Maryamu, Mamake Yesu (sehemu ya 1 kati ya 2): Maryamu ni nani?
Maelezo: Wakristo wanamjua Maryamu, mamake Yesu. Vile vile Waislamu pia wanamtambua kama mamake Isa, au kwa Kiarabu, Umm Issa. Katika Uislamu Maria mara nyingi anaitwa Maryam bint Imran; Maryamu binti wa Imran. Makala haya yanatoa historia fulani kuhusu kulelewa kwake na Zakaria kwa hivyo aliweza kutumika hekaluni.
- Na Aisha Stacey (© 2008 IslamReligion.com)
- Iliyochapishwa mnamo 09 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 19 Sep 2022
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 5,328 (wastani wa kila siku: 5)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Inaweza kuwashangaza watu wengi kujua ya kwamba Maryamu ni mmoja wa wanawake waliotukuzwa na kuheshimiwa sana katika Uislamu na kwamba Kurani vile vile imempatia yeye umuhimu mkubwa sana. Maryam ni jina la sura ya 19 ya Kurani, na Sura ya 3 ni Al Imran, iliyopewa jina la familia yake. Uislamu umeipatia hadhi kubwa sana familia yote ya Imran. Kurani inatuambia kuwa:
“Hakika Mwenyezi Mungu alimteuwa Adam na Nuhu na ukoo wa Ibrahim na ukoo wa Imran juu ya walimwengu wote.” (Kurani 3:33)
Mungu alimchagua Adamu na Nuhu kibinafsi, lakini alizichagua familia za Ibrahim na Imrani.
“Ni wazao wao kwa wao; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mwenye kujua.” (Kurani 3:34)
Familia ya Imran inatokana na ukoo wa Ibrahim, familia ya Ibrahim wanatokana na ukoo wa Nuhu na Nuhu anatokana na ukoo wa Adam. Familia ya Imran pia inajumuisha watu wengi wanaojulikana na kuheshimiwa katika mila za Kikristo - Mitume Zakaria na Yohana (anayejulikana kama Mbatizaji), Mtume na Mjumbe Yesu na mamake, Maryamu.
Mwenyezi Mungu alimchagua Maryamu kuliko wanawake wote ulimwenguni. Alisema:
“Na angalia pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Kwa hakika Mwenyezi Mungu amekuteuwa, na akakutakasa, na akakutukuza kuliko wanawake wote.’” (Kurani 3:42)
Amesema Ali bin Abu Talib:
“Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema yakuwa Maryamu, binti ya Imran alikuwa bora kati ya wanawake.” (Saheeh Al-Bukhari)
Kwa Kiarabu jina la Maryamu linamaanisha mjakazi wa Mwenyezi Mungu, na kama tutakavyoona, Maryamu, mamake Yesu, alitolewa kumtumikia Mwenyezi Mungu hata kabla hajazaliwa.
Kuzaliwa kwa Maryamu
Biblia haina maelezo yoyote kuhusu kuzaliwa kwa Maryamu; hata hivyo, Kurani inatujulisha kwamba mke wa Imran alitoa wakfu mtoto wake ambaye hajazaliwa ili kumtumikia Mwenyezi Mungu. Mamake Maryamu, ambaye ni mke wa Imran, alijulikana kama Hana[1]. Aliyekuwa dada ya mke wa Mtume Zakaria. Hana na mumewe Imran walikuwa wameamini kuwa kamwe hawakujaaliwa kupata watoto, lakini siku moja Hana aliomba dua ya dhati kwa kuyenyekea kwa Mwenyezi Mungu abarikiwe mtoto, na kuweka nadhiri kwamba mtoto wake angetumika katika Nyumba ya Mwenyezi Mungu huko Yerusalemu. Mwenyezi Mungu alisikia maombi ya Hana na kumjaaliya kushika ujauzito. Hana alipotambua habari hizo tukufu alinyenyekea kwa Mwenyezi Mungu na kusema:
“Alipo sema mke wa Imran: Mola wangu Mlezi! Nimekuwekea nadhiri kilichomo tumboni mwangu kuwa wakfu; basi nikubalie. Hakika Wewe ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua..” (Kurani 3:35)
Kuna mafunzo ya kujifunza kutokana na nadhiri ya Hana kwa Mwenyezi Mungu, mojawapo ikiwa ni utunzaji wa elimu ya kidini ya watoto wetu. Hana hakuwa na fikira ya ulimwengu huu, bali, alikuwa akijaribu kuhakikisha kuwa mtoto wake alikuwa karibu na Mwenyezi Mungu na vile vile katika ibada zake. Watu wema hawa wateule wa Mwenyezi Mungu, kama vile familia ya Imran, ni wazazi ambao tunapaswa kuwaiga. Mwenyezi Mungu anasema mara nyingi katika Kurani kwamba Yeye ndiye anayetupatia riziki, na anatuonya tujiepushe sisi pamoja na familia zetu kutokana na moto wa Jehanamu.
Katika dua yake, Hana aliomba mtoto wake awe huru kutokana na shughuli zote za kikazi duniani. Kwa kuahidi kwamba mtoto wake atakuwa mtumwa wa Mwenyezi Mungu, Hana alikuwa akimhakikishia mtoto wake uhuru . Uhuru ni aina ya maisha ambayo kila mwanadamu anajitahidi kupata, lakini Hana alifahamu ya kwamba uhuru wa kweli unatokana na utiifu kamili kwa Mwenyezi Mungu. Chanzo chake cha kutamani kupata mtoto wake ambaye hakuwa amezaliwa kilisababishwa na hili. Hana alitaka mtoto wake awe mtu huru, ambaye hatokuwa mtumwa wa mtu yeyote ama mwenye matamanio, ila atakuwa mtumwa wa Mwenyezi Mungu tu. Baada ya muda, Hana alijifungua mtoto wa kike, na vile vile tena akanyenyekea kwa Mwenyezi Mungu katika sala na akasema;
“‘Basi alipo mzaa alisema: Mola wangu Mlezi! Nimemzaa mwanamke - na Mwenyezi Mungu anajua sana aliye mzaa- Na mwanamume si sawa na mwanamke. Na mimi nimemwita Maryamu. Nami namkinga kwako, yeye na uzao wake, uwalinde na Shet'ani aliye laaniwa.” (Kurani 3:36)
Hana alimwita mtoto wake Maryamu. Kwa kuzingatia nadhiri yake kwa Mwenyezi Mungu, Hana alijipata akikabiliwa na hali ngumu. Haikuwa desturi ya wanawake kuhudumu katika Nyumba ya Maombi. Imran, babake Maryamu, alikuwa amefariki kabla ya kuzaliwa, kwa hivyo Hana alimwendea shemeji yake, Zakaria. ambaye alimfariji Hana kwa kumsaidia kuelewa hilo MwenyeziMungu alijua kuwa amejifungua msichana. Mtoto huyu wa kike, Maryamu, alitokana na uumbaji bora zaidi. Mtume Mohammad alitaja[2] kwamba kila mtoto anapozaliwa Shetani humchoma na hivyo husababisha mtoto kulia kwa sauti kubwa. Hii ni ishara ya uhasama mkubwa baina ya wanadamu na Shetani; hata hivyo kulikuwa na tofauti mbili ya sheria hii. Shetani hakumpiga Maryamu vile vile na mwanawe Yesu[3], kutokana na dua ya mamake Maryamu.
Wakati rasmi ulipofika wa Maryamu kwenda kwenye Nyumba ya Maombi, kila mtu alitaka fursa ya kumtunza binti huyu wa Imran aliyekuwa mcha Mungu. Kama ilivyokuwa desturi ya wakati huo, wanaume hao walijaaliwa fadhila nyingi, na Mungu alihakikisha kuwa mlezi wake alikuwa Mtume Zakaria.
“Tena Mola wake Mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo mema, na akamfanya Zakariya awe mlezi wake.” (Kurani 3:37)
Mtume Zakaria alihudumu katika Nyumba ya Mwenyezi Mungu na alikuwa mtu mwenye hekima na maarifa na aliyejitolea kufundisha. Alikuwa na chumba kilichojengwa maalum kwa ajili ya Maryamu, ili aweze kumwabudu Mwenyezi Mungu na kufanya kazi zake za kila siku faraghani. Kama mlezi wake,Mtume Zakaria alimtembelea Maryamu kila siku, na siku moja alishangaa kuona matunda mabichi kwenye chumba chake. Inasemekana kwamba wakati wa majira ya baridi kali angekuwa na matunda mapya ya kiangazi na wakati wa kiangazi angekuwa na matunda mapya ya majira ya baridi kali.[4] Mtume Zakaria alitaka kujua jinsi tunda lilivyofika pale, na Maryamu akamjibu, hakika ni Mwenyezi Mungu ndiye aliyempa riziki. Alisema:
“Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.” (Kurani 3:37)
Fadhila za Maryamu kwa Mwenyezi Mungu wakati huo haukuwa na kifani, lakini imani yake ilikuwa karibu kujaribiwa
Ongeza maoni