Utangulizi mfupi wa Uislamu (sehemu ya 1 kati ya 2)

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Utangulizi mfupi wa Uislamu, dhana ya Mungu katika Uislamu, na ujumbe Wake wa msingi kwa wanadamu kwa kupitia kwa Manabii.

  • Na Daniel Masters, AbdurRahman Squires, and I. Kaka
  • Iliyochapishwa mnamo 06 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 5,066 (wastani wa kila siku: 5)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Uislamu na Waislamu

Neno "Uislamu" ni neno la Kiarabu ambalo linamaanisha "kujisalimisha kwa mapenzi ya Mungu". Neno hili linatokana na mzizi sawa na neno la Kiarabu "salam", ambalo linamaanisha "amani". Kwa hivyo, dini ya Kiislamu inafundisha kwamba ili kufikia amani ya kweli ya akili na uhakika ya moyo, mtu lazima ajisalimishe kwa Mungu na aishi kulingana na Sheria iliyofunuliwa na Mungu. Ukweli wa muhimu zaidi ambao Mungu alifunua kwa wanadamu ni kwamba hakuna kitu cha kimungu au kinachostahili kuabudiwa isipokuwa kwa Mungu Mtukufu, kwa hivyo wanadamu wote wanapaswa kujisalimisha kwake.

Neno "Muislamu" linamaanisha mtu aliye jisalimisha kwa mapenzi ya Mungu, bila kujali rangi, taifa au asili yao. Kuwa Muislamu kunamaanisha kujisalimisha kwa makusudi na utii kwa Mungu, na kuishi kulingana na ujumbe Wake. Watu wengine kwa makosa wanaamini kuwa Uislamu ni dini ya Waarabu, lakini hili ni uwongo. Sio tu kwamba kuna waliosilimu kwenye Uislamu kila kona ya ulimwengu, haswa Uingereza na Marekani, lakini kwa kutazama Ulimwengu wa Kiislamu kutoka Bosnia hadi Nigeria, na kutoka Indonesia hadi Morocco, mtu anaweza kuona wazi kuwa Waislamu wanatoka katika asili mbali mbali, makabila na mataifa. Inafurahisha pia kutambua kwamba, kwa uhakika, zaidi ya 80% ya Waislamu wote sio Waarabu - kuna Waislamu wengi nchini Indonesia kuliko katika Ulimwengu mzima wa Kiarabu! Kwa hivyo, ingawa ni kweli kwamba Waarabu wengi ni Waislamu, Waislamu wengi sio Waarabu. Ila, mtu yeyote anayejisalimisha kwa Mungu na kumwabudu Yeye peke yake ni Muislamu.

Muendelezo wa Ujumbe

Uislamu sio dini mpya kwa sababu "kujisalimisha katika mapenzi ya Mungu", yaani Uislamu, daima imekuwa dini pekee inayokubalika mbele za Mungu. Kwa sababu hii, Uislamu ni "dini ya asili" ya kweli, na ni ujumbe ule ule wa milele uliofunuliwa kwa nyakati zote kwa manabii na wajumbe wote wa Mungu. Waislamu wanaamini kwamba manabii wote wa Mungu, ambao ni pamoja na Ibrahim, Nuhu,Musa, Yesu na Muhammad, walileta ujumbe sawa sawa wa Mungu Mmoja. Kwa sababu hii, Mtume Muhammad hakuwa mwanzilishi wa dini mpya, kama watu wengi wanavyofikiria kimakosa, lakini alikuwa Mtume wa mwisho wa Uislamu. Kwa kufunua ujumbe wake wa mwisho kwa Muhammad, ambao ni ujumbe wa milele na wa ulimwengu kwa wanadamu wote, mwishowe Mungu alitimiza agano ambalo Alifanya na Ibrahimu, ambaye alikuwa mmoja wa manabii wakuu wa awali.

Inatosha kusema kwamba njia ya Uislamu ni sawa na njia ya nabii Ibrahim, kwa sababu Biblia na Kurani inamwonyesha Ibrahim kama mfano mzuri wa mtu aliyejisalimisha kikamilifu kwa Mungu na kumwabudu Yeye bila waombezi. Mara jambo hili litakapokugunduliwa, inapaswa kuwa wazi kuwa Uislamu una ujumbe unaoendelea zaidi na wa ulimwengu wote ukilinganisha na dini nyingine, kwa sababu manabii na wajumbe wote walikuwa "Waislamu", yaani wale ambao walitii mapenzi ya Mungu, na walihubiri "Uislamu", mf. kujisalimisha kwa mapenzi ya Mungu Mtukufu.

Umoja wa Mungu

Msingi wa imani ya Kiislamu ni kuamini umoja wa Mungu Mtukufu- Mungu wa Ibrahim, Nuhu,Musa na Yesu. Uislamu unafundisha kwamba imani safi kwa Mungu Mmoja ni ya angavu kwa wanadamu na kwa hivyo hutimiza mwelekeo wa asili wa roho. Kwa hivyo, dhana ya Uislamu juu ya Mungu ni ya moja kwa moja, isiyo na utata na rahisi kueleweka. Uislamu unafundisha kwamba mioyo, akili na roho za wanadamu ni vifuniko vinavyofaa kwa ufunuo ulio wazi wa kimungu, na kwamba ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu haujajaa mafumbo yanayopingana au maoni yasiyo ya kweli. Kwa hivyo, Uislamu unafundisha kwamba ingawa Mungu hawezi kufahamika na kushikwa na akili zetu za kibinadamu, Yeye pia hatarajii tukubali imani potofu au ya uwongo juu yake.

Kulingana na mafundisho ya Uisilau, Mungu Mtukufu ni Mmoja kabisa na Umoja Wake haupaswi kamwe kuathiriwa kwa kumshirikisha Yeye - si katika ibada wala kwa imani. Kwa sababu hii, Waislamu wanatakiwa kudumisha uhusiano wa moja kwa moja na Mungu, na kwa hivyo wapatanishi wote wamekatazwa kabisa. Kwa mtazamo wa Kiisilamu, kuamini Umoja wa Mungu kunamaanisha kutambua kwamba sala na ibada zote zinapaswa kuwa za Mungu peke yake, na kwamba Yeye peke yake anastahili vyeo kama "Mola" na "Mwokozi". Dini zingine, ingawa zinaamini "Mungu Mmoja", hazifanyi ibada zao zote na maombi kwa ajili Yake peke yake. Pia, wanapeana jina la "Mola" kwa viumbe ambavyo Havijui yote, Nguvu zote na Hazibadiliki - hata kulingana na maandiko yao wenyewe. Inatosha kusema kwamba kulingana na Uislamu, haitoshi tu kwamba watu wanaamini "Mungu ni Mmoja", lakini lazima watekeleze imani hii kwa mwenendo mzuri.

Kwa kifupi, katika dhana ya Uislamu ya Mungu, ambayo inategemea kabisa Ufunuo wa Kimungu, hakuna utata katika uungu - Mungu ni Mungu na mwanadamu ni mwanadamu. Kwa kuwa Mungu pekee ndiyo Muumbaji na Tegemeo endelevu la Ulimwengu, Yeye ni bora zaidi ya uumbaji wake - Muumbaji na muumbwaji hawajichanganyi. Uislamu unafundisha kwamba Mungu ana asili ya kipekee na kwamba yuko huru kutoka kwa jinsia, udhaifu wa kibinadamu na zaidi ya kitu chochote ambacho wanadamu wanaweza kufikiria. Kurani inafundisha kwamba ishara na uthibitisho wa hekima ya Mungu, nguvu na uwepo wake ni dhahiri katika ulimwengu unaotuzunguka. Kwa hivyo, Mungu anamtaka mwanadamu kutafakari juu ya uumbaji ili kujenga uelewa mzuri wa Muumba wake. Waislamu wanaamini kuwa Mungu ana Upendo, Mwenye huruma na Mwenye rehema, na kwamba anajali mambo ya kila siku ya wanadamu. Katika hili, Uislamu unaunga mkono usawa wa kipekee kati ya dini za uwongo na falsafa kali. Dini zingine na falsafa zinaonyesha Mungu kama "Nguvu ya Juu" isiyo ya kawaida ambayo havutii, au haijui maisha ya kila mwanadamu. Dini zingine huwa zinampa Mungu sifa za kibinadamu na zinafundisha kwamba yupo katika uumbaji wake, kwa kuwa mwili katika mtu, kitu - au hata kila kitu. Katika Uislamu, hata hivyo, Mwenyezi Mungu amebainisha ukweli kwa kuwajulisha wanadamu kwamba Yeye ni "Mwenye huruma", "Mwenye rehema", "Anapenda" na "kujibula Maombi". Lakini pia amesisitiza sana kwamba "hakuna mfano wake", na kwamba Yeye yuko juu ya muda, nafasi na uumbaji wake. Mwisho, inapaswa kutajwa kuwa Mungu anayeabudiwa na Waislamu ni Mungu yule yule ambaye Wayahudi na Wakristo wanamuabudu - kwa sababu kuna Mungu mmoja tu. Ni bahati mbaya kwamba watu wengine wanaamini kimakosa kwamba Waislamu wanaabudu Mungu tofauti na Wayahudi na Wakristo, na kwamba "Allah" ndiye tu "mungu wa Waarabu". Dhana hii, ambayo imeenezwa na maadui wa Uislamu, ni ya uwongo kabisa kwani neno "Allah" ni jina la Kiarabu tu la Mungu Mtukufu. Ni neno lile lile la Mungu ambalo hutumiwa na Wayahudi na Wakristo wanaozungumza Kiarabu. Ila, inapaswa kufafanuliwa kuwa ingawa Waislamu wanaabudu Mungu yule yule kama Wayahudi na Wakristo, dhana yao juu yake inatofautiana kwa kiasi fulani na imani za dini zingine - haswa kwa sababu inategemea kabisa Ufunuo wa Kimungu kutoka kwa Mungu. Kwa mfano, Waislamu wanakataa imani ya Kikristo kwamba Mungu ni Utatu, sio tu kwa sababu Kurani inaikataa, lakini pia kwa sababu ikiwa hii ilikuwa asili ya Mungu, angekuwa ameifunua wazi kwa Ibrahimu, Nuhu, Yesu na manabii wengine wote.

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.