Miujiza ya Muhammad (sehemu ya 1 kati ya 3)
Maelezo: Asili ya miujiza iliyofanywa mikononi mwa manabii.
- Na IslamReligion.com
- Iliyochapishwa mnamo 27 Nov 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 8
- Imetazamwa: 9,142 (wastani wa kila siku: 8)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbali na muujiza mkubwa zaidi aliopewa, Kurani Mtume Muhammad alifanya miujiza mingi ya halisi iliyoshuhudiwa na watu wa zama zake waliofikia mamia, na katika visa fulani maelfu.[1] Ripoti za miujiza zimetufikia kwa njia ya kuaminika na dhabiti ya uenezaji wa kifanisi katika historia ya ulimwengu. Ni kana kwamba miujiza ilifanywa mbele ya macho yetu. Njia ya upokezaji ndiyo inayotusadikisha kuwa Muhammad kwa hakika alifanya miujiza hii mikubwa kwa usaidizi wa kimungu na, hivyo, tunaweza kumwamini aliposema, ‘Mimi ni Mtume wa Mungu.’
Miujiza mikubwa ya Muhammad ilishuhudiwa na maelfu ya waumini na wenye kutilia shaka, kufuatia aya za Kurani zilifunuliwa zikitaja matukio ya ajabu. Kurani ilifanya baadhi ya miujiza kuwa ya milele kwa kuitia katika fahamu za waumini. Wapinzani wa zamani wangekaa kimya tu wakati aya hizi zilikaririwa. Lau miujiza hii isingetokea, wangechukua muda wa kuichafua na kumsingizia Muhammad. Lakini badala yake, kinyume cha matarajio kilifanyika. Waumini walikua na uhakika zaidi wa ukweli wa Muhammad na Kurani. Ukweli kwamba waumini walikua na nguvu zaidi katika imani yao na kunyamaza kwa wasioamini na kutokataa kutokea kwao ni kukiri kutoka kwa wote wawili kwamba miujiza ilifanyika sawa na Kurani inavyoelezea.
Katika sehemu hii tutazungumzia baadhi ya miujiza halisi aliyoifanya Muhammad, rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
Miujiza inatokana na Nguvu ya Mungu
Muujiza ni mojawapo ya mambo ambayo yanaimarisha zaidi madai ya nabii wa Mungu. (nukta inahitajika) Miujiza haipaswi kuwa kiini pekee cha imani, kwani matukio ya kiungu yanaweza pia kutokea kwa kutumia uchawi na ushetani. Ukweli wa utume uko wazi na dhahiri katika ujumbe halisi unaoletwa, kwani Mungu ameweka uwezo, ingawa ni mdogo, kwa wanadamu kutambua ukweli kwa jinsi ulivyo, hasa katika suala la monotheazimu (imani kwamba kuna Mungu mmoja tu) Lakini ili kuimarisha zaidi hoja ya Utume, Mwenyezi Mungu alifanya miujiza mikononi mwa Mitume wake kuanzia Musa, Yesu hadi Muhammad. Kwa sababu hii, Mungu hakuleta miujiza kwa matakwa ya watu wa Makkah, lakini Mungu Mwenye Busara alimpa Muhammad miujiza Aliyotaka wakati aliouchagua:
“Na walisema: Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemchem katika ardhi hii. Au uwe na kitalu cha mitende na mizabibu, na utupitishie mito kati yake ikimiminika. Au utuangushie mbingu vipande vipande kama ulivyo dai; au utuletee Mwenyezi Mungu na Malaika uso kwa uso Au uwe na nyumba ya dhahabu, au upae mbinguni. Wala hatutaamini kupaa kwako mpaka ututeremshie kitabu tukisome. Sema: Subhana Rabbi, Ametakasika Mola wangu Mlezi! Kwani mimi ni nani isipo kuwa ni mwanaadamu na Mtume?’’’ (Kurani 17:90-93)
Jibu lilikuwa:
“Na hapana kinacho tuzuia kupeleka miujiza ila ni kuwa watu wa zamani waliikanusha. Na tuliwapa Wathamudi ngamia jike kuwa ni Ishara iliyo dhaahiri, lakini walidhulumu kwaye. Nasi hatupeleki Ishara ila kwa ajili ya kuhadharisha.” (Kurani 17:59)
Walipotaka kwa nguvu, Mungu kwa hekima yake alijua kwamba hawataamini, kwa hiyo alikataa kuwaonyesha miujiza:
“Na waliapa kwa Mwenyezi Mungu kwa ukomo wa viapo vyao, kuwa ikiwafikia Ishara wataiamini. Sema: Ishara ziko kwa Mwenyezi Mungu. Na nyinyi hamjui kuwa zitapo kuja hawato amini. Nasi twazigeuza nyoyo zao na macho yao. Kama walivyo kuwa hawakuamini mara ya kwanza, tunawaacha katika maasi yao wakitangatanga.’” (Kurani 6:109-110)
Tunakusanya hapa baadhi ya miujiza halisi mikubwa iliyofanywa na Mtume Muhammad.
Rejeleo la maelezo:
[1] Miujiza hiyo imeongezeka zaidi hadi elfu . Tazama ‘Muqaddima Sharh’ Saheeh Muslim’ cha al-Nawawi na ‘al-Madkhal’ cha al-Baihaqi.
Ongeza maoni