Maelezo ya Kurani Kuhusu Giza Chini ya Bahari na Mawimbi ya Ndani
Maelezo: Maelezo ya Kurani kuhusu maisha katika bahari ya kina, na giza ndani yake, na jinsi inathibitisha matokeo ya kisayansi ya kisasa.
- Na islam-guide.com
- Iliyochapishwa mnamo 23 Nov 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 27 Feb 2023
- Ilichapishwa: 1
- Imetazamwa: 4,669 (wastani wa kila siku: 4)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mungu anasema katika Kurani:
“Au (vitendo vya makafiri) ni kama giza katika bahari kuu, iliyo funikiwa na mawimbi juu ya mawimbi, na juu yake yapo mawingu. Giza juu ya giza. Akiutoa mtu mkono wake anakaribia asiuone...” (Kurani 24:40)
Aya hii inataja giza linalopatikana katika majimakuu, ambapo mtu akinyosha mkono wake, hawezi kuiona. Giza chini ya bahari huanza karibu na kina cha mita 200 kuenda chini. Kwa kina hiki, takriban hakuna mwanga.(angalia picha ya 1). Chini ya kina cha mita 1000 hakuna mwanga kabisa. [1] Binadamu hawawezi kupiga mbizi zaidi ya mita arobaini bila msaada wa manowari au vifaa maalum. Binadamu hawawezi kuishi bila msaada katika sehemu ya giza ya bahari, kama vile kwa kina cha mita 200.
Wanasayansi hivi karibuni wamegundua giza hili kwa kutumia vifaa maalum na nyambizi ambazo zimewawezesha kufikia kina cha bahari.
Pia tunaweza kuelewa kutokana na sentensi zifuatazo katika aya iliyopita, “...katika bahari kuu, iliyo funikiwa na mawimbi juu ya mawimbi, na juu yake yapo mawingu....”, kwamba maji ya kina ya bahari yanafunikwa na mawimbi, na juu ya mawimbi haya ni mawimbi mengine. Ni wazi kwamba aina ya pili ya mawimbi ni mawimbi ya juu tunayoyaona, kwa sababu aya inataja kuwa juu ya mawimbi ya aina ya pili kuna mawingu. Lakini mawimbi ya kwanza ni yapi? Wanasayansi hivi karibuni wamegundua kwamba kuna mawimbi ya ndani ambayo “hutokea kwenye mipaka ya wiani kati ya tabaka za wiani tofauti.” [2] (angalia picha ya 2).
Mawimbi ya ndani yanafunika maji ya kina ya bahari kwa sababu maji ya kina yana wiani mkubwa kuliko maji yaliyo juu yao. Mawimbi ya ndani huwa kama mawimbi ya juu. Yanaweza pia kuvuma, kama mawimbi ya juu. Mawimbi ya ndani hayawezi kuonekana kwa jicho la mwanadamu, lakini yanaweza kugunduliwa kwa kuchambua halijoto au mabadiliko ya kiwango cha chumvi katika mahali fulani.[3]
Ongeza maoni