Wanasema nini kuhusu Muhammad (sehemu ya 3 kati ya 3)
Maelezo: Kauli za wasomi wasio Waislamu ambao wamejifunza Uislamu kuhusu Mtume. Sehemu ya 3: Taarifa za nyongeza.
- Na Eng. Husain Pasha (edited by IslamReligion.com)
- Iliyochapishwa mnamo 04 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 4,812 (wastani wa kila siku: 4)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Encyclopedia Britannica:
“....taarifa nyingi katika vyanzo vya mwanzo zinaonyesha kuwa alikuwa mtu mwaminifu na mkweli ambaye alipata kuheshimiwa na kuaminiwa na watu wengine ambao walikuwa watu wenye busara uadilifu kama yeye.” (Juzuu 12)
George Bernard Shaw anasema kuhusu yeye:
“Lazima aitwe Mwokozi wa Mwanadamu. Ninaamini kuwa ikiwa mtu kama yeye angechukua udikteta wa ulimwengu kwa sasa, angefanikiwa kusuluhisha shida zake kwa njia ambayo italeta amani na furaha inayohitajika. ”
(The Genuine Islam, Singapore, Juzuu. 1, nambari 8, 1936)
Alikuwa mtu wa kushangaza zaidi aliyewahi kukanyaga hapa duniani. Alihubiri dini, alianzisha serikali, akaunda taifa, akaweka kanuni za maadili, akaanzisha mageuzi kadhaa ya kijamii na kisiasa, akaanzisha jamii yenye nguvu na yenye kutekeleza na kuwakilisha mafundisho yake na kubadilisha kabisa ulimwengu wa mawazo na tabia ya wanadamu kwa zama zote zijazo.
Mtume Muhammad alizaliwa Uarabuni mnamo mwaka 570 K.W.K., alianza utume wake wa kuhubiri dini ya Ukweli, Uislamu (kujiwasilisha kwa Mungu Mmoja) akiwa na umri wa miaka arobaini na akaondoka ulimwenguni akiwa na umri wa miaka sitini na tatu. Katika kipindi hiki kifupi cha miaka ishirini na tatu cha Utume wake, aliibadilisha Peninsula ya Uarabuni kutoka kwenye upagani na kuabudu masanamu na kuwa na ibada ya Mungu Mmoja, kutoka kwenye ugomvi wa kikabila na vita hadi muungano wa kitaifa na mshikamano, kutoka ulevi na ufisadi na kuwa na subira na utii, kutoka kwenye uasi na uvunjifu hadi maisha ya nidhamu, kutoka kufilisika kabisa hadi kuwa na viwango vya juu vya maadili bora. Historia ya mwanadamu haijawahi kujua mabadiliko kamili kama haya ya watu au mahali ya hapo kabla au tangu hapo - na fikiria maajabu haya ya kushangaza kwa zaidi ya miongo miwili.
Ulimwengu umekuwa na sehemu kubwa ya haiba kubwa. Lakini hawa walikuwa watu wa upande mmoja waliojitofautisha katika uwanja mmoja au miwili, kama vile mawazo ya kidini au uongozi wa jeshi. Maisha na mafundisho ya haiba hizi kubwa za ulimwengu zimegubikwa na ukungu wa muda. Kuna uvumi mwingi juu ya wakati na mahali pa kuzaliwa kwao, muundo na mtindo wa maisha yao, asili na undani wa mafundisho yao na kiwango na kipimo cha kufaulu kwao au kufeli kwao hiyo ni kuwa haiwezekani kwa wanadamu kujenga upya kwa usahihi maisha na mafundisho ya watu hawa.
Sio hivyo kwa mtu huyu. Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, alifanikiwa sana katika nyanja mbali mbali za fikra na tabia ya mwanadamu kwa kasi kubwa ya historia ya mwanadamu. Kila undani wa maisha yake ya kibinafsi na matamshi ya umma yameandikwa kwa usahihi na kuhifadhiwa kwa uaminifu hadi leo. Ukweli wa taarifa ziliyohifadhiwa hauthibitishwi tu na wafuasi waaminifu bali hata na wakosoaji wake wenye chuki.
Muhammad alikuwa mwalimu wa dini, mrekebishaji wa jamii, kiongozi wa maadili, usimamizi, rafiki mwaminifu, rafiki mzuri, mume aliyejitolea, baba mwenye upendo -zote kwa pamoja. Hakuna mtu mwingine katika historia aliyewahi kumshinda au kumfananisha katika mojawapo ya mambo haya tofauti ya maisha - lakini ilikuwa tu kwa utu wa kujitolea wa Muhammad kufikia ukamilifu wa ajabu sana.
Mahatma Gandhi, anaongelea wasifu wa Muhammad,anasema kwenye (Young India):
"Nilitaka kujua zaidi ya ubora wa mtu anayeshikilia ushawishi wa leo usio na ubishani juu ya mioyo ya mamilioni ya wanadamu.... nimeshawishiwa zaidi kuwa sio upanga ulioshinda dhima ya Uislamu kwenye enzi hizo katika mfumo wa maisha. Ilikuwa ni unyenyekevu thabiti, kujitolea kwa Mtume, kujali sana ahadi zake, kujitolea kwake sana kwa marafiki na wafuasi wake, ushujaa, kutokuwa na hofu, imani yake kamili kwa Mungu na utume wake mwenyewe. Hizi na sio upanga zilibeba kila kitu mbele yao na kushinda kila kikwazo. Wakati nikifunga jalada la 2 (la wasifu wa Mtume), nilikuwa na huzuni kuwa hakukuwa na cha zaidi cha mimi kusoma juu ya maisha mazuri. "
Thomas Carlyle katika (Mashujaa na Kuabudu Mashujaa), alishangaa kuwa:
"Jinsi mtu mmoja peke yake, alivyoweza kuunganisha makabila yanayopigana na Wabedouin wanaotangatanga kuwa taifa lenye nguvu zaidi na lililostaarabika katika kipindi kisichozidi miongo miwili."
Diwan Chand Sharma ameandika:
"Muhammad alikuwa roho ya wema, na ushawishi wake ulihisiwa na haukusahauliwa na wale walio karibu naye."
(D.C. Sharma, The Prophet of the East, Calcutta, 1935, uk. 12)
Muhammad hakuwa zaidi au kidogo kuliko mwanadamu. Lakini alikuwa mtu mwenye shughuli tukufu, ambayo ilikuwa kuwaonganisha wanadamu kwenye ibada ya Mungu Mmoja na Pekee na kuwafundisha njia ya kuishi kwa uaminifu na usawa kulingana na amri za Mungu. Siku zote alijielezea kama, "Mtumishi na Mjumbe wa Mungu," na kwa hivyo kila kitendo chake alikitangaza hivyo.
Ukizungumzia suala la usawa mbele za Mungu katika Uislam, mshairi mashuhuri wa India, Sarojini Naidu anasema:
“Ilikuwa dini ya kwanza kuhubiri na kutekeleza demokrasia; kwani, msikitini, wakati wito wa sala unaitwa na waumini wamekusanyika pamoja, demokrasia ya Uislamu inajumuishwa mara tano kwa siku wakati mkulima na mfalme wanapiga magoti kwa pamoja na kutamka: 'Mungu Peke Yake ni Mkuu'...Nimehsngazwa mara kwa mara na kuwa umoja wa Kiislamu unaomfanya mtu kuwa ndugu kindakindaki.”
(S. Naidu, Ideals of Islam, vide Speeches & Writings, Madras, 1918, uk. 169)
Kwa maneno ya Prof. Hurgronje:
"Shirikisho la mataifa lililoanzishwa na mtume wa Uisilamu liliweka kanuni ya umoja wa kimataifa na udugu wa kibinadamu kwenye misingi ya ulimwengu kama kuonyesha mishumaa kwa mataifa mengine." Anaendelea: "Ukweli ni kwamba hakuna taifa lolote ulimwenguni linaloweza kuonyesha ulinganifu na kile Uislamu umefanya kuelekea kutimiza wazo la Jumuiya ya Mataifa."
Ulimwengu haukusita kuinuka kwa ibada, watu ambao maisha yao na ujumbe wao umepotea katika hadithi. Kwa kusema kihistoria, hakuna hata moja ya hadithi hizi zilizofanikiwa hata sehemu ndogo ya kile Muhammad alichokitimiza. Na bidii yake yote ilikuwa kwa kusudi moja la kuwaunganisha wanadamu katika ibada ya Mungu Mmoja kwa kanuni ya ubora wa maadili. Muhammad au wafuasi wake kamwe hawakudai wakati wowote kwamba alikuwa Mwana wa Mungu au Mungu-aliyemwiliishwa au mtu mwenye uungu - lakini alikuwa daima na hata leo anachukuliwa kama Mjumbe aliyechaguliwa na Mungu tu.
K. S. Ramakrishna Rao, Profesa wa India wa Falsafa katika kijitabu chake, ("Muhammad, The Prophet of Islam,") anamwita
“Muundo sahihi wa maisha ya mwanadamu.”
Prof. Ramakrishna Rao anaielezea wazo lake:
“Wasifu wa Muhammad, ni ngumu sana kuupata ukweli wote wa jambo hilo. kwa kidogo unaweza kuupata. Mfululizo mzuri kama wa maudhui! Kuna Muhammad, Mtume. Yuko Muhammad, Shujaa; Muhammad, Mfanyabiashara; Muhammad, Mtawala; Muhammad, Msemaji; Muhammad, Mwanamageuzi; Muhammad, Kimbilio la Yatima; Muhammad, Mlinzi wa Watumwa; Muhammad, muwekaji huru Wanawake; Muhammad, Jaji; Muhammad, Mtakatifu. Kwa majukumu yote haya mazuri, katika idara hizi zote za shughuli za kibinadamu, yeye ni shujaa hasa.”
Leo baada ya kupita kwa karne kumi na nne, maisha na mafundisho ya Muhammad yameishi bila kupotea hata kidogo, kubadilishwa au kuingiliwa. Yanatoa tumaini lile lile la kutibu magonjwa mengi ya wanadamu, ambayo yalifanya kipindi akiwa hai. haya sio madai ya wafuasi wa Muhammad lakini pia ni hitimisho lisiloweza kuepukika linalazimishwa na historia isiyo na upendeleo.
Kidogo unachoweza kufanya kama mwanadamu anayefikiria na anayejali ni kusimama kwa muda mfupi na jiulize: Je! Taarifa hizi zinazoonekana kuwa za kushangaza na za kimapinduzi zinaweza kuwa za kweli kabisa? Na ukidhani ni kweli kabisa na hukumjua huyu mtu Muhammad au kusikia kuhusu yeye, je, huu si ndio muda muafaka wa kushughulikia changamoto hii kubwa na kuweka bidii katika kumjua?
Haitakugharimu chochote lakini inaweza kudhibitisha kuwa mwanzo wa enzi mpya kabisa maishani mwako.
Ongeza maoni