Rangi za Umoja wa Uislamu (sehemu ya 2 kati ya 3)
Maelezo: Usawa wa Kiasili ulioungwa mkono na Uislamu na mifano ya kweli ya kihistoria. sehemu ya 2: Mifano kutoka enzi za Mtume.
- Na AbdurRahman Mahdi, www.Quran.nu, (edited by IslamReligion.com)
- Iliyochapishwa mnamo 01 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 5,950 (wastani wa kila siku: 5)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Salman Muajemi
Kama watu wengi wa taifa lake, Salman alilelewa katika dini ya Majusi. Ila, baada ya kukutana na Wakristo katika kuabudu, aliukubali Ukristo kama ‘kitu bora’. Kisha Salman alisafiri mara nyingi akitafuta maarifa, kutoka kwa mtawa mmoja wa huduma hadi mwingine, wa mwisho alisema: ‘Mwanangu! simjui mtu yoyote mwenye (imani) sawa na sisi . Ila, wakati wa kuja kwa Mtume umewadia. Mtume huyo yupo ndani ya dini ya Abrahamu.’ Mtawa kisha akaendelea kumwelezea Mtume huyo, wasifu wake na wapi atatokea. Salman akaenda Uarabuni, ardhi ya utabiri, na alipomsikia na kukutana na Muhammad, haraka sana akamtambua kutokana na wasifu walioutoa walimu wake na akaukubali Uislamu. Salman alijulikana kutokana na maarifa yake na alikuwa mtu wa kwanza kutafsiri Kurani kwenda kwenye lugha nyingine, Kiajemi. Katika kipindi kimoja, Mtume alipokuwa na Maswahaba wake, alifunuliwa yafuatayo:
“Yeye ndiye aliye mpeleka Mtume kwenye watu wasio jua kusoma... Na kwa wengine ambao bado hawajaungana nao...” (Kurani 62:2-3)
Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kisha akaweka mkono wake kwa Salman na kusema:
“Hata kama Imani ingekuwa karibu na (nyota ya) Kilimia, mtu kutoka (Wahajemi) hakika ataipata.” (Saheeh Muslim)
Suhayb Mrumi
Suhayb alizaliwa katika upendeleo ndani ya nyumba ya kifahari ya baba yake, ambaye alikuwa gavana kwaajili ya utawala wa Kiajemi. Alipokuwa bado mdogo, Suhayb alikamatwa na watembezi wa Byzanti na kuuzwa utumwani ndani ya Konstantinopoli.
Hatimaye, Suhayb alitoroka kutoka utumwa na akakimbilia Makka, sehemu maarufu ya hifadhi, ambapo karibuni atakuwa mfanyabiashara tajiri kwa jina lingine ‘ar-Rumi’, Mrumi, kwasababu ya ulimi wake wa Byzantini na malezi. Pindi Suhayb aliposikia Muhammad anafundisha, mara moja akashawishiwa na ukweli wa ujumbe wake na akaukubali Uislamu. Kama Waislamu wote wa mwanzo, Suhayb aliteswa na wapagani wa Makka. Hivyo, aliuza utajiri wake wote kwaajili ya kuungana na Mtume huko Madina, Ambapo Mtume, alifurahi kumuona Suhayb, akamsalimu mara tatu: ‘Biashara yako imezaa, Wewe [Suhayb]! Biashara yako imezaa!’ Mungu alimtaarifu Mtume kitendo cha Suhayb’s kabla ya kukutana na ufunuo huu:
“Na katika watu yupo ambaye huiuza nafsi yake kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake.” (Kurani 2:207)
Mtume alimpenda Suhayb kuwa jambo kubwa na alimwelezea kuwa Mrumi mwanzilishi wa kuingia kwenye Uislamu. Uchamungu wa Suhaybthat na kusimama pamoja na Waislamu wa mwanzo ulikuwa juu pindi Caliph Umar alipokuwa kwenye kitanda cha mauti, alimchagua Suhayb kuwaongoza hadi atakapopatikana mrithi.
Abdullah Myahudi
Wayahudi walikuwa nchi nyingine ambayo iliwadharau Waislamu Wakiarabu wa mwazo. Wayahudi wengi na Wakristo walikuwa wakimsubiri Mtume mpya kutokea ndani ya Uarabuni katika kipindi cha Mtume Muhammad. Wayahudi haswa kabila la Walawi walikuwa kwa idadi kubwa katika mji wa Medina. Ila, Pindi Mtume aliyetarajiwa alipofika, Sio Myahudi mwana wa Israeli, ila Muarabu mzao wa Ishmaeli, Wayahudi wakamkataa. Isipokuwa, haikuwa, kwa wachache kama Hussein ibn Salam. Hussein alikuwa Mrabbi msomi sana na kiongozi wa Wayahudi Madina ila alishutumiwa na kudhalilishwa na wao alipoukubali Uislamu. Mtume alimpa jina Husayn, ‘Abdullah’, likiwa na maana ya ‘Mtumishi wa Mwenyezi Mungu’, na kumpa ubashiri wa kuingia peponi. Abdullah aliwaambia watu wa kabila lake:
‘Enyi mayahudi! Mjueni Mwenyezi Mungu na kubalini alicholeta Muhammad. Kutoka Kwa Mungu! Kwa hakika mnajua ni Mjumbe wa Mungu na mnaweza kupata utabiri wake kuhusu yeye na utajo wa jina lake na wasifu wake ndani ya Torati. Mimi ninakubali ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. ninaimani nae na ninamuamini ni mkweli. Mimi (peke yangu) nimemtambua.’ Mungu anafunua yafuatayo kuhusu Abdullah:
“na akashuhudia shahidi miongoni mwa Wana wa Israili juu ya mfano wa haya, na akaamini, na nyinyi mnafanya kiburi?.” (Kurani 46:10)
Hivyo, katika vyeo vya Maswahaba wa Mtume Muhammad wanapatikana Waafrika, Waajemi, Warumi na Waisraili; wawakilishi wa kila bara linalojulikana. Kama Mtume alivyosema:
“Hakika, marafiki zangu na wahirika wangu sio kabila hili wala lile. Ila, marafiki zangu na washirika wangu ni wachamungu, Popote walipo.” (Saheeh Al-Bukhari, Saheeh Muslim)
Ongeza maoni