Malaika (sehemu ya 1 kati ya 3): Wameumbwa kumuabudu na kumtii Mungu
Maelezo: Sifa za malaika.
- Na Aisha Stacey (© 2009 IslamReligion.com)
- Iliyochapishwa mnamo 03 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 11 Mar 2024
- Ilichapishwa: 4
- Imetazamwa: 8,500 (wastani wa kila siku: 7)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Waislamu wanaamini uwepo wa malaika. Katika Uislamu kuna nguzo sita za imani; Kumuamini Mungu, Mmoja Pekee, Muumba na Mtunzaji wa yote yaliyopo, kuwaamini malaika Wake, vitabu vyake, wajumbe wake, Siku ya Mwisho na nguvu ya mungu.
Malaika ni sehemu ya ulimwengu wa ghaibu, lakini Waislamu wanaamini uwepo wao kwa uhakika kwa sababu Mungu na mjumbe Wake, Muhammad, wametupatia taarifa kuhusu wao. Malaika wameumbwana Mungu kwaajili ya kumuabudu na kumtii Yeye..
“Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayo amrishwa. ” (Kurani 66:6)
Mungu aliumba malaika kutokana na nuru. Mtume Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, alisema, “Malaika wameubwa kutokana na nuru,”[1]Hatuna maarifa ya kuwa lini malaika waliumbwa, Ila, tunajua kwamba ilikuwa kabla ya kuumbwa kwa wanadamu. Kurani inaelezea kuwa Mungu aliwaambia malaika nia yake ya kutaka kuumba msimamizi duniani. (2:30)
Waislamu wanajua kuwa malaika ni uumbaji mzuri. Ndani ya
Kurani 53:6 Mungu anawaelezea malaika kama dhoo mirrah, neno hili la Kiarabu ambalo wasomi mashuhuru wa Kiislam[2] wanalielezea kuwa, refu na nzuri katika muonekano. Kurani (12:31) pia imemuelezea Mtume joseph kuwa mzuri,kama malaika mwenye kuheshimiwa
Malaika wana mabawa, na wanaweza kuwa kubwa sana. Hakuna chochote katika Kurani, au tamaduni za Mtume Muhammad ambazo zinaonyesha kuwa malaika ni watoto wenye mabawa au wana aina yoyote ya jinsia.[3] lakini tunajua, kuwa malaika wana mabawa na wengine ni wakubwa sana. Kutoka katika tamasuni za Mtume Muhammad tunajua kuwa ukubwa wa malaika Jibrili unajaza “nafasi ya katikakti ya mbingu na ardhi”[4] na ana mbawa mia sita[5].
“...aliye wafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa, mbili-mbili, na tatu- tatu, na nne-nne.....” (Kurani 35:1)
Kuna utofauti pia katika vyeo vya malaika. Malaika ambao walikuwa kwenye vita vya kwanza, Vita vya Badr, wanajulikana kuwa malaika "bora".
“Malaika Jibrili alikuja kwa Mtume na kuuliza, ‘unawakadiliaje baina ya watu waliokuwepo Badr?’ Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, akajibu, ‘Walikuwa Waislam bora,’ au kitu kilicho sawa. Kisha Jibrili akasema: ‘Pia kwa malaika waliokuwepo Badr.’”[6]
Waislamu wanaamini kuwa malaika hawana haja ya kula au kunywa. Uwepo wao ni kumtukuza Mungu na kurudia maneno, hakuna mungu ila Mungu. (Kurani 21:20).
“. . .walioko kwa Mola wako Mlezi wanamtakasa Yeye usiku na mchana, na wao hawachoki.” (Kurani 41:38)
Habari ya Mtume Abraham katika Kurani pia inaonyesha kuwa malaika hawana haja ya chakula. Malaika, kwa mfano wa wanaume, walipomtembelea Mtume Abraham kumpa habari njema ya kuzaliwa kwa mtoto wa kiume, aliwapa ndama kwa heshima yao. Walikataa kula na akaogopa, ndipo walipo jitambulisha kama malaika. (Kurani 51:26-28)
Kuna malaika wengi, lakini Mungu tu ndiye anayejua idadi kamili. Wakati wa kupaa mbinguni, Mtume Muhammad alitembelea Nyumba ya Ibada inayojulikana kama 'nyumba inayotembelewa sana', au, kwa Kiarabu al Bayt al-Mamoor, ya mbinguni inayofanana na Kaaba.[7]
Kisha nikapelekwa hadi kwenye "Nyumba inayotembelewa mara nyingi": kila siku malaika elfu sabini huitembelea na kuondoka, hawarudi tena,(kundi) lingine linakuja baada yao.”[8]
Mtume Muhammad pia ametufahamisha kuwa Siku ya Kiyama, Moto utaletwa na kuonyeshwa kwa watu.Amesema, “Moto utaletwa siku hiyo kwa njia ya kamba elfu sabini, ambayo kila moja itavutwa na malaika elfu sabini.”[9]
Malaika wana nguvu kubwa. Wana uwezo wa kuchukua aina tofauti ya umbo. Walionekana mbele ya Mtume Abraham na Nabii Loti kama wanaume. Malaika Jibrili alimtokea Mariamu mama wa Yesu akiwa mwanadamu, (Kurani 19:17) na alionekana mbele ya Mtume Muhammad kama mwanadamu, ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe sana, na nywele zake zilikuwa nyeusi sana.[10]
Malaika ni wakakamavu. Malaika wanne hubeba kiti cha enzi cha Mungu, na Siku ya Kiyama, idadi yao itaongezeka hadi wanane. Miongoni mwa tamaduni ya Mtume Muhammad inaelezea mmoja wa malaika waliobeba kiti cha enzi cha Mungu. “Umbali kati ya masikio yake na mabega yake ni sawa na safari ya miaka mia saba.”[11]
Malaika hufanya wajibu na majukumu mbali mbali. Wengine wanahusika na mambo ya ulimwengu. Wengine wanahusika na bahari, au milima au upepo. Kipindi kimoja, baada ya kutembelea mji wa Ta’if, mji ulio karibu na Makka, Mtume Muhammad alipigwa mawe. Malaika Jibrili na malaika wa milima walimtembelea.
Malaika wa milima waliomba kuwaharibu watu wakaidi kwa kuwazika chini ya kifusi cha milima miwili iliyo karibu. Mtume Muhammad alikataa ombi hilo kwa sababu aliamini kwamba ikiwa wangepata nafasi ya kutulia na kuutazama Uislam, wangeukubali muunganiko huo na kumpenda Mungu.[12]
Malaika huchukua maagizo ya Mungu bila shaka au kusita. Kila malaika ana jukumu au kazi. Malaika wengine huwalinda na kuwaongoza wanadamu, wengine ni wajumbe. Katika sehemu ya pili tutaangalia majukumu haya na kujifunza majina ya malaika wengine ambao huyafanya.
Rejeleo la maelezo:
[1] Saheeh Muslim.
[2] Ibn Abbas & Qutadah.
[3] Matumizi ya neno Yeye ni kwa matumizi ya urahisi wa kisarufi na kwa njia yoyote haimaanishi kuwa malaika ni wanaume.
[4] Saheeh Muslim
[5] Musnad ya Imam Ahmad.
[6] Saheeh Al-Bukhari
[7] Jengo lenye mchemraba, katikati ya Masjid Takatifu, katika jiji la Makka, Saudi Arabia.
[8] Saheeh Al-Bukhari
[9] Saheeh Muslim
[10] Ibid
[11] Sunan Abu Dawood
[12] Saheeh Al-Bukhari, Saheeh Muslim
Ongeza maoni