Uvumilivu wa Mtume kwa Dini Nyingine (sehemu ya 2 kati ya 2): Uhuru wa Kidini na Siasa

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Wengi wanaamini kimakosa kwamba Uislamu hauvumilii kuwepo kwa dini nyingine zilizopo duniani. Makala haya yanazungumzia baadhi ya misingi ambayo Mtume Muhammad mwenyewe aliiweka katika kushughulika na watu wa imani nyingine, kwa mifano ya vitendo toka enzi za uhai wake. Sehemu ya 2: Mifano zaidi kutoka kwa maisha ya Mtume ambayo inaonyesha uvumilivu wake kwa dini nyingine.

  • Na M. Abdulsalam (© 2006 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 17 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 4,962 (wastani wa kila siku: 4)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Kuna mifano mingine mingi katika zama za uhai wa Mtume, rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, pamoja na Swahiyfah inayoonyesha kivitendo uvumilivu wa Uislamu kwa dini nyinginezo.

Uhuru wa Mikusanyiko ya Kidini na Kujitegemea Kidini

Kwa kupata kibali cha katiba, Wayahudi walikuwa na uhuru kamili wa kufuata dini yao. Wayahudi wa Madina wakati wa Mtume walikuwa na shule yao ya elimu, iliyoitwa Bait-ul-Midras, ambapo walikuwa wakisoma Taurati, kuabudu na kujielimisha.

Mtume alisisitiza katika barua nyingi kwa wajumbe wake kwamba taasisi za kidini zisidhuriwe. Hapa katika barua iliyotumwa kwa mjumbe wake kwa viongozi wa kidini wa Mtakatifu Catherine katika Mlima Sinai ambaye aliomba ulinzi wa Waislamu:

“Huu ni ujumbe kutoka kwa Muhammad ibn Abdullah, kama agano kwa wale wanaofuata Ukristo, walio karibu na walio mbali, tuko pamoja nao. Hakika mimi, waja, wasaidizi, na wafuasi wangu nawa walinda, kwa sababu Wakristo ni raia wangu; na kwa Mungu! Ninashikilia dhidi ya chochote kisichowapendeza. Hakuna kulazimishwa kuwa juu yao. Wala majaji wao hawatakiwi kuondolewa katika kazi zao wala watawa wao kutoka katika nyumba zao za watawa. Hakuna mtu wa kuiharibu nyumba ya dini yao, kuibomoa, au kubeba chochote kutoka humo kupeleka kwenye nyumba za Waislamu. Na yeyote akichukua chochote katika haya basi ataharibu ahadi ya Mwenyezi Mungu na kumuasi Mtume wake. Hakika hao ni washirika wangu na wana hati yangu iliyo salama dhidi ya yale wanayoyachukia. Hakuna mtu wa kuwalazimisha kusafiri au kuwalazimisha kupigana. Waislamu wanapaswa kuwapigania. Ikiwa Mkristo wa kike ameolewa na Muislamu, haitafanyika bila idhini yake. Hatakiwi kuzuiwa kutembelea kanisa lake kuomba. Makanisa yao yanatangazwa kulindwa. Hawapaswi kuzuiwa kuyatengeneza wala kuweka utakatifu wa maagano yao. Hakuna hata mmoja katika nchi (Muislamu) atakayevunja ahadi mpaka Siku ya Mwisho (mwisho wa dunia).[1]

Kama mtu awezavyo kuona, Mkataba huu ulikuwa na vifungu kadhaa vinavyoshughulikia masuala yote muhimu ya haki za binadamu, vikiwemo mada kama vile ulinzi wa walio wachache wanaoishi chini ya utawala wa Kiislamu, uhuru wa kuabudu na kutembea, uhuru wa kuwateua majaji wao wenyewe na kumiliki na kudumisha haki mali zao, kutoenda kwenye utumishi wa kijeshi, na haki ya kulindwa vitani.

Katika tukio jingine, Mtume alipokea ujumbe wa Wakristo sitini kutoka eneo la Najran, ambalo wakati huo lilikuwa sehemu ya Yemeni, kwenye msikiti wake. Wakati wa swala yao ulipofika, walielekea upande wa mashariki na wakaswali. Mtume akaamuru waachwe katika hali yao na wasidhuriwe.

Siasa

Pia kuna mifano katika maisha ya Mtume ambapo alishirikiana na watu wa imani nyingine katika uwanja wa kisiasa. Alimchagua asiye Muislamu, Amr-ibn Umaiyah-ad-Damri, kama balozi atakayetumwa kwa Negus, Mfalme wa Ethiopia.

Hii ni baadhi tu ya mifano ya ustahimilivu wa Mtume kwa imani nyingine. Uislamu unatambua kwamba kuna wingi wa dini katika dunia hii, na unawapa haki watu binafsi kuchagua njia wanayoamini kuwa ni ya kweli. Dini haitakiwi, na kamwe haikulazimishwa kwa mtu binafsi kinyume na matakwa yao wenyewe, na mifano hii kutoka katika maisha ya Mtume ni mukhtasari wa aya ya Quran ambayo inakuza uvumilivu wa kidini na kuweka muongozo wa maingiliano ya Waislamu pamoja na watu wa imani nyingine. Mungu anasema:

“…Hapana kulazimisha katika Dini.…” (Kurani 2:256)



Rejeleo la maelezo:

[1]"Waislamu na Wasiokuwa Waislamu, Uso kwa Uso", Ahmad Sakr. Msingi wa Maarifa ya Kiislamu, Lombard IL.

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.