Maswali Saba ya Kawaida kuhusu Uislam (sehemu ya 1 kati ya 2)

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Baadhi ya maswali ya kawaida yanayoulizwa kuhusu Uislamu. Sehemu ya 1: Uislamu ni nini? Waislamu ni wakina nani? Allah ni nani? Muhammad ni nani?

  • Na Daniel Masters, Isma'il Kaka and Robert Squires
  • Iliyochapishwa mnamo 08 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 3
  • Imetazamwa: 12,125
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

1. Uislamu ni nini?

Seven_Common_Questions_about_Islam_(part_1_of_2)_001.jpgUislamu ni jina la dini, au kiufasaha zaidi ni ‘njia ya maisha’, ambayo Mungu (Allah) aliifunua na ilifanywa na Manabii na Mitume wa Mungu ambao aliituma kwa wanadamu. Hata jina lake lipo juu na la kipekee miongoni mwa dini zingine kwa kumaanisha hali ya kuwa; haimuhusishi mtu flani, kama vile Ukristo, Ubudha au Uzoroasta; kabila kama la Mayahudi; au nchi kama Uhindu. Ni mzizi wa neno la Kiarabu Islam kwa kuchukua maana ya amani, usalama, heshima, ulinzi, kutokuwa na lawama, uzuri, kujitoa, kukubali, kujisalimisha, na wokovu. Hususani Uislamu una maana kuwa katika hali ya kujisalimisha kwa Mungu, kumwabudu Yeye peke Yake, na kukubali na kutii Sheria Yake. Kwa kujisalimisha, amani, ulinzi, na maisha yote yakifanya hivyo maana yake itatimia. Hivyo, Muslim au Muslimah ni mtu (mwanume au mwanamke) wapo ndani ya kujisalimisha huko. Uislamu wa mtu udhoofika kwa dhambi, ujinga, na matendo mabaya, na hutenguka kwa kumshirikisha Mungu au kutokumwamini Yeye.

2. Waislamu ni Akina nani?

Neno la Kiarabu “Muslim” linamaanisha “mtu mwenye kutekeleza mambo ya Uislam (kujisalimisha katika mapenzi na sheria ya Mungu)”. Ujumbe wa Uislamu umemaanishwa kwa ulimwengu wote, na mtu yoyote atakaye ukubali ujumbe huu anakuwa Muislamu. Baadhi ya watu wanaamini vibaya kuwa Uislamu ni dini tu ya Waarabu, Ila ukweli uko mbali sana na hili. Kiuhalisia, zaidi ya 80% ya Waislamu wote duniani siyo Waarabu Japokuwa Waarabu wengi ni Waislamu, kuna Waarabu ambao ni Wakristo, Wayahudi na Wasiokuwa na dini. Kama mtu akiangalia watu mbali mbali wenye kuishi katika dunia ya Waislamu - kuanzia Nigeria hadi Bosnia na kuanzia Morocco hadi Indonesia - ni rahisi kuona Waislamu wanatoka kwenye asili mbalimbali, vikundi vya makabila, tamaduni na uraia. Uislamu umekuwa ujumbe wa kilimwengu kwa watu wote. Hili linaweza kuonekana kwa Maswahaba wa mwanzo wa Mtume Muhammad hawakuwa tu Waarabu, ila pia Waajemi, Waafrika na Waroma wa Byzantine. Kuwa Muislamu kunamaanisha ukubali kikamilifu na utii kikamilifu katika mafundisho ya ufunuo na sheria za Mungu Mkuu. Muislamu ni mtu aliyekubali kwa uhuru akiamini ndani ya imani yake, kuthamini na imani kwa mapenzi ya Mungu Mtukufu. Zamani, japokuwa hauoni sana hivi sasa, neno “Mohammedans” lilitumika kama chapa ya Waislamu. Chapa hii haifai, na ndio matokeo ya labda upotovu wa makusudi au ni ujinga tu. Moja ya sababu ya upotovu huu ni kuwa Wazungu walifundishwa kwa karne kuwa Waislamu wanamuabudu Mtume Muhammad katika njia sawa ya Wakristo wanavyo muabudu Yesu. Hii siyo kweli, Wakati mtu hatachukuliwa kuwa Muislamu kama atamuabudia yoyote au chochote asiyekuwa Mungu Mtukufu.

3. Allah ni nani?

Mara nyinyi mtu anakuwa amesikia neno la Kiarabu la “Allah” likiwa linatumika kwenye maongezi yanayohusu Uislamu. Neno “Allah” ni neno la Kiarabu lenye maana ya Mungu Mtukufu, pia ni neno moja linalotumiwa na wanaoongea Kiarabu Wakristo na Wayahudi. Na kiujumla, neno Allah lilikuwa linatumika zamani sana kabla ya neno God, kwakuwa Kingereza ni lugha mpya. Kama mtu angechukua Biblia iliyo tafsiriwa Kiarabu, mtu angeliona neno “Allah” linatumika ambapo neno “God” linatumika kwa Kingereza. Kwa mfano, Wakristo wanaoongea Kiarabu wanasema Yesu ni, kulingana na dini yao, Mtoto wa Allah. Kwa kuongezea, neno la Kiarabu la Mungu Mtukufu ni, “Allah”, ni neno sawa na God katika lugha nyingine ya Kiyahudi. Kwa mfano, Neno la Kihebrew kwaajili ya Mungu ni “Elah”. Katika sababu mbali mbali, baadhi ya wasiokuwa Waislamu kwa bahati mbaya wanaamini kuwa Waislamu wanamuabudu Mungu mwingine asiye kuwa Mungu wa moses na Abraham na Yesu. Hii siyo kweli, kwakuwa Monotheismu wa kweli wa Uislamu huwaita watu wote kumuabudu Mungu wa Noah, Abraham, Moses, Yesu na Mitume yote mingine, amani iwe juu yako.

4. Muhammad ni nani?

Mwisho na Mtume wa mwisho ambaye ametumwa na Mungu kwa mwanadamu alikuwa Mtume Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake. Katika umri wa miaka arobaini, alipokea ufunuo kwa Mungu. Kisha akatumia muda wake uliobakia kuelezea, na kuishi na kufundisha Uislamu, dini ambayo Mungu amemfunulia. Mtume Muhammad ni mkubwa kuliko wote kwa sababu nyingi, ila kubwa ni kuchaguliwa na Mungu kuwa Mtume wa mwisho - jukumu lake kuwaongoza wanadamu litaendelea hadi Siku ya Mwisho - na kwasababu alitumwa kama rehema kwaajili ya mwanadamu. matokeo ya kazi yake imewaleta watu katika imani ya Mungu Mmoja zaidi ya mtume yoyote. Tangu mwazo wa muda, Mungu ametuma mitume katika dunia, kila mmoja katika nchi mahususi. Mtume Muhammad, hata hivyo, alitumwa kama Mjumbe wa mwisho kwa wanadamu wote.

Japokuwa jamii nyingine za kidini zinadai kumuamini Mungu Mmoja, baada ya muda, mawazo potofu huingia kwenye imani na matendo ikiwapeleka mbali na monotheismu ya mitume. Wengine waliwachukulia manabii na watakatifu wao kuwa waombezi wao kwa Mungu Mtukufu. Wengine hata waliamini mitume yao ni udhihirisho wa Mungu, au “Mungu aliyefanyika mwili” au “Mwana wa Mungu”. Dhana hizi potofu husasabisha ibada ya viumbe vilivyoumbwa badala ya Muumbaji, na kuchangia ibada ya masanamu kuamini kuwa Mungu Mtukufu anaweza kufikiwa kwa makubaliano. Ili kujilinda na uongo huu, Mtume Muhammad alikuwa mara zote anajieleza kuwa yeye ni mwanadamu akiwa na kazi ya kuhubiri na kutii ujumbe wa Mungu. Aliwaambia Waislamu kumchukulia yeye kama “Mjumbe wa Mungu na Mtumwa wake”. Katika maisha yake na mafundisho, Mungu amemfanya Mtume Muhammad kuwa mfano wa watu wote - alikuwa nabii wa mfano, mkuu wa nchi, kiongozi wa jeshi, mtawala, mwalimu, jirani, mume, baba na rafiki. Tofauti na manabii na wajumbe wengine, Mtume Muhammad aliishi kwenye mwanga kamili wa historia,na maneno yake na vitendo vilinakiliwa kwa umakini na kukusanywa. Waislamu hawahitaji kuwa na imani tu kuwa alikuwepo, au kuwa mafundisho yake yamehifadhiwa - wanajua kuwa ni kweli. Mungu amechukua mwenyewe kulinda ujumbe uliofunuliwa kwa Muhammad kutoka kwenye uharibifu au kusahaulika au kupotea. Hii ilikuwa muhimu kwasababu Mungu aliaidi Muhammad kuwa Mjumbe wa mwisho kwa wanadamu. Wajumbe wote wa Mungu walihubiri ujumbe wa Uislamu - mf. kujisalimisha katika sheria za Mungu na kumuabudu Mungu peke yake – ila Muhammad ni mtume wa mwisho wa Uislamu ambaye alileta ujumbe wa mwisho na kamili ambao hautaweza kubadilishwa hadi Siku ya Mwisho.

Mbaya Nzuri zaidi

Maswali Saba ya Kawaida kuhusu Uislam (sehemu ya 2 kati ya 2)

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Baadhi ya maswali ya kawaida yanayoulizwa kuhusu uislamu. sehemu ya 2: Kuhusu mafundisho ya Uislamu na Kurani Tukufu.

  • Na Daniel Masters, Isma'il Kaka and Robert Squires
  • Iliyochapishwa mnamo 08 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 3
  • Imetazamwa: 8,104
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

5. Mafundisho ya Uislamu ni yapi?

Msingi wa imani ya Kiislamu ni kuamini katika Monotheism (Umoja wa Mungu). Hii inamaana kuamini kuna Muumbaji mmoja na tegemeo la kila kitu ulimwenguni , na akuna kitu chenge utukufu au thamani ya kuabudiwa pasina Yeye. Kiuhakika, Kuamini katika Umoja wa Mungu inamaana zaidi ya kuamini “Mungu Mmoja” - tofauti na moja, tatu au nne. Kuna idadi kubwa ya dini zinazo dai kumwamini “Mungu Mmoja” na kuamini mwisho kuwa kuna Muumbaji mmoja na tegemeo la kila kitu ulimwenguni, ila monotheism ya ukweli ni kuamini kuwa Umoja wa Kweli wa Mungu ni kuabudu kulingana na ufunuo Alioutuma kwa Mtume wake. Uislamu unapinga matumizi ya muunganisho wa Mungu na mwanadamu, na kusisitiza watu wamfuate Mungu moja kwa moja na kufanya ibada zote kwake Yeye pekee. Waislamu wanaamini Mungu Mtukufu ni mwenye Huruma, Upendo na Neema.

Upotovu mwingine ni kudai kuwa Mungu hawezi kuwasamehe viumbe wake moja kwa moja. Kwa kuonyesha uzito na adhabu ya dhambi, na pia kudai Mungu hawezi kumsamehe mtu moja kwa moja, watu mara nyingi wanakatia tamaa Rehema ya Mungu. Pindi wakiamini hawawezi kumfuata Mungu moja kwa moja, wanafuata miungu ya uongo kwaajili ya msaada, kama mashujaa, viongozi wa siasa, waokoaji, watakatifu,na malaika. Mara nyingi tunaona kuwa watu wanao abudu kwa, kusali kwaajili ya, au kutafuta muunganisho kutoka kwa miungu ya uongo, haiwafanyi kuwa ‘mungu’. Wanadai kumuamini Mungu Mmoja Mkubwa, ila wanadai kumuabudu na mwingine pasina Mungu ili tu wawe karibu na Yeye. Kwenye Uislamu, kunautofauti mkubwa baina ya Muumbwaji na muumbwaji. Hakuna ubishi au siri katika swala la uungu: kitu chochote kilichotengenezwa hakina haki ya kuabudiwa; Allah pekee, Muumbaji, ana haki ya kuabudiwa. Dini zingine wanaamini vibaya kuwa Mungu Amekuwa sehemu ya alichokiumba, na hii imepelekea watu kuamini wanaweza kuabudia kitu kilichoubwa ili kumfikia Muumbaji.

Waislamu wanaamini kuwa japo Mungu ni Wakipekee na Mkuu zaidi ya mafikirio, Hakika hana mshirika, washirika, wenzake, wapinzani au watoto. Kulingana na imani ya Uislam, Allah “hakuzaa, wala Hakuzaliwa” - hana asili, wala mfano wake, wa mifano, halisi au wa kufanana naye. Ni wa Kipekee na Wamilele. Yeye mwenye udhibiti wa kila kitu na anauwezo wote wa kumpa Rehema na Msamaha kwa yoyote Anaye mchagua Hiyo ndiyo sababu Allah anaitwa Mwenye Nguvu zote na Mwenye Rehema. Allah ametengeneza ulimwengu kwaajili ya mwanadamu, na kwa hivyo kumtakia kilicho bora kwa mwanadamu. Waislamu wanaona kila kitu katika ulimwengu kama ishara ya Uumbaji na Ukarimu wa Mungu Mtukufu. Pia, imani ya umoja wa Allah ni dhana ya metafiziko ni imani yenye nguvu yenye kuathiri mtazamo wa mwanadamu, jamii na dhana zote za maisha. Kama mawazo ya hatma ya imani ya Kiislamu katika Umoja wa Allah, ni imani ya umoja wa mwanadamu na ubinadamu.

6. Kurani ni nini?

Kurani ni ufunuo wa mwisho wa Allah kwa viumbe vyote, ambao uliongelewa na Allah aliye Utukuza Mwenyewe na kupelekwa na Malaika Jibrili kwa Kiarabu kwa Mtume Muhammad, kwa sauti, neno na maana. Kurani, (mara nyingine uandikwa vibaya kama Koran), kisha ikafikishwa kwa maswahaba wa Mtume, na kwa bidii waliihifadhi kwa kukariri neno kwa neno na kuiweka katika maandishi. Kurani Tukufu ilikuwa ikiendelea kusomwa na maswahaba wa Mtume na warithi wao hadi wakati wa sasa. kwa kifupi, Kurani kitabu cha ufunuo wa Maandiko ya Mungu kutoka kwa Allah kwa wanadamu wote kwa mwongozo na wokovu wake.

Leo Kurani bado inakaririwa na kufundishwa na mamilioni ya watu. Lunga ya Kurani, Kiarabu, bado lugha ya maisha ya mamilioni ya watu. Tofauti na maandiko ya dini zingine, Kurani bado inasomwa katika lugha yake ya asili na mamilioni ya watu. Kurani ni muujiza unaoishi katika lugha ya Kiarabu, na inajulikana aina yake ya uzuri, muundo na athari za kiroho, na pia maarifa iliyokuwa nayo. Kurani ilifunuliwa kimfululizo kwa Mtume Muhammad katika kipindi cha miaka 23. Tofauti na vitabu vingine vya dini, Kurani mara zote inaaminiwa kuwa maneno halisi ya Allah. Kurani ilikuwa inasomwa hadharani kwa jamii ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu katika kipindi cha Mtume Muhammad, na baadaye. Kurani nzima ilikamilika kuandikwa katika maisha ya Mtume, na idadi ya maswahaba waliikariri Kurani neno kwa neno kama ilivyofunuliwa. Kurani mara zote ilikuwa katika mikono ya walioamini: mara zote inafikiriwa kuwa maneno ya Mungu; na, kwa sababu ya kukaririwa na watu wengi, ilihifadhiwa vizuri. Haikuwahi kuharibiwa au kupotezwa na uongozi wowote wa kidini. Mafundisho ya Kurani yamejumuisha maandiko ya ulimwengu kwa walimwengu wote sio kwa kabila flani au ‘watu waliochaguliwa’. Ujumbe ulio uleta sio mpya ila ujumbe ule ule wa mitume wote: 'Kujisalimisha kwa Allah Mungu Mmoja na umuabudie Yeye peke yake na wafuate wajumbe wa Allah ili ufanikiwe katika maisha haya na wokozi katika maisha yanayo kuja'. Kama vile, Ufunuo wa Allah ndani ya Kurani umejikita katika kumfundisha mwanadamu umuhimu wa kuamini Umoja wa Allah, na kuangaza maisha yao katika mwongozo ambao Yeye ameutuma, ambao umeelezwa kwenye Sheria ya Kiislamu. Kurani ina hadithi za mitume iliyopita, kama vile Noah, Abraham, Moses na Yesu, amani iwe juu yao wote, ikiwemo amri na makatazo kutoka kwa Mungu. Katika muda wa sasa, ambao watu wengi wamekumbwa na shaka, kukata tamaa ya kiroho na kutengwa na jamii na siasa, Mafundisho ya Kurani yanatoa masuluhisho ya kutokuwa na kusudi katika maisha yetu na misukosuko iliyoikumba dunia ya leo .

7. Waislamu Wanaonaje Asili ya Mwanadamu, Kusudi la Maisha na Maisha baada ya sasa?

Ndani ya Kurani Tukufu, Allah amewafundisha wanadamu kuwa wameumbwa kwaajili ya kumtukuza na kumuabudia Yeye, na msingi wa ibada ya kweli ni ufahamu wa Mungu. Viumbe wote wa Allah wanamuabudia yeye kiasili na mwanadamu pekee ndiyo mwenye uhuru wa kuchagua kumwabudia Allah Muumbaji wao au Kumkataa. Hili ni jaribio kubwa, ila pia ni heshima kubwa. Kwakuwa mafundisho ya Uislamu yanajumuisha nyanja zote za maadili, ufahamu wa Mungu unahimiza katika mambo yote ya kibinadamu. Uislamu umeweka wazi kuwa matendo yote ya wanadamu ni matendo ya kuabudu kama yakifanywa kwaajili ya Mungu pekee kwa kufuata Maandiko ya Mungu na Sheria. Kama vile, Kuabudu katika Uislamu hakumaanishi kufanya vitu vya kidini tu, na kwa sababu hii inajulikana kama ‘njia ya kuishi’ badala ya dini. Mafundisho ya Uislam yanakuwa kama rehema na uponyaji katika roho za wanadamu, na sifa kama vile unyenyekevu, ukweli, uvumilivu na sadaka vinaimizwa sana. Cha kuongezea, Uislamu unapinga kiburi na kujiona, kwasababu Mungu Mtukufu ndiye hakimu peke yake wa haki za mwanadamu.

Mtazamo wa Kiislamu wa asili ya mwanadamu ni wa uhalisia na usawa kuwa hauamini mwanadamu kurithi dhambi, ila anaonekana yupo na uwezo sawa wa kutenda mabaya na mazuri; ni chaguo lao. Uislamu unafundisha imani na vitendo vinakwenda sambamba. Mungu amewapa wanadamu uhuru wa kufanya, na kipimo cha imani ya mtu ni matendo na vitendo . Ila, kwakuwa mwanadamu ameumbwa kuwa mdhaifu na mara nyingi anaangukia kwenye dhambi, anahitaji kutafuta muongozo na toba, ambayo, hiyo yenyewe , ni mfumo wa ibada anaoupenda Allah. Kwakuwa asili ya mwanadamu ameumbwa na Mungu kwa Utukufu Wake na Hekima, siyo ‘udhalimu’ au uhitaji wa marekebisho. Nafasi ya toba ipo wazi muda wote. Mungu Mtukufu alijua binadamu wote watakuja kutenda makosa, hivyo mtihani wa kweli ni kufanya toba ya dhambi zao na kujaribu kuziepuka, au kutafuta maisha ya uasi na dhambi, wakijua kabisa haimpendezi Mungu. Usawa wa kweli katika maisha ya Uislamu ni kutengeneza hofa yenye afya katika Allah hakimu halali wa udhalimu na dhambi, na pia imani ya kweli ya Allah, ndani ya Rehema Zake za Milele, mwenye kufurahia kutoa thawabu zake kwa matendo mema na ibada ya dhati. Maisha bila hofu ya Allah inapelekea kwenye dhambi na udhalimu, japo kuamini kwa kutenda dhambi nyingi Mungu hataweza kutusamehe inapelekea katika kuzikatia tamaa rehema zake. Katika mwanga wa hili, Uislamu unafundisha kuwa wasiokuwa na muongozo hukata tamaa na Rehema za Mola, na madhalimu ndio hawana hofu ya Allah Muumba wako na hakimu. Kurani Tukufu kama ilivyofunuliwa kwa Mtume Muhammad, amani iwe juu yake, pia ina mafundisho mengi kuhusu maisha ya baadae na Siku ya Hukumu. Waislamu wanaamini kuwa wanadamu wote mwisho watahukumiwa na Allah, Mfalme wa Wafalme na Hakimu, kwa imani zao na vitendo katika maisha yao ya mwanzo. Katika kuwahukumu wanadamu, Allah Aliyetukuka atakuwa muadilifu kabisa, kwa kuwapa adhabu wale wenye hatia na madhalimu wasiotubu, na kuwa na Rehema kwa wale watu ambao Yeye, katika huruma yake, ataona wanahitaji huruma. Hakuna atakaye hukumuwa zaidi ya uwezo wake, au kwa asichokitenda. Inatosha kusema Uislamu unafundisha kuwa maisha ni mtihani ulioundwa na Allah, Muumbaji, Mtukufu na mwenye Busara; na wanadamu wote watawajibika kwake Allah kwa kile walichokifanya katika maisha yao. Imani ya dhati juu ya maisha ya baadae ni muhimu katika maisha yenye usawa na maadili. Kinyume chake, maisha yanaonekana kama mwisho wake yenyewe, inayopelekea watu kuwa wabinafsi, wapenda mali na maadili mabaya kwa upofu wao wa kufuata matamanio hata kwa kufuata sababu na maadili.

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.