Hadithi ya Ibrahimu (sehemu ya 5 ya 7): Hadithi ya Ibrahimu (sehemu ya 5 ya 7): Karama ya Hajiri na Shida Yake

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Baadhi ya masimulizi ya safari ya Ibrahimu kwenda Misri, kuzaliwa kwa Ishmaeli, na safari ya Hajiri huko Parani.

  • Na Imam Mufti
  • Iliyochapishwa mnamo 10 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 1
  • Imetazamwa: 7,746 (wastani wa kila siku: 7)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Ibrahimu ndani ya Kanaani na Misri

The_Story_of_Abraham_(part_5_of_7_001.jpgIbrahimu alikaa Kanaani kwa miaka kadhaa akienda jiji hadi jiji akihubiri na kuwaalika watu kwa Mungu hadi njaa ilipomlazimisha yeye na Sara kuhamia Misri. Huko Misri kulikuwa na Firauni mdhalimu ambaye alitamani sana kuwamiliki wanawake walioolewa.[1] Maelezo haya ya Kiislamu ni tofauti kabisa na mila za Kiyahudi-Kikristo, ambayo yanasema kwamba Ibrahimu alidai kwamba Sara[2] alikuwa dada yake ili kujiokoa kutoka kwa Firauni.[3]. Firauni akamchukua Sara katika nyumba yake na akamtukuza Ibrahimu kwa ajili yake, lakini nyumba yake ilipokumbwa na magonjwa makali, alikuja kujua kwamba alikuwa ni mke wa Ibrahimu na akamwadhibu kwa kutomwambia hivyo, hivyo kumfukuza kutoka Misri.[4]

Ibrahimu alijua kwamba Sara angevuta hisia zake, kwa hiyo akamwambia kwamba ikiwa Firauni angemuuliza, aseme kwamba yeye ni dada wa Ibrahimu. Walipoingia katika ufalme wake, kama ilivyo tarajiwa, Firauni aliuliza kuhusu uhusiano wake na Sara, na Ibrahimu akajibu kwamba alikuwa dada yake. Ingawa jibu hilo lilipunguza mapenzi yake, bado alimchukua mateka. Lakini ulinzi wa Mwenyezi Mungu ulimuokoa na njama yake mbaya. Firauni alipomwita Sara ili atende kulingana na tamaa zake za kiakili, Sara alimgeukia Mungu katika sala. Mara tu Firauni alipomfikia Sara, sehemu yake ya juu ya mwili ulikakamaa. Alimlilia Sara kwa huzuni, akiahidi kumwachilia ikiwa angemuombea apone! Aliomba kuachiliwa kwake. Lakini tu baada ya jaribio la tatu lililoshindwa ndipo hatimaye aliacha. Kwa kutambua hali yao ya pekee, alimruhusu aende na kumrudisha kwa aliyedhaniwa kuwa kaka yake.

Sara alirudi wakati Ibrahimu alipokuwa akiomba, akisindikizwa na zawadi kutoka kwa Farao, kwa vile alikuwa ametambua hali yao maalumu, pamoja na binti yake mwenyewe Hagari pia, kulingana na mapokeo ya Kiyahudi-Kikristo, kama mjakazi[5]. Alikuwa ametoa ujumbe wenye nguvu kwa Firauni na Wamisri wapagani.

Baada ya kurudi Palestina, Sara na Ibrahimu waliendelea kutokuwa na mtoto, licha ya ahadi za Mungu kwamba angepewa mtoto. Zawadi ya mjakazi ka mwanamke tasa kwa mumewe ili kuzaa inaonekana kuwa jambo la kawaida nyakati hizo[6], Sara alipendekeza kwa Ibrahimu kwamba amchukue Hajiri kama hawara wake. Baadhi ya wasomi wa Kikristo wanasema kuhusu tukio hili kwamba alimchukua kama mke wake[7]. Vyovyote itakavyokuwa, katika mila ya Wayahudi na Wababiloni, mtoto yoyote aliyezaliwa na hawara angekuwa ni wa bibi wa zamani wa hawara huyo na kutendewa sawa sawa kabisa na mtoto aliyezaliwa naye[8], ikiwemo masuala ya urithi. Akiwa Palestina, Hajari alimzalia mtoto wa kiume, Ishmaeli

Ibrahimu ndani ya Makka

Ishmaeli alipokuwa bado ananyonya, Mungu alichagua tena kuijaribu imani ya mpendwa wake Ibrahimu na kumwamuru awapeleke Hagari na Ishmaeli hadi kwenye bonde lisilo na maji la Bakka maili 700 kusini-mashariki mwa Hebroni. Katika nyakati za baadaye ingeitwa Makka. Hakika ulikuwa mtihani mkubwa sana, kwani yeye na familia yake walikuwa wametamani sana wakati huo wa uzao, na macho yao yalijawa na furaha ya kua na mrithi, amri iliwekwa ya kumpeleka katika nchi ya mbali, inayojulikana kwa utasa na shida.

Ingawa Quran inathibitisha kwamba hii ilikuwa mtihani mwingine kwa Ibrahimu wakati Ishmaeli angali mtoto mchanga, Biblia na mapokeo ya Kiyahudi-Kikristo yanadai kwamba ilikuwa ni matokeo ya hasira ya Sara, ambaye alimwomba Ibrahimu kumfukuza Hajari na mwanawe alipoona Ishmaeli "akimdhihaki"[9] Isaka[10] baada ya kuachishwa kunyonya. Kwa kuwa umri wa kawaida wa kuachishwa kunyonya, katika utamaduni wa Kiyahudi angalau , ulikuwa miaka 3[11], hii inadokeza kwamba Ishmaeli alikuwa na takriban miaka 17[12] tukio hili lilipotokea. Inaonekana kimantiki kuwa haiwezekani, kwamba Hajiri angeweza kumbeba mwanaume kijana mabegani mwake na kumpeleka kwa mamia ya maili hadi alipofika Parani, kisha tu kumlaza, kama Biblia inavyosema, chini ya kichaka[13]. Katika aya hizi Ishmaeli anatajwa kwa neno tofauti na lile lililotumika kuelezea kufukuzwa kwake. Neno hili linaonyesha kwamba alikuwa mvulana mdogo sana, labda mtoto, badala ya kijana.

Kwa hiyo Ibrahimu, baada ya kukaa pamoja na Hajari na Ishmaeli, akawaacha huko wakiwa na kiriba cha maji na mfuko wa ngozi uliojaa tende. Ibrahimu alipoanza kuondoka akiwaacha nyuma, Hagari akawa na wasiwasi juu ya kile kilichokuwa kikitendeka. Ibrahimu hakutazama nyuma. Hajari akamkimbilia, ‘Ewe Ibrahimu, unakwenda wapi, ukituacha katika bonde hili ambapo hakuna mtu ambaye tunaweza kufurahia ushirika wake, wala hakuna kitu hapa?’’

Ibrahimu aliharakisha mwendo wake. Hatimaye, Hagari akauliza, ‘Je, Mungu amekuomba ufanye hivyo?’

Ghafla, Ibrahimu akasimama, akageuka nyuma na kusema, ‘Ndiyo!

Akihisi faraja kwa kadiri fulani katika jibu hili, Hagari aliuliza, ‘Ee Ibrahimu, unatuacha kwa nani?’

‘Nina kuacha chini ya uangalizi wa Mungu,’ Ibrahimu akajibu.

Hajiri alijisalimisha kwa Mola wake Mlezi, ‘Nimetosheka kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu!’[14]

Alipokuwa akifuatilia njia yake ya kurudi kwa Ishmaeli mdogo, Ibrahimu aliendelea mpaka akafika kwenye njia nyembamba mlimani ambapo hawangeweza kumwona. Alisimama hapo na kumwomba Mungu kwa maombi:

"Mola wetu Mlezi! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuriya zangu katika bonde lisilo kuwa na mimea, kwenye Nyumba yako Takatifu, ewe Mola wetu Mlezi, ili washike Swala. Basi zijaalie nyoyo za watu zielekee kwao, na waruzuku matunda, ili wapata kushukuru" (Quran 14:37)

Punde, maji na tende zilikwisha na kukata tamaa kwa Hajari kuliongezeka. Kwa kuwa hakuweza kuzima kiu yake au kumnyonyesha mtoto wake mdogo, Hagari alianza kutafuta maji. Akimuacha Ishmaeli chini ya mti, alianza kupanda mteremko wa mawe wa mlima uliokuwa karibu. ‘Labda kuna msafara unapita,’ alijiwazia. Alikimbia kati ya vilima viwili vya Safa na Marwa mara saba akitafuta dalili za maji au msaada, ambapo baadaye zilifananishwa na Waislamu wote katika Hijja. Akiwa amechoka na kufadhaika, alisikia sauti, lakini hakuweza kupata chanzo chake. Kisha, akitazama chini kwenye bonde, alimwona malaika, ambaye anajulikana kama Gabrieli katika vyanzo vya Kiislamu[15], amesimama karibu na Ishmaeli. Malaika akachimba ardhini kwa kisigino chake karibu na mtoto mchanga, na maji yakatoka. Ilikuwa ni muujiza! Hajari alijaribu kutengeneza beseni kulizunguka ili yasitirike nje, na akajaza chombo chake.[16] 'Msiogope kuachwa,” Malaika akasema, ‘maana hii ndiyo Nyumba ya Mungu itakayojengwa na kijana huyu na baba yake, na Mungu kamwe hawapuuzi watu wake.[17] Kisima hiki kiitwacho Zamzam kinatiririka hadi leo katika mji wa Makka katika Rasi ya Uarabuni.

Haikupita muda mrefu baadaye, kabila la Jurham, likihama kutoka kusini mwa Arabia, lilisimama karibu na bonde la Makka baada ya kuona muonekano usio wa kawaida wa ndege akiruka upande wake, ambayo inaweza kumaanisha uwepo wa maji tu. Hatimaye waliishi Makka na Ismail akakua miongoni mwao.

Simulizi kama hilo la kisima hiki limetolewa katika Biblia katika Mwanzo 21. Katika simulizi hili, sababu ya kumuacha mtoto mchanga ilikuwa ni kuepuka kumwona akifa badala ya kutafuta msaada. Kisha, baada ya mtoto huyo kuanza kulia kwa kiu, alimwomba Mungu amwondoe asimwone akifa. Kuonekana kwa kisima hicho kulisemekana kuwa ni kuitikia kilio cha Ishmaeli, badala ya dua yake, na hakuna jitihada zozote kutoka kwa Hajari kutafuta msaada zinazoripotiwa hapo. Pia, Biblia inaeleza kwamba kisima hicho kilikuwa katika nyika ya Parani, ambako walikaa baadaye. Wasomi wa Kiyahudi-Kikristo mara nyingi hutaja kwamba Parani iko mahali fulani kaskazini mwa Rasi ya Sinai, kutokana na kutajwa kwa Mlima Sinai katika Kumbukumbu ya Torati 33:2. Wanaakiolojia wa kisasa wa kibiblia, hata hivyo, wanasema kwamba Mlima Sinai kwa hakika uko katika Saudi Arabia ya kisasa, jambo ambalo linalazimu Parani iwe huko pia.[18]



Rejeleo la maelezo:

[1] Fath al-Bari.

[2] Ingawa Sara alikuwa dada yake wa kambo kulingana na Mwanzo 20:12, na kuifanya ndoa yake kuwa ya ujamaa, vyanzo vya Kiislamu kama vile al-Bukhari, vinadai kwamba hii ilikuwa ni moja kati ya mara tatu ambazo Ibrahimu alikuwa ametoa kauli ya udanganyifu, Sara alivyokuwa dada yake katika imani na ubinadamu, ili kuepusha uovu mkubwa zaidi.

[3] Pamoja na mapokeo, hadithi isiyo na maelezo mengi pia imetajwa katika Biblia, Mwanzo.12.11-20.

[4] Sarah. Emil G. Hirsch, Wilhelm Bacher, Jacob Zallel Lauterbach, Joseph Jacobs na Mary W. Montgomery. (http://www.jewishencyclopedia.com/view.jsp?artid=245&letter=S). Abraham. Charles J. Mendelsohn, Kaufmann Kohler, Richard Gottheil, Crawford Howell Toy. Kitabu cha Kiyahudi. Tazama pia Mwanzo: 12:14-20.

[5] Sarah. Emil G. Hirsch, Wilhelm Bacher, Jacob Zallel Lauterbach, Joseph Jacobs na Mary W. Montgomery. (http://www.jewishencyclopedia.com/view.jsp?artid=245&letter=S). Abraham. Charles J. Mendelsohn, Kaufmann Kohler, Richard Gottheil, Crawford Howell Toy. Kitabu cha Kiyahudi.

[6] Pilegesh. Emil G. Hirsch and Schulim Ochser. Kitabu cha Kiyahudi. (http://www.jewishencyclopedia.com/view.jsp?artid=313&letter=P&search=pilegesh).

[7] (http://whosoeverwill.ca/womenscripturehagar.htm, http://www.1timothy4-13.com/files/proverbs/art15.html).

[8] (http://www.studylight.org/com/acc/view.cgi?book=ge&chapter=016).

[9] Mwanzo 21:9.

[10] Ishmael. Muimbaji Isidore, M. Seligsohn, Richard Gottheil na Hartwig Hirschfeld. Kitabu cha Kiyahudi. (http://www.jewishencyclopedia.com/view.jsp?artid=277&letter=I).

[11] 2 Mk 7:27, 2 Mambo ya Nyakati 31:16.

[12] Ibrahimu ana umri wa miaka 86 wakati wa kuzaliwa kwa Ishmaeli (Mwanzo:16:16), na 100 wakati wa kuzaliwa kwa Isaka (Mwanzo 21:5).

[13] Mwanzo 21:15.

[14] Saheeh Al-Bukhari.

[15] Musnad Ahmad

[16] Simulizi kama hilo limetajwa katika Biblia, ingawa maelezo yake ni tofauti kabisa. Tazama Mwanzo 21:16-19

[17] Saheeh Al-Bukhari

[18] Je, Mlima SINAI uko SINAI? B.A.S.E. Taasisi. (http://www.baseinstitute.org/Sinai_1.html).

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.