa na maana ndani ya Jahannamu. Hewa ya Jahannamu itakuwa upepo wa moto, na maji yatakuwa ya kuchemka. Kivuli hakitakuwa na faraja au baridi, kivuli cha Jahannamu kitakuwa kivuli cha moshi mweusi kama ilivyoelezwa katika aya:

"Na kivuli cha moshi mweusi." (Kurani 56:43)

Katika kifungu kingine, Mungu anasema:

"Na yule ambaye mizani yake itakuwa nyepesi. Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya, Na nini kitachokujuilisha nini hiyo (Hawiya) ?Ni Moto mkali." (Kurani 101:8-11)

Mwenyezi Mungu anaeleza jinsi kivuli cha moshi wa Jahannamu kitakavyopanda juu ya Moto. Moshi unaotoka Jahannamu utagawanywa katika nguzo tatu. Kivuli chake hakitatoa baridi wala kulinda dhidi ya Moto mkali. Cheche za kuruka zitakuwa kama majumba makubwa yanayofanana na safu ya ngamia wanaoandamana:

"Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu, ambayo haikingi moto wala hakiwaepushi na mwako, na hakika moto huo unatoa macheche kama majumba, kana kwamba ni Ngamia wa rangi ya manjano (waliofungwa pamoja wakifuatana)." (Kurani 77:30-33)

Moto huchoma kila kitu, bila kuacha chochote. Unachoma ngozi kufikia hadi mifupa, na kuyeyusha yaliyomo tumboni, ukiruka hadi kwa mioyo, na kufichua viungo muhimu. Mwenyezi Mungu anaongelea juu ya ukubwa na ukali wa Moto:

"Hakika nitakuja kumtia kwenye Moto wa Saqar. Na nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar? Haubakishi wala hausazi ( haiwachi chochote bila kuchomwa) na unababua ngozi iwe nyeusi." (Kurani 74:26-29)

Nabii wa Uislamu alisema:

"Moto kama tunavyo ujua ni kipande cha sehemu sabini ya Moto wa Jahannamu. Na mtu akasema: 'Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, inatosha kama ilivyo'!. Akasema: 'Ni kana kwamba sehemu sitini na tisa ziliongezwa juu ya moto kama tunavyoujua.’" (Saheeh Al-Bukhari)

Moto hauzimiki kamwe:

"Basi onjeni (matokeo ya maovu yenu). Hatutakupa ongezeko ila katika adhabu tu." (Kurani 78:30)

"…Kila moto ukifanya kusinzia tutazidi kuuchochea uwake kwa nguvu." (Kurani 17:97)

Kamwe adhabu haitapunguzwa wala makafiri kupewa nusura.

"…Hawatapunguziwa adhabu wala hawatanusuriwa." (Kurani 2:86)

Chakula cha Wakazi Wake

Na chakula cha watu wa Motoni kinaelezwa katika Qur'ani. Mungu anasema:

"Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba ambacho hakinenepeshi wala hakiondoi njaa." (Kurani 88:6-7)

Chakula hakinenepeshi wala hakitaonja vizuri. Hakitakuwa ila ni adhabu kwa watu wa Motoni. Katika vifungu vingine, Mungu anaelezea mti wa zaqqum, chakula maalum cha Jahannamu. Zaqqum ni mti wa kuchukiza, mizizi yake huingia ndani kwa sakafu ya Jahannamu, na matawi yake yaenea kote. Matunda yake mabaya ni kama vichwa vya mashetani. Anasema:

"Hakika Mti wa Zaqqum, chakula cha mwenye dhambi ni kama shaba iliyo yayushwa, hutokota matumboni kama kutokota kwa maji ya moto." (Kurani 44:43-46)

"Je! Kukaribishwa hivi (peponi) si ndio bora, au mti wa Zaqqum? Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa walio dhulumu. Hakika huo ni mti unao toka katikati ya Jahannamu, mashada ya matunda yake kama kwamba vichwa vya mashet'ani. Basi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo, kisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji ya moto yaliyo chemka. Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu." (Kurani 37:62-68)

"Kisha nyinyi, mlio potea, mnao kanusha, Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu na kwa mti huo mtajaza matumbo na juu yake mtakunywa maji yanayo chemka, tena mtakunywa kama wanavyo kunywa ngamia wenye kiu. Hiyo ndiyo karamu yao Siku ya Malipo." (Kurani 56:51-56)

Watu wa Jahannamu watapata njaa kiasi kwamba watakula mti wa kuchukiza wa zaqqum. Na watakapojaza matumbo yao, itaanza kutikisika kama mafuta yanayochemka, na kusababisha mateso makubwa. Wakati huo watakimbilia kunywa maji ya moto sana. Watakunywa kama ngamia walio na kiu, wala haitazima kiu yao. Badala yake viungo vyao vya ndani vitakatikakatika. Mungu anasema:

"…watapewa kunywa maji ya moto, ili kuyakata matumbo yao." (Kurani 47:15)

Misitu ya miiba pamoja na zaqqum itawavuta na kushika katika koo zao kutokana na harufu yake mbaya:

"Hakika Sisi tunazo pingu nzito na Moto unao waka kwa ukali kabisa na chakula kinacho kwama kooni, na adhabu inayo umiza." (Kurani 73:12-13)

Nabii wa Uislamu alisema:

"Na lau kuwa tone kutoka zaqqum lingekuwa duniani, watu wa dunia na riziki zao zote zingeoza. Basi ni vipi kwa yule atakaye kula?" (Tirmidhi)

Na chakula kingine wanachopewa watu wa Jahannamu ni usaha utokao katika ngozi zao, na uchafu unaotoka katika sehemu za siri za watu wazinifu, na ngozi yenye kuoza na nyama ya wanaochomwa motoni. Hiyo ndiyo 'sharubati' ya watu wa Motoni. Mungu anasema:

"Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea huruma, wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni. Chakula hicho hailiwi ila wakosefu." (Quran 69:35-37)

"Ndio hivi! Basi na wayaonje maji ya moto na ya usaha, na adhabu nyenginezo za namna hii." (Kurani 38:57-58)

Hatimaye, baadhi ya wenye dhambi watalishwa Moto kutoka Jahannamu kama adhabu. Mungu anasema:

"Hakika wanao kula mali ya mayatima kwa dhulma, hapana shaka yoyote wanakula matumboni mwao moto, na wataingia Motoni." (Kurani 4:10)

"Hakika wale wafichao aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu katika Kitabu, wakanunua kwa thamani ndogo, hao hawali matumboni mwao isipokuwa moto." (Kurani 2:174)

Vinywaji Vyake

Mwenyezi Mungu anasimulia katika Qur'ani kinywaji cha watu wa Jahannamu:

"watapewa kunywa maji ya moto, ili kuyakata matumbo yao." (Kurani 47:15)

"…Na wakiomba msaada watasaidiwa kwa kupewa maji kama mafuta yaliyo tibuka. Yatayowababua nyuso zao. Kinywaji hicho ni kiovu mno! Na matandiko hayo ya kupumzikia ni maovu mno." (Kurani 18:29)

"Ambaye nyuma yake ipo Jahannamu, na atanywishwa maji ya usaha. Awe anayagugumia, wala hawezi kuyameza. Na mauti yawe yanamjia kutoka kila upande, naye wala hafi. Na zaidi ya hayo ipo adhabu nyengine kali vile vile." (Kurani 14:16-17)

"Ndio hivi! Basi na wayaonje maji ya moto na ya usaha." (Kurani 38:57)

Vinywaji ambavyo watu wa Jahannamu hupata ni kama vifuatavyo:

·Maji ya moto sana kama Mungu anavyosema:

"Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto yanayo chemka." (Kurani 55:44)

"Watanyweshwa kutoka chemchem inayo chemka." (Kurani 88:5)

·Usaha unaotiririka kutoka mwili na ngozi ya mkafiri. Mtume alisema:

"Mtu yeyote ambaye hunywa za kulevya atafanywa kunywa matope ya khabal.“ Wakamuulizaa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni matope gani haya ya khabal? Akasema: “Jasho la watu wa Jahannamu au usaha ya watu wa Motoni.’" (Saheeh Muslim)

·Kinywaji kama mafuta ya moto kilichofafanuliwa hivi na Mtume:

"Ni kama mafuta ya moto, yanapoletwa karibu na uso wa mtu, ngozi ya uso huanguka ndani yake." (Musnad Ahmad, Tirmidhi)

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.