Je, kuenea kwa Uislamu Kuliathiri Vipi Maendeleo ya Kisayansi?
Maelezo: Katika usawa wa roho ya Uislamu katika kutafuta maarifa, Waislamu na jamii ya Kiislamu wamecheza nafasi nyeti ndani ya maendeleo ya sayansi na teknolojia ndani ya ulimwengu tunaoujua leo.
- Na islam-guide.com
- Iliyochapishwa mnamo 01 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 2
- Imetazamwa: 2,692 (wastani wa kila siku: 2)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Uislamu inamuagiza mwanadamu kutumia nguvu ya akili yake na uchunguzi. Katika miaka michache ya kuenea kwa Uislamu, ustaarabu mkubwa na vyuo vikuu vilishamiri. Mchanganyiko wa mawazo ya Mashariki na Magharibi, na mawazo mapya yakiwa na yale ya zamani,yalileta maendeleo makubwa katika madawa, hesabati, fizikia, unajimu, jiografia, usanifu, sanaa, fasihi, na historia. Mifumo mingi muhimu, kama vile algebra, namba za kiarabu, na wazo la sifuri (muhimu katika hisabati ya juu), ilipitishwa Ulaya ya enzi za kati kutoka katika ulimwengu wa Kiislamu. Vyombo vya kisasa ambavyo vilifanikisha safari za kigunduzi za vyombo vya Ulaya, kama vile astrolabu, roboduara, na ramani nzuri za kusafiria, pia zilitengenezwa na Waislamu.
Ongeza maoni