Kuwafanyia Wema Wake
Maelezo: Wema kati ya wanandoa kama kielelezo cha imani.
- Na Imam Mufti
- Iliyochapishwa mnamo 14 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 4,288 (wastani wa kila siku: 4)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Utunzaji wa Wake kwa Heshima
Mungu anawaamuru wanaume kuwa wazuri kwa wake zao na kuwatendea wema kwa kadri wanavyoweza:
"… Na kaeni nao kwa wema,…" (Kurani 4:19)
Mtume wa Mungu alisema, Muumini aliye mkamilifu zaidi katika imani ndiye mbora kuliko wote kwa tabia. Mbora kati yenu ni wale ambao ni wabora kwa wake wao.'[1] Mtume wa Rehema anatuambia kuwa vitendo vya mume kwa mkewe vinaonyesha tabia njema ya Muislamu, ambayo nayo ni ishara ya imani ya mtu huyo. Mume wa Kiislamu anawezaje kuwa mwema kwa mkewe? Anapaswa kutabasamu, sio kumuumiza kihisia, kuondoa chochote kitakachomdhuru, kuishi kwa upole, na kumvumilia.
Kuwa mzuri ni pamoja na mawasiliano mazuri. Mume anapaswa kuwa tayari kuwa muwazi, na kuwa tayari kumsikiliza mkewe. Mara nyingi mume anataka kuonyesha maudhi yake (kama kazi). Haipaswi kusahau kumuuliza mkewe kuhusu ya kile kinachomkera (kama watoto hawafanyi kazi zao za nyumbani). Mume hapaswi kuzungumza naye mambo ya muhimu kipindi yeye au mke wake ana hasira, amechoka, au ana njaa. Mawasiliano, maelewano, na kuzingatia ni msingi wa ndoa.
Kuwa mzuri ni pamoja na kumtia moyo mkewe. Pongezi inamaana zaidi inapotoka katika moyo wa dhati unaogundua yale yaliomuhimu- kile mke anathamini sana. Kwa hivyo mume anapaswa kujiuliza ni nini anahisi kinacho muogopesha zaidi na kugundua anachokithamini. Hiyo ni sehemu nzuri ya sifa ya mke. Kadiri mume anavyopongeza, ndivyo mke atakavyopenda, ndivyo tabia hii itakavyoishi zaidi. Maneno mazuri ni kama, "Ninapenda jinsi unavyofikiria," "Unaonekana mzuri kwenye nguo hizo," na "Ninapenda kusikia sauti yako kwenye simu."
Binadamu si wakamilifu. Mtume wa Mungu alisema, "Mwanaume anayeamini hapaswi kumchukia mwanamke aliyeamini. Ikiwa hapendi kitu katika tabia yake, anapaswa kufurahishwa na tabia yake nyingine."[2] Mwanamume hapaswi kumchukia mkewe kwa sababu hapendi kitu ndani yake, atakipata kitu anachopenda juu yake ikiwa atampa nafasi. Njia moja ya kufahamu kile anachopenda kwa mkewe ni kwa mume kufanya orodha ya vitu kadhaa ambavyo anavithamini juu yake. Wataalam wa ndoa wanapendekeza mtu awe mahusui kadri iwezekanavyo na azingatie kwenye tabia - kama vile Mtume wa Uislamu alipendekeza, sio tu yale anayomfanyia mume. Kwa mfano, mume anaweza kujua jinsi anavyopanga nguo kwa usafi, lakini tabia ya msingi inaweza kuwa anafikiria vizuri. Mume anapaswa kuzingatia sifa za kupendeza kama vile kuwa mwenye huruma, mwema, mkarimu, mchaji, mbunifu, mzuri, mkweli, mwenye mapenzi, mtanashati, mpole, mwenye matumaini, aliyejitolea, mwaminifu, mwenye ujasiri, mchangamfu, na kadhalika. Mume anapaswa kujipa muda wa kuunda orodha hii, na kuipitia wakati wa mizozo wakati ana uwezekano wa kuhisi kuchukizwa na mkewe. Itamsaidia kufahamu zaidi sifa nzuri za mkewe na ana uwezekano mkubwa wa kuzipongeza.
Swahaba alimuuliza Mtume wa Mungu haki ya mke juu ya mumewe ni nini? 'Akasema, "Kwamba unamlisha wakati unapokula na kumvika wakati unapovaa na usiupige uso wake. usijitenge mbali naye, isipokuwa nyumbani. "[3]
Migogoro katika ndoa haikwepeki na husababisha hasira nyingi. Ingawa hasira ni moja ya hisia ngumu sana kuidhibiti, hatua ya kwanza ya kuidhibiti inaweza kuwa kujifunza jinsi ya kuwasamehe wale wanaotuumiza. Ikiwa kuna mzozo, mume hapaswi kuacha kuzungumza na mkewe na kumuumiza kihisia, lakini anaweza kuacha kulala kwenye kitanda kimoja ikiwa itapunguza hasira hizo. Katika hali yoyote, hata kipindi cha hasira au katika namna fulani ya kuhisi kuwa na haki, mume hana haki ya kumdhalilisha kwa kutumia maneno ya kuumiza au kumsababishia jeraha lolote.
Ongeza maoni