Hali ya Hewa ya Rasi ya Arabia
Maelezo: Uvumbuzi wa hivi karibuni wa kijiolojia na wa akiolojia unathibitisha kile Mtume Muhammad alisema kuhusu nchi ya Arabia, kwamba kuna mara ilikuwa na milima na mito.
- Na IslamReligion.com
- Iliyochapishwa mnamo 23 Nov 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 1,741 (wastani wa kila siku: 2)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Kutokana na miujiza ya hadith za Mtume Muhammad, huruma na baraka za Mungu ziwe juu yake, ni kwamba Rasi ya Arabia hapo awali ilikuwa ardhi ya kijani kibichi iliyojaa miti na mito. Mtume Muhammad alisema, 'Saa ya Mwisho (kiama) haitakuja mpaka nchi ya Arabia iwe na makonde na mito kwa mara nyingine'[1]
Hakuna vile Mtume Muhammad ambaye hakuwa mwenye kusoma wala kuandika angeweza kujua, kutokana na uchache wa uwezo wa kisayansi na teknolojia wakati huo, jambo kama hilo kivyake. Cha kushangaza ni kwamba kwa sasa Rasi ya Arabia ni kinyume kabisa na mahali pa majani na mito. Badala yake ina hali ya hewa ambayo ni mojawapo ya hali ya hewa kali zaidi duniani, na haina hata mto moja wa kudumu na takriban asilimia 85 ya jangwa la pili kwa ukubwa duniani, “Jangwa la Arabia” liko ndani yake pamoja na jangwa kubwa la mchanga duniani, “robo tupu” (“Robo tupu” ina wastani wa kiwango cha mvua cha inchi 4 kwa mwaka na joto linaweza kufika nyuzi 54 sentigredi)[2]
Uchunguzi wa jiolojia na akiolojia wa hivi karibuni umethibitisha bila ya shaka yoyote kwamba kuna wakati Rasi ya Arabia ilikuwa na hali ya hewa baridi sana na kwamba kwa kweli ilikuwa eneo lenye majani , maziwa na mito. Hayo yanathibitishwa na yafuatayo:
1) Wanasayansi wamerekodi kwamba dunia ilishuhudia enzi yake ya barafu ya mwisho katika kipindi cha Pleistocene Epoch kilichoanza takriban miaka milioni 2.59 iliyopita na kumalizika takriban miaka 11,700 iliyopita. [3] Katika kipindi hiki sehemu kubwa za dunia zilifunikwa kwa barafu na hali ya hewa ilikuwa baridi sana kuliko ilivyo leo na wastani wa halijoto duniani ulikuwa kuanzia 5°C hadi 10°C chini ya halijoto ya sasa. Wakati barafu lilifunika sehemu za Ulaya, Asia na Amerika, Rasi ya Arabia ilishuhudia hali nzuri ya hewa inayofanana na hali ya sasa ya Ulaya.
2) Mwaka wa 2014 watafiti nchini Saudi Arabia waligundua mabaki ya tembo katika Jangwa la Nafud. Huku zaidi ya asilimia 60 ya mifupa ya tembo yakiwa yameshikana, ikiwa ni pamoja na pembe nzima, inaonyesha wazi kwamba jangwa la Nafud liliwahi kuwa na hali ya hewa iliyoruhusia tembo kuishi. Pia ni muhimu kutaja kwamba tembo aliyegunduliwa alikuwa mkubwa kwa asilimia ya 50 kuliko tembo wa sasa, na takribani mara mbili ya uzito wake.[4]
Zaidi ya hayo, mwaka wa 2017 Kituo cha Mawasiliano cha Kimataifa cha Saudi Arabia kilitangaza ugunduzi wa mabaki ya viumbe wengine ikiwa ni pamoja na mamba na farasi wa bahari, na zaidi ya hayo, ugunduzi, kwa jumla, wa maziwa na mito 10,000 katika Rasi ya Arabia.[5] Zaidi ya hayo, mwaka wa 2017 Dk. Eid Al Yahya , ambaye ni mwanaaikiolojia mashuhuri, aligundua tembo-majitu (mammoth) wa kwanza nchini Saudi Arabia; na katika miaka kumi iliyopita aligundua na kurekodi zaidi ya mikuki elfu ya jiwe (iliyotengenezwa kutoka kwa silika) na zana nyingine za uwindaji wa wanyama wakubwa katika maeneo ya jangwa ya mbali ambayo yanaonyesha kuwa kuna wakati watu waliwahi kuwinda katika maeneo haya ya majangwa.
3) Ugunduzi wa mafuta na gesi katika Rasi ya Arabia. Mafuta ni mabaki ya mimea na wanyama waliokufa waliowahi kuishi katika bahari, mito au maziwa mamilioni ya miaka iliyopita. Ukosefu wa oksijeni uliwezesha viumbe hawa waliokufa kudumisha vifungo vyao vya hidro-kaboni vinavyohitajika katika uundaji wa mafuta na gesi. Mabonde ya mito hasa yana viwango vya chini vya oksijeni kutokana na mzunguko wa maji wenye nguvu unaoyafanya kuwa mahali pazuri kwa uundaji wa mafuta na gesi. Joto na shinikizo na kupita kwa mamilioni ya miaka kisha kulisababisha uundaji wa mafuta na gesi.[6]
Saudi Arabia, Kuwait, Falme za Kiarabu (UAE), pamoja na nchi nyingine katika Rasi ya Arabia hazihitaji kutambulishwa linapokuja kwa hifadhi zao za mafuta. Cha kushangaza ni kwamba visima vya mafuta katika Rasi ya Arabia hupatikana baharini na pia barani (juu ya ardhi; sio baharini). Kisima cha Ghawar katika mashariki mwa Saudi Arabia ni kisima kikubwa zaidi cha mafuta duniani (kulingana na hifadhi yake iliyothibitishwa), kimekuwa kikitumika tangu miaka ya 1950, kina mapipa ya bilioni 70 ya hifadhi iliyobaki, na cha kushangaza kijiografia ni kwamba kiko barani katika robo tupu na Jangwa la Arabia. Vivyo hivyo, Kisima cha Burgan katika nchi ya Kuwait ni kisima cha pili duniani kwa ukubwa wa hifadhi ya mafuta na pia kiko barani ndani ya Jangwa la Arabia. Ugunduzi wa visima hivi vya mafuta ya nchi kavu ina maana kuwa kwa mamilioni ya miaka, hata kabla ya enzi ya barafu ya mwisho, Rasi ya Arabia haikuwa nchi kavu kama ilivyo leo, badala yake ilikuwa paradiso ya maziwa, mito na mabonde ya mito.
4) Picha za satelaiti zilizochukuliwa kutoka angani zimethibitisha kuwa Rasi ya Arabia ilikuwa na jiografia na hali ya hewa tofauti kabisa. Tume ya Saudia ya Utalii na Urithi wa Taifa iliripoti kuwa katika miaka ya 1990 “Landsat” ilitoa picha za sehemu za mashariki na kusini mwa Saudi Arabia, ikiwa ni pamoja na Robo Tupu. Picha za satelaiti zilifunua njia za biashara za zamani, njia za mito na mabonde; zote ambazo sasa zimefunikwa na matuta ya mchanga.
In Kwa kumalizia, uvumbuzi wa kijiolojia na wa akiolojia unathibitisha msemo wa Mtume Muhammad, kwamba kunao wakati Rasi ya Arabia ilikuwa imejaa milima na mito; jambo ambalo Mtume Muhammad hakuweza kulijua kivyake isipokuwa kwa njia ya ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Vielezi-chini:
[1] Saheeh Muslim, Kitabu # 05, Hadeeth # 2208
[2] Elizabeth Howell, Agosti 2013, The 10 Biggest Deserts on Earth, Live Science, Imetolewa https://www.livescience.com/38592-biggest-deserts.html
[3] Kim Ann Zimmermann, August 2017, Pleistocene Epoch: Facts about the Last Ice Age, Live Science Contributor, Retrieved from https://www.livescience.com/40311-pleistocene-epoch.html
[4] Kim Ann Zimmermann, August 2017, Pleistocene Epoch: Facts about the Last Ice Age, Live Science Contributor, Imetolewa https://www.livescience.com/40311-pleistocene-epoch.html
[5] Habib Toumi, September 2018, Ancient Saudi Arabia was once lush and green, Gulf News, Retrieved from https://gulfnews.com/news/gulf/saudi-arabia/ancient-saudi-arabia-was-once-lush-and-green-1.2153218
[6] Roger N. Anderson, Why is oil usually found in deserts and arctic areas? 'Scientific American', Retrieved from https://www.scientificamerican.com/article/why-is-oil-usually-found
Ongeza maoni