Maelezo ya Kurani kuhusu tando za buibui (sehemu1 kati ya 2)
Maelezo: Aya ya Kurani inaonyesha kwa usahihi udhaifu wa kijamii wa nyumba ya buibui ambao tumeanza kuujua na kuuelewa hivi karibuni.
- Na IslamReligion.com
- Iliyochapishwa mnamo 23 Nov 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 4,290 (wastani wa kila siku: 4)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
"Mfano wa walio wafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni mfano wa buibui alivyo jitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui, laiti kuwa wanajua." (Kurani 29:41)
Aya hii ya Kurani inatoka katika sura ya 29, Buibui. Sehemu tunayoangalia hapa ni kwamba Mungu anataja kuwa nyumba dhaifu zaidi ni ile ya buibui. Katika lugha tajiri ya Kiarabu, neno “Awhan” linatafsiriwa kuwa (dhaifu zaidi); na kuangalia zaidi katika maana hiyo kunaonyesha kwamba inamaanisha udhaifu mkubwa na kutokuwa na msaada kimwili na kiakili.
Kutokana na upanuzi wa utafiti wa maumbile na wanyamapori katika karne ya 20 na 21, wanasayansi wamefichua, wamerekodi na kupiga video mambo ya ajabu kikweli katika maisha ya buibui.
Uwindaji wa ngono
Kati ya aina zaidi ya 45,000 za buibui zinazojulikana , ni kawaida sana buibui wa kiume kuuawa na kuliwa na wenzi wao wa kike[1]; neno linalojulikana kama uwindaji wa ngono. Haijulikani kwa nini hii inatokea, hata hivyo, nadharia moja iliyopendekezwa na wanasayansi ni kwamba mwili wa kiume humpa mwanamke virutubisho vinavyohitajika sana vinavyomwezesha kutaga mayai yenye afya. Utafiti uliofanywa na Kituo cha Majaribio cha Hispania cha Eneo la Ukame umebaini kuwa katika aina nyingi za buibui, wanawake huwaua wenzi wao bila kujali kama ndume anaonekana kuwa duni au la.[2] Katika aina nyingi, buibui wa kike humuua hata kiume yeyote ambaye hana nia ya kushirikiana naye kimapenzi.[3]
Katika baadhi ya aina za buibui, kama vile buibui mvuvi mweusi, buibui wa kiume hufa moja kwa moja baada ya kujamiana kutokana na sababu za ndani; na kisha huliwa kikatili na bibi yake. [4] Katika aina zingine za buibui, buibui wa kiume hufa moja kwa moja baada ya kujamiana mara chache tu, na katika idadi kubwa ya aina za buibui, wale wa kike huwa na umri mrefu kuliko wa kiume; huku viume huishi kwa miezi michache tu na wa kike kwa miaka michache.
Wanapokuwa na bahati nzuri ya kujamiana na kufanikiwa kuishi, buibui wa kiume wenye miili ndogo, huku wakijua hulka ya mwenzio ya uwindaji, hukimbia hapo hapo kwa ajili ya kuokoa maisha yao [5] na kumuacha mwenzao wa kike akilea pekee yake mayai ya idadi tofauti kutoka machache hadi kufikia karibu na mayai elfu. Hiyo ndio hali ya Buibui Mzururaji wa Brazil.
Maajabu zaidi katika mila hatari ya ngono ya buibui, utafiti uliyofanywa na watafiti Lenka Sentenska na Stano Pekar, kutoka Chuo Kikuu cha Masaryk katika Jamhuri ya Cheki mwaka wa 2013, uligundua kuwa katika aina ya buibui ya 'Microcaria Sociabilis' ya buibui inayojulikana kama mjane mweusi, buibui wote wa kike na wa kiume kawaida huuana na mwenye uwezo humla mwenzake baada ya kujamiana; na kwamba katika aina hii kwa mahususi, kinyume na kile kilichoaminika mbeleni, buibui wa kiume huua zaidi na kula mwenzao kuliko buibui wa kike.[6]
Maisha ya buibui wadogo
Katika aina nyingi, buibui wadogo waliozaliwa karibuni wana mama yao tu wa kuwalisha na kuwalinda. Chakula kinapokuwa kichache mama analazimika kuwalisha mayai yake yasiyoanguliwa; hivyo buibui mdogo lazima apitie mshtuko na changamoto ya kula ndugu zake ambao hawajaanguliwa bado ili aendelee kuishi.[7]
Wakati hakuna mayai mengine ya kula tena, na hakuna wadudu wa kutosha wa kuanguka kwenye utando au hawakupatakiana na mama, uchunguzi mwingine unaonyesha ya kwamba buibui wadogo, baada ya kukata tamaa, hugeukiana wenyewe na kila mmoja kumla mwenzake, na utando mdogo huo wenye msongamano hugeuka kuwa jela ya mauaji. Kwa kukosa msaada, buibui mama pia huwaua na kuwala wadogo wake ili kuweza kuishi siku nyingine.
Vielezi-chini:
[1]Pappas, Stephanie. Juni 2016. Male Orb-Web Spiders Are Choosy About Their Cannibal Mate. Live Science. Imetolewa http://www.livescience.com/54944-male-orb-web-spiders-choosy-about-cannibal-mate.html
[2]Gannon, Megan. Aprili 2014. Food vs. Sex: Why Some Female Spiders Eat Males Before Mating. Live Science. Imetolewa http://www.livescience.com/45066-virgin-female-spiders-eat-males.html
[3]Gannon, Megan. Aprili 2014. Food vs. Sex: Why Some Female Spiders Eat Males Before Mating. Live Science. Imetolewa http://www.livescience.com/45066-virgin-female-spiders-eat-males.html
[4]Lewis, Tanya. Juni 2013. Tough Love: Male Spiders Die for Sex. Live Science. Imetolewa http://www.livescience.com/37536-spiders-die-for-sex.html
[5]Szalay, Jessie. Desemba 2014. Tarantula Facts. Live Science. Imetolewa http://www.livescience.com/39963-tarantula.html
[6]Cadieux-Shaw, Lillianne. Mei 2013. Study: Male Black Widow Spiders eat their Mates too. Canadian Geographic. Imetolewa http://www.canadiangeographic.ca/article/study-male-black-widow-spiders-eat-their-mates-too
[7]Englehaupt, Erika. Februari 2014. Some Animals …facts. Science News. Imetolewa https://www.sciencenews.org/blog/gory-details/some-animals-eat-their-moms-and-other-cannibalism-facts
Ongeza maoni