Wokovu kutoka kwenye Jahanamu
Maelezo: Njia ya wokovu kutokana na mtazamo wa Kiislamu.
- Na islam-guide.com
- Iliyochapishwa mnamo 29 Nov 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 2,660 (wastani wa kila siku: 2)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mwenyezi Mungu amesema kwenye Kurani:
"Hakika wale walio kufuru, na wakafa hali ni makafiri haitakubaliwa kutoka kwa yeyote wao fidia ya dhahabu ya kujaza dunia nzima lau wangeli itoa. Hao watapata adhabu chungu, wala hawatakuwa na wa kuwanusuru." (Kurani 3:91)
Kwa hivyo, maisha haya ndiyo nafasi yetu ya pekee ya kupata Pepo na kuepukana na Moto wa Jahannamu, kwa sababu mtu akifa akiwa hajaamini, hatakuwa na nafasi nyingine ya kurejea katika ulimwengu huu ili aweze kuamini. Kama Mwenyezi Mungu alivyosema katika Kurani kuhusu yatakayowapata wasioamini Siku ya Hukumu:
"Na unge ona watakapo simamishwa kwenye Moto, wakawa wanasema: Laiti tungeli rudishwa, wala hatutakanusha tena Ishara za Mola wetu Mlezi, na tutakuwa miongoni wa Waumini!" (Kurani 6:27)
Lakini hakuna mtu atakaye pata nafasi hii ya pili.
Amesema Mtume Muhammad,rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: “Mtu mwenye furaha kuliko wote duniani miongoni mwa wale waliohukumiwa Motoni Siku ya Kiyama atatumbukizwa Motoni mara moja. Kisha ataulizwa, ‘Mwana wa Adamu, je! umewahi kuona kheri yoyote? Umeshawahi kuona baraka yoyote?' Kisha atasema 'Hapana, kutoka kwa Mungu, Eee Mola!'"[1]
Ongeza maoni