Utabiri wa Bibilia Kuhusu Muhammad (Sehemu ya 3 kati ya 4): Utabiri wa Muhammad katika Agano Jipya
Maelezo: Ushahidi wa Biblia kwamba Muhammad si nabii wa uongo. Sehemu ya 3: Majadiliano juu ya utabiri uliotajwa katika Yohana 14:16 wa Paraklete, au “Msaidizi”, na jinsi Muhammad anavyoafikiana na utabiri huu zaidi ya wengine.
- Na Imam Mufti
- Iliyochapishwa mnamo 23 Nov 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 2
- Imetazamwa: 45,938 (wastani wa kila siku: 40)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Yohana 14:16 "Nami nitamwomba Baba, naye atawapeni Msaidizi mwingine akae nanyi siku zote."
Katika aya hii, Yesu anaahidi kwamba “Msaidizi” mwingine atatokea, na hivyo, ni lazima tuzungumze baadhi ya masuala kuhusu huyu “Msaidizi”.
Neno la Kigiriki paravklhtoß, ho parakletos, limetafsiriwa kama 'Msaidizi.' Parakletos kwa usahihi ina maana 'yule anayeomba kwa niaba ya mwingine, mwombezi.'[1] Ho parakletos (Msaidizi ) ni mtu katika lugha ya Kigiriki, si kipengele kisichokuwa na mwili. Katika lugha ya Kigiriki, kila nomino ina jinsia; yaani, ni kiume, kike au ni huru. Katika Injili ya Yohana, Sura 14, 15 na 16 ho parakletos ni mtu halisi. Viwakilishi vyote kwa Kigiriki lazima vikubaliane kijinsia na neno ambalo vinawakilisha, na kiwakilishi “yeye(kiume)” kimetumika kurejelea parakletos. Agano jipya linatumia neno pneuma, ambalo linamaanisha “pumzi” au “roho,” na lina maana sawa na neno ruah, neno la Kiebrania linalo maanisha “roho” linalotumiwa katika Agano la kale. Pneuma ni neno la kisarufi huru na daima linawakilishwa na kiwakilishi “ni.”
Biblia zote za kisasa zimekusanywa kutoka “miswada ya kale,”ambapo mswada wa zamani zaidi ni wa karne ya nne B.K. Hakuna miswada miwili ya kale inayofanana. [2] Biblia zote za leo zinaandikwa kwa kuchanganya miswada bila kumbukumbu moja ya uhakika. Watafsiri wa Biblia hujaribu “kuchagua” toleo sahihi. Kwa maana nyingine, kwa kuwa hawajui ni “mswada wa kale” upi ndio sahihi, wanaamua kwa niaba yetu ni “toleo” lipi la aya fulani ndio sahihi. Chukua Yohana 14:26 kama mfano. Yohana 14:26 ndiyo aya pekee ya Biblia inayohusisha Parakletos na Roho Mtakatifu. Lakini “miswada ya kale” hayakubali kuwa “Parakletos” ndiye 'Roho Mtakatifu. ' Kwa mfano, Kodeks Syriakus, iliyoandikwa takriban karne ya tano B.K., na kugunduliwa mwaka wa 1812 juu ya mlima Sinai, maandishi ya 14:26 yanasoma; “Paraklete, Roho”; na si “Paraklete, Roho Mtakatifu.”
Kwa nini hii ni muhimu? Kwa sababu katika lugha ya Biblia, “roho,” inamaanisha tu “nabii.”
“Wapendwa, msiamini kila roho bali zipimieni roho zote kwa makini muone kama zinatoka kwa Mungu: Kwa maana manabii wengi wa uongo wametokea duniani."[3]
Ni jambo la kuelimisha kujua kwamba wasomi kadhaa wa Bibilia waliona parakletos kuwa 'mwokovu huru (aliye na uwezo wa kuokoa), 'na si Roho Mtakatifu.[4]
Swali, basi, ni: Je, parakletos wa Yesu, Msaidizi,alikuwa ni 'Roho Mtakatifu' au mtu - nabii - ambaye angekuja baada yake? Ili kujibu swali, ni lazima tuelewe maelezo ya ho parakletos na kuona kama yanaafikiana na roho au mwanadamu.
Tunapoendelea kusoma zaidi ya sura ya 14:16 na sura ya 16:7, tunaona kwamba Yesu anatabiri maelezo maalum ya kuwasili kwa na utambulisho wa parakletos. Kwa hiyo, kulingana na Yohana 14 na 16 tunagundua mambo yafuatayo.
1. Yesu alisema parakletos ni mwanadamu:
Yohana 16:13 "Atanena..."
Yohana 16:7 "…kwa maana nisipoondoka, yule Msaidizi hatakuja kwenu."
Haiwezekani kwamba Msaidizi awe ni “Roho Mtakatifu” kwa sababu Roho Mtakatifu alikuwepo kwa muda mrefu kabla ya Yesu na wakati wa huduma yake.[5]
Yohana 16:13 Yesu alimwongelea paraklete kama 'yeye' na si kama 'kitu' kwa mara saba, hakuna mstari mwingine katika Biblia ambao una viwakilishi saba vya kiume. Kwa hivyo, paraklete ni mtu, na sio roho.
2. Yesu anaitwa parakletos:
"Lakini kama mtu yeyote akitenda dhambi, tunaye mtetezi (parakletos) wetu kwa baba, Yesu Kristo mwenye haki." (1 Yohana 2:1)
Hapa tunaona kwamba parakletos ni mwombezi aliye na mwili na ni mwanadamu.
3. Uungu wa Yesu ni Uvumbuzi uliokuja baadaye
Yesu hakukubaliwa kuwa mungu hadi Baraza la Nikea, 325 BK, lakini kila mtu, isipokuwa Wayahudi, anakubaliana kuwa alikuwa nabii wa Mungu, kama ilivyoonyeshwa na Biblia:
Matayo 21:11 "...Huyu ni Yesu, yule nabii kutoka Nazareti katika Galilaya."
Luka 24:19 "...Yesu wa Nazareti. Yeye alikuwa nabii mwenye mkuu katika maneno yake na matendo yake, mbele za Mungu na mbele za wanadamu."
4. Yesu alimwomba Mungu awape parakletos mwingine:
Yohana 14:16 "Nami nitamwomba Baba, naye atawapeni Msaidizi mwingine akae nanyi siku zote."
Vielezi-chini:
[1] Kamusi ya Ufafanuzi ya Vine ya Maneno ya Agano Jipya.
[2]"Mbali na utofauti mkubwa, kama huu, ni nadra sana kuona mstari ambao hauna tofauti ya maneno katika baadhi ya nakala [ya miswada ya kale ambayo Biblia imekusanywa kutoka kwayo]. Hakuna mtu anayeweza kusema kwamba nyongeza hizi au mapungufu au mabadiliko ni mambo madogo ya hitilafu tu.” 'Biblia Yetu na Maandishi ya Kale, ' Dk. Frederic Kenyon, Eyre na Spottiswoode, ukurasa wa 3.
[3]1 Yohana 4: 1-3
[4]‘...Mapokeo ya Kikristo yametambua kitu hiki (Paraklete) kuwa ni Roho Mtakatifu, lakini wasomi kama Spitta, Delafosse, Windisch, Sasse, Bultmann, na Betz wana shaka kama kitambulisho hiki ni kweli kwa picha ya awali na wamependekeza kuwa Paraklete mwanzoni alikuwa mwokovu huru, ila baadaye alichanganywa na Roho Mtakatifu.” 'Biblia ya Mtangazaji, Doubleday & Company, Inc, Garden City, N.Y 1970, Volume 29A, uk. 1135.
[5]Mwanzo 1: 2, 1 Samueli 10: 10, 1 Samueli 11: 6, Isaya 63: 11, Luka 1: 15, Luka 1: 35, Luka 1: 41, Luka 1: 67, Luka 2: 25, Luka 2: 26, Luka 3:22, Yohana 20: 21-22.
Ongeza maoni