Rangi za Umoja wa Uislamu (sehemu ya 1 kati ya 3)
Maelezo: Usawa wa Kiasili ulioungwa mkono na Uislamu na mifano ya kweli ya kihistoria. sehemu ya 1: Ubaguzi ndani ya Uyaudi Jadi za Kikristo.
- Na AbdurRahman Mahdi, www.Quran.nu, (edited by IslamReligion.com)
- Iliyochapishwa mnamo 10 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 01 Jul 2024
- Ilichapishwa: 1
- Imetazamwa: 5,734
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
“Mwenyezi Mungu akasema: Nini kilicho kuzuia kumsujudia nilipo kuamrisha? Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo” (Kurani 7:12)
Mwanzo wa historia ya ubaguzi. Shetani alijiona mkubwa kwa Adam kwasababu ya asili yake. Kuanzia siku ile, Shetani amekipoteza kizazi cha Adam katika kuwaaminisha kuwa wao ni bora kwa wengine, iliyo wasababishia kutesa na kuwanyonya wengine. Mara nyingi, dini imekuwa ikitumiwa kuhalalisha ubaguzi. Uyahudi, kwa mfano, licha ya kuwa na asili ya Mashariki ya Kati, uchukuliwa kama dini ya Kimagharibi; Ila kuingia kwa wayaudi kwenye viwango vyote vya jamii ya kimagharibi hakika inasaliti ukweli wa mafundisho ya kiyaudi. Maandiko matakatifu ya aya ya biblia:“Akuna Mungu duniani kote ila ndani ya Israel.”
(2 Kings 5:15)
…Ingependekezwa kuwa katika siku hizo za Mungu, au Mungu, akuabudiwa ila tu kwa waisraeli. Ila, leo Uyaudi umebaki katikati ya kujisifu kuwa 'wateule' wa asili kwa ubora .
“Sema: Enyi mlio Mayahudi! Ikiwa nyinyi mnadai kuwa ni vipenzi vya Mwenyezi Mungu pasipo kuwa watu wengine, basi yatamanini mauti, ikiwa mnasema kweli.’” (Kurani 62:6)
Kwa upande mwingine, Wakristo wengi sio wayaudi, Yesu, kama mtume wa mwisho wa waisraeli, hakutumwa kwa watu wengine bali wajaudi.[1]
“Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad[2]...’” (Kurani 61:6)
Na kadhalika, kila Mtume alitumwa mahususi kwa watu wake,[3] Kila Mtume, kwa maana hiyo, isipokuwa Muhammad.
“Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote…’” (Kurani 7:158)
Kwa Muhammad kuwa Mtume wa mwisho wa Mungu na Mjumbe, misheni yake ilikuwa ya ulimwengu wote, alikusudiwa sio tu kwa watu wa taifa lake, Waarabu, ila kwa watu wa ulimwengu wote. Mtume amesema:
“Mitume mingine walitumwa mahususi kwa watu wao, bali mimi nimetumwa kwa watu wote.” (Saheeh Al-Bukhari)
“Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri, na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui.” (Kurani 34:28)
Bilal Muhabeshi
Mmoja wa watu wa kwanza kuukubali Uislamu alikuwa mtumwa wa Kiabeshi aliyeitwa Bilal. Kikawaida, Waafrika weusi walikuwa watu wa chini katika mtazamo wa Waarabu ambao waliwaona kuwa na matumizi madogo ya burudani na utumwa. Pindi Bilal aliukubali Uislamu, bwana wake wa kipagani alimfanya ateswe vibaya kwenye joto kali la jangwani hadi Abu Bakr, rafiki wa karibu wa Mtume, alimwokoa kwa kununua uhuru wake.
Mtume alimchagua Bilal kuwaita waumini kwenye sala. Athan ilisikika kutoka kwenye kila kona ya ulimwengu toka wakati huo, mwangwi wa maneno sawa sawa yaliyosomwa na Bilal. Hivyo, hapo mwanzoni mtumwa alipata heshima kama muezzin wa kwanza katika Uislamu.
“Na hakika Tumewatukuza Wanaadamu...” (Kurani 17:70)
Utukufu wa magharibi unasifu Ugiriki ya kale kuwa eneo la uzao wa demokrasia.[4] Ukweli ni kwamba, kama watumwa na wanawake, idadi kubwa ya Waatheni walinyimwa haki ya kuchagua watawala wao. Ila, Uislamu uliamuru kuwa mtumwa anaweza kuwa mtawala! Mtume Aliamuru:
“Mtii mtawala wako hata kama atakuwa mtumwa wa Kiabeshi.” (Ahmad)
Rejeleo la maelezo:
[1] Biblia inakubali. Inaelezwa yesu alisema: ‘Sijatumwa ila tu kwa kondoo waliopotea katika Nyumba ya Israeli. ’ (Matthew 15:24). Hivyo, kila mmoja ya wanafunzi wake kumi na mbili walikuwa Wayaudi wa Kiisraeli . Kifungu kimoja ambacho Yesu anawaambia: ‘Nendeni kafundisheni mataifa yote; wabatize kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.’ (Matayo 28:19), iliyonukuliwa kuthibitisha Wamataifa pia Utatu, haipatikani kwenye maandiko ya mwanzo ya karne ya -16 ambayo inaonekana kama ‘Udanganyifu wa kitakatifu.’
[2] Moja ya jina la Muhammad, Rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
[3] Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba(aseme): Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. (Quran 16:36)
[4] Demokrasia ni uvumbuzi wa Mashariki ya Kati, kwazo ilionekana kwenye tamaduni za Ebla katika milenia ya 3 KK, na pia Phoenicia naMesopotamia kipindi cha karne ya 11 KK. haikuonekana ndani ya Athen hadi karne ya 15KK.
Ongeza maoni