Miujiza ya Muhammad (sehemu ya 3 kati ya 3)

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Kutajwa kwa miujiza mingine mbali mbali ya Mtume, rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.

  • Na IslamReligion.com
  • Iliyochapishwa mnamo 29 Nov 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 6,594 (wastani wa kila siku: 6)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Ipo miujiza mingine mingi aliyoifanya Mtume inayohusiana na Sunnah, au muunganiko wa maneno, matendo, idhini na maelezo ya Mtume.

Shina la Mti

Huko Madina Muhammad alikuwa akitoa mahubiri akiwa ameegemea shina la mti. Pindi idadi ya wanaoabudu ilipongezeka, mtu mmoja alipendekeza mimbari ijengwe ili aweze kuitumia kutoa mahubiri. Mimbari ilipojengwa, aliliacha shina la mti. Abdullah ibn Umar, mmoja wa masahaba, alitoa ushuhuda wa shahidi wa kile kilichotokea. Shina likasikika likilia, Mtume wa rehema akaliendea na kulifariji kwa mkono wake.[1]

Tukio hilo pia linathibitishwa kupitia ushuhuda wa mashahidi uliopitishwa kwa mda mrefu kwa wasomi wanaoaminika (hadith mutawatir).[2]

Mtiririko wa Maji

Zaidi ya wakati mmoja katika tukio ambalo watu walikuwa na uhitaji mkubwa wa maji, baraka ya Muhammad iliwaokoa. Katika mwaka wa sita baada ya kuhama kutoka Makka kwenda Madina, Muhammad alikwenda Makka kwa ajili ya kuhiji. Katika safari ndefu ya jangwani, watu waliishiwa maji yote, ni Mtume tu ndiye aliyebakiwa na chombo ambacho alichukulia udhu kwa ajili ya kuswali. Akaingiza mkono kwenye chombo, maji yakaanza kutoka katikati ya vidole vyake. Jabir ibn Abdullah, ambaye alishuhudia muujiza huo, anasema watu elfu moja na mia tano, ‘Tulikunywa na tukatawadha.'[3] Muujiza huu umepitishwa kwa wasomi wakuaminika (hadith mutawatir).[4]

Kutoka kwa maji kutoka kwa vidole vya binadamu ni sawa na muujiza wa Musa wa kutokeza maji kutoka kwenye mwamba.

Baraka ya Chakula

Zaidi ya tukio moja, Mtume alibariki chakula kwa kuswali au kukigusa ili wote waliokuwepo wapate kushiba. Hili lilitokea nyakati ambapo uhaba wa chakula na maji uliathiri Waislamu.[5] Miujiza hii ilifanyika mbele ya idadi kubwa ya watu, hivyo, haiwezekani kukataa.

Kuwaponya Wagonjwa

Abdullah ibn Ateek alivunjika mguu wake na Muhammad akauponya kwa kuufuta mkono wake juu yake. Abdullah akasema ni kana kwamba hakuna kilichotokea kwake! Mtu aliyeshuhudia muujiza huo alikuwa ni sahaba mwingine, Bara’ ibn Azib (Saheeh Al-Bukhari)

Wakati wa msafara wa Khaybar, Muhammad aliponya macho yenye kuuma ya Ali ibn Abi Talib mbele ya jeshi zima. Ali, miaka mingi baadaye, akawa khalifa wa nne wa Waislamu.[6]

Kutoa Mashetani

Muhammad alimtoa shetani kutoka kwa mvulana aliyeletwa na mama yake kwa ajili ya uponyaji kwa kusema, ‘Toka! Mimi ni Muhammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu!’ Yule mwanamke akasema, ‘Naapa kwa Yule aliyekutuma kwa haki, hatujaona tatizo lake lolote kutoka kipindi hicho.'[7]

Maombi Kujibiwa

(1) Mama yake Abu Huraira, sahaba wa karibu wa Muhammad, alikuwa akiusema vibaya Uislamu na Mtume wake. Siku moja, Abu Huraira alikuja kwa Muhammad akilia na akamwomba amwombee mama yake apone. Muhammad aliomba na Abu Huraira aliporudi nyumbani alimkuta mama yake yupo tayari kuukubali Uislam. Alitoa ushuhuda wa imani mbele ya mwanawe na akaingia katika Uislamu.[8]

(2) Jarir ibn Abdullah alipewa maagizo na Mtume kuliondoa katika ardhi sanamu lililoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu, lakini alilalamika kuwa hawezi kumpanda farasi vizuri! Mtume akamuombea, ‘Ewe Mola, mjaalie kuwa mpanda farasi mwenye nguvu na mjaalie kuwa ni muongozaji na mwenye kuongozwa.’ Jarir anashuhudia kuwa hakuwahi kumdondosha farasi wake baada ya Mtume kumswalia.[9]

(3) Watu walipatwa na njaa wakati wa Muhammad. Mtu mmoja alisimama wakati Muhammad alipokuwa akitoa hutuba yake ya kila Ijumaa, akasema, ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mali zetu zimeharibiwa na watoto wetu wanakufa njaa. Tuombee kwa Mungu.’ Muhammad aliinua mikono yake katika sala.

Wale waliohudhuria wanashuhudia kwamba mara tu aliposhusha mikono yake baada ya kusali, mawingu yalianza kutanda kama milima!

Wakati anashuka kutoka kwenye mimbari yake, mvua ilikuwa inadondoka kutoka kwenye ndevu zake!

Mvua ilinyesha wiki nzima hadi Ijumaa iliyofuatia!

Mtu huyo huyo akasimama tena, akilalamika mara hii, ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, majengo yetu yameharibiwa, na mali zetu zimezama, tuombee kwa Mungu!’

Muhammad aliinua mikono yake na kuomba, ‘Ewe Mungu, (inyeshe mvua) karibu nasi, lakini isiwe juu yetu.

Waliohudhuria wanashuhudia kwamba mawingu yaliondoka kuelekea upande aliouelekeza, mji wa Madina ulizungukwa na mawingu, lakini hapakuwa na mawingu juu yake![10]

(4) Hii hapa hadithi nzuri ya Jabir. Anashuhudia kwamba wakati mmoja, ngamia aliokuwa amepanda alikuwa amechoka kwa sababu ilitumika kubebea maji. Ngamia hakuweza kutembea. Muhammad akamuuliza, ‘Kuna nini juu ya ngamia wako?’ Alipogundua jinsi ngamia alivyochoka, Muhammad alimswalia mnyama na kuanzia wakati huo, Jabir anatuambia, ngamia alikuwa daima mbele ya wengine! Muhammad akamuuliza Jabir, ‘unamuonaje ngamia wako?’ Jabir akajibu, ‘Yuko vizuri, baraka yako imemfikia’ Muhammad alimnunua ngamia kutoka kwa Jabir pale pale kwa kipande cha dhahabu, kwa sharti kwamba Jabir ampande. kurudi mjini! Alipofika Madina, Jabir anasema alimleta ngamia kwa Muhammad asubuhi iliyofuata. Muhammad akampa kipande cha dhahabu na akamwambia amchunge ngamia wake![11]

Si ajabu kwa nini wale waliokuwa karibu naye walioshuhudia miujiza hiyo mikuu ikifanywa mbele ya umati walikuwa na hakika juu ya ukweli wake.



Rejeleo la maelezo:

[1] Saheeh Al-Bukhari.

[2]Zaidi ya masahaba kumi wa Mtume walisambaza taarifa hizo baada ya kusikia kilio cha shina la mti. Tazama kazi za mabwana wa hadithi: ‘Azhar al-Mutanathira fi al-Ahadith al-Mutawatira’ cha al-Suyuti uk. 267, ‘Nadhm al-Mutanathira min al-Hadith al-Mutawatir,’ cha al-Kattani uk. 209 na ‘Shamail’ cha Ibn Kathir uk. 239.

[3] Saheeh Al-Bukhari.

[4]Zaidi ya masahaba kumi wa Mtume (s.a.w.w.) walisambaza taarifa hizo baada ya kusikia kilio cha shina la mti. Tazama ‘Nadhm al-Mutanathira min al-Hadith al-Mutawatir,’ cha al-Kattani uk. 212, ‘al-Shifa’ cha Qadhi Iyyad, juzuu ya 1, uk. 405, na ‘al-’Ilaam’ cha al-Qurtubi, uk. 352.

[5] Saheeh Al-Bukhari. Angalia ‘Nadhm al-Mutanathira min al-Hadith al-Mutawatir,’ by al-Kattani p. 213 and ‘al-Shifa’ by Qadhi Iyyad, juzuu ya 1, uk. 419.

[6] Saheeh Al-Bukhari, Saheeh Muslim

[7] Musnad wa Imam Ahmad, and Sharh’ al-Sunnah

[8] Saheeh Muslim

[9] Saheeh Muslim

[10]Saheeh Al-Bukhar, Saheeh Muslim

[11] Saheeh Al-Bukhar, Saheeh Muslim

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

(Soma zaidi...) Ondoa